Kitabu gani ambacho kimewahi kubadilisha maisha yako na unatamani wengine tukisome?


kwa maelezo hayo tu ni dhahili mwandishi alidhamiria kurekebisha jamii, nitajaribu kukitafuta nikisome.
 
yeah, hata mimi nakipenda sana
 
Biblia ndiyo mpango mzima ni kitabu pekee duniani kinachosomwa na watu wengi duniani. na kinachofahamika na watu wengi na ndiyo njia ilinyooka .zaidi ya 80% ya watu duniani wamewai kusoma au kisikia habari ya kitabu hiki kitakatifu.jina la bwana libarikiwe .ni utabiri wa biblia kwamba injili itaubiriwa kwa watu wote mathayo 28:19~20
 
The Devil's Double, its a true story, kimeandikwa na Latif Yahia.

vitabu vya Alfu Lela u Lela pia ni vizuri.
 
The Big picture by Ben Carson kilinifanya nijue vitu gani vya kuvipa kipaumbele katika maisha yangu. Hakika nimenifanya nione na kufikiria baadhi ya masuala ambayo hayaonekani na kufikirika kirahisi
 
Kuna vitabu vitatu ambavyo vimeshangia kubadili maisha yangu kwa kiwango kikubwa sana. Ningependekeza kila mtanzania avisome.
1. THINK AND GROW RICH
Hiki kimenisaidia kuweza kufikia uwezo mkubwa ulio ndani yangu na kuniwezesha kuona fursa nyingi zinazonizunguka.
2. RICH DAD, POOR DAD
Hiki kimenisaidia kuhusu utofauti kati ya elimu ya darasani na elimu halisi ya mtaani. Kimenisaidia kuona mambo ambayo nilifichwa darasani na ambayo ni ya msingi sana ili kufanikiwa.
3. THE RICHEST MAN IN BABYLON
Hiki kimenisaidia kuhusiana na maswala yote yanayohusuana na fedha kuanzia kuweka akiba mpaka kuwekeza. Kimeniwezesha kuweza kujilipa mimi mwenyewe hata kwa kipato kidogo sana na kuweza kujenga akiba iliyotosha kuanzia biashara.
Hivyo ni vitabu ambavyo natamani kila mtanzania avisome. Kama huna vitabu hivi nitumie email kwenye amakirita@gmail.com na nitakutumia vyote vitatu bure kabisa.
Au unaweza kutembelea AMKA MTANZANIA na ukajifunza mengi pamoja na uchambuzi wa vitabu hivi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…