Kitabu kipya: Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania

Kitabu kipya: Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania

Mzee ni muda wa kustafu sasa... Waachie ambao kidogo umri unaruhusu
Da Vinci,
Napenda kusoma na kuandika toka udogo wangu.
Kazi nimestaafu napumzika lakini siwezi kustaafu kusoma, kuandika na kufikiri.

Hivi hutumii misuli.
Ingekuwa ni kazi ya misuli nadhani siku nyingi ningekuwa nje ya ulingo.

Au unakereka na kalamu yangu?
 
Mohamed Said,
Nipo Rusumo Mohamed Said nawezaje kukipata kitabu hiki?

Ila kabla sijakitia mkononi kwangu je waweza tafasiri ya michoro na alama zilizokatika cover ya kitabu hiki?

Naona kuna mifano ya watu, wamegawanywa kwa rangi nyekundu kulia (vila shaka ukanda wa pwani) na nyeusi upande wa (kushoto bila shaka ni bara)

Lakini idadi ya vitu hivi vinapungua kwa upande mwekundu na kuongezeka upande wa kulia!

Ingawa katika base (labda miaka ya mwanzo wa uhuru. Labda) wekundu walikuwa wengi kuliko weusi na kadri pyramid inavyopanda juu uwiano kati ya weusi na wekundu unatofautiana.

Naomba tafasiri shekh wangu!
 
Sooth,
Kitabu changu kinaeleza changamoto za uhuru na miaka 25 baada yake.

Ikiwa kuna dhulma kazifanya Rais Kikwete tafadhali zieleze hapa tuzifahamu.
Kama wewe huzijui dhuluma zilizoratibiwa kitaasisi zilizokuwa zinafanywa dhidi ya wakristo wakati wa JK, basi unapoteza mamlaka ya kuzungumzia malalamiko dhidi ya waislamu.

Shida yetu kuu ni ushabiki, kufumba macho na kupenda chako hata kama kina ukakasi. Ndo maana hatuwezi kufanikiwa ktk suala hili la upendeleo wa kidini. Kuna wapuuzi wanadhan ni sawa kumng'oa jicho mwenzio kwa sababu na yeye alikung'oa. #NiZamuYetu

Ushauri wangu ni kwamba jikite kwenye kutafuta suluhisho, haitoshi tu kulalamika. Wewe umwsimuliwa, sisi wengine tumejionea na kudhulumiwa miaka michache tu iliyopita wakati wa JK. Tusonge mbele.
 
Hiki kitabu kina tofauti gani na cha Prof. Njozi "Mwembechai Killings"? Mada zile zile, vyanzo vilevile, ila majina tofauti.
 
Naomba nikipate hiki kitabu kesho,
Sina nafasi ya kufika huko mtaa wa manyema vipi uwezekano upo ?@Mohamed Said,
 
Da Vinci,
Napenda kusoma na kuandika toka udogo wangu.
Kazi nimestaafu napumzika lakini siwezi kustaafu kusoma, kuandika na kufikiri.

Hivi hutumii misuli.
Ingekuwa ni kazi ya misuli nadhani siku nyingi ningekuwa nje ya ulingo.

Au unakereka na kalamu yangu?
Shekh wangu @Mohaded Said

Hata kama unapenda kusoma na kuandika toka utoto wako, je ni sahihi kutumia upenzi huo kufitinisha jamii?

Kwa nini usiandike yale yanayotuunganisha zaidi?...ya nini kuandika yanayotujengea shimo kubwa kati yenu Waislamu, Wakristu na sie wa dini za asili?

Unafaidika na nini wajukuu zako wakwanza mafarakano na ndugu zao wa imani tofauti nao?
 
Rusumo,
Kuna mtu kaniuliza tafsiri ya hiyo cover.
Mimi sijui kwani usanifu wa cover kafanya publisher.

Nitamuuliza In Shaa Allah.
Kitabu hiki muombe mtu akununulie hapa Dar es Salaam.
Kama hata wewe mwandishi hujui tafasiri ya kava la kitabu hiki basi ni hatari zaidi yaliyoandikwa humo!

Naomba uninunulie unitumie nipe mawasiliano yako nikurudishie hela utakayotumia!
 
Kama hata wewe mwandishi hujui tafasiri ya kava la kitabu hiki basi ni hatari zaidi yaliyoandikwa humo!

Naomba uninunulie unitumie nipe mawasiliano yako nikurudishie hela utakayotumia!
Mhadzabe,
Kweli cover sijui mimi najua kutafiti na kuandika lakini usanifu wa cover sina utaalamu.

Nimechapa vitabu na Oxford University Press Nairobi mimi naletewa kitabu kimekamilika wala siulizwi cover.
 
Mohamed Said,
Mbona prof. Njozi alishaandika kitabu kuhusu suala la EAMWS? Kwann unarudiarudia mambo yale yale kutoka vyanzo vile vile? Ndo kusema hapajawahi kuwa na udini baada ya Nyerere kufariki?

Vinginevyo wewe ni broker wa mtafaruku wa kidini. Zikitokea rabsha kama za Book haram(Mungu apishie mbali), basi utakuwa na ushawishi na mali nyingi sana.
 
Back
Top Bottom