Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
- #121
Kichuguu,Huenda hujawahi kusoma vitabu vyake na kujua maudhui yake; hiki siyo kitabu chake cha kwanza..
Kitabu cha kufungua mwaka.
Sent using Jamii Forums mobile app
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kichuguu,Huenda hujawahi kusoma vitabu vyake na kujua maudhui yake; hiki siyo kitabu chake cha kwanza..
Mzee ukijibu hili swali nitafurahi sana unaposema "KANISA" unamanisha nini?Sorry Mimi ndie nimeleta maneno mengi.
Turudi kwenye swali langu LA msingi unaposema "kanisa" unamanisha nini?
Ndio maana my first point ilikuwa kuhusu usawa timilifu. Haupo duniani. Kila jamii itakuwa tu na watu ambao ama kwa halali au kwa hisia, wataona wanaonewa na kudhulumiwa.Mtama...
Vijana gani umewakusudia wahimizwe kazi?
Vijana gani hawahitaji kuhimizwa kazi?
Wakishahimizwa kazi dhulma dhidi yao itakuwa ishaondoka?
Mtama...Ndio maana my first point ilikuwa kuhusu usawa timilifu. Haupo duniani. Kila jamii itakuwa tu na watu ambao ama kwa halali au kwa hisia, wataona wanaonewa na kudhulumiwa.
Kuhusu kuhimiza vijana, point yangu ni kuwa; kulalamika kuhusu dhulma kila siku, hakutawasaidia hao unaosema wanadhulumiwa. Maana hapa tulipo sasa hivi sijui kama kuna mtu ana appetite na kufukua makaburi ya 1960's, yalikoanza haya mambo.
Binafsi sina shida na kujifunza historia, na naamini kuna mambo mengi sana ambayo yanatakiwa either kuwa updated au kubadilishwa kama kuna ushahidi wa upotoshoshaji, kwa lengo la kuweka historia sawa. Ila kama lengo ni kuonyesha tu dhulma dhulma kila siku; unatengeneza mazingira ambayo kusikilizana itakuwa ngumu.
Ni hayo tu, kila la kheri. Nitatafuta copy yangu
Waachie wanaotuhumiwa wajibu tuhuma zao.Mtama...
Kitabu cha Abdul Sykes nilikiandika kwa nia ya kusahihisha historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Kitabu ulichosoma ni matokeo ya utafiti huu.
Kutokana na utafiti ule yakaingia mambo mengi mathalan kwa nini walioandika historia ile walifanya juhudi kubwa ya kupotosha ukweli.
Moja ya mambo niliyogundua ni hofu iliyokuwapo ya kuwaadhimisha wale waliopigania uhuru ambao wengi walikuwa Waislam.
Kuanzia hapa ndipo yakaanza kufunguka mengi na yote ni ya kutisha.
Wewe umeliona hili na unajaribu kuhalalisha dhulma iliyojengwa na kupangwa kwa kutaka iaminike kuwa yanayowasibu Waislam ni ya kutegemewa kwa kuwa hakuna chembelecho, "usawa timilifu."
Lakini ukiingia katika historia ya Tanganyika utakuta kuwa sababu ni kutamalaki kwa njama wala mimi sikukusudia kuwepo na usawa uliokamilika.
Ushauri wangu kwako ni huu.
Jizuie.
Waachie wanaotuhumiwa wajibu tuhuma zao.
Lau una hamu ya kushiriki mjadala huu himiza mtuhumiwa ajibu tuhuma zake.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mtama...Waachie wanaotuhumiwa wajibu tuhuma zao.
Tatizo unapotuhumu kwamba viongozi wa nchi wanaotoka dini fulani, by extension unawagusa na watu wa dini hiyo.
Naomba kuuliza maswali yafuatayo:
Baada ya kifo cha Mwalimu Julius Kambarage Nyerere (Rais wa Kwanza wa Tanganyika na pia Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania) tarehe 14 Oktoba 1999 mengi yamesemwa na kuandikwa kuhusu msimamo wake na uadilifu kuhusu Uislam Tanzania.
Nia ya kitabu hiki ni kueleza jinsi Mwalimu Nyerere katika kipindi chake cha uongozi alivyoshughulikia suala la Uislam na Waislam wa Tanzania.
Hii ni historia ya uhusiano wa Mwalimu Nyerere na Waislam kwa kipindi cha takriban robo karne toka pale aliposhika madaraka ya nchi mwaka 1961 hadi alipoachia madaraka mwaka 1985.
Ni mategemeo ya mwandishi kuwa kitabu hiki kidogo kitaweka wazi yale ambayo hayafahamiki kwa wengi.
Kitabu kinapatikana Ibn Hazm Media Centre: Msikiti wa Manyema, Mtoro na Mtambani kwa bei ya Shs: Elfu Mbili.
Huyu mzee ana tabia ya kukimbia maswali au ufafanuzi kuhusu maandishi yake mwenyewe. Inaonekana hajiamini au hajui anachoandika. Kanisa kwa maana/definition ipi na ya nani? Dhehebu/madhehebu gani? Taasisi zipi? Jee ni Uongozi pekee au inajumuisha Uongozi pamoja na Waumini wao?Mkuu Kichuguu maalim MS kunaswali LA kumuuliza anaposema "KANISA" anamaanisha nini?
Kinyungu,Naomba kuuliza maswali yafuatayo:
1. Kwenye kitabu chako kuna maoni yoyote ya upande wa viongozi wa kanisa?
2. Kanisa unaloliongelea ni lipi kwa sababu Tanzania kuna makanisa mengi sana.
3.Kwa nini unadhani hilo kanisa ulilolichagua peke yake ndiyo linachagiza mambo serikalini?
Ukinijibu haya nitaleta mengine.
Ndjabu...Huyu mzee ana tabia ya kukimbia maswali au ufafanuzi kuhusu maandishi yake mwenyewe. Inaonekana hajiamini au hajui anachoandika. Kanisa kwa maana/definition ipi na ya nani? Dhehebu/madhehebu gani? Taasisi zipi? Jee ni Uongozi pekee au inajumuisha Uongozi pamoja na Waumini wao?
Kwanini ushindwe kumjibu maswali yake hadi anunue kitabu chako kwanza na kukisoma? Huoni hapo inaleta walakini kwamba unafanya kila jitihada kuepuka kujibu moja kwa moja maudhui ya maandishi yako mwenyewe? Mfano, mimi nimesoma mchango wako fulani wa warsha/semina moja uliyofanya Berlin, lakini umeshindwa kunijibu swali langu hadi leo. Jee, hiyo imekaaje?
Hiyo picha ya mwisho ni wakati wq vita vya MAJIMAJIMWENZAKO PASCAL ANAPOANDIKA HAYA UNAKAA KIMYA NA KUMTEREMSHIA LIKES
PASCAL WACHA KUTULETEA PROPAGANDA ZA MAKANISA NA WAZUNGU
Uliweka picha hizi eti ndio waarabu walivyowatesa watumwa wa kiafrika
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
![]()
Hizi picha wajemeni sio picha ya kuchorwa, ni picha za kweli na halisi zilizopigwa na kamera za wadhungu na sii lazima ziwe zimepigwa Zanzibar.
Pascal Utumwa ulipigwa marufuku mwaka 1833
Britain abolished slavery throughout its empire by the Slavery Abolition Act 1833 (with the notable exception of India), the French colonies re-abolished it in 1848 and the U.S. abolished slavery in 1865 with the 13th Amendment to the U.S. Constitution.
Abolitionism - Wikipedia
CAMERA ILIVUMBULIWA MWAKA 1888
1888
The use of photographic film was pioneered by George Eastman, who started manufacturing paper film in 1885 before switching to celluloid in 1888–1889. His first camera, which he called the "Kodak", was first offered for sale in 1888.
History of the camera - Wikipedia
HIZO PICHA ULIZOLETA ZILIPIGWA NA CAMERA IPI ??
BADO TU MNAENDELEZA HIZI PROPAGANDA NA CHUKI DHIDI YA WAARABU NA WAISLAMU ?? HASA HUKU KWETU ZANZIBAR
NJIA YA MWONGO NI FUPI
Ndjabu...Kwanini ushindwe kumjibu maswali yake hadi anunue kitabu chako kwanza na kukisoma? Huoni hapo inaleta walakini kwamba unafanya kila jitihada kuepuka kujibu moja kwa moja maudhui ya maandishi yako mwenyewe? Mfano, mimi nimesoma mchango wako fulani wa warsha/semina moja uliyofanya Berlin, lakini umeshindwa kunijibu swali langu hadi leo. Jee, hiyo imekaaje?
Nilimwuliza swali hilo mwanzo hakunijibu. Mara nyingi maandiko yake ni ya kushtumu sana dini ya Nyerere; na anaposema udini, huelekea kuamini kuwa Nyerere aliwaacha waislamu na kuweka watu wa dini yake (wakatoliki). Mara zote neno Udini kwake ana maana ya Ukatoliki dhidi ya Usilamu, na neno kanisa lina maana ya Ukatoliki.Mkuu Kichuguu maalim MS kunaswali LA kumuuliza anaposema "KANISA" anamaanisha nini?
Tuseme keshasoma hicho kitabu lakini bado ana maswali? Kwanini inakuwia vigumu sana kujibu tu ya maswali ya wachangiaji bila ujanja ujanja wenye kuashiria unakwepa wajibu wako kama Mwandishi?Ndjabu...
Nani kazungumza kuhusu kununua kitabu?
Nimesema asome kitabu.
Haya si masuala ya kujibiwa kwa mstari mmoja.
Nisingeweza kusahihisha historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika kwa kuandika sentensi hata 100.
Nimeandika kitabu cha kurasa zaidi ya 300+.
Huu wangu si uwanja wa watu wasio na uwezo wa kusoma.
Sent using Jamii Forums mobile app
Asante nitavitafutaMtama...
Hapana mtu wa kawaida haingii humo.
Ikiwa unataka kujua haya vipo vitabu unaweza kusoma kupanua uelewa wako.
Msome Bergen (1981), Sivalon (1992)na Njozi (2002).
Bahati mbaya kitabu cha Njozi kimepigwa marufuku lakini kipo katika mtandao unaweza kukipata.
Kitabu vyote hivyo vina historia yake nikiwa na maana ya kuwa vilipotoka na kujulikana yaliyomo ndani hofu ilitanda.
Bergen na Sivalon havimo tena katika mzunguko yapata sasa miaka 20 na zaidi.
Sent using Jamii Forums mobile app
Well said!Nilimwuliza swali hilo mwanzo hakunijibu. Mara nyingi maandiko yake ni ya kushtumu sana dini ya Nyerere; na anaposema udini, huelekea kuamini kuwa Nyerere aliwaacha waislamu na kuweka watu wa dini yake (wakatoliki). Mara zote neno Udini kwake ana maana ya Ukatoliki dhidi ya Usilamu, na neno kanisa lina maana ya Ukatoliki.
Katika serikali ya Nyerere kulikuwa na wakatoliki wawili tu; Nyerere mwenyewe na George Kahama. Lakini kuna wakati huyu bwana aliwahi kuashilia kuwa Nyerere aliweka Padri wa katoliki kuwa waziri wa Elimu (Padri Simon Chiwanga) kusudi apendelee wakatoliki tu na kuwazima waislamu kielimu. Yaani haufanya hata utafiti kidogo tu kujua kuwa Chiwanga huyo hakuwa mkatoliki. Yeye anposikia ukiristo anaamani kuwa ni taasisi moja inayopingana na usilamu, yaani hajui kuwa ukiristo una denomination nyingi sana ambazo hazikubali kiitikiadi, ni kama uislamu ulivyo na deneomination nyingi ziszo kubaliana kiitikadi, mfano sunni vs Shiite. Kwa mheshimiwa huyu mambo yangekuwa sawa kama nchi yoote ingekuwa inaongozwa na wasilamu tu, ingawa sijui huwa anataka waislamu wa namna gani!
Kichuguu,Nilimwuliza swali hilo mwanzo hakunijibu. Mara nyingi maandiko yake ni ya kushtumu sana dini ya Nyerere; na anaposema udini, huelekea kuamini kuwa Nyerere aliwaacha waislamu na kuweka watu wa dini yake (wakatoliki). Mara zote neno Udini kwake ana maana ya Ukatoliki dhidi ya Usilamu, na neno kanisa lina maana ya Ukatoliki.
Katika serikali ya Nyerere kulikuwa na wakatoliki wawili tu; Nyerere mwenyewe na George Kahama. Lakini kuna wakati huyu bwana aliwahi kuashilia kuwa Nyerere aliweka Padri wa katoliki kuwa waziri wa Elimu (Padri Simon Chiwanga) kusudi apendelee wakatoliki tu na kuwazima waislamu kielimu. Yaani hakufanya hata utafiti kidogo tu kujua kuwa Chiwanga huyo hakuwa mkatoliki. Yeye anaposikia ukristo anaamani kuwa ni taasisi moja inayopingana na uislamu, yaani hajui kuwa ukiristo una denomination nyingi sana ambazo hazikubali kiitikadi, ni kama uislamu ulivyo na denomination nyingi zisizo kubaliana kiitikadi, mfano Sunni vs Shiite. Kwa mheshimiwa huyu mambo yangekuwa sawa kama nchi yoote ingekuwa inaongozwa na waislamu tu, ingawa sijui huwa anataka waislamu wa namna gani!
Mhadzabe,
Rusumo,
Kuna mtu kaniuliza tafsiri ya hiyo cover.
Mimi sijui kwani usanifu wa cover kafanya publisher.
Nitamuuliza In Shaa Allah.
Kitabu hiki muombe mtu akununulie hapa Dar es Salaam.