Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
MWANAMKE MWANAMAPINDUZI
Hiki ni kitabu kinachohusu maisha ya Biubwa Amour Zahor kilichoandikwa na Zuhura Yunus.
Kitabu hiki kinahusu maisha yake Bi. Ubwa akiwa msichana mdogKio wa Kiarabu katika mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka wa 1964.
Nilipoanza kukisoma kitabu ghafla ikanijia filamu fupi niliyooana udogoni ya siku ‘’El Comandante,’’ Fidel Castro alipoingia Cuba baada ya kumuangusha Fulgencio Batista.
Pamoja na Castro ile filamu ilikuwa ikimuonyesha msichana kavaa unifomu za jeshi amebaba bunduki na kashika, ‘’megaphone,’’ anatoa matangazo akiwa juu kwenye gari lililojaa askari Wapinduzi (neno hili nimejifunza ndani ya kitabu hiki mwalimu wangu mwandishi wa kitabu Zuhura Yunus).
Kweli bint huyu kashuka kutoka Sierra Maestra na Fidel Castro na hakuna shaka ni mwanamke shujaa.
Lakini ushujaa wake haufikii hata robo ujasiri wa Biubwa.
Fikra zangu zikashuka kutoka kwa huyu bint zikenda Zanzibar katika hekaheka ya mapinduzi ndani ya kitabu hiki kuna picha ya Biubwa mwanamke pekee kisha wa Kiarabu katikati ya wanaume Wapinduzi ameshika bunduki kama vile kashika kikapu anaelekea Soko Muhogo.
Biubwa mwanachama wa ASP kashiriki katika mapinduzi ya kuiangusha serikali ya mseto wa ZNP na ZPPP.
Mapinduzi yaliyojaa umwagaji wa damu ambayo harufu ya damu ile haijapata kwisha.
Biubwa kafikaje hapa?
Lakini kitabu hiki cha maisha ya Bi. Ubwa Amour Zahor si kitabu utakishika na kukiacha.
Salama yako katika kitabu hiki ni wala usikiguse.
Ukikigusa ni sawa na ndege shorwa katua katika ulimbo.
Ndege huyu mdogo wa umbo akitua kwenye ulimbo hawezi kwamwe kujinasua mwenyewe.
Ukikigusa kitabu hiki ukakifungua na kuanza kusoma basi jua ushanasa.
Hiki si kitabu cha maskhara.
Shaaban Robert alipata kuandika kitabu, ‘’Ashiki Kitabu Hiki.’’
Mimi nakusihi na nakuambia maneno haya, ‘’Kisome kitabu hiki.’’