Mohamed Said, ]Mzee wangu Mohamed Said;
Kwanza kabisa kwa moyo wa dhati nikupe hongera kwa uthubutu wa kuendelea kuandika,na nakushauri endelea kufanya kazi hiyo hadi pale Mola wako atakapokuita,utakuwa umetuachia hazina safi sisi na vizazi vyetu.
Pili,sifurahishi sana baadhi ya maoni yatolewayo na baadhi ya watu kuhusu kitabu chako na shutuma zinazotolewa juu yako,si busara hata kidogo kukuita majina yasiyoendana na umri wala hulka yako,mfano,mchochezi,mfitinishaji nk.
Nasema si busara kwa sababu zifuatazo;
1: Wote wanaokushutumu hawajasoma kitabu chako;hata ukiwauliza wanukuu japo mstari mmoja kutoka humu kitabuni hawawezi na wala hawajui nini kilichoandikwa ndani yake.
*Busara ilikuwa ni kununua kitabu na kukisoma,ikiwa kina tatizo hoja zingejengwa juu ya contents na sio abstract ideas,ambazo mkosoaji hajui ni nini anakosoa ila tu anatumia ufundi wa maneno,hili ni kosa ndugu zangu.
2: Kutajwa kwa neno "kanisa" haiwezi kukifanya kitabu kizima tu kiwe INVALID kisa kutajwa kwa neno kanisa.Huu ni wakati wa kuwa huru kifkira na kimtazamo,ikiwa tu tutataka kusikia ama kusoma kile tu kinachoendana na mawazo yetu na kinachotufurahisha tunakuwa si viumbe huru bali wafungwa wa mawazo.
3: Kuficha historia/ukweli wa mambo mabaya/uovu uliotendwa nyuma na watu,dini,dhehebu au mtu kwa kigezo cha teknolojia hakiifanyi jamii kuwa salama bali hujenga chuki za ndani kabisa na mwisho wa siku madhara huwa mabaya zaidi ya kama ingesemwa na kukemewa hadharani na kutafuta suluhu.
4:Mimi nikiwa mkristo nakushukuru mzee wangu,nitakitafuta kitabu nitasoma,hakuna mwisho wa kujifunza na kupata maarifa hakuchagui yametolewa na nani,ana nini,anaamini nini,yuko wapi na wakati gani?..
Swali;Leo tunajifunza historia za biashara ya Watumwa (Slave trade),American civil War,Socialism,WW1 & WWII,Cold war,Jews massacre,Maji maji,nk; matukia haya yote yalishapita,lengo la kujifunza ni nini basi?.
- Je;lengo ni kutufanya tuwe waovu kama waliowafanya babu zetu watumwa na kuwafunga minyororo na kuwatumikisha?.
- Au ni kutufanya tujifunze kuuwa wanadamu wenzetu kama Hitler na Mussolini?.
Na je,kujifunza historia hii ya mzee wetu ndiyo italeta chuki na madhara kwa jamii,zaidi ya hizi za Mkwawa kukatwa kichwa na wajerumani,Au mfalme Leopolds kuwakata mikono babu zetu wenye ujuzi?.
Bila shaka kuna la kujifunza kwa mwenye kufikiri.