Kitabu kipya: Dola, Kanisa na Tatizo la Udini Tanzania

Mazindu...
Kwa kuleta suala la picha za chupa za Coca Cola sidhani kama ndiyo tunachojadili hapa.

Wala sijashindwa kuweka ''reviews,'' za vitabu vyangu.

''Reviews'' zote ninazo wala si kazi kubwa kuziweka hapa.

Nilichomweleza Ndjabu ni kuwa wala asijiitabishe kuwa nimeandika kitabu kwa kuwa hili linamsumbua kwa miaka mingi hapa Barzani.

Nimemwambia kuwa na achukulie kuwa mimi sijaandika chochote na kama sijaandika chochote ''review'' itatoka wapi?

Kinachonichekesha mimi kama wewe unavyocheka kuona picha za Coca Cola ni mtu kushughulishwa na ''review'' ya kitabu asishughulishwe na kitabu chenyewe.

Mimi nikikusoma na hizi kejeli za ''huyu mzee'' basi nakuwa nimeshakufahamu na wala sipati tabu na wewe kwani wewe si wa kwanza wala hutakuwa wa mwisho kunikejeli hadi ukweli utakapokudhihirikia.

Wengi wanaponifahamu taratibu heshima hurejea.

Wewe hunijui na inawezekana ndiyo mara yako ya kwanza kunisoma au kunisikia.

Nimeandika vitabu saba na kipo kingine In Shaa Allah kitabu cha nane kinakuja.

Ninazo pia ''paper'' kadhaa wala sijui hesabu yake nilizoandika kuwasilisha katika vyuo mbalimbali hapa nyumbani na nje ya mipaka ya Tanzania.

Lakini mimi furaha yangu huzidi pale unapotokea mtu kama wewe ukanikejeli.

Wala mimi sitakuuliza wewe umeandika nini kwani nakujua kutokana na unavyoandika na kujenga hoja hapa Barzani na kutiatia maneno ya Kiiingereza kuwa lipo tatizo.

Wewe kama nilivyomfahamisha mwenzio nakuomba jiaminishe kuwa mimi si lolote wala sijaandika chochote cha kutambulikana katika dunia ya usomi.

Hayo mengine wala sijaona haja ya kuyasemea.

Kitabu changu cha mwisho kimeingia Tanzania mwanzo wa mwaka huu hicho hapo chini pamoja na baadhi ya vingine.

Kitabu cha watoto nimekusudia kuwafunza Kiingereza na historia ya Zanzibar.

Sidhani kama bado unacheka.
 

Attachments

  • SYKES BOOK ALL EDITIONS.jpg
    54.1 KB · Views: 6
  • THE SCHOOL TRIP GUGU.jpg
    71.5 KB · Views: 6
  • THE TORCH ON KILIMANJARO SECOND EDITION.png
    33.3 KB · Views: 7

Mzee nimesoma alichoandika
Kitwana Kondo lakini sijaona ushahidi wowote ule kuthibitisha alichoandika

Nilitarajia kuona takwimu zilizoshiba ushahidi na sio porojo za aliyekusudia kuwajengea imani kuwa mnaonewa
 
Huu uzi ulipaswa kufungwa hapa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…