Kitabu gani ambacho kimewahi kubadilisha maisha yako na unatamani wengine tukisome?

Kitabu gani ambacho kimewahi kubadilisha maisha yako na unatamani wengine tukisome?

Awaken the giant within - Tonny Robbins
The monk who sold his Ferari- Robin Sharma
The power of subconcious mind Joseph murphy
The richest man in Babylon
Love is not enough-- Aaron Bek
Think and Grow rich - Napoleon Hill


Binafsi vitabu hivi vimenipanua mawazo sana - na kuona kuwa ni muhimu kuishi maisha ya malengo na daima kulenga kutumia vipaji vyangu (ambavyo sikufikiri am this poweful) kuachieve the greatest in life. Na pia vimenisaidia sana kuwashawishi ndugu na jamaa wasome ili wawe na mitazamo hasi katika maisha .

Hicho cha love is not enough ni kizuri sana kwa walio kwenye mahusiano na ndoa : talks of how communication, expectations can ruin or build relationshiops. The things you know but never imagined they have power to change relationships. I wish kungekuwa na reading club itasaidia kufikisha malengo yetu ya usomaji .

Kudoz mleta mada.
 
AWAY FROM HOME.jpg DOTTO NSHIMBA.jpg LOST IN LIES.jpg navikubali vitabu vya huyu jamaa anaitwa Dotto Nshimba,; Away from home pamoja na Lost in lies,nimesoma review zake nimekipenda sanaa,ingawa nashindwa namna ya kukipata,inaonekana ndio aliyeandika kitabu cha FUNDAMENTALS OF HISTORY
 
Vipo 3
Bible
What a Catholic should do in marriage by I think is Bruno
Dynamic principles of the mind by Adam Bryan
 
1. The Millionair Fastlane by MJ DeMarco
2. Rich Dad Poor Dad by R. Kiyosaki
3. E-Myth by Michael Gerber

Namba 2 wengi wamekisoma, kama umesoma namba 2 basi anza na 1 malizia na 3. Kama hujasoma vyote nakushauri uvisome kama nilivyovipanga, yaani uanze na 1 umalize na 3.
 
Wasalaaam ndugu zangu, natumai wote ni wazima.

Leo hii naanzisha huu uzi kwa dhumuni zuri na maalumu la kusambaza maarifa kwa wanajukwaa hili na pengine watu wengine wa nje ya jukwaa hili.

Mpango ni kurusha vitabu mbalimbali kwenye jukwaa hili ambavyo vitaweza kuwasaidia watu na kuweza kuwapanua uwezo wa kiakili endapo utakuwa umesoma vitabu vizuri na bado unavyo itakuwa ni vema ukirushe kwenye uzi huu ili watu mbalimbali wasome na waelewe.

Natumai watu wa kada mbalimbali watapita na hakuna mtu ambaye atakosa cha kujifunza hapa. Sasa vitabu vinaweza kuja kwa mfumo wa PDF, MOBI, EPUB etc. Na kama utakuwa na hard copy basi watu wanaweza kukutafuta kama tu mtakuwa mekubaliana.

Natanguliza shukrani zangu.

Mimi naanza na kitabu kizuri sana ambacho kimenisadia kwenye kukuza uwezo wa kufikiri mambo kwenye biashara. Kinaitwa "The Go Giver" nashauri mtu akipata muda akisome.
Kama kimenisaidia basi natumai hata wewe kitakusaidia.

Kwa kifupi kinaelezea jinsi gani ambavyo mtu anaweza kufanya biashara kubwa lakini bado biashara hiyo itaipa jamii inayomzunguka faida.
Tofauti na mawazo ambayo wafanya biashara wengi na wajasiriamali wanakuwa nayo kwamba biashara ni faida tu na utafanya biashara sehemu yenye faida tu.

Kinaanza na mtu moja alikuwa ni kijana mdogo anafanya kazi kwenye kampuni fulani huko MAREKANI sasa akawa anahangaika sana kupata utajiri wa haraka. Kila siku alikuwa na mipango mikubwa ya biashara lakini hafanikiwi. Siku moja akapata nafasi kukaa na tajiri mkubwa huko MAREKANI na akaambiwa sifa ya kuwa Tajiri ni lazima ujifunze kutoa kwa watu kabla ya kutanguliza faida.

Mbeleni kinaonyesha jamaa analalamika kwamba ukifanya biashara kwa huruma huwezi kutajirika hata siku. Lakini akakutana na tajiri mwingine ambaye alimueleza vilevile. Na mwishowe akaja kujua kama matajiri wakubwa wote wanakuwa na sifa zinazofanana.

Young Malcom.

CC: UncleBen , FisadiKuu , MSEZA MKULU , Consigliere

 
Back
Top Bottom