Kitabu gani ambacho kimewahi kubadilisha maisha yako na unatamani wengine tukisome?

Maisha yangu yote nilikuwa natafuta kitabu kinachoelezea historia ya binadamu kwa kifupi bila mafanikio mpaka pale nilipokutana na "Sapiens" cha Prof Yuval Noah Harari.
 
Maisha yangu yote nilikuwa natafuta kitabu kinachoelezea historia ya binadamu kwa kifupi bila mafanikio mpaka pale nilipokutana na "Sapiens" cha Prof Yuval Noah Harari.
Hiki kitabu kipo vizuri sana,

Unapata kufahamu Mambo mengi sana bila kusahau burudani ya kutosha toka kwa Mwandishi(Noah Harari) mwenyewe njisi anavyoelezea kwa urahisi mno.

Mimi huwa napenda wapenzi wa vitabu wapate kukisoma.
 
Prof Yuval Noah Harari anakitumia kiingereza kama vile ni mother tongue ya kwake vile. Mie nasumbuliwa na hearing complications lakini nikimsikiliza huwa nasikia vizuri tu neno kwa neno.
 
Kaka,
Huyu Noah Harari yupo vizuri Mno ni Mwandishi mzuri sana anayeelezea mambo yanayo onekena mazito au magumu kwa urahisi Mno.

Siku za nyuma nilipata kumsikiliza akiwa kwa Hard Talk-Al Jazeera anahojiwa nilifurahi.

Homo dues: Pia nimekisoma, kwakweli vitabu vyake ukianza kuvisoma hutotamani uvishushe mkononi.
 
Prof Yuval Noah Harari anakitumia kiingereza kama vile ni mother tongue ya kwake vile. Mie nasumbuliwa na hearing complications lakini nikimsikiliza huwa nasikia vizuri tu neno kwa neno.
Ndio ndio kiingereza chake kinaeleweka mno na yupo makini katika kuwasilisha hoja zake.
Nilipata kumtazama Al Jazeera.

Myahudi huyu anastahili pongezi kwa Uandishi wake.
 
Wewe unamjua huyu inaonekana,anaelezea vizuri sana.

Kama hujakisoma hiki kipya "21 Lessons for The 21st Century" kitafute usome. Karibu nakimaliza hapa.

Jamaaka cover mambo kibao, kutoka Bhagavad Gita , Talmud, Quantum Physics, mpaka Kinjekitile Ngwale.

Mimi mtu anayesoma vitabu kama hivi, na kuvielewa, hata kama hatukubaliani mambo, nitamuheshimu kwa kujua tu ana exposure ya mambo aliyoyasoma humu kwenye vitabu hivi.

Ahsante kwa kuwa katika kundihili mkuu.Hata kujadiliana na mtu kama wewe napata confidence kwamba nikitaja mambofulani tutaelewana.
 
Ndio ndio kiingereza chake kinaeleweka mno na yupo makini katika kuwasilisha hoja zake.
Nilipata kumtazama Al Jazeera.

Myahudi huyu anastahili pongezi kwa Uandishi wake.
Weka hapa basi mkuu hicho kitabu tufaidike nasi
 
Noah Harari nimemsoma katika Money na sasa nasoma Homo Deus ni mwanahistoria mzuri sana. Ni kama nabii yaani.
 
Nakuelewa sana Kaka,huwa najifunza mambo mengi kupitia michango yako hapa Jamvini,Heshima kwako.

Homo Deus hiki nadhani open minded person atikufurahia sana.

Mfano freewill alivyopata kuielezea kwa kutumia Robo-rat Laboratory.Panya anadai anafreewill wakati maisha yake yanaendeshwa kwa remote.

Wacha nikitafute hicho kipya lakini kama una pdf nitashukuru sana ukikiweka hapa,Japo vitabu vyake ngumu sana kuvipata kwa Pdf.

Shukran!!
 
Nitakutafutia, hivyo viwili vya kwanza ninavyo PDF home, hicho kipya nitakitafuta.

Huyu jamaa watu wanamfuatilia sana, akitoa kitabu tu kinakuwa maarufu, kwa hivyo vitakuwepo tu mitandaoni.
 
Noah Harari nimemsoma katika Money na sasa nasoma Homo Deus ni mwanahisroria mzuri sana. Ni kama nabii yaani.
Kabisa Mkuu,

Kuna siku Mkurugenzi wa Tbc Dr. Ayoub Rioba alikuwa kwa Tv,akiomba watu wapate kuvisoma vitabu vya Noah harari Homo Sapiens & Deus Yeye alikuwa na "Hard copy" kabisa kavishika...Nilifurahi kuona kwamba anavifahamu vitabu hivi.

Kusoma vitabu kwa Watanzania Wengi ni Shughuli Pevu(Visingizio lukuki vya kuhararisha Uzembe)...Labda mpaka watu wasukumwe kwa bakora.

"Kama Elimu ni Gharama fikiri kuhusu Ujinga"
 
Nitakutafutia, hivyo viwili vya kwanza ninavyo PDF home, hicho kipya nitakitafuta.

Huyu jamaa watu wanamfuatilia sana, akitoa kitabu tu kinakuwa maarufu, kwa hivyo vitakuwepo tu mitandaoni.
Pamoja sana Kaka,
 
Mtanzania kusoma hata umshikie bunduki..

Mimi mwenyewe nilikuwa mvivu ila nimeanza kusoma hivi vitabu taratibu taratibu na sasa umekuwa ni utaratibu wangu..
 
navipata wapi mkuu
 
Mtanzania kusoma hata umshikie bunduki..

Mimi mwenyewe nilikuwa mvivu ila nimeanza kusoma hivi vitabu taratibu taratibu na sasa umekuwa ni utaratibu wangu..
Safi sana,

Kila Jambo Jema linagharama yake.

Miezi miwili iliyopita nilikuwa namsoma kijana mmoja Walter Rodney,

Huku nikiwa na kumbukumbu ya M'jamaica Marcus Garvey "People without a knowledge of their past history,origin and culture is like a tree without roots"

Mwafrika huyu Walter kiufupi alikuwa Smart/Brilliant huku akipata first degree akiwa na miaka 21 kwa first class na PHD Miaka 24.
Alipata kufundisha University of Dar el salaam UDSM Mwaka 1969-74.

How Europe underdeveloped Afrca; Moja ya kitabu chake kizuri katika kuitambua vyema Africa na yaliyotokea katika Enzi za ukoloni.
Kimeelezea mambo mengi mfano growth without development & development by contradiction.

Pia hakusahau kuwachachafya apologists & Bourgeois writer wa Ukoloni barani africa huku akiwaita wapuuzi wakubwa sana kwa kufanya balance sheet credits & debits wakihitimisha good & bad mema yamezidi mabaya hivyo ukoloni ulileta neema kwa Africa, labda umeleta neema ya maize na viazi na Cash crops kama banana republic's....na kusambaza Elimu ya kitumwa na kuwagawa watu na unyonyaji wa kiwango cha Juu mno.

Pia Kelezea ulafi na uchu wa Portugal na Spain waliodai wao ni kizazi na wanapaswa kurithi Mali zote za dunia hivyo Papa Vatican apigie mstari ghafla England,Holland na France wakasema nyinyi mabwana habari gani za ajabu mwatuletea..? Hilo jambo haliwezekani hata kidogo.

Kitabu kinaelezea kwa uzuri sana Africa yetu.

Walter alizaliwa 1942 akafa mwaka 1980 kwa Gari kutegewa bomu.

"Reading books makes you a wonderful person, an Intellegent, a creative person and What not,When you read good books"

Ni jambo zuri sana kutafuna vitabu Kama viwavi Jeshi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…