Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Baada ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Rais wa Kwanza wa Tanganyika na pia Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) tarehe 14 Oktoba 1999 mengi yamesemwa na kuandikwa kuhusu msimamo wake na uadilifu kuhusu Uislam Tanzania.
Nia ya kitabu hiki ni kueleza jinsi Mwalimu Nyerere katika kipindi chake cha uongozi alivyoshughulikia suala la Uislam na Waislam wa Tanzania.
Hii ni historia ya uhusiano wa Mwalimu Nyerere na Waislam kwa kipindi cha takriban robo karne toka pale aliposhika madaraka ya nchi mwaka 1961 hadi alipoachia madaraka mwaka 1985.
Ni mategemeo ya mwandishi kuwa kitabu hiki kidogo kitaweka wazi yale ambayo hayafahamiki kwa wengi.
Kitabu kinapatikana Ibn Hazm Media Centre: Msikiti wa Manyema, Mtoro na Mtambani kwa bei ya Shs: Elfu Mbili.