Mohamed Said,
Kwa hiyo kitabu ulichoandika kikawa na jina lako juu na picha ya Nguruwe na title Uislam ni upuuzi hakitakushughulisha kwa sababu ni kazi ya Publishers na kinakuingizia hela nzuri tu?
Shekh wangu, umekuwaje Siku hizi?
Hii ni serious intellectual poverty; kwa vile vitabu kama vyako haviwezi kupitia peer review process basi utaandika vingi tu ili kuwapa "red meat" wafuasi wako. Baada ya uhuru Tanganyika, kanisa la katoliki na la lutheran walikuwa wanamiliki mashule na mahospitali mengi sana zaidi ya asilimia 70 nchini lakini Nyerere akataifisha vyote hivyo na kuvifanya mali ya serikali kusudi watanzania wote wahudumiwe bila kujali dini zao halafu wewe unakuja na udini wa "Kanisa" leo hii mwaka 2020.
Keyser Söze anasema hakuna udini nchini wewe unasema kuwa wale waliojitolea kupigania uhuru kwa nafsi na mali zao hawaoni hivyo; je wao wanaona nini Tanzania? kwamba nchi imegwanyika kidini? Mzee Mwinyi naye anasema hivyo? (ingawa yeye hakupigania uhuru.) Kawawa naye alikuwa anasema hivyo? Amil Jamal naye alikuwa anasema hivyo, Derek Bryceson aliyejenga Magomeni naye alikuwa anasema hivyo? Said Maswanya naye alikuwa anasema hivyo? Tewa Said Tewa anaye alikuwa anaona hivyo? Sheikh Amri Abedi naye alikuwa anaona hivyo? Ukoo wake unakumbukwa kwa barabara ya Kaluta hapo Dar na Uwanja wa Amri Abeid huko Arusha.
Achana na hii rubbish ya waislamu kuonewa uanze kuandika vitabu vya kuhamasisha watu wako wajitafutie maendeleo kupitia fursa zilizopo kiushindani. Kwa mahesabu ya haraka haraka inaonekana kuwa kwa Tanzania mpaka sasa waislamu ndio matajri zaidi ya wakristo na wala matajiri hao hawalalamikii udini. Huoni kuwa unapiga riwaya zilizopitwa na wakati?
Kuna siku moja nilikuambia kuwa Christopher Columbus alipokwenda West Indies, hakuwa na meli zake mwenyewe, bali alitumia meli za watu wengine ambao alikuwa nao kwenye msafara ule. Jumla msafara mzima ulikuwa na watu zaidi 85. Columbus alikuwa mtaliano, na crew nzima walikuwa wahispania. Lakini kwa vile Columbus ndiye aliyekuwa kamanda na mongozaji, basi ndiye anayekumbukwa na historia mpaka leo ingawa Juan de la Cosa aliyekuwa mmiliki wa Meli ya Sata Maria alikuwamo na aliwalipa wafanyakazi wa meli ile kwa fedha zake mwenyewe, Cristobal Quintero ambaye alikuwa anamiliki meli ya Pinta, naye alikuwamo kwenye msafara na naye pia aliwalipa wafanyakazi wa meli ile kwa fedha zake mwenyewe, na vile vile Juan Nino aliyekuwa mmiliki wa meli ya Nina alikuwamo pia kwenye msafara, naye pia aliwapa wafanyakazi wa meli yake kwa fedha zake mwenyewe. Unashindwaje kukubaliana na misingi ya historia halafu eti ujiite mwanahistoria wa kuchokonoa mambo ya udini? Furaha yako ni kuona mambo kama haya?
Kwa hiyo kitabu ulichoandika kikawa na jina lako juu na picha ya Nguruwe na title Uislam ni upuuzi hakitakushughulisha kwa sababu ni kazi ya Publishers na kinakuingizia hela nzuri tu?
Shekh wangu, umekuwaje Siku hizi?
Hapa chini ni nukuu kutoka mchango wa Mwandishi uitwao "Baraza" kwenye warsha/semina/mkutano mjini Berlin mwaka 2011 (angalia attachment):
"If the status endures signs are that Muslims will confront the Catholic Church as they had confronted Germany and British colonialism."
Maswalo ya kujiluizal:
1. Jee, tokea 2011 hadi hivi leo (miaka 8 baadaye), kuna dalili zozote kuwa ukaribu mkubwa na ushirikiano anaodai upo kati ya Serikali na Kanisa Katoliki umebadilika au bado?
2. Tishio lake la Waislamu kukabiliana na Kanisa Katoliki kama Waislamu walivyowadhibiti Wakoloni iwapo hali haitabadilika vingechukua sura gani?
3. Kwanini Mwandishi adai Waislamu watakabiliana na Kanisa Katoliki na siyo Serikali?
WAKOLONI wetu walikuwa WAJERUMANI na baadae WAINGEREZA kama tulivosoma shuleni! Vp Mkuu una chuki na hao Mabwana? Tangu uwasome ushawahi kuwarushia japo kokoto 1 achilia mbali tofali? 4by94,
Kichuguu, Kichuguu,
Umeandika vyema na nimekusoma na kukuelewa lakini nakusihi uondoe lugha kali hili neno ''rubbish,'' ni tusi na linaharibu mjadala.
Kitabu changu cha kwanza na ndicho kilicholeta mshtuko mkubwa katika historia ya nchi yetu ni kitabu cha maisha ya Abdul Sykes ambacho kupitia maisha yake nilieleza historia ya TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.
Mshtuko ulisababishwa na kule kutofautiana kukubwa kwa historia hii niliyoandika mimi na historia rasmi iliyokuwa ikifahamika na kuaminika.
Kitabu kilifanyiwa ''review'' na mabingwa wa historia ya Afrika - John Iliffe, Jonathan Glassman na James Brennan na ''review'' hizi zilichapwa katika Cambridge Journal of African History.
Katika mabingwa hawa watatu wa Historia ya Afrika wawili tunafahamiana vizuri - James Brennan na Jonathon Glassman na tumepata kuwa pamoja hapa Tanzania na Marekani.
Kitabu hiki kupita katika mikono ya mabingwa hawa ndiyo kukawa mwanzo wa kitabu hiki kufahamika na kusababisha mwandishi kualikwa kwingi na pia kutiwa katika miradi miwili ya uandishi wa historia ya Afrika chini ya Oxford University Press Nairobi na New York na kazi nilizoandika zote zilichapwa.
Umetaja majina ya viongozi kama Ali Hassan Mwinyi, Rashid Kawawa, Tewa Said Tewa na wengine wengi.
Bahati mbaya hukuwataja Aboud Jumbe na Kitwana Kondo ambao wamepata kutahadharisha kuhusu udini Tanzania.
Katika nafasi yangu kama mwandishi nina mengi nayafahamu kuhusu viongozi hawa ambayo wengi hawayajui na wenyewe hawawezi kuyasema hadharani.
Nina mswada ambao haujachapwa kitabu, ''Christian Hegemony and the Rise of Muslim Militancy in Tanzania,'' ndani ya mswada huu kuna sura ambayo nimeeleza yale ambayo Rais Mwinyi alikutananayo katika utawala wake na yalimtaabisha sana.
Moja ya matatizo yaliyomkabili ni taarifa kutoka kwa Waziri wa Elimu Prof. Kighoma Malima akimfahamisha yale aliyoshuhudia katika wizara hiyo ya vijana wa Kiislam kunyimwa nafasi za elimu ya juu.
Mzee Tewa kanieleza mengi kabla ya kifo chake na nilimwandikia taazia na unaweza kusoma maisha yake katika kitabu changu, ''Watu Maarufu Katika Uhuru wa Tanganyika,'' (2018).
Naandika mambo ambayo nimeyafanyia utafiti na nina hakika nayo.
Siandiki riwaya kama unavyodhani.
Huenda aandikae riwaya ukawa ni wewe.
Nakuwekea hapo chini links ambazo zitakusaidia wewe kujua zaidi hili somo na pia kunielewa:
Lako sio suala la chuki ndio ukweli wenyewe huo. Kwani huoni kila kukicha wanafunzi wa vyuo mbalimbali kutoka Tanzania Bara, wanajeshi na Taasisi mbalimbali huwa zinapelekwa Zanzibar kwenda kutiwa chuki za uwarabu pale mkunazini cathedral.?
Wanaelezwa kwamba wazee (bibi zao) walifagilishwa chini kwa kutumia matiti yao, hivi huyajuwi hayo au Waarabu walikuwa wakiwalawiti mababu zao. Mbona hukupiga kelele za kusomeshwa siasa za chuki. Mwache Mohammed Said atusomeshe bado angali hai maana hatutaweza kuyajuwa kama hakutuelezea.
Huyu Sheikh Mohamed Said,ni mwana historia tu,anachofanya hakina tofauti na wana historia wanaofukua habari za Hitler,Mussolini na hata mauaji ya kimbari ya Rwanda
Sidhani kama kumshambulia binafsi kuna tija,aidha tusome ili tupingane nae kwa hoja au tumkwepe tufanye mambo mengine
Mbona shule tulifundishwa somo la historia mambo ya kuudhi sana ya chifu mangungo na karl peters,lakini hakuna anaelalamika kuwa tunajazwa chuki
Waelimishe waislamu wafanyeje ili kujikwamua hapa sasa hivi walipo, sio kuwajaza chuki kwa mambo yaliyopita ambayo hayarekebishiki, wewe ni mchochezi mkubwa wa chuki, kwa iyo unataka waislamu wabebe mapanga wawakate waliowadhulumu, kuwa na busara hata kidogo
Baada ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Rais wa Kwanza wa Tanganyika na pia Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) tarehe 14 Oktoba 1999 mengi yamesemwa na kuandikwa kuhusu msimamo wake na uadilifu kuhusu Uislam Tanzania.
Nia ya kitabu hiki ni kueleza jinsi Mwalimu Nyerere katika kipindi chake cha uongozi alivyoshughulikia suala la Uislam na Waislam wa Tanzania.
Hii ni historia ya uhusiano wa Mwalimu Nyerere na Waislam kwa kipindi cha takriban robo karne toka pale aliposhika madaraka ya nchi mwaka 1961 hadi alipoachia madaraka mwaka 1985.
Ni mategemeo ya mwandishi kuwa kitabu hiki kidogo kitaweka wazi yale ambayo hayafahamiki kwa wengi.
Kitabu kinapatikana Ibn Hazm Media Centre: Msikiti wa Manyema, Mtoro na Mtambani kwa bei ya Shs: Elfu Mbili.
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.