Kitabu: Maisha ya Malcom X

Kitabu: Maisha ya Malcom X

Mkuu samahani......allah ndio nani????
Mungu wa wakoloni wa kiarabu au kizungu????
Waafrika hatumtambui huyo

ٱللَّهُ لَآ إِلَٰهَ إِلَّا هُوَ ٱلْحَىُّ ٱلْقَيُّومُ لَا تَأْخُذُهُۥ سِنَةٌ وَلَا نَوْمٌ لَّهُۥ مَا فِى ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَمَا فِى ٱلْأَرْضِ مَن ذَا ٱلَّذِى يَشْفَعُ عِندَهُۥٓ إِلَّا بِإِذْنِهِۦ يَعْلَمُ مَا بَيْنَ أَيْدِيهِمْ وَمَا خَلْفَهُمْ وَلَا يُحِيطُونَ بِشَىْءٍ مِّنْ عِلْمِهِۦٓ إِلَّا بِمَا شَآءَ وَسِعَ كُرْسِيُّهُ ٱلسَّمَٰوَٰتِ وَٱلْأَرْضَ وَلَا يَـُٔودُهُۥ حِفْظُهُمَا وَهُوَ ٱلْعَلِىُّ ٱلْعَظِيمُ

Allah - there is no deity [worthy of worship] except Him, the Ever-Living, the Sustainer of [all] existence. Neither drowsiness overtakes Him nor sleep. To Him belongs whatever is in the heavens and whatever is on the earth. Who is it that can intercede with Him except by His permission? He knows what is [presently] before them and what will be after them, and they encompass not a thing of His knowledge except for what He wills. His Kursi extends over the heavens and the earth, and their preservation tires Him not. And He is the Most High, the Most Great.

(Qur'an 2:255)
 
Mkuu samahani......allah ndio nani????
Mungu wa wakoloni wa kiarabu au kizungu????
Waafrika hatumtambui huyo

قَالَ فَمَن رَّبُّكُمَا يَٰمُوسَىٰ

Fir'aun (Pharaoh) said: "Who then, O Musa (Moses), is the Lord of you two?"

قَالَ رَبُّنَا ٱلَّذِىٓ أَعْطَىٰ كُلَّ شَىْءٍ خَلْقَهُۥ ثُمَّ هَدَىٰ

[Musa (Moses)] said: "Our Lord is He Who gave to each thing its form and nature, then guided it aright."

(Qur'an 20 : 49-50)
 
Moja kati ya vitabu nilivyovipenda sana.

Nilikisoma cha Kiingereza nikiwa Tambaza Secondary School miaka ya mwanzo ya 1990s.

Kwa muktadha mzuri zaidi, ukitaka kujua maisha ya Malcolm X vizuri, ukimaliza hiki tafuta "Malcolm X : A Life of Reinvention" cha Manning Marable.

View attachment 2926508
Unacho mdau soft copy?
 
Sura ya 14 inaendelea.

Kuna mashushushu weusi waliopandikizwa ndani yetu. Lakini mashushushu hawa wa mzungu walitanguliza weusi wao kwanza. Siwezi kusema wote walikuwa hivyo maana si rahisi kuwatambua wote-lakini baadhi yao baada ya kuungana nasi na kusikia, kuona na kuguswa na ukweli juu ya mtu mweusi, walikiri n kusema kazi waliyotumwa. Baadhi yao waliacha kazi ya mzungu na kuja kufanya kazi kwenye Taifa la Kiislamu. Wengine waliendelea na kazi yao na kufanya upelelezi kwa ajili yetu, wakituambia mipango ya mzungu juu ya Taifa. Hivyo ndivyo tulivyofahamu kuwa baada ya lengo kuu la kutaka kujua yanayoyoendelea kwenye Mahekalu yetu, jambo jingine lililomuhangaisha mzungu lilikuwa ni jinsi ambavyo wafungwa weusi walivyojiunga kwenye Uislamu kwa kasi. Naamini hilo linawahangaisha maafisa wa magereza hata leo hii.

Kwa kawaida watu waliosilimu wakiwa bado wafungwa, walijiweka sawa mapema ili kuendana na viwango vyetu vya maadili. Kama ilivyokuwa kwangu, walipotoka gerezani waliingia hekaluni kama Waislamu kamili waliosajiliwa. Kwa kawaida waliosilimu wakiwa wafungwa walikuwa Waislamu imara kuliko ambao hawajawahi kuonja jela.
Haikuwa rahisi kuingia kwenye taasisi yetu kama ilivyo kwenye makanisa ya Kikristo. Mtu hajiiti mfuasi wa Elijah Muhammad na kisha kuendelea na maisha yake ya dhambi na ukosefu wa maadili. Kitu cha kwanza kabisa Muislamu alitakiwa kufanya ni kubadili maisha yake ili kufikia viwango vyetu vya maadili. Na ili kuendelea kuwa Muislamu alipaswa kuendelea kushika viwango hivyo.

Ni Mahekalu machache sana yaliendesha ibada bila ya Imam kuona ndugu wapya wa Kiislamu wenye vipara vya kung’aa. Walikuwa wameachana milele na zile nywele za kung’aa zilizotiwa dawa. Inanisikitisha sana kuwa kila
uendapo utaona alama hii ya ujinga na kujichukia kwenye vichwa vingi vya watu weusi. Najua kuwa kuna baadhi ya rafiki zangu wasio Waislamu walioweka nywele dawa wataaumia kwa mimi kusema hivi, lakini ukimchunguza vizuri mtu mweusi yeyote ambaye huweka nywele dawa utagundua kuwa ni mjinga. Hata ajifanye ni mtu wa namna gani, lakini nywele zake alizoweka dawa ili zionekane kama za mzungu zinapaza sauti kwa kusema, “Nachukia kuwa mtu mweusi.” Kama mimi tu, atagundua kuwa ataimarika sana kiakili iwapo ataamua kujivunia weusi wake na kutoa ule uchafu na kuwa na nywele za asili ambazo Mungu aliwapa watu weusi.

Hakuna Muislamu aliyeruhusiwa kuvuta sigara, hiyo ilikuwa ni moja ya sheria zetu. Kuna baadhi ya Waislamu walipata wakati mgumu sana katika kuacha kuvuta sigara kuliko baadhi ya watu wanavyopata wakati mgumu kuacha kutumia madawa ya kulevya. Lakini watu weusi, wanaume kwa wanawake waliacha kirahisi tulipowaeleza kuwa mzungu hajali chochote kuhusu afya ya umma, anachojali ni kuiendeleza biashara ya tumbaku na kuendelea kupata mabilioni ya dola kama kodi. “Askari wananunua katoni ya sigara kwa kiasi gani?” aliulizwa mtu aliyependezwa na mafundisho yetu. Ilimsaidia kuona kuwa kwa kila katoni ya sigara aliyonunua, serikali ya mzungu huchukua kama dola mbili ikiwa ni kodi kutoka kwa pesa ya mtu mweusi aliyopata kwa taabu.

Utakuwa umesoma mahali fulani-imezungumzwa sana jinsi ambavyo Taifa la Kiislamu limefanikiwa kutibu waraibu sugu kwa kiwango cha kushangaza. Hata gazeti la New York Times liliandika jinsi ambavyo taasisi za kijamii zilivyowaomba wawakilishi wa Taifa la Kiislamu ushauri juu ya mpango wa kutibu uraibu.

Mpango wa kutibu uraibu wa Waislamu ulianza kwa kutambua kuwa rangi ya mtu na uraibu vinaenda pamoja. Si kwa bahati mbaya kwamba katika eneo lote la magharibi, mrundikano mkubwa wa waraibu unapatikana Harlem.
Kitu cha kwanza kwenye kwenye mpango wa Waislamu ilikuwa ni kazi ngumu na chungu iliyofanywa na Waislamu waliokuwa waraibu hapo zamani. Kwenye maeneo ambako madawa ya kulevya yanatumika, Muislamu aliyekuwa mraibu hapo zamani alienda kuwatafuta na kuwahubiria waraibu aliofahamiana nao hapo zamani. Kisha kwa bidii na uvumilivu, Waislamu hao waliokuwa waraibu hapo zamani waliwapitisha waraibu wale kupitia hatua sita za kutibu uraibu, iliweza kuchukua miezi sita hadi mwaka.

Kwanza mraibu alitakiwa kukiri kuwa ni mraibu. Hatua ya pili alifundishwa kwa nini alitumia madawa ya kulevya. Hatua ya tatu alionyeshwa kuwa kuna njia ya kuachana na uraibu. Nne,mraibu alijengewa kujiheshimu na kujiamini mpaka pale alipotambua kuwa ndani yake ana nguvu ya kuushinda uraibu. Hatua ya tano mraibu kwa hiari yake aliacha madawa na kuvumilia alosto yake. Sita na mwisho, sasa mraibu akiwa amepona anamaliza tiba yake kwa “Kuvua” waraibu wengine anaowafahamu na kusimamia matibabu yao.

Mbinu hii ya hatua sita mara nyingi ililishinda tatizo lililozisumbua taasisi zingine za kijamii zilizojaribu kutibu waraibu-chuki na mashaka kutoka kwa waraibu. Mraibu “anayevuliwa” anaelewa vyema kuwa Muislamu anayemfuata naye muda si mrefu alikuwa mraibu wa kutumia dola kumi na tano hadi thelathini kwa siku kwa ajili ya madawa. Muislamu huyu anaweza kuwa alikuwa rafiki wa mraibu huyo na walitumia madawa pamoja. Mraibu huyo huko nyuma amemuona rafiki yake Muislamu akiwa amelala na kuegemea majengo kwa ulevi au akiruka njiti ya kiberiti kama vile anaruka mbwa. Na Muislamu huyu anapomfuta mraibu huyu anakuwa anatumia lugha zilezile za kiteja.
Kama tu mlevi wa pombe, teja wa madawa ya kulevya hawezi anza kujitibu mpaka atambue na kukubali hali yake. Muislamu alinga’ng’ana kama luba, akimwambia mraibu mwenzake wa zamani kuwa ana tatizo bila kukoma. Iliweza kuchukua miezi kadhaa kwa mraibu kukubaliana na hali yake. Tiba haikuanza mpaka hili litokee.

Hatua iliyofuata ilikuwa ni kwa mraibu kutambua kwa nini anatumia dawa za kulevya. Akiwa anashughulika na mraibu huyu kwenye maeneo ambayo huwezi kuamini kama yapo, mara nyingi Muislamu huyu alivuta mateja kadhaa kuja kumsikiliza, walisikiliza kwa sababu walitambua kuwa Muislamu huyu nadhifu alikuwa kama wao.

Muislamu aliwaeleza kuwa kila mraibu hutumia dawa za kulevya ili kukabiliana na kitu fulani. Aliwaambia kuwa mateja wengi weusi walitumia madawa kwa sababu tu ya hali yao ya kuwa watu weusi ndani ya Marekani ya mzungu. Na kuwa kitendo cha mtu mweusi kutumia madawa kinamsaidia mzungu kudai kuwa mtu mweusi si kitu.
Muislamu huyu aliongea kwa kujiamini na waziwazi, “Daddy unajua kabisa kuwa nafahamu unavyohisi. Je sikuwa hapa pamoja nawe? Nikinuka na kujikuna kama nyani, nikiishi kama mwehu, nikipigwa na njaa, nikiiba na kukimbia na kujificha kutoka kwa mzungu. Kitendo cha mtu mweusi kununua dawa za kulevya kinamtajirisha mzungu huku yeye akijidhuru mwenyewe!

Kuonyeshwa kwamba njia pekee ya yeye kuachana na dawa za kulevya ni kwa kujiunga na Taifa la Kiislamu. Mraibu alipelekwa kwenye mgahawa wa Kiislamu katika eneo hilo-na pengine alipelekwa maeneo mengine ambako kulikuwa na Waislamu wanaojiamini na wanaojiheshimu, watu wanaoheshimiana tofauti na wanaozozana kwenye maeneo ya Maghetto. Kwa mara ya kwanza baada ya miaka mingi, mraibu yule anasikia akiitwa “Ndugu” na “Bwana.” Hakuna anayejali juu ya maisha yake ya nyuma. Uteja wake unaweza tajwa lakini uliongelewa kama tu changamoto ngumu inayomkabili na si kwa kumnyanyapaa. Kila mtu ambaye mraibu huyu alikutana naye alikuwa na imani juu yake kuwa ataushinda. Hayo ni mambo yenye nguvu sana kwa mtu aliyekuwa matopeni. Na ukweli ni kuwa hakuna mtu anayeweza badilisha kabisa maisha yake kama mtu aliyekuwa katika hali mbaya kabisa, anahitaji tu kutiwa moyo. Mimi mwenyewe ni mfano mzuri kuhusu hilo.

Mwishowe, na muhimu zaidi—mraibu aliamua mwenyewe iwapo ataacha kutumia madawa na kuvumilia alosto na madhara yake. Wakati huu ukifika, Waislamu ambao walikuwa mateja huko nyuma, walipeana zamu ya kumhudumia mtu huyu aliyeamua kuachana na Madawa ili awe Muislamu.

Alosto inapomkumba teja huyu na akaanza kupiga kelele, kutukana na kuomba kupewa madawa, “Nipate japo kidogo tu jamaa,” Waislamu wanakuwa naye bega kwa bega wakimtuliza kwa lugha za kiteja, “Baby, knock that monkey ofl your back! . . . “ Teja yule alijinyonganyonga kwa maumivu, machozi yakimtoka machoni na kamasi zikimvuja, jasho likimtoka mwili mzima. Anajaribu kupiga kichwa ukutani na kupigana na wanaomhudumia, anaharisha na kutapika, “Jikaze, utashinda. Nakuona ukiwa mmoja wa fruit of Islam.”

Mara mateso ya alosto yanapoisha, na pingu za madawa ya kulevya kukatwa, Waislamu walimtia moyo mraibu yule aliyepona na kumlisha supu ili kumrudishia afya yake. Kamwe hatawasahau ndugu hawa waliosimama pamoja naye katika nyakati hizo. Kamwe hatasahau kuwa ni Taifa la Kiislamu ndilo lililomuokoa kutoka kuzimu ya madawa ya kulevya. Ilikuwa ni nadra sana kwa ndugu na dada(Ambao walihudumiwa na dada wa Kiislamu) hao kurudia tena matumizi ya madawa ya kulevya. Mtu huyu aliyepona uraibu alisubiri kwa hamu kuwa tayari ili na yeye aingie kwenye msitu wa mateja kuvua na kumsaidia mtu fulani kuchana na uraibu.

Iwapo ingekuwa ni mzungu au ni mtu mweusi “anayekubalika” ndiye amegundua mpango-tiba wa uraibu wa madawa ya kulevya wenye mafanikio kama ule uliofanywa na Waislamu, serikali ingemuwezesha, angesifiwa na habari zake zingeandikwa kila sehemu. Lakini badala yake tulishambuliwa. Kwa nini Waislamu wasiwezeshwe na serikali na majiji kuokoa mamilioni ya dola kwa mwaka? Sifahamu hasara isababishwayo na uhalifu wa mateja katika nchi nzima, lakini inasemwa kuwa ni mabilioni kwa mwaka katika jiji la New York pekee. Kwa makadirio, dola milioni 12 hupotea kila mwaka ndani ya Harlem kwa sababu ya wizi.

Teja hafanyi kazi ili apate pesa ya madawa, na matumizi yake kwa ajili ya madawa ni kama dola kumi hadi hamsini kwa siku. Anapataje kiasi hicho cha pesa? Teja anaiba, anatapeli, anavizia watu wengine kama vile mwewe-kama tu nilivyokuwa. Uwezekano mkubwa anakuwa aliacha shule- kama ilivyokuwa kwangu. Mtu ambaye hafai kujiunga na jeshi, hali yake ya kisaikolojia inamzuia kufaa kufanya kazi hata akipata, kama tu nilivyokuwa.

Mateja wanawake walikuwa wakiiba vitu madukani au walijiuza. Dada wa Kiislamu waliwanasihi vilivyo makahaba weusi ambao walikuwa wakihangaika kuacha dawa za kulevya ili wafae kuwa Waislamu. “Unafanya mzungu azidi kukuona kama pipa la taka-”

Imesemwa sana kuwa sehemu kubwa ya wafuasi wa bwana Muhammad ni wafungwa na mateja wa zamani. Ni kweli kuwa kwenye miaka ya mwanzo waliosilimu wengi walikuwa ni kutoka sehemu ya chini kabisa ya jamii. Siku zote bwana Muhammad alituhimiza, “Nendeni kwa watu weusi walio matopeni.” Alisema mara nyingi hao ndiyo huwa Waislamu safi kabisa.

Lakini polepole watu weusi wengine wakaanza kujiunga nasi. “Wakristo safi tuliowavua” kutoka kwenye makanisa yao. Kisha watu weusi wasomi na wenye taaluma wakaanza kuongezeka. Kila mkutano wa hadhara ulivutia watu weusi wa “Daraja la kati” walioishi katika mji uliofanyika kujiunga na Hekalu la mji huo, watu ambao hapo mwanzo walitudhihaki na kutuita “Waislamu weusi” na “Demagogues” na “Walimu wa chuki” “wabaguzi wa rangi weusi” na majina mengine mengi. Kweli zilizohubiriwa na Waislamu zilivutia vijana wengi, wakike na wakiume. Kwa wale waliokuwa na ujuzi na vipaji, Taifa la Kiislamu lilikuwa na sehemu nyingi za kuwatumia.

Kulikuwa na Waislamu waliosajiliwa ambao kwa sababu ya nafasi zao katika jamii ya mzungu kamwe hawakufunua kuwa ni wanachama isipokuwa kwa Waislamu wenzao tu. Niliwafahamu wachache ambao kutokana na nafasi zao walifahamika kwa maimam wao na kwa bwana Muhammad tu.

***

Kufikia mwaka 1961 Taifa letu lilikuwa limekua sana. Ukurasa mzima wa mwisho katika gazeti letu, Muhammad Speaks, ulikuwa na mchoro wa jengo letu la thamani ya dola milioni 20. Lilikuwa ni jengo la makao makuu lililopangwa kujengwa huko Chicago. Kila Muislamu alikuwa akitoa mchango binafsi kukamilisha ujenzi huo. Ndani ya jengo hilo kulikuwa na msikiti, shule, maktaba, hospitali na jumba la makumbusho ya historia iliyotukuka ya mtu mweusi.

Bwana Muhammad alifanya ziara kwenye nchi za Kiislamu na aliporudi alitoa maelekezo kuwa tuanze kuyaita Mahekalu yetu “misikiti.”

Wakati huo biashara ndogondogo zilizomilikiwa na Waislamu ziliongezeka kwa kasi sana. Biashara zetu zilikuwa ni mifano kwa watu weusi kuwaonyesha yale watu weusi wanayoweza kujifanyia wenyewe-iwapo wangeungana na kufanya biashara kati yao wenyewe kadri inavyowezekana-na kupeana ajira wao kwa wao, na kwa kufanya hivyo kubakisha pesa za watu weusi ndani ya jamii ya watu weusi, kama tu jamii zingine za wachache zinavyofanya.
Pia hotuba zilizorekodiwa za bwana Muhammad zilikuwa zikirushwa kwenye vituo vidogo vya redio kotekote Marekani. Huko Chicago na Detroit, watoto wa Kiislamu waliofikia umri wa kuanza shule walisoma kwenye vyuo vyetu viwili hadi sekondari. Tokea darasa la awali walisoma historia iliyotukuka ya mtu mweusi, na kuanzia darasa la tatu walisoma lugha ya asili ya mtu mweusi, Kiarabu.

Kufikia sasa wakati huo watoto nane wa bwana Muhammad walijishughulisha sana na mambo ya Taifa la Kiislamu. Nilijivunia sana kwa kuwa na mchango katika kuwezesha hilo kwa namna fulani. Miaka ya nyuma kabla bwana Muhammad hajanituma kwenda kuhudumu kama Imam wake, nilianza kuhisi aibu kwa kuona baadhi ya watoto wake wakifanya kazi kwa mzungu, walifanya kazi viwandani, kwenye ujenzi, udereva taksi na nyingine kama hizo. Nilihisi kuwa natakiwa kufanya kazi kwa familia ya bwana Muhammad kwa moyo wote kama nilivyomfanyia kazi yeye. Niliongea na bwana Muhammad aniruhusu nifanye mpango wa kuchangisha pesa kwenye misikiti yetu michache ili kuwezesha kuwaajiri watoto wake kwenye Taifa la Kiislamu. Alikubali na polepole watoto wake wakaanza kufanya kazi ndani ya Taifa la Kiislamu. Leo hii mtoto wake mkubwa, Emmanuel, anaendesha kiwanda cha kufua nguo. Dada Ethel(Muhammad)Sharrieff ni mkufunzi mkuu wa wanawake wa Kiislamu. (Mume wake, Raymond Sharrieff ni Kapteni mkuu wa Fruit of Islam). Dada Lottie Muhammad ni msimamizi wa vyuo viwili vya Kiislamu. Nathaniel Muhammad anamsaidia Emmanuel kuendesha kiwanda cha ufuaji. Herbert Muhammad sasa ndiye mchapishaji wa Muhammad Speaks, gazeti la Taifa la Kiislamu nililoanzisha. Elijah Muhammad, jr., ni Kapteni mkuu msaidizi wa Fruit of Islam. Wallace Muhammad alikuwa ni Imam wa msikiti wa Philadelphia mapaka pale aliposimamishwa pamoja nami kwa sababu ambazo nitazielezea hapo baadaye. Mtoto wake wa mwisho, Akbar Muhammad, ni mwanafunzi kwenye Chuo Kikuu cha Al-Azhar huko Cairo, Misri. Akbar Muhammad pia ametengana na baba yake.

Naamini ni hotuba ndefu ambazo bwana Muhammad alitoa kwenye mihadhara yetu mikubwa ndizo ziliyofanya ugonjwa wake wa pumu uliomsumbua kwa muda mrefu uwe mbaya zaidi. Hata mkiwa mnaongea tu, aliweza kuanza kukohoa ghafla, na kukohoa kuliendelea mpaka alipoishiwa nguvu.

Mara nyingi ilimbidi kuahirisha kuhutubia kwenye mihadhara mikubwa. Maelfu ya watu walinyong’onyea kunisikia mimi au mtu mwingine akihutubia badala yake.

Watu wa Taifa la Kiislamu walihangaishwa sana na hali hiyo. Madaktari walishauri aishi kwenye hali ya hewa ya ukame. Basi taifa la Kiislamu likamnunulia bwana Muhammad nyumba huko Phoenix Arizona. Siku moja nilimtembelea bwana Muhammad kule, niliposhuka tu kwenye ndege nikapokelewa na kamera hadi nikajiuliza mpaka nikajiuliza ni nani walikuwa nyuma yangu. Kisha nikaona bunduki za wapiga picha. Walikuwa ni watu wa usalama tawi la Arizona.

Habari kuwa hali ya hewa ya Arizona ilipunguza sana makali ya ugonjwa wa Muhammad iliwafurahisha sana Waislamu. Kuanzia wakati huo alitumia sehemu kubwa ya mwaka akiwa Phoenix.
Pamoja na kuwa bwana Muhammada hakuweza tena kufanya kazi kwa saa nyingi kama alivyofanya kule Chicago
lakini sasa alikuwa na mzigo mkubwa zaidi wa kufanya maamuzi makubwa na kazi za uongozi. Kila sehemu Taifa la Kiislamu lilikuwa limetanuka, nje na ndani. Bwana Muhammad hakuweza tena kunipangia na kuniamulia ni redio gani au kituo gani cha televisheni nikubali mualiko wao, pamoja na mambo mengine ambayo nilikuwa namletea kwa ajili ya ushauri au maamuzi.

Bwana Muhammad alionyesha imani yake kwangu kwenye maeneo hayo. Aliniambia niwe nafanya maamuzi mwenyewe. Alisema kuwa muongozo wangu uwe juu ya kile nafikiria kuwa ni busara na chenye manufaa kwa Taifa la Kiislamu.

“Ndugu Malcom nataka ufahamike vyema,” aliniambia bwana Muhammad siku moja. “Sababu kama ukijulikana itanifanya nami nijulikane,” aliendelea kusema. “Lakini ndugu Malcom kuna kitu kimoja unatakiwa kufahamu. Utakapojulikana sana utachukiwa. Kawaida watu huwaonea wivu watu maarufu.”

Katika mambo aliyoniambia bwana Muhammad, hakuna jambo lililotimia kinabii kuzidi hilo.

Mwisho wa sura ya 14​
 
SURA YA KUMI NA TANO

ICARUS
Kadri nilivyozidi kumuwakilisha bwana Muhammad kwenye maeneo mengi- televisheni, redioni, vyuoni na maeneo mengine, ndivyo nilivyozidi kupokea barua nyingi zaidi kutoka kwa watu walionisikia. Nadhani asilimia tisini na tano ya barua hizo zilitoka kwa wazungu.

Ni barua chache tu zilizoanza kwa “Mpendwa Nigger X” au kwa kunitishia maisha. Barua hizo zilinijulisha hofu kuu mbili zilizowakabili wazungu. Kwanza ni imani yake kuwa Mungu kwa hasira ataharibu mfumo uliopo. Na hofu yake kuu nyingine ni taswira ya mwanaume mweusi kumuingilia mwanamke wa kizungu.

Ilishangaza kuona wazungu wengi walioniandikia barua walikubaliana na tatizo alilolielezea bwana Muhammad-lakini si suluhu lake. Baadhi ya barua zilimpongeza sana bwana Muhammad isipokuwa jina “Shetani wa kizungu.” Nilijaribu kufafanua hilo kwenye hotuba zilizofuata:

“Isipokuwa pale tunapomwita mzungu fulani ‘Shetani’ lakini tunaposema “Shetani wa kizungu” hatuzungumzii mtu mmoja mmoja, tunazungumzia jumla ya historia yote ya mzungu. Tunazungumzia jumla yote ya ukatili wa mzungu, uovu wake, pupa yake, mambo yaliyomfanya atende kama shetani kwa watu wasio wazungu. Mtu yeyote mwenye akili na aliye salihi hawezi shindwa kuona kuwa biashara ya utumwa iliyofanywa na mzungu na matendo yake ya kishetani ndivyo hasa vimesababisha mtu mweusi awepo Marekani na awe hali aliyonayo leo. Huwezi kumkuta hata mtu mmoja mweusi ambaye kwa namna fulani hajaathiriwa kibinafsi na matendo ya kishetani ya wazungu kwa ujumla wao!”

Karibu kila siku “Waislamu weusi” walishambuliwa kwenye magazeti. Mashambulizi yalianza kulenga hasa mambo niliyosema, “Malcom X ni Demagogue.” Nilikuwa nakasirika sana niliposoma mashambulizi yoyote makali yakielekezwa kwa bwana Muhammad. Sikujali waliyosema juu yangu.

Wataalamu wa sayansi ya jamii na watu wa ustawi wa jamii wale walitaka kunigawanya vipandevipande, hasa weusi, ilishangaza sana lakini walikuwa na sababu zao. Ndiyo, nilijua sababu zilizowafanya wawe hivyo: Mzungu ndiye aliyewalipa. Kulingana na watu hawa, “Kama nilikuwa sichochei migawanyiko katika jamii” basi “nilikuwa nimelielewa vibaya swala la ubaguzi wa rangi.” Na hata pale niliposema hoja iliyo wazi wao walisema, “Malcom X anapindisha ukweli makusudi. . . .”

Wakati fulani, ndugu yangu mmoja kutoka Msikiti Namba Saba-mtu aliyekuwa anashughulika na vijana kwenye kituo fulani cha jamii katika Harlem alinionyesha ripotii moja ya siri. Baadhi ya wafanyakazi weusi wa ustawi wa jamii wenye uzoefu walikuwa wamepewa likizo ya mwezi mmoja ili wawachunguze “Waislamu weusi.” Kila aya niliyosoma ilinirudisha kwenye kamusi. Nafikiri pengine ndiyo maana sijasahau mstari mmoja ulionihusu. Sikiliza hiki: “Utamaduni wa Harlem unaobadilikabadilika umerahisishwa na kupotoshwa na Malcom X ili kufikia malengo yake.”

Sijui kati yangu na wao ni nani aliyefahamu vyema utamaduni wa maeneo ya maghetto ya Harlem? Mimi niliyepambana kwenye mitaa ya Harlem kwa miaka au huyu mtu mweusi wa ustawi wa jamii mwenye kiburi cha elimu?

Lakini hilo si jambo muhimu. Jambo nililoona ni muhimu zaidi ni kuona kati ya watu weusi milioni 22, ni wachache sana waliobahatika kufika chuo-na huyu anayenishutumu ni mmoja ya waliobahatika kufika chuo. kwa maoni yangu huyu alikuwa ni mmoja wa negro ambaye hajawahi elewa lengo kuu na matumizi ya elimu. Elimu mfu ambayo haijawahi kutumika isipokuwa kujionyesha kwa maneno ya kisomi.

Unatambua kuwa hii ndiyo moja ya sababu kuu zinazomfanya mzungu wa Marekani amdhibiti na kuendelea kumkandamiza mtu mweusi wa Marekani? Sababu mpaka hivi karibuni, imekuwa ni nadra sana kwa watu weusi wachache walioelimika kutumia elimu yao. Nalazimika kusema kuwa wazungu wanaitumia elimu yao kufanya tafiti na tafakari za kina, kujiendeleza wao na watu wa jamii yao kwenye hii dunia ya mzungu yenye ushindani na kuabudu mali. Lakini kwa miaka mingi wale watu weusi wanaoitwa “wameelimika” wamewaongoza ndugu zao kwa fikra za mzungu ambazo kiasili ni za kinyonyaji kwa faida ya mzungu.

Mzungu mpe sifa zake-ana akili ya pekee sana. Dunia yake imejaa ushahidi kuonyesha hilo. Huwezi taja kitu ambacho mzungu hawezi unda. Si rahisi ukataja tatizo la kisayansi ambalo hawezi kulitatua. Sasa yupo kutatua tatizo la kutuma watu kwenye anga za mbali na kuwarudisha duniani salama.

Lakini katika uwanja wa kushughulika na binadamu wengine akili yake imeshindwa. Na akili yake inashindwa kabisa iwapo binadamu hao si wazungu. Hisia za mzungu zinaizidi akili yake. Anaweza kuwatendea watu wasio wazungu matendo ya ajabu kabisa kutokana na hisia zake kumwambia kuwa yeye ni bora kuliko watu wote.

Ni wapi bomu la atomiki lilidondoshwa . . . “ili kuokoa maisha ya Wamarekani”? Je mzungu haelewi mambo kiasi kwamba hawezi kufikiri kuwa theluthi mbili ya watu ambao si wazungu hawatasahau hilo?

Kabla ya bomu hilo kudondoshwa ni nini kiliwapata mamia elfu ya Wajapani-raia wazalendo wa Marekani ambao waliswagwa kwenda makambini na kuzuiwa kwa nyaya za seng’eng’e? Lakini ni Wajerumani wangapi ambao ni raia wa Marekani waliswagwa na kufungwa makambini kwa nyaya za seng’eng’e? Sababu walikuwa wazungu!

Kihistoria, uwepo wa watu wasio wazungu umefunua asili ya “Ushetani” aliyonayo mzungu.

Ni kitu gani kingine kama siyo “Shetani” kilichopofusha akili ya mzungu wa Marekani kiasi kwamba inashindwa kuona kimbele kuwa mamilioni watumwa weusi waliochiwa huru, na kisha kupewa elimu hata kidogo tu siku moja watakuwa dubwana la kutisha katikati yao? Akili ya mzungu ambayo leo hii inachunguza anga za mbali ilitakiwa kumwambia bwana-watumwa kwamba mtumwa yeyote, kama akipata elimu hatamuogopa bwana wake. Historia inaonyesha kuwa mtumwa mwenye elimu sikuzote huanza kuuliza maswali, na kinachofuata anaanza kutaka usawa na bwana wake.

Leo hii watu weusi milioni 22 wametambua kwamba, kimwili, kiuchumi, kisiasa na hata kwa kiasi fulani kijamii, kuwa mtu mweusi aliyeamshwa anaweza kumletea mzungu balaa kubwa na hata kuchafua picha ya Marekani kimataifa.

***

Sikuwa na lengo la kutoka nje ya mada, nilikuwa naelezea jinsi ambavyo katika mwaka 1963 nilikuwa najaribu kushughulika na magazeti ya mzungu, redio na wanahabari wa televisheni waliokuwa wamedhamiria kuyafutilia mbali mafundisho ya bwana Muhammad.

Kichwani mwangu ilijengeka picha ya kuwaona waandishi wa habari kama Chororo-kaya(Ferrets) wakinusanusa, wakirukaruka na kuchokonoachokonoa wakitafuta njia ya kunitega-wanibane kwenye mahojiano yetu.

Ikitokea “Kiongozi” wa kupigania haki za kiraia ameongea jambo lililouudhi mfumo wa mzungu unaotawala, waandishi wa habari, ili kumrudisha kwenye mstari walijaribu kunitumia: “Bwana Malcom X, mara nyingi umekuwa haukubaliani na migomo ya kugoma kuondoka na njia nyingine kama hizo ambazo hutumiwa na watu weusi kugoma, una maoni gani juu ya mgomo unaoongozwa na Dr. King huko Montgomery?”

Fikra zangu zilikuwa hivi, japo “Viongozi” wa kudai haki za kiraia walitushambulia Waislamu tena na tena, lakini bado walikuwa ni watu weusi, bado walikuwa ni watu wa jamii yetu, ningekuwa mpumbavu iwapo ningeruhusu mzungu anitumie kuhujumu harakati za kudai haki za kiraia.

Nilipoulizwa kuhusu mgomo wa Montgomery, nilichunguza kwa makini kilichopelekea utokee. Bibi Rosa Parks alikuwa amepanda basi kuelekea nyumbani, baada ya kufika kituo fulani cha basi, dereva wa kizungu alimuamuru bibi Parks amuachie kiti abiria wa kizungu aliyeingia. Nilisema, “Hebu fikiria hilo! Mwanamke huyu mweusi anayefanya kazi kwa bidii, na Mkristo mwema, amelipa nauli na yupo kwenye siti yake. Lakini kwa sababu tu ni mweusi, anaamrishwa asimame! Nyakati nyingine hata mimi mwenyewe napata wakati mgumu kuamini ujikwezaji wa mzungu!”

Au ningesema, “Hakuna anayeelewa vyema kilichopekea tukio lile dogo kufanya watu weusi wa Montgomery walipuke. Kwa karne kadhaa kumekuwa na ukatili wa kutisha dhidi ya watu weusi wa kusini-kuuwawa, kubakwa, kupigwa! Lakini kama unavyojua, matukio makubwa ya kihistoria yameanzishwa na matukio madogo tu. Nyakati fulani, kuna mwanasheria mmoja mhindi alishushwa kwenye treni, alikuwa amechoshwa na ukosefu wa haki hivyo akamshika simba wa Uingereza mkia. Jina lake lilikuwa Mahatma Gandhi!”

Au nilitumia ujanja ambao niliona wanasheria wakitumia, kwenye maisha halisi na kwenye televisheni. Ni namna ambavyo wanasheria waliingiza jambo lisilokubalika mbele ya baraza la wazee.(Wakati mwingine huwa nafikiri kuwa ningeweza kabisa kuwa mwanasheria, kama nilivyomwambia yule mwalimu wa darasa la nane kule Mason, Michigan naye akanishauri niwe seremala.) Basi nilimdondoshea muandishi aliyeniuliza swali jambo fulani asilotaka kusika.

“Naona watu weusi wanagoma kwa sababu kama hizohizo pale wanapoambiwa wajiunge na jeshi. Kwa nini tuende kufa ili kulinda kinachoitwa ‘Demokrasia’ ambayo inampa mhamiaji wa kizungu aliyeishi siku moja tu ndani ya nchi hii haki nyingi kuliko mtu mweusi aliyeishi miaka 400 akiwa mtumwa na mfanyakazi wa nchi hii?”

Wazungu walionelea ni afadhali migomo 50 midogomidogo kuliko watu weusi milioni 22 waanze kutafakari kile nilichosema. Sina haja ya kukwambia kuwa kamwe hawakuchapisha vile nilivyosema. Kama ingetokea wangechapisha, basi walichapa kinyume kabisa. Na niliweza kutambua pale maneno yalipowaingia waandishi wa habari wa kizungu; waliacha kuniuliza baadhi ya maswali.

Nami nilikuwa nawatega. Nilijidai kuteleza na kutaja baadhi ya mafanikio ya karibuni ya harakati za kudai uhuru wa kiraia. Unafahamu vile makampuni makubwa yanaajiri watu weusi kumi wa maonyesho; jinsi ambavyo baadhi ya migahawa imeanza kutengeneza pesa zaidi kwa kuanza kuwahudumia watu weusi; chuo fulani cha kusini kimemuandikisha mtu mweusi chuoni hapo bila matata kutokea, na mambo kama hayo. Nilipochomekea hayo, muendesha kipindi alidakia, “Kabisa bwana Malcom X, huwezi kupinga kuwa hizo ni hatua kwa jamii yako!”

Hapo nilimgeuka. ‘Kila ninakogeuka nasikia hatua zilizopigwa kuelekea kupata haki za kiraia’! Inaonekana wazungu wanafikiri kuwa mtu mweusi anatakiwa kupiga kelele ‘Haleluya’! Kwa miaka mia nne mzungu amemchoma mgongoni mtu mweusi kwa kisu chake cha futi moja. Sasa ameanza kukichomoa polepole, labda kwa inchi sita! Na mtu mweusi ashukuru kwa hilo? Maana hata akikichomoa bado kitaacha kovu!”

Hivyo hivyo, meya wa mji fulani aliweza kusikika “Hakuna tatizo la watu weusi kwenye mji wetu” Habari kama hizo nilijulishwa mara moja kwenye vipindi hivi. Niliwaambia hakukuwa na haja waniambie hilo limetokea wapi, kwa sababu najua vyema kuwa hilo linamaanisha kuwa ni watu weusi wachache sana wanaishi huko. Hilo liko hivyo duniani kote. Chukulia mfano wa wakati watu weusi 100,000 kutoka West Indies walipoingia Uingereza, Uingereza ikaamua kupiga marufuku uhamiaji wa watu weusi. Finland ilimkaribisha balozi wa Marekani ambaye ni mweusi, lakini hebu acha weusi wengine wamfuate huko! Au chukulia Urusi wakati wa utawala wa Khrushchev, alitishia kusitisha visa za wanafunzi weusi pale maandamano yao ya kupinga ubaguzi yalipoiambia dunia kuwa “Urusi nayo. . . .”

***

Vyombo vya habari vya wazungu wa kusini mara nyingi havikuandika na kuripoti habari zangu, lakini viliandika kwenye kurasa za mbele yale niliyosema juu ya wazungu wa kaskazini na wale wanaotoka kaskazini kwenda kusini kupigania uhuru wa mtu mweusi(Abiria wa uhuru). Nilisema hicho ni “kituko,” makazi yao wenyewe ya maghetto huko kaskazini yana panya na mende wa kutosha kiasi kwamba wote wanaosafiri wangeweza kufanya kazi ya kuwaua. Nilisema kuwa New York yenye uliberali mkali ilikuwa na tatizo la ubaguzi kuliko hata Mississippi. Kama Abiria wa Uhuru kutoka kaskazini walitaka kufanya zaidi, wangeenda kwenye kiini cha matatizo ya meneo ya maghetto, kama uwepo wa watoto wadogo mitaani usiku, wakiwa na funguo za nyumbani kwao shingoni iwapo watataka kurudi nyumbani, huku baba na mama zao wakiwa ni walevi, mateja, wezi na makahaba. Abiri hao wa uhuru wangeweza kupiga kelele huko kaskazini-kwenye serikali za majiji, vyama vya wafanyakazi na viwanda vikubwa vitoe kazi zaidi kwa watu weusi na kuwatoa kwenye utegemezi wa misaada ya serikali, kitu ambacho kinawatengenezea uvivu na kuharibu kabisa maeneo ya maghetto na kufanya kuwa maeneo ya hovyo kabisa kuishi binadamu. Niliongea kweli tupu lakini kwa nini niuseme? Nyoka wasingeweza geuka kunishambulia kwa kasi kama walivyofanya waliberali wale.

Nilitoa kilemba walichojivika waliberali, kilemba walichotumia jitihada nyingi kujivika! Kwa muda mrefu waliberali wa kaskazini wamekuwa wakiinyooshea kidole Kusini na kufanikiwa kuonekana wema wakati ndiyo wanafiki wakubwa kabisa duniani.

Naamini maisha yangu mwenyewe yanaakisi unafiki huu. Sijui chochote kuhusu Kusini ya Marekani. Mimi ni zao la mzungu wa Kaskazini na unafiki wake kuelekea mtu mweusi.

Mara zote bwana Muhammad alimzungumzia mzungu wa kusini bila kuuma maneno. Kitu unachoweza kusema kwa mzungu wa kusini ni kuwa hana unafiki. Anamuumia meno mtu mweusi na kumwambia wazi kuwa kamwe wazungu wa kusini hawatakubali ‘Uchangamano’ wa kinafiki. Anaenda mbali hata kumwambia mtu mweusi kuwa hatampa haki zake hata kiduchu, na yuko tayari kupambana naye kwa nguvu zote kuzuia hilo. Faida ya hili ni kuwa mtu mweusi wa kusini anajua wazi ni upinzani gani anaokabiliana nao.

Unaweza kuwazungumzia wazungu wa kusini kuwa, kwa mmojammoja wamekuwa na msaada mkubwa kwa watu weusi wengi. Lakini mzungu wa kaskazini anakenua kwa meno yake lakini kinywa chache kimejaa hila na ulaghai wa “usawa” na “uchangamano.” Siku moja mtu mweusi kotekote Marekani amshike mzungu bega, na baada ya mzungu kugeuka aone ni mtu mweusi anayesema, “Na mimi pia . . .” kwa nini mzungu huyo mliberali wa Kaskazini dhamira imsute na ajawe na hofu kama yule wa kusini?

Na hata mtu mweusi hatari zaidi katika Marekani ni yule yule aliyekuwa amefungiwa kwenye maeneo ya maghetto na wazungu wa kaskazini. Wazungu wa kaskazini wanaendelea kuongea kuhusu demokrasia huku wakimuweka mtu mweusi pembeni-huko mbali nao.

Neno uchangamano lilibuniwa na waliberali wa kaskazini. Neno hilo halina maana yoyote. Nikuulize: neno hilo linatumika sana kuhusiana na ubaguzi wa rangi, lina maana gani kwenye eneo hilo, linaweza kuelezewa likaeleweka? Ukweli ni kuwa “Uchangamano” ni kiini macho. Ni mbinu za hila za waliberali wa kaskazini ambazo lengo lake ni kumchanganya mtu mweusi asijue matakwa ya kweli ya mtu mweusi wa Marekani. Hapa kwenye majimbo hamsini yanayoendeleza ubaguzi wa rangi, na ubaguzi wa rangi mamboleo, neno hili “kuchangamana” limewafanya mamilioni ya wazungu kuchanganyikiwa na kujawa na hasira, wakiamini kuwa umma wa watu weusi unataka kuishi na kujichanganya nao. Hili lipo kwa weusi wachache sana wanaoshupalia “Uchangamano.”

Nazungumzia watu weusi ambao “wamechangamanishwa kama geresha” watu waliokimbia kutoka kwa ndugu zao weusi wanaokandamizwa-watu wanaojichukia na hiyo ndiyo sababu kubwa inawafanya washabikie uchangamano. Watu weusi hawa wachache wanafikira za kizungu na wanachukia watu weusi kuliko wazungu wenyewe.

Unachotaka umma wa watu weusi wa Marekani ni haki za binadamu! Kuheshimiwa kama binadamu. Hilo ndilo tatizo halisi. Watu weusi hawataki kutendewa kama vile wamejaa ukoma. Hawataki kufungiwa kwenye maeneo ya mabanda na maghetto kama vile ni wanyama. Wanataka kuishi kwenye jamii huru, sehemu wanayoweza kutembea vifua mbele kama watu.

Ni wazungu wachache wanaotambua kuwa siku hizi watu weusi wanakwepa na hawapendi kutumia muda mwingi pamoja na wazungu. Habari hii ya “kuchangamana” kwa namna inavyosemwa inawafanya mamilioni ya wazungu waamini kuwa watu weusi wanataka kulala pamoja nao kitandani, kitu ambacho si kweli. Huwezi mwambia mwanaume wa kizungu kuwa tamaa kuu ya mwanaume mweusi si kulala na mwanamke wa kizungu-uongo mwingine wanaoamini! Kama ambavyo ndugu mmoja alivyoniambia hivi karibuni, “Umewahi sikia harufu yao wakiwa wamelowa?”

Umma wa watu weusi unapendelea kujumuika na watu wao wenyewe. Hata hawa watu weusi wenye kujidai-wanaporudi nyumbani kutoka kwenye karamu za “Kuchangamana” wanachofanya ni kurusha kule viatu na kuongea kuhusu waliberali wa kizungu waliotoka kuagana nao kama vile waliberali hao ni mbwa. Na pengine waliberali wa kizungu wakifika makwao hufanya kitu hicho hicho, sina hakika. Sijawahi kuwa pamoja nao kwa faragha-lakini watu mabwanyenye weusi wanafahamu vyema kuwa siongopi.

Naongea mambo kama yalivyo. Kamwe usiwe na wasiwasi kuwa nitauma maneno iwapo kuna kitu nakifahamu ni kweli kipo akilini mwangu. Kuambiana ukweli wa wazi usio na unafiki kati ya mzungu na mtu mweusi ndicho kitu kinachohitajika sana katika nchi hii-ili kusafisha anga dhidi ya viini macho na ulanghai ambao umekuwepo kwenye anga la nchi hii kwa miaka mia nne.

Kwenye jamii nyingi za wazungu, hasa jamii zenye watu wachache, wazungu wamejitengenezea picha ya kuwa wao ni wakarimu sana kwa watu weusi. Kila mara anapoibuka mtu mweusi na kuanza kuwaambia wazungu ukweli-kwamba watu weusi wamechoka kuwa kama takataka na kufanywa raia daraja la pili, ndipo utakaposikia kwa masikitiko ikisemwa, ‘Bahati mbaya kwa sababu ya huyu wazungu wetu wakarimu wanaanza kutugeukia . . . tulikuwa tumepiga hatua lakini sasa mawasiliano kati ya jamii zetu mbili yamevunjika!’

Wanaongea kitu gani? Hakujawahi kuwa na mawasiliano. Kabla ya vita ya pili ya dunia, hakukuwa na sehemu hata moja ndani ya Marekani yote ambayo mzungu alisikia kutoka kwa “viongozi” wa watu weusi wa eneo hilo ukweli halisi wa jinsi watu weusi wanavyohisi kutokana na wanavyotendewa na jamii ya kizungu.

Unataka ushahidi? Kama si hivyo, basi ni kwa nini watu weusi walipoanza kuasi nchini kote karibu jamii nzima ya wazungu wa Marekani ilishangazwa na kupata mshtuko? Nisingependa kabisa kuwa jenerali wa jeshi ambaye hana taarifa kama ambavyo mzungu wa Marekani hakuwa na taarifa kuhusu mtu mweusi wa nchi hii.

Hii ndiyo hali iliyopelekea ghadhabu ya mtu mweusi kujijenga polepole hadi kufikia hatua ya kuasi bila ya mzungu kufahamu chochote. Marekani kote, ili “viongozi” wa watu weusi waendelee kuwa viongozi kwenye sehemu zao, iliwabidi kumhakikishia mzungu kuwa “Kila kitu kinaenda sawa bosi!” Na “kiongozi” huyo alipotaka kitu fulani kwa ajili ya watu wake: “Er, bosi kuna baadhi ya watu wanaongea kuwa tunahitaji shule bora bosi.” Na kama “kiongozi” huyo hajawahi kuleta matata yoyote, mzungu “mkarimu” anaweza kukubali na kuwapa shule au kazi.

Wazungu ambao wapo kwenye mamlaka nchini kote wanafahamu kuwa naongea ukweli! Wanajua ninaelezea kile ambacho kimekuwa kikitokea kwenye “Mawasiliano” kati ya “wazungu wakarimu”na watu weusi wa kwenye maeneo yao. Ni utaratibu ulioanzishwa na wazungu wakandamizaji na waliojaa majivuno. Ni mfumo uliowekwa ili kumfanya mzungu ajione bora na mwema pale anapomtupia mtu mweusi makombo badala ya dhamira kumsuta juu ya mfumo katili wa kijamii unaomnyonya mtu mweusi.

Lakini nataka nikuambie kitu. Utaratibu huu, “Mfumo” huu ambao mzungu ameuunda, yaani wa kuwafundisha watu weusi kumficha ukweli kwa kukenua na kusema, “Ndiyo bosi” huku wakichezesha miguu na kukuna kichwa-ni mfumo ambao umemletea madhara mzungu wa Marekani kuliko ambayo yangeweza kumpata iwapo angevamiwa na jeshi.

Kwa nini nasema hivyo? Kwa sababu yote hayo yamemsaidia mzungu wa Marekani kujenga kichwani mwake saikolojia ya kuwa yeye ni “mkuu na bora.” Ni kwenye maeneo mangapi wazungu ambao hawajamaliza hata shule ya sekondari huwachukulia kwa dharau “viongozi”, wakuu wa shule, walimu, madaktari na wanataaluma wengine weusi?

Mfumo huu wa mzungu umetumika kwa watu wasio wazungu duniani kote. Hii ndiyo sababu kila mahali wanakoishi watu wasio wazungu duniani hapa, serikali za kizungu zinajikuta kwenye matatizo na hali mbaya kila uchao.

Acha tuone ukweli. Haijalishi kama mzungu anaweza kukabiliana na ukweli au la, ukweli juu ya sababu hasa za matatizo anayokabiliana nayo-matatizo yanayoamua iwapo ataokoka au la.

Leo tunashuhudia mapinduzi ya watu wasio wazungu, watu ambao miaka michache tu iliyopita wangetetemeka kwa hofu iwapo mataifa ya kizungu yangeinua tu kope za macho. Kilichopo ni kuwa watu weusi, wa kahawia, wekundu na wa njano-baada ya mamia ya miaka ya kunyonywa na kudunishwa na kuteswa, mwishowe wamefikia hatua ya kufa au kupona, wamechoshwa na kisigino cha mzungu shingoni mwao.

Serikali ya marekani inawezaje kutangaza “demokrasia” na”Undugu” kwa watu wasio wazungu iwapo kila siku wanasikia na kusoma yanayoendelea hapa Marekani, na wakiona picha zinazoongea zaidi ya maneno elfu, picha za mzungu akiwanyima “demokrasia” na “undugu” hata wakazi wa asili wa Marekani?

Dunia ya wasio wazungu inajua jinsi mtu mweusi wa Marekani alivyompenda mzungu na kumtumikia, na kumtunza. Mtu mweusi huyu amevaa sare za jeshi na kwenda kufa pale taifa hili lilipovamiwa na maadui wa kizungu na wasio wa kizungu. Yaani mtu asiye mzungu muaminifu namna hii na bado Marekani inampiga mabomu, na kumshambulia kwa mbwa, na kwa maji yenye presha, na kumfunga wa maelfu, na kumpiga vibaya na kumfanyia kila aina ya uhalifu.

Ni wazi kuwa mambo haya, yakiwa yanafahamika na kukumbushwa kila siku kwa watu wasio wazungu, ni moja ya sababu kuu ya haya matendo ya kuchoma gari la balozi, kupiga mawe na kuharibu majengo ya balozi na kelele za “Mzungu rudi kwenu!” mashambulizi dhidi ya wamishionari wa Kikristo, na kupigwa mabomu na kuchanwa kwa bendera.

Inaeleweka wazi kwa nini nimesema kuwa kujiona bora kwa mzungu wa Marekani kumemletea madhara makubwa kuliko ya kuvamiwa na jeshi?

***​
 
Kama CRIPS BLOODLINE FROM BLACK PANTHER MOVEMENT.......HUYU MALCOM (PRO ARABS) NA LUTHER
( PRO EUROPEANS) WALIKUA SNITCH,Z OVER BLACK RACE KUANZIA KITAMADUNI NA KIIMANI MPAKA KISIASA....THAT'S WHY BIG HOMIEZ TAKE BOTH OUT...!!!!!
ELIJAH MUHAMMAD NA LOUIS WALIAMUA KUKAA PEMBENI NA KUOMBA CEASE FIRE
LONG LIVE CRIP,S.....BLOODLINE.....IN 60,S.......!!!!
WITHIN CRIP,S MALCOM X DESERVE TO BE SMOKED.......HE SELL OUT OUR RACE....!!!
Wewe jamaa haujui kitu ni mweupe kichwani , watu weusi wanamchukia Malcom X kama shujaa wao mpaka Leo bado anaheshimika na watu weusi Marekani na ulimwenguni kwa ujumla acha mbali wazungu wenyewe na watu wengine.

Bahati nzuri clips video na audio zake zipo hivyo sio rahisi kudanganya watu Malcom X alikuwa nani na nini alichokuwa anapambania .
 
Moja kati ya vitabu nilivyovipenda sana.

Nilikisoma cha Kiingereza nikiwa Tambaza Secondary School miaka ya mwanzo ya 1990s.

Kwa muktadha mzuri zaidi, ukitaka kujua maisha ya Malcolm X vizuri, ukimaliza hiki tafuta "Malcolm X : A Life of Reinvention" cha Manning Marable.

View attachment 2926508
Ngoja nikipitie na hiki maana Mimi nimesoma Malcolm X Autobiography Cha Alex Haley na "Dead are arising" kingine ambacho nina hamu nikisome ni chini pichani ila sijabahatika kupata soft copy yake.
61V7tMtHcmL._AC_UF1000,1000_QL80_.jpg
 
SURA YA 15 INAENDELEA​

Mtu mweusi wa Marekani anatakiwa kuelekeza jitihada zake zote katika kujenga biashara zake mwenyewe, na nyumba bora kwa ajili yake. Kama ambavyo watu wa jamii zingine walivyofanya, acha watu weusi, kila inapowezekana wanunue kutoka biashara za weusi wenzao na kuajiri weusi wenzao. Na njia hizo ziwe mwanzo wa watu weusi kujifanyia mambo yao wenyewe. Hiyo ndiyo njia pekee ambayo mtu mweusi anaweza kujipati heshima. Kitu pekee ambacho mzungu hawezi kamwe kumpatia mtu mweusi ni kujiheshimu. Mtu mweusi hawezi kuwa huru na kutambulika kama binadamu ambaye yuko sawa na binadamu wengine mpaka pale atakapokuwa kama walivyo, na mpaka pale atakapoweza kujifanyia mwenyewe mambo ambayo wengine wanajifanyia wenyewe.
Mtu mweusi wa maeneo ya maghetto anatakiwa kuanza kwa kujirekebisha upotofu na uovu wake wa kimaadili, kiroho na kimwili. Mtu mweusi anatakiwa kuanzisha mpango wake mwenyewe wa kutokomeza ulevi, uraibu wa dawa za kulevya na ukahaba. Mtu mweusi wa Marekani anatakiwa kupandisha hadhi yake mwenyewe.

Ni watu weusi elfu chache sana, wachache mno ukilinganisha na watu weusi wote ndiyo wanajihusisha na “uchangamano” Ni mabwanyenye wachache weusi ndiyo wanakimbilia kupeleka pesa chache walizonazo kwenye hoteli za kifahari za wazungu, kwenye club zake za dansi na migahawa yake ya kifahari. Wazungu wanaotembelea maeneo hayo wanaweza kuzimudu gharama zake. Lakini hawa weusi unaowaona sehemu hizo hawawezi kuzimudu, ni hakika kuwa wengi wao hawazimudu. Kwa nini mtu mweusi mwenye maisha ya kuungaunga anaonekana mjini-kati akila kwenye migahawa ya gharama, akiwakenulia meno wahudumu ambao wana pesa kumzidi? Watu weusi hao ambao wanaoweka mapajani vitambaa vikubwa kama vitambaa vya mezani wakati wa kula, na kuagiza kware na konokono, kwa nini! Kwanza watu weusi hawapendi konokono. Wanafanya hivyo kuonyesha kuwa wamechangamana.

Kama unataka kuchunguza matokeo hasa ya uchangamano, utafikia kwenye ndoa za watu wa rangi tofauti. Nakubaliana na wazungu wa kusini wanaoamini kuwa huwezi kuwa na “Uchangamano”—huwezi kuwa nao kwa muda mrefu bila ya ndoa za watu wa rangi tofauti kuanza kuongezeka. Na hilo linafaida gani kwa watu? Tuongee ukweli, kwenye dunia kama hii ambayo kuna chuki kutokana na rangi, mwanaume na mwanamke gani, mzungu au​
mweusi-anayetaka kuwa na mwenza wa rangi tofauti?

Iko wazi kuwa wazungu wameshaonyesha chuki yao kwa watu weusi walio katika familia na mitaa yao. Na kwa jinsi watu weusi wanavyohisi siku hizi, wenza wa rangi tofauti watakuta kuwa familia na jamii za watu weusi zinachukia ndoa ya watu wa rangi tofauti kuliko hata wazungu. Basi ndoa za “Kuchangamana” zitakuwa na hatima gani zaidi ya kuchukiwa, kutotakiwa na kutokubalika na jamii zote? Hitimisho tunalofikia ni kuwa, kijamii, “Kuchangamana” hakuna faida kwa pande zote mbili . . . mwisho wake utaharibu watu wote, weusi na weupe.

Tayari kitendo cha mwanaume wa kizungu “Kuchangamana” na mwanamke mweusi kimewabadili watu weusi wa Marekani. Watu “weusi” ambao ni “weupe” kuliko wazungu wengi wanatuonyesha jambo gani? Nimeambiwa kuwa leo hii katika Marekani kuna watu weusi milioni mbili hadi tano ambao wanaishi kati ya wazungu kama nao ni wazungu. Fikiria maisha yao ya hofu, kwamba siku moja mtu mweusi wanayemfahamu atawaumbua. Piga picha kuishi kwa ulaghai kila siku. Piga picha wakiwasikia wake au waume zao wazungu, au hata watoto wao wa kizungu wakiongea kuhusu watu weusi.

Sidhani kama ndani ya Marekani kuna mtu amewasikia watu weusi wenye machungu na wazungu kama baadhi ya niliowasikia mimi. Lakini nikwambie ukweli, watu weusi wenye chuki zaidi na wazungu kuwahi kuwaisikia ni wale walioishi kama wazungu; kati ya wazungu; watu ambao kila siku wanasikia yale ambayo wazungu wanasema kuhusu watu weusi-vitu ambavyo mweusi halisi hangeweza kusikia kamwe. Kama kungekuwa na vita vya rangi, watu hawa weusi wanaoishi kama wazungu wangekuwa mashushushu na washirika wazuri sana wa watu weusi.
Machotara wa huko Ulaya ambao sasa wamekuwa vijana wa kuoa na kuolewa na kuwa na familia zao . . . wamepitia maisha yao yote wakionekana kama viumbe vya ajabu, je wanatuonyesha kuna jambo lolote jema linaloweza tokana na “uchangamano”?
Hata “Uchangamano”unaohusisha jamii za wazungu tu nao unapingwa vikali na wale wanaotaka “Kutochafua” jamii yao na kulinda tamaduni zao. Angalia jinsi Wa-Irish walivyowafurumusha Waingereza kutoka Ireland. Wa-Irish walijua kuwa Waingereza watawameza. Angalia jinsi Wafaransa wa Canada wanavyopambana kulinda utamaduni wao.
Ukweli ni kuwa madhara mabaya kabisa ya uchangamano, na matokeo yake ya kuharibu utambulisho wa kijamii yamewapata wazungu-Myahudi wa Ujerumani.

Myahudi wa Ujerumani ana mchango mkubwa kwa Ujerumani kuliko Wajerumani wenyewe. Wayahudi wameshinda zaidi ya nusu ya tuzo za Nobel zilizotolewa kwa Ujerumani; amechapisha magazeti makubwa kabisa. Wayahudi ndiyo walikuwa wasanii wakubwa, washairi wakubwa na katika karibu kila Nyanja ya sanaa. Lakini wayahudi hao walifanya kosa kubwa sana, walichangamana.

Kutoka vita ya kwanza ya dunia hadi umaarufu wa Hitler, Wayahudi wa Ujerumani waliongeza za kuoa na kuolewa nje ya jamii yao. Wengi walibadili majina na dini yao. Dini yao wenyewe ya Kiyahudi na utajiri wa kitamaduni waliokuwa nao walivitupilia mbali . . . hadi wakaanza kujiona nao ni Wajerumani. Ghafla Hitler huyu hapa, kutoka kwenye vilabu vya pombe hadi madarakani-akiwa amebeba dhana yake ya “Ukuu wa jamii ya Aryan.” Na mbuzi wa kafara waliokuwa karibu walikuwa ni Wayahudi wa Ujerumani waliokuwa wamejitia udhaifu na kujidanganya kuwa nao ni Wajerumani.

Jambo la kushangaza ni kuwa ilikuwaje kwa Wayahudi wale na akili zao zote, na nguvu walizokuwa nazo kwenye kila nyanja ndani ya Ujerumani, kwa nini Wayahudi hao walipigwa na butwaa, wakishangaa kitu ambacho hakijatokea
tu ndani ya siku moja bali kilichokua polepole-mpango mkubwa wa kuwaua!

Walijichota sana akili kiasi kwamba hata baadhi yao walipokuwa wakiuawa kwenye vyumba vya gesi ya sumu bado walikuwa wakisema, “Haiwezekani kutendewa hivi!”

Wazo la Hitler kutawala dunia kama alivyodhamiria linawafanya Wayahudi walio hai leo watetemeke kwa hofu.
Kamwe Wayahudi hawatasahau somo hilo. Macho ya mashushushu wa Kiyahudi yanakitazama kila kikundi cha Unazi mamboleo. Mara tu baada ya vita ya pili ya dunia, baraza la wadhamini la Wayahudi likachochea majadiliano na Uingereza yaliyoanza muda mrefu. Lakini sasa genge la Stern lilikuwa likipambana kwa bunduki na Waingereza, Waingereza wakafyata na kukubali kuwasaidia kuipora Palestina kutoka kwa Waarabu, wamiliki wake halali. Kisha Wayahudi wakaanzisha taifa la Israeli, nchi yao wenyewe- kitu pekee ambacho kila jamii ya watu duniani inakielewa na kukiheshimu.

***

Muda si mrefu uliopita, mtu mweusi wa Marekani alilishwa dozi nyingine ya inayodhoofisha na kulaza na kuchota akili ya kile kinachoitwa “uchangamano” Ni kile ninachoita “Kituko kilichotokea Washington,” Nakiita kituko.

Wazo la umati wa watu weusi kuandamana huko Washington lilikuwa ni wazo la ndugu A. Philip Randolph. Kwa kama miaka ishirini wazo la kuandamana kwenda Washington limekuwepo kwa watu weusi. Lakini ghafla wazo hilo limepata nguvu sasa. Watu weusi kutoka kwenye maeneo ya mashambani ya kusini, watu weusi waishio maeneo ya maghetto ya kaskazini, na hata maelfu ya vibaraka wa zamani walianza kuongea kuhusu “Maandamano.”

Toka Joe Louis hakuna kitu kiliwaunganisha watu weusi kama hiki. Watu weusi walikuwa wanaongea kuhusu kwenda Washington kwa njia yoyote ile, kwa mabasi, kwa magari yaliyokongoroka, kwa kuomba lifti na hata kwa kutembea kama wakilazimika. Waliwazia kuona maelfu ya watu weusi wakimiminika Washington- na kulala na kufunga mitaa, viwanja vya ndege na kwenye viunga vya majengo ya serikali, wakidai bunge na ikulu ya Marekani kuwapatia haki za kiraia.

Hiki kilikuwa ni kisicho na utaratibu wala kiongozi. Wengi wao walikuwa ni vijana weusi, wajeuri na wasiojali chochote, wakiwa wamechoshwa na mzungu kumuwekea mtu mweusi mguu wa shingo.

Mzungu alikuwa na kila sababu ya kuwa na wasiwasi. Cheche kidogo tu ingeweza kusababisha uasi wa watu weusi. Serikali ilifahamu kuwa maelfu ya watu weusi wenye hasira si tu wanaweza kukwamisha shughuli za serikali katika jiji la Washington, bali pia wanaweza kulipuka na kuwa vurugu.

Mara moja ikulu ikawaalika “Viongozi” wakubwa wa harakati za kupigania haki za kiraia za mtu mweusi. Waliambiwa wasimamishe maandamano yaliyopangwa. Walisema ukweli kuwa hawakuyapanga na wala hawana udhibiti juu yake, wazo la kuyaanzisha lilikuwa limezuka ghafla tu, hakukuwa na utaratibu wala kiongozi. Kwa maneno mengine yalikuwa ni pipa la unga wa risasi.

Mtu yeyote analiyetaka kujifunza jinsi ambavyo “Uchangamano” unavyoweza kudhoofisha harakari za mtu mweusi alikuwa karibu kushuhudia somo kubwa sana.

Ikulu, kwa shangwe na matangazo duniani kote, “iliyaruhusu” na “kuyakaribisha” maandamano kwenda Washington. Vikundi vikubwa vya kupigania haki za kiraia wakati huo vilikuwa vikigombania michango hadharani. Gazeti la The New York Times limefichua. N.A.A.C.P. Imedai kuwa vikundi vingine vimepata sehemu kubwa ya michango iliyotokana na maandamano ya kupigania haki za kiraia sababu ya kutangazwa sana huku N.A.A.C.P. wakibaki na mzigo mkubwa wa kugharamia huduma za kisheria kwa waandamanaji wa vikundi vingine.

Ilikuwa kama filamu. Onesho lililofuata ilikuwa ni kwa “viongozi” wakubwa sita wa harakati za kupigania haki za kiraia za mtu mweusi kukutana jijini New York, huko walionana na mzungu ambaye ni kiongozi wa taasisi kubwa ya misaada. Waliambiwa kupigania kwao pesa hadharani kunaharibu taswira yao. Taasisi hiyo ilichangia dola 800,000 kwenda kwenye baraza la viongozi wa harakati za kupigania haki za kiraia, baraza lililoundwa haraka haraka na viongozi hao sita.

Sasa ni nini kilichofanya umoja wa watu weusi upatikane kwa kasi namna hiyo? Pesa za mzungu. Masharti gani yaliambatana na pesa hizo? Mbali na mchango huu, kiasi kama hicho hicho kiliahidiwa kutolewa baadaye baada ya maandamano . . . hakuna shaka kingetolewa iwapo tu maandamano yangeenda vyema.

Maandamano ya hasira yaliyopangwa yalianza kubadilika kabisa.

Kotekote duniani wale wakuu sita walitangazwa kama viongozi wa maandamano ya kwenda Washington. Habari hizo ziliwaongezea hasira wale watu weusi wa chini na kuchochea zaidi mipango ya maandamano. Pengine walidhani kuwa sasa “viongozi”wale maarufu waliwaunga mkono na kujumuika nao.

Kilichofuata ilikuwa ni kualikwa kwa wazungu wanne maarufu kwenye maandamano: mmoja myahudi, mmoja Mkatoliki, mmoja Mprotestanti na mmoja bosi wa chama cha wafanyakazi.

Sasa matangazo yakaanza kugusia kuwa “Wakuu hao kumi” wataongoza na kuratibu maandamano ya Washington. Wazungu wale wanne wakaanza kuonekana na kuhimiza maandamano. Taarifa zikasambaa kwa kasi kuwafikia wale wanaoitwa “waliberali” wa Kiyahudi, Kikatoliki, Kiprotestanti na wafanyakazi: wakaanza kuona kuwa ni jambo la ”Kidemokrasia” kujiunga kwenye maandamano haya ya watu weusi. Basi ghafla tu wazungu ambao walikuwa wanahofia maandamano wakaanza kutangaza kuwa​
watashiriki.

Watu weusi wa “daraja la kati” walikuwa kama wamepigwa na shoti ya umeme. Watu ambao mwanzoni walipinga vikali mipango ya maandamano ya kwenda Washington iliyokuwa inapangwa na watu weusi wa hali ya chini-lakini sasa baada wazungu nao kujiunga na maandamano hayo, watu weusi hao wenye kuhusudu “uchangamano,” walikanyaganawakijaribu kupata sehemu ya kusaini kwa ajili ya maandamano. Maandamano ya “hasira” ya watu weusi yakawa ghafla yamegeuka fasheni. Ghafla yakawa kama mechi kubwa zinavyokuwa. Kwa wale wanaotaka kujikweza, maandamano yakawa sehemu ya kujipatia sifa. “Ulikuwepo kwenye maandamano?” Hata leo unaweza kusikia wakiulizana. Yakabadilika na kuwa “mtoko.”​

Asubuhi ya maandamano yale, magari kuukuu yaliyojaa watu weusi kutoka miji midogo, watu waliojaa hasira, wakiwa wamejaa vumbi na jasho yalimezwa na ndege za kukodi, mabehewa yenye hadhi na mabasi yenye viyoyozi. Kitu ambacho mwanzo kilipangwa kuwa kama mkondo mkali wa bahari, kikawa, kama ambavyo gazeti moja lilisema, “mafuriko ya kistaarabu.” Kila kitu “kilichangamana” kama chumvi na pilipili. Sasa kulikuwa hakuna kitu ambacho hakijaratibiwa.

Waandamanaji waliambiwa wasije na mabango, walipewa mabango. Waliambiwa kuimba wimbo mmoja tu: “We Shall Overcome.(Tutayashinda.)” Waliambiwa jinsi ya kuwasili, wakati na mahali kwa kufikia, mahali pa kukusanyika, mahali pa kuanzia maandamano, njia ya kupita wakati wa maandamano. Vituo vya huduma ya kwanza viliwekwa kwa sehemu maalumu-watu walielekezwa hata mahali pa kuzimia!

Ndiyo, nami nilikuwepo. Niliona maigizo yale. Nani amewahi kusikia wanamapinduzi wenye hasira wakiimba kwa pamoja “We Shall Overcome . . .Suum Day . . .(Tutayashinda siku moja)” Huku wakiwa wameshikana mikono na kuirusha huku na kule pamoja na watu ambao walitakiwa kuwa wakiasi dhidi yao kwa hasira? Nani amewahi kusikia wanamapinduzi wenye hasira wakirusha miguu iliyo peku ndani ya vidimbwi pamoja na wakandamizaji wao, huku magitaa yakipigwa, nyimbo za dini zikiimbwa na hotuba za “I Have, A Dream(Nina Ndoto)”?

Watu weusi wa Marekani hata leo bado wanakumbwa na jinamizi badala ya ndoto. “Wanamapinduzi hawa wenye hasira” walifuata hata maeekezo ya mwisho yaliyowataka kuondoka mapema. Kati yamaelfu elfu ya “wanamapinduzi wenye hasira,” ni wachache walilala Washington kiasi kwamba asubuhi iliyofuata chama cha hoteli za Washington kilitoa taarifa kuwa walipata hasara kwa sababu ya vyumba kuwa tupu. Hata filamu za Hollywood zisingeweza kufikia kiwango kile.

Kwenye tafiti zilizofanywa na magazeti, hakuna hata mbunge mmoja ambaye alikuwa akipinga haki za kiraia aliyesema kuwa amebadili maoni yake sababu ya maandamano. Kuna mtu alitegemea tofauti? Inawezekanaje kwa mtoko wa “kuchangamana” wa siku moja kupambana na wawakilishi hawa wa ubaguzi, ubaguzi uliojikita kwenye akili ya mzungu wa Marekani kwa miaka mia nne?

Kitendo cha mamilioni ya watu weusi na wazungu kuamini kituko kile kikubwa, ni mfano mmojawapo unaoonyesha jinsi nchi hii inavyochukulia mambo kijuujuu tu, badala ya kushughulika hasa na kiini cha matatizo.

Yalichofanya maandamano yale ya Washington ilikuwa ni kuwapumbaza tu watu weusi kwa muda. Lakini polepole watu weusi walianza kuona kuwa waliingizwa mjini na mzungu. Na hasira yake ikawaka tena. Ikiwa kali kuliko wakati wowote ule, na ikaanza kulipuka kwenye majiji mbalimbali-kwenye vurugu kubwa za kupinga ubaguzi wa rangi za kipindi cha kiangazi cha mwaka 1964.

***

Mwezi mmoja kabla ya “Kituko cha Washington,” gazeti la The New Yok Times liliniandika, kulingana na utafiti waliofanya kwenye vyuo, mimi nilikuwa mhutubiaji wa pili niliyetafutwa sana na vyuo. Mhutubiaji pekee aliyekuwa mbele yangu alikuwa ni Barry Goldwater, mbunge.

Naamini kilichonifanya niwe maarufu kiasi kile vyuoni kilikuwa ni kitabu cha Dr. Lincoln, The Black Muslims in America. Kilikuwa kimefanywa kuwa cha lazima kusoma kwenye kozi kadhaa za chuo. Kisha baadaye nilifanya mahojiano marefu na ya kina na jarida la Playboy, jarida linaloongoza kusomwa vyuoni kuliko yote. wanafunzi wengi baada ya kusoma kitabu cha Dr. Lincoln na baadaye kusoma mahojiano yangu kwenye jarida la Playboy, wakawa na hamu ya kumsikia “Muislamu huyu mweusi mwenye hasira.”

Utafiti wa gazeti la The New York Times ulipochapishwa, nilikuwa nimehutubia kwenye zaidi ya vyuo hamsini, nilikuwa nimeishahutubia kwenye vyuo kama Brown, Yale, Harvard, Columbia na Rutgers, vyuo vyenye kuheshimika na pia vingine vingi nchini. Sasa nina mualiko wa kwenda kuhutubia vyuo vikuu vya Princeton na Cornell, na pengine vingine kadhaa mara tu tutakapoweka ratiba zetu sawa. Katika vyuo vya watu weusi, nimehutubia chuo kikuu cha Atlanta na chuo cha Clark vya jijini Atlanta, Chuo Kikuu cha Howard cha jijini Washington, D.C., na vingine kadhaa vyenye wanafunzi wachache.

Umati wa pili niliopenda kuhutubia baada ya ule wa watu weusi, ulikuwa ni wanafunzi wa vyuo. Wakati mwingine mihadhara ya chuo ilienda kwa saa mbili hadi nne, mara nyingi ilienda zaidi ya muda uliopangwa. Mara nyingi nilishambuliwa kwa waswali, hoja na shutuma kutoka kwa wanafunzi wa shahada, shahada za juu na wahadhiri wao, wengi wao walikuwa na kiu ya maarifa. Siku zote mihadhara ya chuo ilikuwa imechangamka sana. Mara zote ilinisaidia kuzidi kujielimisha. Kila mhadhara wa chuo ulinipa njia fulani ya kuboresha namna ya kutetea na kufundisha mafundisho ya bwana Muhammad. Wakati mwingine kwenye mijadala hiyo nilijikuta peke yangu nikikabiliana na wanafunzi sita au nane pamoja na wahadhiri wao kutoka idara za sosholojia, saikolojia, falsafa, historia na dini, kila mmoja akinishambulia kwenye eneo lake alilobobea.

Mara nyingi mwanzoni kabisa mwa mijadala hiyo nilianza kwa kusema, ‘Mabwana, mimi ni mhitimu wa darasa la nane huko Mason, Michigan. Elimu yangu ya sekondari niliipata kwenye maeneo ya maghetto ya watu weusi huko Roxbury, Massachusetts. Chuo changu kilikuwa ni mitaa ya Harlem, na shahada yangu ya uzamili niliipata gerezani.
Bwana Muhammad amenifundisha kwamba sihitaji kuogopa elimu ya mtu yeyote anayejaribu kutetea na historia ya uhalifu wa mzungu dhidi ya watu wasio wazungu, hasa ule waliotenda wazungu dhidi ya watu weusi hapa Amerika ya Kaskazini.’

Ilikuwa ni kama kuwa vitani na silaha ni risasi za akili na falsafa. Ilichangamsha sana kupambana kwa hoja. Nilianza kuwa na uwezo wa kuona hisia za wasikilizaji. Nimezungumza na wahutubiaji wengine, wanasema kuwa uwezo huu ni kipawa walichonacho watu wanaokubalika na umma, watu wanaoweza kufikia mioyo ya watu na kuwabadilisha. Ni kama ambavyo daktari anavyoweza kuhisi mapigo ya moyo kwa vidole vyake, nilipokuwa jukwaani naongea niliweza kuhisi muitikio wa wasikilizaji.

Nafikiri ninaweza kuhutubia nikiwa nimefungwa macho na baada ya dakika tano nikawa na uwezo wa kukwambia iwapo umati uliopo mbele yangu ni wa watu weusi tupu au watu weupe tupu. Wasikilizaji weupe na weusi walikuwa
tofauti sana. Wasikilizaji weusi walikuwa moto, niliweza kuhisi hayo hata pale walipokuwa kimya.

Eneo lingine ambalo ningeweza kukuambia rangi ya muuliza swali hata kama nimefungwa macho ilikuwa ni kipindi cha maswali na majibu. Rahisi zaidi kuwagundua walikuwa ni Wayahudi na watu weusi “waliochangamana.”
Kilichonijulisha kuwa muulizaji ni Myahudi, ni sababu katika jamii zote za watu, maswali yake ni ya kimkakati zaidi. Na Myahudi ni mtu wa “kujishtukia” sana, hauwezi hata kusema “Myahudi” bila ya kukushutumu kuwa ni mchukia Wayahudi. Sijali iwapo Myahudi ni mwanataaluma, daktari, mfanyabiashara, mama wa nyumbani, mwanafunzi au vyovyote vile- kitu cha kwanza anachofikiria ni Uyahudi wake.

Ndiyo, naelewa kwa nini Myahudi anajishtukia sana. Kwa miaka elfu mbili, ubaguzi wa kidini na wa kibinafsi kuelekea Myahudi umefanyika kwa nguvu zote kama tu ubaguzi wa wazungu dhidi ya wale wasio wazungu. Lakini nafahamu kuwa Wayahudi milioni tano na nusu wa Marekani(Milioni mbili wakiwa New York) kwa kujua au kutojua wanafaidika kwa ujinga na chuki zote zinazoelekezwa kwa mtu mweusi, kitendo hicho kinamuokoa Myahudi dhidi ya chuki ambazo zingeelekezwa kwake.

Mfano mmoja wa juu ya ninachozungumza ni huu- Wayahudi ndiyo wamiliki wa biashara kubwa kwenye kila maeneo ya maghetto ya watu weusi. Kila siku usiku wamiliki wa biashara hizo hurudi makwao na pesa hizo kutoka kwenye jamii ya watu weusi, na hilo linazidi kufanya maeneo ya maghetto kuendelea kubaki maskini. Lakini sidhani kama nimewahi sema ukweli huu kwenye umati bila ya kushambuliwa vikali na kuambiwa kuwa nachukia Wayahudi. Kwa nini? Nadhani nimewaambia watu zaidi ya mia tano walionishutumu hivyo kuwa Wayahudi, wakiwa kama kikundi hawawezi kukubali jamii nyingine ya wachache kunyonya utajiri wa jamii yao bila kufanya kitu. Niliwaambia kuwa kuongea kwangu ukweli hakunifanyi kuwa mchukia Wayahudi; kunamaanisha tu kuwa napinga unyonyaji.
Waliberali wa kizungu watashangaa kusikia kuwa kutoka kwa wasikilizaji weusi tupu sijawahi kupata hata swali moja lililomtetea mzungu. Hili halikutokea hata pale ambapo wale watu weusi wenye “Kujiweza” na waliohusudu “Uchangamano” walipokuwepo. Watu weusi wote walikubaliana na historia ya uhalifu ya mzungu. Pengine hawakujua suala hilo kiundani kama mimi, lakini walilielewa vya kutosha.

Lakini ngoja nikwambie jambo moja la muhimu. Watu weusi hawa wenye kujiweza, ambao kati ya weusi wenzao hawakuthubutu kujiabisha kwa kujaribu kumtetea mzungu- watazame hao hao kwenye umati ulio na mchanganyiko wa wazungu na watu weusi, akiwa anajua kuwa anasikika na ”Bwana Charlie.” Utawasikia wakinishambulia huku wakijaribu kutetea na kusamehe uhalifu wa mzungu. Watu weusi hawa ndiyo hunifanya nikaribie kuvunja moja ya kanuni zangu kuu, nayo ni kamwe kutozidiwa na hisia na kuwaka hasira. Wakati mwingine nilihisi kutaka kushuka jukwaani na kupigana na mmoja wa vibaraka wale wa mzungu, vibaraka waliochotwa akili, vibaraka na kasuku! Kwenye mijadala ya chuo nilikuwa na njia ya kuwanyamazisha “Bila shaka wewe ni mwanafunzi wa sheria, siyo?” Itawapasa kujibu ndiyo au hapana. Kisha niliendelea kwa kusema, “Nilidhani ni mwanafunzi wa sheria. Unamtetea mzungu huyu mhalifu kwa nguvu kuliko yeye mwenyewe anavyojitetea! Sitasahau mtu mweusi mmoja kutoka chuo fulani, “aliyechangamanishwa”, mwenye PhD na profesa; alinikasirisha kiasi kwamba sikuwa naona vizuri. Kwa jinsi ambavyo watu weusi milioni 22 walionyimwa elimu walivyo na uhitaji wa msaada kutoka kwa wachache walioipata—yeye alikaa pale kati ya wahadhiri wenzake wa kizungu, akiwa kama nzi kwenye maziwa—akijaribu kunitafuna. Alikuwa akiropoka jinsi nilivyo “Demagogue” na kuwa “Nawarudishia wazungu ubaguzi wa rangi.” Kichwa kiliniwaka kwa kutaka kummaliza mpumbavu yule; mwishowe niliinua mkono na aliacha kuongea. “Unafahamu wabaguzi wa rangi wa kizungu wanawaitaje watu weusi wenye PhD?” Alijibu kitu kama, “Naamini sijapata nafasi ya kufahamu hilo”-Unawajua wale watu weusi wanaojidai kuongea kwa ufasaha. Nilimshushia jina wanalomwita, kwa sauti: “Nigger!”

***

Kuongea kwenye vyuo hivi kulikuwa ni jambo zuri kwa Taifa la Kiislamu, nilimwambia bwana Muhammad kuwa sababu ni kuwa akili ya kishetani ya mzungu ilijengwa na kuamuliwa na vyuo. Lakini kwa sababu fulani, ambazo nilikuja kuzielewa hapo baadaye, bwana Muhammad hakutaka niende kuhutubia kwenye vyuo hivi.

Baadaye nilikuja kufahamu kutoka kwa watoto wake mwenyewe kuwa bwana Muhammad alihisi wivu sababu alihisi hana uwezo wa kuhutubia vyuoni. Lakini wakati huo, nikiwa kama muwakilishi wa bwana Muhammad, niliona umati huu wa watu wenye akili ni watu waliotayari kupokea mambo mapya, na kupokea ukweli mchungu niliowaambia bila ya kutanguliza hisia.

‘Tena na tena, watu weusi, wa kahawia, wa njano na wekundu wameshuhudia na wamekuwa wahanga wa uwezo mdogo wa mzungu kuelewa mambo rahisi ya kiroho. Inaonekana mzungu ni kiziwi kabisa juu ya taratibu za kibinadamu. Kila siku magazeti yake yanatuonyesha kwenye kurasa za mbele dunia aliyotengeneza.
‘Hukumu ya hasira kutoka kwa Mungu iko karibu kumshukia mzungu huyu anayetembea kama kipofu katika giza la kiroho, uovu na ushetani.

‘Tazama—leo ni mataifa makubwa mawili tu ya wazungu ndiyo yamebakia, Marekani na Urusi, kila moja likiwa na washirika wasioaminika. Marekani inayainua mataifa mengine ya kizungu ili yasianguke. Wafaransa, Wabelgiji, Wahispania, Wadachi, Wajerumani na mataifa mengine ya kizungu yamedhoofika kutokana na mataifa yasiyo ya wazungu ya Asia na Afrika yanavyozidi kurudisha nchi zao mikononi mwao.

‘Marekani inaigharamia kwa sehemu Uingereza ili iendelee kubaki na sehemu ya ukuu iliokuwa nao. Jua limetua milele kwenye milki ya Uingereza ambayo jua halikutua kamwe. Jua limetua milele kwa mkoloni mwenye miwani- akinywa chai na mwanamke wake kwenye makoloni ya watu wasio wazungu aliyokuwa akipora kila mali yaliyokuwa nayo. Sasa familia ya kifalme ya Uingereza inaishi kwa kutegemea pesa za utalii wa kutembelea majumba ya kifalme, na kwa kuuza, manukato, vitabu na hata kwa kujiuza wao wenyewe.

‘Dunia yote inafahamu kuwa mzungu hawezi kupona vita nyingine. Iwapo mojawapo ya mataifa mawili makubwa ya wazungu likabonyeza swichi, zama za mzungu zitatoweka!

‘Na tumeona kwa mara nyingine kuwa kitu kinachowaunganisha binadamu si itikadi, bali bali rangi na jamii. Je, ni bahati mbaya kuwa kadri ambavyo wakomunisti wa China wanavyoingia kwenye nchi za Afrika na Asia, ndivyo Marekani na Urusi zinavyozidi kuwa karibu?

“Historia ya mzungu imewafanya watu wasio wazungu wasiwe na jinsi nyingine zaidi ya kuungana pamoja. Na kama kawaida yake, shetani wa kizungu amekosa maadili ya kuweza kushinda kujikweza kwake. Leo hii anataka ‘kununua marafiki kutoka kwa watu wasio wazungu. Anajaribu kuficha historia yake ya nyuma. Hana dhamira ya kujisuta wala uwezo wa kujishusha utakaomfanya akubali makosa na kujaribu kuomba msamaha kwa dhambi zake. Mzungu ameuharibu ujumbe wa upendo ambao Nabii Yesu aliuhubiri na kuuishi alipokuwa duniani.”

Wasikilizaji huonekana kushangaa pale ninapomuongelea Yesu. Niliwaambia kuwa sisi Waislamu tunaamini juu ya Nabii Yesu. Alikuwa ni moja ya Manabii watatu muhimu kabisa katika Uislamu, wengine wakiwa ni Musa na Muhammad. Jerusalem kuna madhabahu za Waislamu zilizojengwa kwa ajili ya Yesu.

Niliwaeleza kuwa ni imani yetu kuwa Ukristo hautendi yale ambayo Yesu alifundisha. Sijawahi kuacha kuwakumbusha kuwa hata Bill Graham alipobanwa kwa hoja huko Afrika, alikiri kuwa, “Naamini katika Kristo na si Ukristo.”

Sitamsahau msichana mmoja mdogo wa kizungu aliyekuwa akisomea ualimu. Nilikuwa nimehutubia kwenye kwenye chuo chao huko New England. Atakuwa alipanda ndege iliyokuwa nyuma ya niliyopanda kwenda New York. Alifika kwenye mgahawa wa Waislamu huko Harlem, wakati huo nilikuwepo mgahawani hapo. Nguo zake, mwenendo na lafudhi yake vilionyesha kuwa ni mwenyeji wa kusini, kutoka familia tajiri. Chuoni kwao nilikuwa nimezungumza jinsi wamiliki wa watumwa wa Kusini ya Marekani walivyowatendea kwa hila hata wanawake wao. Alimuaminisha mwanamke wake kwamba alikuwa ni “mtukufu” sana kuweza kutimiza tama zake za kinyama. Alimlaghai mke wake na kumfanya atazame pembeni matendo yake ya kutembea na mwanamke mweusi. Basi bibi huyo “mtakatifu” alikaa tu na kuendelea kuona vitoto chotara shambani pale vilivyozaliwa na baba yake, mume wake, kaka yake na wana wake. Kwenye chuo hicho nilisema wazi kuwa sababu moja inayowafanya wazungu wasutwe na dhamira ni kujua kuwa kwa kumchukia Mnegro, walikuwa wakiichukia na kuikataa damu yao wenyewe.

Sijawahi kuona mtu aliyeguswa na maneno yangu kama msichana huyu wa kizungu. Aliniuliza bila ya kuuma maneno, “Hauamini kama kuna wazungu ambao ni watu wema?” Sikutaka kuumiza hisia zake. Nilimwambia, “Naamini katika matendo ya watu na si maneno yao.”

“Natakiwa kufanya nini?” Aliniuliza. “Hakuna unachoweza kufanya,” nilimjibu. Aliangua kilio na kukimbilia barabara ya Lenox kuchukua taxi.

***

Kila mara nilipoenda kumtembelea bwana Muhammad huko Chicago au Phoenix, alinichochea kwa maneno yake ya kuonyesha kuwa ananikubali na ana imani nami.

Aliniacha kusimamia masuala yote ya Taifa la Kiislamu alipoenda mji mtakatifu wa Mecca kwenye Hija ya Umrah.
Nilimuamini sana bwana Muhammad kiasi kwamba nilikuwa tayari kujiweka kati yake na muuaji. Tukio moja lililotokea kwa bahati tu, lilinifunulia kuwa kuna kitu kimoja ambacho ni kikuu kuliko jinsi ninavyomhusudu bwana Muhammad.

Nilikuwa nimekaribishwa kuhutubia kwenye kongamano la Shule ya Sheria ya chuo kikuu cha Harvard. Nilipotupa jicho dirishani, nikajikuta naangalia upande ambao yalikuwako maficho yetu nilipokuwa jambazi.

Kumbukumbu zilinisukishasukisha kama mawimbi. Taswira za maisha yangu ya uovu zilipita kichwani mwangu. Maisha niliyoishi na kufikiri kama mnyama.

Nilitambua jinsi ambavyo dini ya Kiislamu ilishuka hadi matopeni ili kuniinua. Kuniokoa kutoka kwenye mwisho usioepukika: mhalifu aliyekufa na kuzikwa, au pengine mfungwa wa miaka thelathini na saba kwenye gereza fulani, au kwenye hospitali ya vichaa. Au pengine kwa namna nzuri ningekuwa Detroit Red mzee, nikipambana na kuiba kwa ajili ya chakula na madawa, na mimi nikiviziwa na wapambanaji vijana, makatili na wanaotaka kujikweza-kama ambavyo alivyokuwa Detroit Red.

Lakini Allah alikuwa amenibariki na kuniwezesha kujifunza Uislamu, na huo umeniwezesha kujiinua kutoka kwenye uchafu na matope ya dunia hii iliyooza. Sasa nimesimama pale nikiwa nimealikwa kuhutubia chuo cha Harvard.
Hekaya moja niliyosoma gerezani nilipokuwa nasoma hekaya za Kigiriki ilinijia kichwani.

Unaikumbuka hekaya ya mvulana aliyeitwa Icarus? Baba yake Icarus alitengeneza mbawa alizoziunganisha kwa nta. “Usiruke juu sana kwa mbawa hizi,’ baba yake alimuonya Icarus. Lakini baada ya kuruka huku na kule, Icarus alijikubali sana kiasi kwamba alihisi anaruka kwa uwezo wake mwenyewe. Aliruka juu-juu sana hata joto la jua likaanza kuyeyusha nta iliyounganisha mbawa. Icarus akaanza kuporomoka.

Nikiwa nimesimama pale kwenye dirisha, niliapa kwa Allah kuwa kamwe sitasahau kuwa mbawa nilizonazo zimewekwa na Dini ya Kiislamu. Sijawahi sahau hilo . . . hata kwa sekunde moja.

Mwisho wa sura ya 15​
 
Mzigo umejitosheleza,,, napenda ukipost mzigo unakidhi haja ya msomaji

Tupo pamoja
 
Sura ya 16.
KUTOKA
Mnamo mwaka elfu moja mia tisa sitini na moja, afya ya bwana Muhammad ikawa imekuwa mbaya ghafla.
Alipokuwa akiongea na watu tuliomtembelea alikuwa akipatwa na kikohozi cha ghafla, kikohozi kilikuwa kikali hadi aliishiwa nguvu, na hapo ilimlazimu kwenda kulala. Ilikuwa huzuni sana kumuona katika hali ile.

Sisi maafisa wa Muhammad na watu wa familia yake tulifanya suala hilo siri kadri tulivyoweza. Waislamu wachache wakawa wamejua hali ya bwana Muhammad ilivyo. Kuna wakati ilimbidi kuahirisha kuhutubia mikutano yetu mikubwa. Waislamu walifahamu kuwa ni jambo kubwa tu ndilo linaloweza kumzuia Mtume kutimiza ahadi yake ya kuwa pamoja nao kwenye mihadhara. Ililazimu kujibu maswali yao, hapo habari za ugonjwa wa kiongozi wetu zikasambaa kwa kasi ndani ya Taifa la Kiislamu.

Mtu yeyote ambaye si Muislamu hawezi kuelewa kifo cha bwana Muhammad kingekuwa na matokeo gani kwa wafuasi wake. Kwetu sisi bwana Muhammad ndiye alikuwa Taifa la Kiislamu. Kilichofanya tuwe kikundi bora kabisa cha watu weusi kuwahi kutokea katika Marekani ni ujitoaji wa kikamili kwa bwana Muhammad uliofanywa na kila Muislamu kama kiongozi wetu wa kiroho na kimaadili.

Kwa maneno mengine, Waislamu tulijichukulia kama mfano wa kimaadili, kiroho na kiakili kwa watu weusi wengine wa Marekani kwa sababu tulifuata mfano uliowekwa na bwana Muhammad. Watu weusi waliongea kwa heshima jinsi ambavyo Waislamu walitengwa iwapo walidanganya, walicheza kamari, kutapeli au kuvuta sigara. Kwa makosa ya kimaadili kama uasherati, bwana Muhammad mwenyewe alitoa hukumu ya kutengwa kuanzia mwaka mmoja hadi miaka mitano, au hata kufukuzwa kabisa kutoka Taifa la Kiislamu. Bwana Muhammad aliwaadhibu maofisa wake kwa haraka zaidi kuliko waumini wapya. Alisema kuwa ofisa yeyote aliyetenda dhambi alikuwa amejisaliti mwenyewe na kama kiongozi na mfano kwa Waislamu wengine.

Kwa kila Muislamu, kukataa kwake dhambi kuliongozwa na bwana Muhammad. Waslamu tulijiona wamoja kwa sababu yake, na kuwa bila yeye tungekuwa gizani.

Kama nilivyosema, madaktari walikuwa wamependekeza hali ya hewa kavu kwa ajili ya afya ya bwana Muhammad. Mara moja tulipata nyumba inayouzwa huko Phoenix, ilikuwa nyumba ya Louis Jordan, mpiga saxophone mmoja. Hazina ya Taifa la Kiislamu ilinunua nyumba hiyo na bwana Muhammad akahamia.

Nilifanya kazi kwa bidii sana kutumikia Taifa la Kiislamu. Nilisaidia kulikuza nchini kote kiasi kwamba hakuna mtu ambaye angetushutumu kuwa ni waongo iwapo tungesema kuwa bwana Muhammad ndiye mtu mweusi mwenye nguvu zaidi katika Marekani. Nilimsaidia bwana Muhammad na maimam wake wengine kuleta mapinduzi katika mawazo ya mtu mweusi wa Marekani. Kumfungua macho mpaka pale alipoacha kumuangalia mzungu kwa macho yaliyojaa hofu na kusujudu. Nilishiriki kusambaza ukweli uliosaidia sana kumfanya mtu mweusi wa Marekani aondoe kiini macho kilichomwambia kuwa jamii ya wazungu ni jamii inayoundwa na “watu bora.” Nimekuwa sehemu ya kitu kilichogusa roho iliyojificha ya mtu mweusi.

Kama sikuridhika kwa namna yoyote basi ni vile nilihisi moyoni mwangu kuwa Taifa la Kiislamu lingekuwa na nguvu zaidi kwenye harakati za mtu mweusi ndani ya Marekani iwapo tungekuwa watu wa vitendo zaidi. Kusema hivyo namaanisha tungelegeza kidogo sera yetu ya kutopambana. Nilihisi kwamba popote pale watu weusi walipokuwatayari kufanya harakati, iwe ni Little Rocks, Birminghams au maeneo mengine, Waislamu wenye nidhamu ya kijeshi walitakiwa nao kuwepo ili dunia nzima iwaone, na kuwaheshimu na kuwajadili.

Ilianza kusikika kwenye maeneo ya watu weusi: “Waislamu wale wanaongea tu lakini hawafanyi chochote labda mtu amchokoze Muislamu mwenzao.” Nilikutana na watu wasio Waislamu mara nyingi kuliko afisa mwingine yeyote wa Taifa la Kiislamu. Kwa jinsi ambavyo msimamo wa watu weusi ulivyokuwa wa kubadilikabadilika, niliona jinsi ambavyo kuitwa “Wanaongea tu” kungetuathiri, na siku moja kusababisha tutengwe toka mstari wa mbele wa mapambano ya mtu mweusi.

Zaidi ya jambo hilo moja, sikuwa na ombi kwa Allah kubariki jitihada zangu zaidi ya alivyokuwa amefanya. Uislamu katika New York ulikuwa unakua kwa kasi kuliko sehemu nyingine yoyote ya Marekani. Kutoka msikiti mmoja mdogo ambao bwana Muhammad alinituma kuuhudumia, sasa nilikuwa nimejenga misikiti mitatu yenye nguvu na imara zaidi ndani ya Taifa la Kiislamu. Msikiti Namba Saba – A wa Harlem, Manhattan; Namba Saba B wa Corona, Queens na Msikiti Namba Saba C wa Brooklyn. Na kitaifa nilikuwa nimeanzisha au nimesaidia kuanzisha misikiti mingi kati ya misikiti mia moja na kidogo iliyokuwepo kwenye majimbo yote hamsini. Nilikuwa nasafiri kukatiza Marekani yote, wakati mwingine hata mara nne kwa wiki. Mara nyingi muda mchache niliolala ilikuwa ni kwenye ndege. Nilikuwa nakimbizana na ratiba za magazeti, redio, vituo vya televisheni na kuhutubia hadhara. Kitu pekee kilichoniwezesha kufanya kazi ya bwana Muhammad ni mbawa alizonipa.

***

Tokea mwaka 1961, wakati ambao hali ya bwana Muhammad ilipoanza kuwa mbaya, nilikuwa nimeanza kusikia maneno hasi kunihusu. Nilisikia maneno ya mafumbo. Nilianza kuona ishara ndogo ndogo za wivu na husda, kama ambavyo bwana Muhammad alivyokuwa amenitabiria. Kwa mfano, ilikuwa inasemwa kuwa, “Imam Malcom anataka
kujitwalia Taifa la Kiislamu,” ilisemwa kuwa nadai mafundisho ya bwana Muhammad ni yangu. Ilisemwa kuwa najaribu kuunda miliki yangu mwenyewe. Ilisemwa kuwa napenda kujikweza nchini kote.”

Lakini sikupata hasira kusikia mambo haya. Yalinisaidia kuimarisha msimamo wangu na kudhamiria kuwa kamwe uzushi huo hautakuja kutokea kwangu. Siku zote nilikumbuka kuwa bwana Muhammad alitabiri kutokea kwa wivu na husda hizo. Na hilo lilinisaidia kupuuzia uzushi huo maana nilijua atakapousikia atajua nini kinachoendelea.

Uzushi uliosemwa mara nyingi na wale wasio Waislamu ulikuwa ni “Malcom X anatengeneza pesa nyingi sana.” Lakini Waislamu wote walielewa kuwa haikuwa hivyo. Eti ninatengeneza pesa za kutosha? F.B.I, C.I.A na I.R.S, wote hawakuweza kuonyesha mali zangu zaidi ya gari nililotembelea na nyumba ya vyumba saba niliyoishi. (Kwa sasa Taifa la Kiislamu kwa tamaa linataka kuchukua hata hiyo nyumba). Ni kweli kuwa nilikuwa naweza kupata pesa muda wowote. Bwana Muhammad alikuwa tayari kuidhinisha nipate kiasi chochote nilichohitaji. Lakini alifahamu vyema, kama ambavyo maafisa wote wa Taifa la Kiislamu walivyofahamu kuwa kila senti niliyoomba ilikuwa ni kwa ajili ya maslahi ya Taifa la Kiislamu.

Mtazamo wangu juu ya pesa ndiyo kitu pekee kilichosababisha mgogoro kati yangu na mke wangu mpendwa Betty. Kadri ambavyo idadi ya watoto wetu ilivyozidi kuongezeka ndivyo Betty alivyozidi kugusia kuwa natakiwa kutenga kiasi fulani kwa ajili ya familia. Lakini nilikataa na hilo likapelekea tuwe na mzozo. Nilisimamia msimamo wangu, nilijua Betty ni mke ambaye alikuwa tayari kujitolea maisha yake kwa ajili yangu iwapo itabidi, lakini bado nilikataa na kumwambia kuwa taasisi nyingi zimekufa sababu ya viongozi wake kutaka kujinufaisha wao binafsi, na mara nyingi wakishawishiwa kufanya hivyo na wake zao. Ilikuwa karibu tuachane sababu ya mzozo huu. Mwishowe niliweza kumhakikishia Betty kuwa iwapo jambo lolote litanipata, Taifa la Kiislamu litamhudumia yeye maisha yake yote, na watoto wetu hata watakapokuwa watu wazima. Nisingeweza kuwa mjinga wa kujidanganya zaidi ya pale!

Kwenye kila kipindi cha redio na televisheni nilichohudhuria, kwenye kila mahojiano niliyofanya na magazeti, niliweka wazi kuwa nilikuwa ni muwakilishi wa bwana Muhammad. Kila mtu aliyewahi kunisikia nikiongea wakati huo atakuwa amewahi kunisikia nikisema, “Mtukufu Elijah Muhammad anafundisha-” nilikataa kuongea na yeyote ambaye alidhihaki jinsi nilivyomrejelea bwana Muhammad mara nyingi. Mtu aliposema au kuandika, “Malcom X, Muislamu mweusi namba mbili-” Niliwaka, nilikuwa nawapigia simu waandishi wa habari na watangazaji wa redio na television kuwa wasitumie tena maneno hayo, niliwaambia, “Waislamu wote mbali na bwana Muhammad ni namba mbili.”
Mkoba wangu ulikuwa umejaa picha za bwana Muhammad. Niliwapatia wapiga picha waliokuwa wakinipiga picha. Niliwapigia simu wahariri wa magazeti na kuwaambia, “Tafadhali tumia picha ya bwana Muhammad badala ya picha yangu.” Nilifurahi sana Muhammad alipokubali kufanya mahojiano na waandishi wa habari wa kizungu. Ni mara chache sana niliongea na waandishi wa habari, weusi na wa kizungu bila ya kuwahimiza waende kumtembelea bwana Muhammad nyumbani kwake huko Chicago-” Nendeni mkapate ukweli kutoka kwa Mtume mwenyewe”-na baadhi yao walienda kuonana naye na kufanya mahojiano naye.

Watu wote, wazungu na weusi walifanya nijihisi vibaya kwa kunipa sifa nyingi juu ya maendeleo ya kasi ya Taifa la Kiislamu. “Sifa zote zimuendee Allah,” niliwaambia wote. “Jambo lolote zuri nililofanya ni sababu ya bwana Muhammad.”

Naamini kuwa hakuna mtu ndani ya Taifa la Kiislamu ambaye angeweza kupata umaarufu kimataifa kama niliopata kutokana na mbawa nilizopewa na bwana Muhammad na kupewa uhuru wa kufanya mambo kama alionipa na bado akaendelea kuwa mhudumu muaminifu kwake kama nilivyokuwa.

Nadhani ilikuwa ni mwaka 1962 ndipo nilipoanza kuona kuwa habari zangu zilianza kuandikwa kwa uchache sana kwenye gazeti la Muhammad Speaks. Nilikuja kufahamu kuwa, Herbert, mtoto wa bwana Muhammad ambaye ndiye alikuwa mchapishaji wa gazeti, alikuwa ametoa maelekezo kwamba habari zangu zichapishwe kwa uchache kadri iwezekanavyo. Ukweli ni kuwa ndani ya gazeti letu kulikuwa na habari nyingi kuhusu “viongozi” wa watu weusi waliounga mkono uchangamano kuliko mimi. Nilisoma habari zangu kwa wingi kwenye magazeti ya Ulaya na Africa kuliko kwenye gazeti letu.

Binafsi sipambanii umaarufu. Tayari nimekuwa maarufu kuliko watu wengi duniani. Lakini nilichukia kitendo cha gazeti la Kiislamu kuwanyima Waislamu habari juu ya mambo muhimu yaliyoendelea sababu tu mambo hayo yalifanywa na mimi. Nilikuwa nikiandaa mihadhara ya kutangaza mafundisho ya bwana Muhammad, lakini sababu ya wivu na ufinyu wa akili nikakosa kabisa kuandikwa kwenye gazeti-maana baadaye ilitoka amri ya kutoniandika kabisa kwenye gazeti letu. Kwa mfano, nilikuwa nimeongea na wanafunzi elfu nane kutoka chuo kikuu cha California, magazeti ya kule yaliandika kwa kirefu juu ya niliyosema kuhusu nguvu na kazi ya bwana Muhammad. Lakini nilipofika Chicago, nikitegemea habari ile kuwa imeandikwa, nilikutana na ukimya tu. kitu hichohicho kilitokea nilipofanya mhadhara wa watu elfu saba katika Harlem. Wakati huo makao makuu huko Chicago hata yakaanza kunishauri kutofanya mihadhara mikubwa. Lakini juma lililofuata nilifanya mhadhara mwingine uliokuwa mkubwa na wenye mafanikio kuliko ule wa kwanza. Hili lilizidi kuchochea wivu na husda kutoka makao makuu huko Chicago.
Lakini nilijitahidi kadri niwezavyo kutotilia maanani mambo haya. Sitaki kuonekana mwema au muungwana sana. Ninaongea tu ukweli. Nililipenda Taifa la Kiislamu na bwana Muhammad. Niliishi kwa ajili ya Taifa la Kiislamu na bwana Muhammad.

Maafisa wengine wa Taifa la Kiislamu waliingiwa na wivu kuona picha yangu kwenye magazeti kila siku. Hawakukumbuka kuwa picha yangu ipo pale sababu ya jitihada zangu za kumtangaza na kumuwakilisha bwana Muhammad. Hawakuwaza kuwa kwa jinsi Taifa la Kiislamu lilivyokuwa likishambuliwa kwa uzushi na uongo, basi lilihitaji msemaji wake awe akipambana na uzushi huo kila siku. Akili ya kawaida tu ingemwambia kila afisa kuwa bwana Muhammad hangeweza kutembea kila sehemu ya nchi akiongelea mambo yahusuyo Taifa la Kiislamu na yeye mwenyewe. Na kuwa yeyote atakayemteua kama msemaji wake hawezi kuepuka kuandikwa na kusemwa sana na vyombo vya habari.

Kila mara nilipohisi kuudhika sababu ya mambo hayo, nilijisikia aibu na fedheha, niliona kama ni ishara ya udhaifu. Walau nilifahamu kuwa bwana Muhammad alifahamu vyema kuwa nimetoa maisha yangu kwa ajili ya kumuwakilisha.

Lakini ilipofika mwaka 1963, sikuweza kujizuia kuhangaisha na shutuma zozote kutoka uongozi wa juu wa Taifa la Kiislamu. Niliacha kuchagua baadhi ya ndugu kutoka New York na kuwapa pesa kwa ajili ya kwenda kuanzisha misikiti kwenye miji mingine, sababu kuna msemo uliibuka “Maimam wa Malcom.” Wakati huo, wakati ambao ilikuwa ni muhimu sana kwa sauti za kiharakati za watu weusi kuufikia umma wa Marekani, jarida la life likawa limetaka kuandika habari kunihusu, nilikataa. Nilikataa pia pale gazeti la Newsweek lilipotaka kuandika kuhusu maisha yangu. Nilikataa pia nilipoalikwa kuwa mgeni kwenye kipindi maarufu na kilichoheshimika cha televisheni kilichoitwa “Meet the Press” Kila nilipokataa ilikuwa ni hasara kwa mtu mweusi na kwa taifa la Kiislamu. Na kukataa kote huko kulitokana na muelekeo wa makao makuu huko Chicago. Kulikuwa na wivu sababu nilikuwa ninaombwa kuandikwa na kufanya mahojiano na vyombo vya habari.

Wakati Medgar Evers, katibu wa N.A.A.C.P, alipouawa kwa risasi huko Mississippi, nilitaka kusema ukweli bila ya kumung’unya maneno. Bomu lilipolipua kanisa la watu weusi huko Birmingham, Alabama, na kuua wasichana wale wadogo wanne, nilitoa maoni yangu-lakini sikusema kile kilichotakiwa kusemwa, yaani jinsi ambayo uhalifu wa mzungu wa Marekani ulivyokuwa umetengeneza mazingira ya chuki na kuyastawisha. Kadri ambavyo chuki iliachwa kuendelea wakati kuna njia ya kuidhibiti, ndivyo ilivyozidi kukomaa, na mwishowe itawawakia wazungu wenyewe, wakiwemo viongozi wake. Mfano mmoja ni jinsi ambavyo Lyndon Johnson na mkewe walipotukanwa vibaya huko Dallas, Texas wakati akiwa makamu wa Rais. Na jinsi ambavyo Adlai Stevenson, balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa alivyotemewa mate na kupigwa kichwani na mwanamke wa kizungu aliyekuwa akigoma.

Bwana Muhammad alikuwa amenifanya kuwa Imam mkuu wa Taifa la Kiislamu katika Marekani. Kwenye mhadhara wa mwishoni mwa mwaka 1963 huko Philadelphia, bwana Muhammad alinisifu mbele ya umati kwa kusema, “Huyu ndiye Imam muaminifu na mwenye bidii zaidi. Atanifuata mpaka kifo chake.”

Hakuwahi kumsifu Muislamu yeyote namna hiyo. Hakuna mtu duniani ambaye ningethamini sifa zake kama nilivyothamini sifa kutoka kwa bwana Muhammad. Lakini hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mimi na bwana Muhammad kuonekana pamoja hadharani.

Muda mfupi kabla ya hapo nilikuwa nimealikwa kwenye kipindi cha redio cha Jerry Williams huko Boston, nikiwa huko kuna mtu alinipatia gazeti lililotoka tu kuchapishwa. Ilisomeka kuwa Baraza la Wananchi wa Lousiana lilikuwa limeahidi zawadi ya dola 10,000 kwa ajili ya kifo changu. Lakini kifo kilikuwa karibu yangu zaidi kuliko huko Lousiana.
Ninachokwambia ni kweli tupu. Nilipokuja kugundua mtu mwingine aliyetaka kuniua, nilikuwa karibu kuwehuka.

***

Katika miaka yangu kumi na mbili kama Imam wa Kiislamu, nilifundisha juu ya maadili vikali sana kiasi kwamba Waislamu wengi walinishutumu mchukia wanawake. Msingi wa mafundisho yangu na imani yangu thabiti ulikuwa ni imani yangu kuwa Elijah Muhammad alikuwa ni ishara ya mabadiliko ya kimaadili, kiakili na kiroho kwa mtu mweusi wa Marekani. Kwa miaka yote kumi na mbili nilifundisha kuwa katika Taifa lote la Kiislamu; mabadiliko yangu mwenyewe ndiyo mfano bora kabisa ninaoufahamu wa jinsi nguvu za bwana Muhammad zinavyoweza kubadili maisha ya watu weusi. Toka nilipoingia gerezani hadi nilipofunga ndoa, karibu miaka kumi na mbili baadaye; sikuwahi kugusa mwanamke, na yote ni sababu ya mafundisho ya bwana Muhammad.

Lakini kufikia mwaka 1963 na kuendelea, watu walionifuatilia watagundua kuwa nilianza kuzungumzia dini kwa uchache sana. Niliwafundisha Waislamu mambo ya kijamii, siasa na matukio yanayoendelea. Nilikaa mbali na somo la maadili.

Sababu ya jambo hilo ni kuwa imani yangu ilikuwa imetetereka kwa namna ambayo siwezi kuelezea. Nilikuwa nimegundua kuwa Waislamu walikuwa wamesalitiwa, na msaliti alikuwa ni Elijah Muhammad mwenyewe.
Nataka kuelezea jambo hilo kwa ufupi kadri niwezavyo, nieleze tu kiasi cha kutosha watu kuelewa msimamo wangu na kwa nini nilichukua hatua nilizochukua. Hakuna haja ya kujiuliza iwapo nifichue hili au la, maana tayari umma unaelewa jambo lenyewe. Hivyo nitanukuu taarifa moja kama ilivyoandikwa magazetini na kutangazwa kwenye redio na televisheni nchini kote:
“Los Angeles, 3, mwezi wa saba, kiongozi wa kundi la Kiharakati la Waislamu weusi, bwana Elijah Muhammad(67), leo amekabiliwa na mashtaka kutoka kwa makatibu wake wanne wa zamani wakidai kuwa ni baba wa watoto wao . . . wanawake wote wako kwenye umri wa miaka ya ishirini . . . bi Rosary na bi Williams wanadai walikuwa na mahusiano na bwana Elijah Muhammad kuanzia mwaka 1957. Bi Rosary anadai kuwa alizaa watoto wawili na bwana Muhammad na akadai kuwa anatarajia mtoto wa tatu pamoja naye. Bi Williams anadai kuwa amezaa na bwana Muhammad binti mmoja.”

Tokea mwaka 1955 nilikuwa nimesikia tetesi. Lakini niamini nikuambiapo jambo hili: kwangu mimi ilikuwa ni vigumu sana kuamini ukosefu wowote wa maadili kufanywa na bwana Muhammad. Wazo tu la jambo hilo lilinifanya nitetemeke kwa hofu. Hivyo akili yangu ilikataa kabisa kukubali jambo zito kama uzinzi kutajwa pamoja na jina la bwana Muhammad.

Uzinzi! Muislamu yeyote aliyepatikana na kosa la uzinzi alifukuzwa mara moja. Moja ya kashfa ya Taifa la Kiislamu iliyolindwa vikali ilikuwa ni kitendo cha makatibu kadhaa wa bwana Muhammad kupatikana na mimba. Waliletwa mbele ya mahakama ya Kiislamu na kukiri kufanya uzinzi. Walipewa adhabu ya kutengwa kuanzia mwaka mmoja hadi mitano. Hilo lilimaanisha kuwa hawakutakiwa kuwasiliana na Muislamu mwingine yeyote.

Nadhani siweza kusema jinsi nilivyomuamini bwana Muhammad na nikaeleweka. Kifupi ni kuwa nilipingana kabisa na akili yangu mwenyewe pale lilipokuja suala la kumuamini bwana Muhammad. Sikutaka Allah “aunguze ubongo wangu” kama ambavyo nilihisi kuwa ubongo wa ndugu yangu Reginald ulikuwa umechomwa kwa kuweka mawazo mabaya juu ya bwana Elijah Muhammad. Mara ya mwisho kumuona Reginald ilikuwa ni siku moja alipoingia kwenye mgahawa wa Msikiti Namba Saba. Nilienda kumsalimu. Nilimuangalia ndugu yangu machoni na kumwambia kuwa hatakiwi kati ya Waislamu, naye aligeuka na kuondoka, tokea hapo sijamuona tena. Nilifanya hayo kwa ndugu wangu wa damu kwa sababu miaka kadhaa nyuma bwana Muhammad alikuwa amemhukumu Reginald kutengwa kutoka kwa Waislamu-nami nilijichukulia kama Muislamu kwanza kisha ndiyo ndugu wa Reginald.

Hakuna mtu ambaye angeweza kuniaminisha kuwa bwana Muhammad angeweza kusaliti heshima aliyopewa na Misikiti yote iliyojaa Waislamu wanaomuamini, wakitoa michango kadri walivyoweza ili kugharamia Taifa la Kiislamu wakati wengi wao malipo ya pango la nyumba yaliwapa taabu.

Lakini ilipofika mwaka 1962 nikagundua kuwa Waislamu wengi walikuwa wanaondoka kutoka Msikiti Namba Mbili wa huko Chicago. Tetezi hizo za aibu zilikuwa zinasambaa kwa kasi, hata kwa watu weusi ambao hawakuwa Waislamu. Nilipokuwa nawaza njia ambazo vyombo vya habari vingeweza kulichafua taifa la Kiislamu, nilijawa na hofu nilipoingiwa na wazo la tetesi hizo kuwafikia waandishi wa habari, weusi au wazungu.

Ukweli ni kuwa nilianza kupatwa na majinamizi . . . nikiona vichwa vya habari juu ya jambo lile.

Kila nilipokuwa nikitoa hotuba Marekani kote nilikuwa nimejawa na hofu. Muda wowote muandishi wa habari angeweza kunifuata na kuuliza, “Bwana Malcom X, ni kweli hizi tetesi tusizikiazo . . .” Ningewajibu nini?

Sikumbuki ni wakati gani hasa nilikubaliana na ukweli wa mambo. Nilijikuta tu akili yangu inakubaliana na ukweli mchungu.

Kote, Chicago na New York nikaanza kusikia kutoka kwa watu wasio Waislamu niliofahamiana nao, walianza kuniambia lakini si moja kwa moja-waliniuliza iwapo nimesikia tetesi zozote. Nilijidai sijui chochote juu ya yale waliyozungumza. Na nilishukuru hawakusema waliyoyafahamu. Nilikuwa natembea kati yao nikijua kabisa walikuwa wananiona kama mpumbavu fulani hivi. Nami nilijiona mpumbavu, kila siku nikienda kuhubiri lakini sijui chochote kuhusu mambo yanayoendelea mbele yangu— ndani ya taasisi yetu, yakimhusisha mtu yuleyule niliyekuwa nikitangaza sifa zake. Kuonekana mjinga kuliibua hisia ambazo sikuwahi kuwa nazo tokea enzi za umpambanaji kwenye mitaa ya Harlem. Kitu kibaya kabisa kwenye dunia ya wapambanaji ni kufanywa mjinga.

Nitakupa mfano mmoja. Siku moja nyuma ya jukwaa la ukumbi wa Apollo huko Harlem, mchekeshaji Dick Gregory aliniangalia na kusema, “Jamaa, Muhammad si kitu bali . . .” -Siwezi kusema neno alilotumia. Bam! Hisia zangu za Kiislamu ziliniambia nimshambulie Dick-lakini nikajikuta nimenyong’onyea na kufedheheka. Nadhani Dick aliona nilivyofedheheka hivyo akaacha kuongelea suala hilo. Nilimfahamu Dick, mwenyeji wa Chicago na mjanja wa mjini
aliyeongea bila kuuma maneno. Nilitamani kumwambia asimwambie mtu mwingine mambo aliyoniambia lakini sikuweza; ingekuwa sawa na kukiri ukweli wake.

Siwezi kuelezea mateso niliyopitia.

Hapo kabla, siku zote kulipokuwa na utata nilipanda ndege haraka kwenda kuonana na bwana Muhammad. Kwangu alikuwa kama mtu aliyenifufua kutoka katika wafu. Kila sifa niliyopata ilikuwa ni kwa sababu yake. Nilihisi kuwa sitakiwi kumtupa hata iweje.

Sikuwa na mwingine wa kumuendea juu ya tatizo hili isipokuwa bwana Muhammad mwenyewe. Hata hivyo hilo halikuepukika. Lakini kwanza nilienda Chicago kuonana na mtoto wa pili wa bwana Muhammad, Wallace Muhammad. Nilihisi kuwa kati ya vijana wa wa Muhammad, Wallace ndiye alikuwa anachukulia kwa uzito sana mambo ya kiroho na muelewa. Siku zote mimi na Wallace tumekuwa tukielewana na kuaminiana.

Wallace aliponiona tu alijua kwa nini nimeenda kumtembelea. “Nafahamu,” alisema. Nilimwambia kuwa inatakiwa tuungane kumsaidia baba yake. Wallace akaniambia kuwa hahisi kama baba yake atakubali msaada wowote. Kichwani mwangu nilijiambia kuwa Wallace atakuwa amewehuka.

Hatua iliyofuata ilikuwa ni kuvunja sheria, sheria iliyosema kuwa Muislamu yeyote hatakiwi kuwasiliana na mtu aliyetengwa. Niliwatafuta na kuongea na makatibu watatu wa zamani wa bwana Muhammad. Kutoka kwenye

vinywa vyao nilisikia wakisema ni nani baba wa watoto wao. Na kwa vinywa vyao niliwasikia wakisema kuwa bwana Muhammad aliwaambia kuwa mimi nilikuwa Imam wake bora kuliko wote aliowahi kuwa nao, lakini siku moja nitamuacha na kuwa mpinzani wake, hivyo ni mtu “hatari.” Nilifahamu kutoka kwa makatibu hawa kuwa, wakati alipokuwa ananisifu hadharani, kwa nyuma alikuwa adui yangu.

Jambo hilo liliniumiza sana.

Kila siku nilikuwa kwenye vinasa sauti, mbele ya kamera, nikiongea na waandishi wa habari na kazi zingine ikiwemo kuhudumia Waislamu wa Msikiti wangu Namba Saba kwa bidii. Nilihisi naota.

Mwishowe akili ikanirejea. Niliona kuwa kukaa bila kufanya kitu ni usaliti. Nilihisi sitakuwa namsaidia bwana Muhammad kwa kukaa tu wakati ilihitajika mtu asimame.

Basi usiku mmoja nilimuandikia bwana Muhammad barua kuhusu sumu iliyokuwa inaenezwa kumuhusu. Alinipigia simu na kusema kuwa tutakapoonana tutalizungumzia suala hilo.

Nilijitahidi sana kutafuta njia ya kuepusha Taifa la Kiislamu lisijiangamize. Nilikuwa na imani na Taifa la Kiislamu. Hatukuwa kikundi cha Wakristo weusi waliorukaruka na kupiga kelele huku wakiwa wamejaa dhambi.
Niliwaza njia moja ya kutumia iwapo mambo yote yatakuwa hadharani. Waislamu waaminifu wangeweza kufundishwa kuwa mambo mema anayotimiza mtu maishani mwake yanapita udhaifu wake wa kibinadamu. Wallace Muhammad alisaidia kupitia Quran na Biblia kwa ajili ya vifungu. Uzinzi aliofanya Daudi na Bathsheba hauna nguvu katika historia kama kitendo cha Daudi kumuua Goliati. Tunapomfikiria Lutu, hatufikirii kuhusu ngono ya maharimu, bali tunafikiria alivyookoa watu wake kutoka maangamizi ya Sodoma na Gomora. Au kuhusu Noah, hatumuwazii akiwa amelewa na uchi bali kwa jinsi alivyojenga safina na kufundisha watu wajiokoe kutokana na gharika. Tunamfikiria Musa kwa jinsi alivyowaokoa Waebrania kutoka utumwani na si jinsi alivyofanya uasherati na wanawake wa Kiethiopia. Kwenye kila kisa nilichopitia, mazuri yalizidi mabaya.

Nilianza kufundisha kwenye Msikiti Namba Saba wa New York kuwa mambo mazuri aliyotimiza mtu maishani mwake yanauzidi uzito udhaifu wake wa kibinadamu. Nilifundisha kuwa mema ya mtu yanazidi uzito mabaya yake. Lakini kamwe sikutaja uasherati, uzinzi wala ukosefu mwingine wa maadili.

Kwa miujiza fulani, habari za uzinzi ambazo zilizungumzwa saa huko Chicago zilionekana kupenya kidogo sana huko Boston, Detroit na New York. Huko Chicago Waislamu wengi walizidi kuondoka kutoka Msikiti Namba Mbili, na nilisikia kuwa watu wengi ambao hawakuwa Waislamu lakini walituunga mkono, wakaanza kutupinga waziwazi. Mnamo mwezi wa pili mwaka 1963, nilisimamia mahafali kwenye Chuo cha Kiislamu; nilipowatambulisha washiriki kadhaa wa familia ya Muhammad niliona jinsi Waislamu walivyoingiwa na ubaridi.

Mwezi wa nne wa mwaka 1963, bwana Elijah Muhammad aliniita huko Phoenix.

Tulisalimiana kwa bashasha kama ilivyo kawaida, na kisha mara moja akanichukua mpaka nje, tukawa tunatembea karibu na bwawa lake la kuogelea.

Alikuwa ni Mtume wa Allah wakati ambao mimi nilikuwa mfungwa muovu, muovu kiasi kwamba wafungwa wengine waliniita shetani, mtu huyu ndiye aliyeniokoa. Ndiye aliyenifundisha na kunitendea kama vile nilikuwa mwanawe. Alikuwa ndiye mtu aliyenipa mbawa za kuniwezesha kwenda mbali na kufanya vitu ambavyo sikuwahi hata kuviota. Tulitembea huku nikiwa nimeelemewa na hisia.

“Ndiyo mwanangu,” alisema bwana Muhammad, “Ni nini ulitaka kusema?”

Bila kumung’unya maneno nilimwambia bwana Muhammad yale yaliyokuwa yakisemwa. Na bila kusubiri majibu yake, nikamwambia kuwa mimi na mwanawe Wallace tumetafuta vifungu kwenye Biblia na Quran ambavyo vinaweza kufundishwa kwa Waislamu kuwa ni utimizo wa unabii-kama ikibidi.

“Mwanangu hata hujanishangaza,” alisema Elijah Muhammad. “Siku zote umeelewa vyema mambo ya kiroho na unabii. Umetambua jambo hili ni kitu gani hasa-unabii. Una uelewa ambao ni wazee tu ndiyo wanao.

“Mimi ni Daudi,” alisema. “Unaposoma jinsi daudi alivyochukua mke wa mtu mwingine, mimi ni Daudi huyo. Unasoma kuhusu Noah aliyelewa pombe-ni mimi. Unasoma juu ya Lutu aliyelala na binti zake mwenyewe. Nimepaswa kutimiza mambo yote hayo.”

***

Nilikumbuka kuwa iwapo ugonjwa wa mlipuko ulitaka kutokea, watu walichanjwa chanjo iliyokuwa na vimelea vilevile vilivyotarajiwa. Na hilo liliwaandaa kupambana na vimelea wanaokuja.

Niliamua kuwaandaa maafisa wengine sita wa pwani ya mashariki niliowachagua mwenyewe.

Niliwaambia ukweli. Na pia niliwaambia kwa nini niliwafunulia ukweli huo-niliwaambia kuwa haitakiwi wapatwe na mshtuko iwapo itawapasa kuwafundisha Waislamu kwenye misikiti yao “kutimizwa kwa unabii.” Niligundua kuwa baadhi yao walikuwa wameishasikia habari zile; mmoja wao alikuwa ni Imam Louis X wa Boston, alikuwa amesikia miezi saba iliyopita. Nao walikuwa wakiishi kwenye mtanziko, wasijue waegemee wapi.

Sikutegemea kwa maafisa wa Kiislamu wa Chicago kuona kuwa jitihada zangu zilikuwa sawa na kuongeza mafuta kwenye moto. Sikutegemea wangenishutumu kuanzisha ugonjwa wa mlipuko wakati nilikuwa natoa chanjo.
Mazingira ya Chicago yalikuwa yametengenezwa ili watu waachane na ugonjwa uliolipuka na kunigeukia mimi.

Kunichukia ilikuwa ndiyo sababu ya watu waliopoteza imani kukusanyika pamoja tena.

Watu weusi wasio Waislamu walionifahamu vyema, na hata baadhi ya waandishi wa habari wa kizungu ambao niliongea nao mara nyingi, walikuwa wakiniambia kila tulipokutana, “Malcom X unaonekana kuchoka sana, unahitaji kupumzika.”

Hawakujua kinachoendelea hata kidogo. Tokea niwe Muislamu, hiyo ilikuwa ni mara ya kwanza kwa mzungu kunionyesha kunijali. Niliweza kuona wazi kuwa baadhi yao hawakuwa na unafiki ndani yao. Mmoja wao- siwezi kumtaja sababu anaweza kupoteza kazi yake-alisema, “Malcom X, wazungu wanahitaji sauti yako kuliko hata watu weusi.” Nakumbuka vizuri maneno hayo kwa sababu toka niwe Muislamu ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kuongea na mzungu kwa kirefu kuhusu jambo jingine mbali na Taifa la Kiislamu na harakati za mtu mweusi wa Marekani.

Sikumbuki ni kwa nini au ilikuwajekuwaje hadi mzungu yule akataja kuhusu vitabu vya kukunjwa vilivyopatikana huko Bahari ya Chumvi. Nilimwambia, “Ndiyo, vitabu hivyo vitaondoa kabisa michoro ya Yesu inayomuonyesha akiwa mweupe na kuweka historia sawa kuwa Yesu hakuwa mzungu.”mwandishi yule alionekana kushangazwa sana. Nikaendelea kumwambia kuwa pia vitaonyesha kuwa Yesu alikuwa mshiriki wa kikundi cha wanajimu wa Misri kilichoitwa Essene. Ukweli ambao Philo, mwanahistoria maarufu wa Misri katika enzi za Yesu aliufahamu vyema. Basi
tukajikuta tunaongea kwa saa mbili kuhusu mambo ya vitu vya kale, historia na dini. Yalikuwa maongezi mazuri sana. Kwa muda ule mfupi nilisahau mambo yaliyokuwa yakinihangaisha kichwani. Nakumbuka tulikubaliana kuwa, kufikia mwaka 2000, wanafunzi wote watafundishwa rangi za kweli za watu wa kale.
****
 
Sura ya 16 inaendelea​

Nimeshasema kuwa nilitegemea vyombo vya habari kuandika kashfa ile muda wowote ule. Lakini sikutegemea habari iliyokuja. Hakuna anayetakiwa kukumbushwa kuwa ni nani aliuawa huko Dallas, Texas mnamo tarehe 22 ya mwezi wa kumi na moja, 1963. Ndani ya saa moja baada ya mauaji, na huu ninakwambia ni ukweli mtupu-kila Imam wa Kiislamu alipokea maelekezo kutoka kwa bwana Elijah Muhammad-yalikuwa maelekezo mawili. Kila Imam aliamrishwa kutosema chochote juu ya mauaji yale. Bwana Muhammad alisema kuwa iwapo tutaulizwa tutoe maoni yetu, tuseme: “Hatuna maoni.”

Katika siku zile tatu ambazo hakukuwa na habari zozote isipokuwa za kuuawa kwa Rais, bwana Muhammad alikuwa na ratiba ya kuzungumza kwenye ukumbi wa Manhattan Centre, New York. Alihairisha kuja kuongea, na kwa vile tulikuwa tumeishalipia ukumbi na haikuwezekana kurudishiwa pesa zetu, bwana Muhammad aliniambia niongee badala yake, nami nikafanya hivyo.

Tokea siku ile, nimeangalia notisi za hotuba ile mara nyingi sana, ni hotuba niliyokuwa nimeiandaa zaidi ya juma
moja kabla ya kuuawa kwa Rais. Kichwa cha hotuba yangu kilikuwa, “Hukumu ya Mungu juu ya Marekani ya mzungu.” Ilielezea jambo nililozoea kuliongelea, “Utavuna utakachopanda” au jinsi ambavyo mzungu wa Marekani alivyokuwa akivuna alichopanda.

Kukawa na kipindi cha majibu na maswali. Ilikuwa haiepukiki kwa mtu kuniuliza, “Una maoni gani juu ya kuuawa kwa Rais Kennedy?”
Bila kupoteza hata sekunde moja, nilijibu kile nilichohisi kilikuwa kimetokea, “Yaani kitendo cha kuku kurudi nyumbani kulala(Chickens coming home to roost).” Nilisema kuwa chuki ya mzungu haijaishia tu kuua watu weusi wasio na ulinzi, kwa kuwa imeachwa kuenea bila kuzuiwa, mwishowe imemdhuru mkuu wa nchi. Nilisema kuwa ni kitu kile kile kilichowapata Medgar Evers, Patrice Lumumba na mume wa bi Nhu.

Mara moja vyombo vya habari vilitangaza na magazeti kuandika: Malcom X kutoka kwa Waislamu weusi: Chickens Come Home to Roost.’”

Hata leo ninapofikiria jambo lile najihisi kuchoka kabisa. Marekani kote, duniani kote, na hata watu mashuhuri zaidi duniani walikuwa wanasema kwa namna moja ama nyingine, na wengine kwa maneno makali kuliko mimi, walisema kwamba mazingira ya chuki yaliyopo Marekani yalikuwa ndiyo chanzo cha kifo cha Rais. Lakini Malcom X aliposema kitu kilekile, ikawa nongwa kubwa.

Ratiba yangu ya kumtembelea bwana Muhammad kila mwezi ilikuwa ni siku iliyofuata. Nilipokuwa kwenye ndege nilipatwa na hisia kuwa jambo fulani litatokea. Siku zote nimekuwa na hisia kali juu ya mambo.

Tulisalimiana na bwana Muhammad kwa bashasha. Lakini nilihisi kuna kitu hakiko sawa kwenye ucheshi wake wa kawaida. Kwa miaka mingi nilijivuna kuwa mimi na bwana Muhammad tulikuwa karibu sana kiasi kwamba nilijua alivyohisi kutokana na nilivyohisi, kama alikuwa na wasiwasi basi nilikuwa na wasiwasi, kama nilikuwa mtulivu basi nilifahamu naye alikuwa mtulivu. Sasa nilikuwa nahisi mkazo. . . .

Tulianza kwa kuongelea mambo mengine. Kisha akaniuliza, “Umeona magazeti ya leo asubuhi?”
Nilijibu, “Ndiyo, nimeyaona.”
“Hiyo ilikuwa ni kauli mbaya sana, nchi hii ilimpenda sana mtu yule. Nchi yote ipo katika maombolezo. Haukuwa wakati muafaka kusema yale. Kauli kama ile inaweza kuwapa wakati mgumu Waislamu wote.”
Kisha kwa kama sauti iliyosikika kutoka mbali, alisema, “Itanibidi kukuzuia kuongea kwa siku tisini zijazo ili Waislamu wote waweze kuepukana na kosa hilo.”
Nilipigwa na ganzi. Lakini nilikuwa mfuasi wa bwana Muhammad. Siku zote nilikuwa nawaambia wasaidizi wangu kuwa mtu yeyote aliye kwenye nafasi ya kutoa adhabu, yeye mwenyewe anatakiwa kuwa tayari kupokea adhabu.

Nilimwambia bwana Muhammad, “Nakubaliana nawe na niko tayari kutumikia adhabu hiyo kwa asilimia mia moja.”
Nilipanda ndege kurudi New York huku nikijiandaa kisaikolojia kuwaambia wasaidizi wangu wa Msikiti Namba Saba kuwa nimesimamishwa au “Nimenyamazishwa.”

Lakini kwa mshangao, nilipofika nilikuta wasaidizi wangu walikuwa tayari wamepewa taarifa. Na kilichonishangaza zaidi ni kuwa ujumbe wa telegram ulikuwa umetumwa kwa kila gazeti, redio na kituo cha televisheni cha New York. Kusambaza ujumbe huo ilikuwa ni kazi ya haraka na ya ufanisi kabisa kuwahi kuona ikifanywa na maafisa wa Chicago.

Simu zote nilizoweza kupatikana ziliita. London. Paris. AP., U.P.I. Na kila kituo cha redio na televisheni na magazeti yote walinipigia simu. Wote niliwaambia kuwa “Nilikosa kumtii Muhammad. Na nakubaliana kabisa na busara zake. Na pia kuwa nategemea kuendelea kuongea tena baada ya siku tisini.”

“Malcom X anyamazishwa!” vilisema vichwa vya habari.

Hofu yangu kubwa ilikuwa iwapo kashfa ile ikaibuka ndani ya siku tisini zijazo, basi sitakuwa na uwezo wa kuisemea nami nilikuwa ndiye Muislamu mwenye uzoefu zaidi katika kushughulika na vyombo vya habari ambavyo vingeikuza kashfa yoyote iliyotokea ndani ya Taifa la Kiislamu.

Baadae nilikuja kufahamu kuwa kunyamazishwa kwangu kulienda mbali kuliko nilivyofikiria. Sikuzuiwa tu kuongea na
vyombo vya habari, bali sikuruhusiwa hata kufundisha ndani ya Msikiti wangu Namba Saba.

Baadaye likatoka tangazo ndani ya Taifa la Kiislamu kuwa nitarudishwa ndani ya siku tisini, “Iwapo atatubu.”
Kwa mara ya kwanza hili lilinifanya nianze kuwa na mashaka. Nilikuwa nimetubu kabisa. Lakini kwa makusudi kabisa, Waislamu walikuwa wakionyeshwa kuwa nilikuwa nimeasi.

Sikupambana mtaani kwa miaka mingi na kuwa mjinga. Nilifahamu nilipokuwa nategwa.

Siku tatu baadaye nilipata habari kuwa afisa mmoja wa Msikiti Namba Saba ambaye alikuwa msaidizi wangu wa karibu sana, alikuwa akiwaambia baadhi ya ndugu wa Msikiti pale kuwa, “Kama mngefahamu alichofanya Imam Malcom X, mngeenda kumuua kwa mikono yenu.”

Na hapo nikafahamu wazi. Kama ambavyo kila afisa ndani ya Taifa la Kiislamu alifahamu, kwamba tishio la kuuawa liliweza kutolewa na mtu mmoja tu.

***

Kichwa changu kilikuwa kama vile kinavuja damu kwa ndani. Nilihisi ubongo wangu umeharibika. Nilienda kumuona Dr. Leona. A. Turner ambaye alikuwa daktari wa familia yangu kwa miaka mingi, alikuwa anafanyia kazi yake huko East Elmhurst, Long Island. Nilimuomba anichunguze ubongo.

Alinichunguza na kusema kuwa nilikuwa kwenye mkazo mkubwa na nilihitaji kupumzika.

Mimi na Cassius Clay(Muhammad Ali) hatuko pamoja leo hii. Lakini siku zote nitamshukuru kuwa katika kipindi hiki, alipokuwa huko Miami akijifua kupigana na Sonny Liston, alitukaribisha, mimi, Betty na watoto kwenda huko kama wageni wake-ikiwa kama zawadi ya miaka sita ya ndoa yangu na Betty.

Nilikutana na Cassius Clay mnamo mwaka 1962 huko Detroit. Yeye na kaka yake Rudolph walikuja kwenye mgahawa mdogo wa wanafunzi uliokuwa karibu na Msikiti wa Detroit, wakati huo Elijah Muhammad alikuwa karibu kuhutubia mhadhara mkubwa. Kila Muislamu alivutiwa na ndugu wale. Cassius alinifuata na “Kunipa tano.” Na kujitambulisha kama ambavyo alivyokuwa akijitambulisha baadaye duniani, “Naitwa Cassius Clay.” Alijitambulisha kama vile ninapaswa kuwa nafahamu yeye ni nani. Basi nikafanya kama vile namfahamu. Lakini ukweli ni kuwa mpaka wakati ule nilikuwa sijawahi kumsikia kabisa. Tulikuwa watu wa dunia mbili tofauti kabisa. Ukweli ni kuwa Elijah Muhammad alikuwa ametuzuia Waislamu kushiriki aina yoyote ile ya michezo.

Muhammad alipokuwa anaongea, ndugu wawili wale waliongoza katika kupiga makofi. Hilo lilimpendeza kila mtu kwa kutokuwa kwao wanafiki—haiwezi kusemwa walikuwa wanatafuta mashabiki maana eneo la mwisho duniani kwa mtu kwenda kupata mashabiki wa ndondi ilikuwa ni kwenye mihadhara ya Waislamu.

Kutoka siku hiyo, nikawa nasikia hapa na pale kuwa Cassius alikuwa akihudhuria Misikiti na migahawa ya Kiislamu kwenye miji mbalimbali. Na kila ilipotokea nilikuwa nikihutubia sehemu ambayo yupo na aliweza kufika basi alihudhuria.
Nilipendezwa sana naye. Tabia yake ilimfanya kuwa mmoja wa watu wachache sana niliowahi kuwaalika nyumbani kwangu. Betty pia alipendezwa naye. Na watoto wetu walimpenda sana. Cassius alikuwa kijana aliyeweza kumpendeza mtu yeyote, mwenye urafiki, nadhifu na mnyenyekevu. Alikuwa ni mtu makini sana hata kwa mambo madogomadogo. Kwa jinsi alivyokuwa anajitia hamnazo kwenye umma nilihisi kuwa alikuwa na mpango wa kumuwezesha kushinda, na alikiri hilo kwa kuniambia kuwa alikuwa na mpango wa kucheza na akili ya Sonny Liston ili aingie ulingoni akiwa na hasira, asiyejifua vizuri na mwenye kujiamini kupita kiasi—akitegemea ushindi wa haraka kama kawaida yake. Si tu kwamba alisikiliza ushauri, bali aliuomba pia. Mwanzoni nilimsisitiza jinsi ambavyo mafanikio ya mtu maarufu yanavyotegemea anavyofahamu na kuelewa tabia na malengo halisi ya watu wanaomzunguka. Nilimuonya kuhusu “mbweha-wajanja” kama alivyowaita wanawake vijana na warembo waliomzonga; nilimwambia Cassius kuwa hao hawakuwa “Mbweha-wajanja” walikuwa mbwa mwitu hatari. Hii ilikuwa ndiyo safari ya likizo ya kwanza ya Betty tokea tumeoana. Watoto wetu watatu walicheza na kurukaruka na
bingwa aliyepigania mkanda wa uzito wa juu.​

Sijui ningefanya nini iwapo ningebaki New York katika nyakati zile tete—nikiwa nimezingirwa na simu zilizoita muda wote. Kutoka kwa waandishi wa habari, na wengine wote waliokuwa na shauku ya kufurahia anguko langu.
Nilikuwa nimepata mshtuko wa kihisia. Nilikuwa kama mtu aliyekuwa kwenye ndoa nzuri kwa miaka kumi na miwili, na kisha ghafla asubuhi moja wakati wa kifungua kinywa mwenza wake akamsukumia karatasi za talaka.

Nilihisi kama kuna kitu fulani cha asili kiliharibika, labda jua au nyota. Lilikuwa ni jambo kubwa kwangu kiasi kwamba akili yangu ilishindwa kulikubali. Kwenye kambi ambayo Cassius alikuwa akijifua, na kwenye Motel ya Hampton House ambako familia yangu iliishi, niliongea na mke wangu na watu wengine, na ukweli ni kuwa nilikuwa naongea maneno ambayo hayakuwa na maana yoyote. Chochote nilichosema kilitoka kwenye sehemu ndogo tu ya ubongo wangu, sehemu kubwa ilikuwa imejawa na mambo zaidi ya elfu yaliyotokea katika miaka kumi na mbili iliyopita . . . mambo yalivyokuwa Misikitini . . . jinsi tulivyokuwa pamoja na familia ya bwana Muhammad. . . nyakati tuilizokuwa pamoja na Waislamu wengine—kibinafsi, nikiwahutubia na katika mijumuiko ya kijamii . . . na nyakati nilipohutubia umati uliokuwa na wazungu ndani yake, na kuongea na vyombo vya habari.

Pale kwenye kambi ya Cassius Clay niliongea na waandishi kadhaa wa habari za michezo, niliwaambia tena na tena kuwa nilianza kuona habari ya kuwa nitarudishwa baada ya siku tisini kuwa ni uongo. Lakini kisaikolojia sikuwa tayari
kukubaliana na ukweli: kwamba mimi na Taifa la Kiislamu tulikuwa tumepeana talaka ya moja kwa moja. Unaelewa ninachomaanisha? Sahihi ya jaji kwenye karatasi inaweza kuwaachanisha wanandoa—lakini kwao wote, kama walikuwa na ndoa nzuri, itawachukua miaka mingi sana kuachana kisaikolojia.

Sikuweza kuepuka mbinu na hila za wazi kutoka Chicago za kuniondoa kabisa kutoka katika Taifa la Kiislamu kama
siyo kutoka duniani kabisa. Nilianza kuuona kabisa mpango wao wa kunitoa.

Muislamu yoyote atakuwa alifahamu kuwa kauli yangu ya “Kuku kurudi nyumbani kulala” ilikuwa ni kisingizio tu cha kuandaa mpango wa kunitoa. Na hatua ya kwanza ilikuwa tayari imeishatimizwa. Waislamu waliaminishwa kuwa nilikuwa nimemuasi bwana Elijah Muhammad. Sasa niliweza kuona jinsi hatua ya pili itakavyokuwa. Nitaendelea kusimamishwa na baadaye kutengwa moja kwa moja. Hatua ya tatu itakuwa kuwachochea Waislamu fulani wasiojua ukweli waniue ikiwa kama kutimiza wajibu wao wa kidini, au kunitenga kabisa hadi nipotee kwenye macho ya umma.

Mtu pekee aliyefahamu hali halisi alikuwa ni mke wangu. Sikuwahi kuwaza kuwa nitakuja kumtegemea mke wangu kama nilivyokuja kumtegemea Betty. Si kwamba tulikuwa tunazungumza sana. Betty hakusema chochote, lakini niliweza kuona kuwa kuna jambo linamzonga japo anaonekana mtulivu. Nilifahamu kuwa alikuwa mtumishi
muaminifu wa Allah kama nilivyokuwa. Na nilifahamu kuwa atasimama nami kwa hali yoyote ile.

Maneno ya kifo hayakuniogopesha. Kwa miaka kumi na miwili niliyokuwa na bwana Muhammad, nilikuwa tayari kujitolea maisha yangu wakati wowote ule kwa ajili yake. Kitu ambacho kwangu kilikuwa kibaya kuliko kifo ilikuwa ni usaliti. Niliweza kuelewa kifo, lakini sikuweza kuelewa usaliti—hasa kutokana na uaminifu nilioonyesha kwa Taifa la Kiislamu na kwa bwana Muhammad. Katika miaka kumi na miwili iliyopita, iwapo bwana Muhammad angetenda kosa na kuhukumiwa kifo, ningejaribu kusema mimi ndiye niliyetenda ili kumuokoa na ningeenda kwenye kiti cha umeme kama mtumishi wa bwana Muhammad.

Basi nikiwa kwenye ile kambi ya Cassius Clay kama mgeni wake, nilijitahidi kutoa matatizo yangu binafsi akilini na kukazia matatizo ya Taifa la Kiislamu. Bado nilikuwa napambana kujiaminisha kuwa ni kweli bwana Muhammad alikuwa anatimiza unabii. Maana kiukweli kabisa niliamini kuwa kama bwana Muhammad siyo Mungu, basi hakika alisimama pembeni ya Mungu.

Lakini kilichovunja imani yangu ilikuwa ni kitendo cha bwana Muhammad. Badala ya kukiri mbele ya wafuasi wake yale aliyotenda kama udhaifu wa kibinadamu au utimizo wa unabii—kitu ambacho niliamini kabisa kuwa Waislamu wangekielewa au walau wangekubaliana nacho, yeye akataka kuficha aliyofanya.
Hilo ndilo lilikuwa pigo kubwa zaidi kwangu.

Hapo ndipo nilipoanza kutambua kuwa nilimuamini bwana Muhammad kuliko imani yake juu yake yeye mwenyewe.
Na huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa kuanza kujifikiria mimi mwenyewe baada ya kutoweza kufanya hivyo kwa miaka kumi na miwili.

Niliondoka Florida kwa muda mfupi ili kuwarudisha Betty na watoto nyumbani kwetu huko Long Island. Nilipata habari kuwa maafisa wa Chicago walikuwa wamechukizwa na kitendo changu cha kwenda kwenye kambi ya Cassius Clay. Walihisi kwamba Cassius hana nafasi yoyote ya kushinda. Na kwamba mimi kujihusisha naye kutawaabisha Waislamu. (Sifahamu kama bingwa leo hii anakumbuka kuwa magazeti mengi yaliandika habari za kabla ya pambano isipokuwa gazeti la Muhammad Speaks. Japokuwa Cassius alikuwa ndugu wa Kiislamu lakini gazeti la Kiislamu halikuona umuhimu wa kuandika pambano lake.)

Nilirudi tena Miami, nikiamini kuwa ni mpango wa Allah kunifanya mimi nimsaidie Cassius kuuonyesha ulimwengu ukuu wa Uislamu—kuonyesha kuwa akili huzidi nguvu. Sihitaji kukukumbusha jinsi watu walivyodhihaki uwezekano wa Cassius Clay kumpiga Liston.

Safari hii nilikuja na picha za Floyd Patterson na sonny Liston kutoka kwenye kambi zao za kujifua, wakiwa na makasisi wakizungu kama washauri wao wa kiroho. Cassius Clay, akiwa kama Muislamu, hakuhitaji kuambiwa yale ambayo Ukristo wa kizungu umemfanyia mtu mweusi wa Marekani. “Hili ni pambano juu ya kweli,” nilimwambia Cassius. “Ni pambano la kwanza la ulingoni kati ya Msalaba na Mwezi. Ni vita ya kisasa ya kidini. Mkristo na Muislamu wakikabiliana huku televisheni zikiuonyesha ulimwengu mzima kinachotokea!” Nilimwambia Cassius, “Unafikiri Allah amepanga yote haya ili wewe utoke ulingoni bila ushindi?” (Utakuwa unakumbuka kuwa wakati wa kupima uzito wa mabondia, Cassius alikuwa akipiga kelele, “ushindi wangu umetabiriwa! Siwezi kupigwa!”)

Washauri wa Sonny Liston walimfanya apambanie zaidi “uchangamano” kuliko kujifua kupambana na Cassius. Mwishowe akawa amefanikiwa kupanga nyumba kubwa kwenye eneo la wazungu. Nyumba hiyo ilimilikiwa na mmiliki wa timu ya Baseball ya New York, Dan Topping. Baadhi ya jioni mimi na Cassius tulikuwa tukitembelea maeneo ya watu weusi. Watu weusi wale walibaki midomo wazi, wakishangaa kuwa alikuwa kati yao badala ya maeneo ya wazungu kama ambavyo mabingwa wengi weusi walivyopendelea. Mara kwa mara Cassius aliwashangaza watu weusi wale kwa kuwaambia, “Nyie ni watu wangu. Ninapata nguvu zangu kwa kuwa kati ya weusi wenzangu.”

Kitu alichokuja kukutana nacho Sonny kilikuwa si cha kawaida—kitu kutoka kwa mtu anayemuabudu Allah na asiyeogopa chochote.

Katika viti zaidi ya elfu nane vilivyokuwepo ndani ya ukumbi wa mikutano wa Miami, nilipata kiti namba saba. Siku zote namba saba imekuwa namba yangu ya bahati.

Imefuatana nami maisha yangu yote. Nilichukulia hilo kama ujumbe kutoka kwa Allah kuwa Cassius Clay alikuwa anaenda kushinda pambano. Mbali na Cassius, pia nilikuwa na wasiwasi juu ya ndugu yake Rudolph ambaye alikuwa anafanya pambano lake la kwanza la kulipwa kwenye pambano la utangulizi.

Cassius alimuangalia ndugu yake akimshinda mtu mmoja mweusi kutoka Florida aliyeitwa “Chip” Johnson. Alikuwa amekaa nyuma ya ukumbi kwa utulivu na amevalia suti. Baada ya miezi mingi ya vioja na vituko vya wakati wa kupima uzito, sasa alikuwa na utulivu wa ajabu. Utulivu huu ulitakiwa kuwashtua wachambuzi wa michezo waliyemtabiria kupigwa vibaya.

Basi Cassius akapotea, kwenda kuvaa kwa ajili ya kumkabili Liston. Kama tulivyokubaliana, nilijumuika naye katika kuomba Baraka za Allah. Mwishowe wakawa ulingoni na Liston, kila mtu kwenye kona yake. Nilikunja mikono yangu na kuwa mtulivu kabisa, kamera za televisheni zingeweza kukufanya uonekane mpumbavu unapokuwa unashangilia pambano.

Pambano lilienda kama Cassius alivyopanga isipokuwa kwa kemikali fulani iliyomuingia machoni na kumfanya asione vizuri kwenye raundi ya nne na ya tano. Aliweza kuepuka makonde yenye nguvu ya Liston. Kufika raundi ya tatu, Liston ambaye umri ulikuwa umeanza kwenda alianza kuchoka, alikuwa amejifua na kujiaminisha kuwa atamaliza pambano ndani ya raundi mbili tu. Mwishowe Liston akapoteza pambano. Siri ya matokeo ya pambano lile la kihistori ilikuwa ni kuwa miezi kadhaa kabla ya usiku wa pambano, Clay alikuwa ameishamshinda Liston kiakili.
Pengine hakujawahi kuwa na sherehe ya bingwa mpya iliyokuwa na utulivu kama ile. Mfalme kijana wa ulingoni alifika kwenye Motel niliyoishi. Alikula aiskrimu na alikunywa maziwa na mcheza mpira mashuhuri, Jimmy Brown, rafiki wengine na baadhi ya waandishi wa habari. Kutokana na usingizi, alilala kidogo kitandani kwangu kisha baadaye akaenda kwenye makazi yake.

Asubuhi iliyofuata tulipata kifungua kinywa pamoja, baada ya hapo alifanya mkutano na waandishi wa habari na kutoa tangazo lililokuwa kichwa cha habari duniani kote, alitangaza kuwa yeye ni “Muislamu Mweusi.”
Lakini ngoja nikuambie kitu kimoja kuhusu hilo. Cassius hakujitangaza kama “Muislamu Mweusi.” Waandishi wa habari ndiyo walioandika hivyo, alichowaambia ni kuwa: “Naamini katika dini ya Kiislamu, nikimaanisha naamini kuwa hakuna Mungu isipokuwa Allah na Muhammad ni mtume wake. Hii ni dini ileile inayoaminiwa na watu zaidi ya milioni mia saba ambao si weupe huko Afrika na Asia.”

Hakuna kitu cha ajabu katika mambo yote yaliyofuata kama kitendo cha Floyd Patterson kutangaza kuwa; akiwa kama Mkatoliki anataka kupambana na Cassius Clay ili mkanda wa ubingwa wa juu usiwe mikononi mwa Muislamu. Kilikuwa kitendo cha kusikitisha sana kutoka kwa Mkristo mweusi aliyechotwa akili, akiwa tayari kumpigania mzungu
ambaye hataki kabisa kujihusisha naye. Kama majuma matatu mbele, magazeti yakaandika taarifa kuwa huko Yonkers, New York, Patterson alikuwa anauza nyumba yake ya dola 140,000 kwa pungufu ya dola 20,000. Alikuwa “Amechangamana” kwenye mitaa ya wazungu ambao walifanya maisha yake kuwa ya taabu sana. Hakuna aliyemtendea kirafiki, na watoto wao waliwaita watoto wake “Niggers.” Jirani yake mmoja alikuwa amemfundisha mbwa wake kwenda kujisaidia kwenye uwanja wa Patterson. Mwingine alijenga uzio ili watu weusi wasionekane. “Nilijaribu lakini haikuwezekana,” Patterson aliviambia vyombo vya habari.

***

Agizo la kwanza la kuuawa kwangu, lilitolewa kupitia afisa wa Msikiti Namba Saba ambaye alikuwa msaidizi wangu wa karibu. Msimamizi wangu mwingine wa karibu wa zamani alipewa jukumu na kutekeleza jambo hilo. Alikuwa ni ndugu mwenye uzoefu na vilipuzi; alielekezwa ategeshe bomu kwenye gari langu ambalo litalipuka mara tu nikiliwasha. Lakini inaonekana ndugu huyu aliona jinsi nilivyokuwa muaminifu kwa Taifa la Kiislamu hivyo hakutekeleza amri ile, na badala yake alinifuata. Nilimshukuru kwa kuokoa maisha yangu. Nilimwambia ukweli ya yaliyokuwa yakiendelea huko Chicago. Alipatwa na mshangao mkubwa sana.

Ndugu huyu alikuwa na ukaribu sana na ndugu wengine kutoka Msikiti Namba Saba ambao wangeweza kutumika
kuniua. Alisema kuwa atachukua jukumu la kuwaelimisha wote ili wasije kutumika vibaya.

Agizo hili la kuuawa kwangu ndilo lililosababisha nianze kukubali talaka ya kisaikolojia kati yangu na Taifa la Kiislamu.
Kila nilipokuwa—mitaani, maeneo ya biashara, kwenye lifti, kwenye magari nk, nilianza kuona sura za Waislamu niliowafahamu, na nilifahamu kuwa yeyote kati yao anaweza kuwa anasubiri apate nafasi nzuri ya kunimiminia risasi.
Nilikuwa naumiza kichwa juu ya nini cha kufanya. Haikuwezekana kutenganisha maisha yangu na harakati za mtu mweusi wa Marekani. Jamii ilinichukulia kama “Kiongozi.” Kwa miaka mingi nilikuwa nimewashambulia wale walioitwa “Viongozi” wa watu weusi kutokana na kasoro zao. Sasa ilinipasa kujitafakari na kujiuliza iwapo nina sifa za kuweza kumsaidia mtu mweusi katika mapambano yake ya kupigania haki. Nilikuwa na uzoefu wa kutosha kuelewa kuwa ili kuratibu na kusimamia kitu chochote na kikafanikiwa, unatakiwa kwanza kuchunguza hali halisi na kweli za msingi.

Kwanza kabisa nilijua kuwa nina mtaji wa kujulikana kimataifa. Hakuna kiasi cha pesa ambacho kingeweza kununua hilo. Nilifahamu vyema kuwa iwapo nitasema jambo lolote linalostahili kuwa habari watu watalisoma na kulisikia, pengine hata duniani kot—kutegemeana na jambo lenyewe. Pia ndani ya jiji la New York, ambako ingekuwa ndiyo sehemu yangu ya kazi, nilikuwa na wafuasi wengi ambao hawakuwa Waislamu. Wafuasi hao wamekuwa wakiongezeka tokea siku ile niliyowaongoza Waislamu kuandamana kwenda polisi wakati walipompiga ndugu yetu Hinton. Mamia ya watu weusi wa Harelm waliona hilo, na maelfu wengine walisikia jinsi ambavyo tulionyesha kuwa watu weusi wanaweza kutimiza jambo lolote iwapo watamkabili mzungu bila woga. Tokea siku hiyo, Harlem yote ilijionea jinsi polisi walivyowaheshimu Waislamu. (Hicho ndicho kipindi ambacho inspekta wa polisi msaidizi wa kituo namba 28 aliponiambia, “Hakuna mtu anatakiwa kuwa na nguvu kiasi hicho.”)

Kwenye miaka iliyofuata nilipata ushahidi mbalimbali unaaonyesha kuwa asilimia kubwa ya watu weusi wa New York waliitikia yale niliyosema, kutia ndani wengine wengi sana ambao hawawezi kukiri hilo hadharani. Kwa mfano, karibu mara zote nilipohutubia mihadhara ya mitaani, nilikusanya watu mara kumi hadi kumi na mbili ya wale waliokusanywa na “Viongozi” wengine wa watu weusi. Nilifahamu kuwa kwenye jamii yoyote, kiongozi wa kweli ni yule anayestahili kufuatwa kutokana na matendo yake. Wafuasi wa kweli wanakuja wenyewe kwa hiari yao. Nilifahamu kuwa tatizo kubwa la “Viongozi” wa watu weusi wenye majina makubwa ni kukosa kwao kueleweka na watu weusi walioishi maeneo ya maghetto. Wangewezaje kueleweka wakati muda mwingi waliutumia “kuchangamana” na wazungu? Nilifahamu kuwa watu wa maghettoni walifahamu vyema kuwa kiroho sikuwahi ondoka maeneo ya maghetto, na hata kimwili sikuondoka zaidi ya ilivyolazimu. Nilikuwa na silika za kighetto; kwa mfano, niliweza kuhisi iwapo mkazo haukuwa wa kawaida kwenye hadhira ya watu wa maghettoni. Na niliweza kuongea na kuelewa lugha ya maghettoni. Kulikuwa na kisa kimoja ambacho kilinijia akilini kila mara nilipomsikia mmoja wa “viongozi wa watu weusi” wenye majina makubwa akidai kuwa anaongea kwa niaba ya watu weusi waishio maeneo ya maghetto.
Siku moja baada ya mkutano kwenye mitaa ya Harlem, nilipokuwa naongea na mmoja wa “Viongozi” hawa kutoka mjini-kati, tukafuatwa na mpambanaji mmoja wa mitaa ya Harlem. Sikuwahi muona mpambanaji yule hapo kabla. Alituongelesha kwa sekunde kadhaa akitumia lugha ya mtaani hasa, kisha akaendelea na safari yake kwenye barabara ya saba.

“Kiongozi” yule kutoka mjini-kati alibaki anamuangalia mpambanaji yule kama vile amemsikia mtu akiongea Kihindi. Aliniuliza alichoongea nami nikamwambia.

Ninachotaka kumaanisha ni kuwa, nikiwa kama “kiongozi,” ninauwezo wa kuongea kwenye vinasa sauti vya vyombo vya habari kama ABC, CBS , NBC au chuo cha Harvard na Tuskegee; ninaweza kuongea na watu weusi wa “daraja la kati” na watu weusi waishio maeneo ya maghetto(watu ambao viongozi wengine hawaishi kuwazungumzia) na kwa vile nami niliwahi kuwa mpambanaji, nilielewa vyema kuliko wazungu wote na vyema kuliko karibu “viongozi” wote wa watu weusi—kwamba mtu mweusi hatari kuliko wote ndani ya Marekani ni mpambanaji kutoka maeneo ya maghettoni.

Kwa nini nasema hivyo? Mpambanaji kwenye msitu wa maghettoni anaheshimu mamlaka ya mzungu kwa kiasi kidogo kuliko mtu mweusi yoyote katika Amerika ya Kaskazini. Mpambanaji wa maghettoni hana kitu chochote ndani yake kinachomzuia kufanya lolote. Hana dini, hana wazo la maadili, hawajibiki kama raia, haogopi chochote. Ili aishi, muda wote yuko macho akitafuta mtu wa kumnyonya, muda wote anatafuta binadamu dhaifu kama mnyama Chororo-kaya afanyavyo. Mpambanaji wa maghettoni siku zote na muda wote ni mtu wa vurugu. Kila anachofanya anajitoa mzimamzima.

Na kinachomfanya mpambanaji wa maghettoni awe hatari zaidi ni “picha” inayopendeza anayowaonyesha vijana wa maghettoni walioacha shule. Vijana hawa wameona jinsi wazazi wao walivyotaabika kutafuta maisha au jinsi walivyokata tamaa ya kupambana kwenye ulimwengu wa mzungu wa kibaguzi na usio na uungwana. Wanaamua kuwa ni bora wawe kama wapambanaji ambao wanawaona wamevalia “nadhifu” na kuonyesha pesa, na kutojali yoyote wala chochote. Hivyo vijana wa maghettoni wanaanza kuvutiwa na maisha ya wapambanaji, maisha ya madawa, wizi, ukahaba—kwa ujumla uhalifu na ukosefu wa maadili.

Mara ya kwanza nilipoona hatari ya vijana hawa iwapo watachochewa kufanya vurugu niliogopa sana. Mchana mmoja wakati wa majira ya joto nilihudhuria mkutano mmoja kwenye mitaa ya Harlem ambao ulikuwa na vijana hawa wengi sana. Nilikuwa nimealikwa na viongozi “makini” wa watu weusi ambao kwa kawaida walikuwa hawaongei nami; nilifahamu kuwa walitumia tu jina langu ili kuvuta watu. Nilipofika jukwaani, niliuambia umati ule kuwa ukweli ni kuwa sitakiwi pale, jina langu limetumika tu kuvuta watu, kisha nikashuka.

Sijui kwa nini nilifanya vile! Wale vijana wakaanza kughadhabika na kupiga kelele. Ndani ya muda mfupi barabara zikawa zimefungwa na umati wenye hasira. nilipanda juu ya gari na kupunga mkono nikiwataka watulie. Walitulia, kisha nikawaomba waondoke nao wakafanya hivyo. Huo ndiyo wakati ilipoanza kusemwa kuwa nilikuwa mtu mweusi pekee ndani ya Marekani aliyeweza ‘Kuzuia machafuko ya watu wa rangi tofauti au kuyaanzisha.’ Sijui kama ninaweza kufanya lolote kati ya hayo. Lakini nafahamu kitu kimoja: kwa dakika chache zile nilijifunza kuheshimu moto uliopo ndani ya wapambanaji na vijana wanawaowahusudu—watu wa maghettoni ambao mzungu wa kaskazini amewafungia humo kwa miaka mia moja.
Majira ya joto ya mwaka 1964 huko Harlem, Rochester na katika majiji mengine, yametoa picha ya kitu kinachoweza kutokea—na ni picha tu sababu vurugu zote zile zilitokea kwenye maeneo ya watu weusi tu. Ukiacha watu hawa wa maghettoni wenye hasira wachochewe sawasawa na tukio fulani, na kisha walipuke hasira na kutoka kwenye maeneo yao hadi kwenye maeneo ya wazungu! Ndani ya jiji la New York ukiwaruhusu watu weusi wenye hasira watoke Harlem na kuvuka bustani ya Central Park, au chukulia Chicago South Side, ikiwaacha watu weusi wale waingie mjini-kati. Ukiwaacha watu weusi wa Washington D. C waingie barabara ya Pennsylvania. Detroit tayari imeshuhudia maandamano ya amani ya watu weusi zaidi ya laki moja—fikiria kuhusu hilo. Bomu la kijamii la watu weusi liko karibu kila jiji, Cleveland, Philadelphia, San Francisco, Los Angeles . . . kote huko hasira ya mtu mweusi inatokota.

***

Nimetoka nje ya mada na kuzungumzia baadhi ya matukio yaliyonifundisha kuheshimu hatari iliyopo maeneo ya maghetto. Nilikuwa najaribu kuelezea jinsi nilivyochunguza sifa zangu kwa makini iwapo ninafaa kuwa “kiongozi” huru wa watu weusi.

Mwisho wa uchunguzi wangu nikafikia hitimisho kuwa uchaguzi juu ya jambo hilo ulikwisha fanyika. Umati wa watu wa maghettoni uliniamini na kuniona kama kiongozi miongoni mwao. Nilifahamu vyema kuwa watu wa maghettoni humuamini yule tu ambaye ameonyesha kuwa hawezi kuwauza kwa mzungu. Na si tu kuwa sikuwa na nia ya kuwazua, lakini jambo hilo halikuwa hulka yangu.

Niliiona changamoto ya kuunda taasisi ambayo itasaidia kutibu ugonjwa wa mtu mweusi wa Amerika ya Kaskazini— ugonjwa unaomfanya aendelee kuwa chini ya miguu ya mzungu.

Mtu mweusi wa Amerika ya Kaskazini alikuwa mgonjwa wa kiakili kutokana na jinsi alivyokubali na kufuata utamaduni wa mzungu kama kondoo.

Mtu mweusi wa Amerika ya Kaskazini alikuwa mgonjwa kiroho sababu kwa karne kadhaa ameukubali Ukristo wa mzungu—Ukristo unaomwambia Mkristo mweusi asitarajie undugu wa kweli kati ya binadamu wote, bali avumilie ukatili wa wale wanaojiita Wakristo wakizungu. Ukristo umewafanya watu weusi wasiweze kufikiri sawasawa.

Umemfanya mtu mweusi afikirie kuwa; iwapo hana viatu na hana chakula-“Tutapata viatu, na maziwa na asali, na samaki wa kukaanga Mbinguni.”

Mtu mweusi wa Amerika ya Kaskazini alikuwa mgonjwa kiuchumi na hilo lilinaonyeshwa wazi na jambo moja: akiwa kama mteja, alipata kidogo kuliko anachostahili, na kama mzalishaji, alitoa kidogo zaidi. Mtu mweusi wa Marekani anatuonyesha picha halisi ya tegemezi—chawa mweusi ambaye yupo kwenye kiini macho kuwa anapiga hatua sababu yupo kwenye chuchu za ng’ombe mnene ambaye ni Marekani ya mzungu. Kwa mfano, kwa mwaka watu weusi hutumia dola bilioni 3 kwa ajili ya magari, lakini Marekani hakuna muuza magari mweusi wa maana. Kwa mfano, asilimia arobaini ya Scotch Whisky ghali zinazoingizwa nchini hushuka kwenye makoo ya mtu mweusi anayetafuta hadhi; lakini viwanda pekee vya pombe vinavyomilikiwa na mtu mweusi vipo bafuni au mahali fulani huko porini. Au kwa mfano jambo la aibu linaloendelea katika jiji la New York. Ndani ya jiji hili kuna watu weusi milioni moja lakini biashara za watu weusi zilizoajiri zaidi ya watu kumi hazifiki ishirini. Ni kwa sababu watu weusi hawamiliki na kudhibiti biashara kwenye maeneo yao ndiyo maana hawana jamii imara. Mbaya kuliko yote ni kuwa mtu mweusi wa Amerika ya Kaskazini alikuwa mgonjwa kisiasa. Amemruhusu mzungu amgawe kwenye upumbavu wa “mrepublikani” mweusi na “mdemokrati” mweusi, “mliberali” mweusi na “mhafidhina” mweusi . . . wakati kura milioni kumi za watu weusi ndizo zingeweza kuwa zinaamua siasa za Marekani—maana kura za wazungu zimegawanyika sawa sawa kati ya warepublikani na wademokrati. Sanduku la kura ndipo mahali pekee ambapo mtu mweusi anaweza kufanya harakati zake kwa heshima, na kwa kutumia nyenzo na nguvu ambayo mzungu anaielewa, anaiheshimu, anaiogopa na kukubaliana nayo. Ngoja nikuambie kitu! Iwapo kamati ya wapiga kura weusi ingewaambia wanasiasa “wenye chuki kali” dhidi ya watu weusi, “Tunawakilisha kura milioni kumi,” mtu huyo mwenye chuki angeruka na kusema, “Unaendeleaje rafiki? Karibu ndani!” iwapo watu weusi wa Mississippi wangepiga kura kama kikundi kimoja, Eastland angejidai kuwa mliberali kuliko Jacob Javits—au vinginevyo asingeweza kusalia madarakani. Unafikiri ni kwa nini mwanasiasa huyo mbaguzi anapambana kufanya watu weusi wasiweze kupiga kura?

Kama kuna kikundi cha watu kinaweza kupiga kura kwa pamoja na kuamua matokeo ya uchaguzi na kinashindwa kufanya hivyo, basi kikundi hicho kinaumwa kisiasa. Kuna wakati wahamiaji waliufanya ukumbi wa Tammany kuwa mahali penye nguvu sana katika siasa za Marekani. Mwaka 1880, meya wa kwanza Mkatoliki mwenye asili ya Ireland alichaguliwa kuongoza jiji la New York, na kufikia mwaka 1960, Marekani ikawa na Rais wa kwanza Mkatoliki mwenye asili ya Ireland. Iwapo watu weusi wa Marekani wangepiga kura kama kitu kimoja, wangekuwa na nguvu zaidi ya hizo.
Siasa za Marekani zinaongozwa na maslahi ya vikundi mbalimbali na uwezo wa kushawishi. Ni kundi gani ambalo maslahi yao yanatakiwa kushugulikiwa haraka, kundi gani linahitaji kupiga kura kwa pamoja zaidi ya watu weusi? Chama cha wafanyakazi kinamiliki ndani ya jiji la Washington moja ya majengo makubwa yasiyo mali ya serikali—jengo ambalo lipo mahali ambapo wanaweza kuona kila kitu kinachoendelea kwenye ikulu ya Marekani, na hakuna hatua yoyote ya kisiasa inayochukuliwa bila ya kupitia ushawishi wao. Makampuni makubwa ya mafuta yanapata ruzuku kupitia ushawishi. Mkulima, kupitia ushawishi wake amekuwa kikundi kinachopokea ruzuku kubwa kuliko vyote ndani ya Marekani, sababu ni kuwa mamilioni ya wakulima hawapigi kura kama wademokrati, warepublikani, waliberali au wahafidhina, bali wanapiga kura kama wakulima.

Madaktari wanaushawishi wenye nguvu zaidi katika Washington. Walipigania maslahi yao na kufanikiwa kuzuia mpango wa Medicare uliohitajiwa na mamilioni ya watu. Kwa nini kuna vikundi vyenye ushawishi vya walima ngano, mbogamboga, wafugaji wa ng’ombe, na hata cha Wachina!

Nchi ndogo kabisa ambazo watu hawajawahi kuzisikia zina watu wao wenye ushawishi ndani ya Washington, wakiwakilisha maslahi yao.

Serikali ina idara zinazoshughulika na vikundi vinavyopambana kuonekana na kusikika. Idara ya kilimo inashughulika na mahitaji ya wakulima. Kuna idara za elimu, afya na ustawi wa jamii. Kuna idara ya mambo ya ndani ambayo ndani yake inashugulika na mambo ya Wahindi. Je mkulima, daktari na Mhindi ndiyo matatizo makubwa yanayoikabili Marekani leo hii?Hapana—ni mtu mweusi! Kulitakiwa kuwe na idara yenye ukubwa wa Pentagoni, ikishughulikia kila aina ya matatizo ya watu weusi.

Watu weusi milioni ishirini na mbili! Wameitumikia Marekani kwa miaka mia nne, tokea vita ya uhuru, wamepambana na kufa katika vita zote; wamekuwepo ndani ya Marekani kabla ya wahamiaji wa mwanzo, na miaka mingi kabla ya mafuriko ya wahamiaji—lakini leo hii wako chini kwenye kila nyanja.

Ikitokea kesho kila mtu mweusi kati ya watu weusi milioni ishirini na mbili akatoa dola moja ili kujenga jengo lao ndani ya jiji la Washington. Na kila asubuhi, kila mbunge apokee ujumbe unaomjulisha matakwa na matarajio ya mtu mweusi wa Marekani—sauti ya matakwa ya mtu mweusi inatakiwa kuwa kwenye kila sikio la kila mbunge.
Nguzo zinazoendesha nchi hii ni nguvu za kiuchumi na kisiasa. Mtu mweusi hana nguvu za kiuchumi—na itamchukua muda mrefu kuwa nazo. Lakini sasa mtu mweusi wa Marekani ana nguvu za kisiasa kuweza kubadili mustakabali wake ndani ya siku moja tu.

***

Taasisi niliyokuwa naiwazia kuunda kichwani mwangu ili kumsaidia mtu mweusi kupata haki zake kama binadamu, kumtibu maradhi yake ya kiuchumi, kisiasa na kiroho ilikuwa ni kubwa sana. Lakini kama unataka kujenga kitu chochote cha maana, unatakiwa kuanza na mpango wa maana.

Taasisi niliyopanga kuunda ilikuwa tofauti kabisa na Taifa la Kiislamu kwa sababu ilikuwa ya watu weusi wa dini zote, na itaenda kutimiza kile ambacho Taifa la Kiislamu lilihubiri tu.

Tetesi zilienea kwa kasi, hasa kwenye miji ya mashariki— nimepanga kufanya nini? Kitu cha kwanza kufanya ilikuwa kuvutia watu ambao wako tayari. Kila siku, ndugu wanaharakati, watu wa vitendo ambao walikuwa nami katika Msikiti Namba Saba, walikuwa wanatangaza kujitoa kutoka Taifa la Kiislamu na kujiunga nami. Kila siku nilipata uungwaji mkono kutoka kwa watu weusi ambao hawakuwa Waislamu, na cha kushangaza walikuwepo wengi kutoka kwa watu weusi wa “daraja la kati” na “daraja la juu” yaani wenye “kujiweza,” watu waliochoshwa na na hadhi za uongo. Watu walianza kuwa na mshawasha: “Lini utaitisha mkutano, lini tutajipanga?”

Nilikodi ukumbi wa dansi kwenye hoteli ya Theresa kwa ajili ya mkutano wetu wa kwanza. Hoteli hiyo ilikuwa kwenye makutano ya mtaa wa 125 na ya barabara ya saba, moja ya maeneo ya Harlem yenye pilika nyingi.

Gazeti la Amsterdam News liliandika habari za kikao chetu na kusema kuwa tulipanga kuanzisha Msikiti wetu kwenye hoteli ya Theresa. Barua, simu na ujumbe wa telegram kutoka nchini kote vilifika hotelini pale vikinitafuta. Ujumbe wao mkubwa walisema kuwa kitu hiki ndicho watu walichokuwa wakikisubiria. Watu ambao sikuwahi hata kuwasikia walionyesha imani kubwa sana kwangu kwa namna iliyonigusa sana.

Watu wengi walisema kuwa sheria kali za kimaadili za Taifa la Kiislamu zilikuwa kikwazo kwao, hivyo walitaka kuungana nami.

Daktari mmoja aliyekuwa anamiliki hospitali ndogo, alinipigia simu akitaka kujiunga. Wengine wengi sana walituma michango yao hata kabla hatujatangaza sera zetu hadharani. Waislamu kutoka miji mingine waliniandikia barua kuwa watajiunga nami. Wengi wao wakidai kuwa “Taifa la Kiislamu halifanyi chochote” . . . “Taifa la Kiislamu lilikuwa linajikongoja sana.”

Wazungu wengi nao walitupigia simu na kutuandikia barua wakitaka kutoa michango na kuuliza iwapo wanaweza kujiunga. Jibu lilikuwa ni hapana, hawawezi kujiunga, ni watu weusi tu ndiyo waliruhusiwa, lakini kama waliweza wangeweza kuchangia fedha kwa ajili ya harakati zetu za kutatua tatizo la ubaguzi wa rangi ndani ya Marekani.
Mialiko ya kuhutubia ikaanza kumiminika—asubuhi moja ya Jumatatu tulipokea mialiko ishirini na mbili.

Nilishangazwa sana kuona idadi isiyo ya kawaida ya mialiko ilitoka kwa wachungaji wa Kikristo wazungu.
Niliitisha mkutano na waandishi wa habari. Nilikaa mbele ya kinasa sauti, Taa za kamera zilimulika huku na kule. Waandishi wa habari, wanaume, wanawake, wazungu, weusi—wakiwakilisha vyombo vya habari vilivyofika duniani kote, walikaa wakiniangalia, wameshika kalamu zao na vitabu vyao tayari kuandika.

Nilitangaza kuwa: ‘Nitakwenda kuanzisha na kuongoza Msikiti mpya ndani ya jiji la New York, na utaitwa Muslim Mosque Inc(Msikiti wa Waislamu, Inc.” Hilo lingetupa msingi wa kidini na nguvu ya kiroho ambayo ni muhimu ili kuondoa mambo yanayoharibu maadili ya watu katika jamii yetu.

“Msikiti wa Waislamu, Inc utakuwa na makao yake makuu kwa muda kwenye hoteli ya Theresa, katika Harlem. Utakuwa ndiyo kambi kwa ajili ya harakati za kutokomeza ukandamizaji wa kisiasa, unyonyaji wa kiuchumi na mmomonyoko wa kijamii ambao kila siku unawakabili watu weusi milioni ishirini na mbili wa Marekani.” Baada ya hayo waandishi wa habari wakaanza kuniporomoshea maswali.

***

Haikuwa rahisi kama ninavyosimulia. Nilitembelea mara nyingi nilitembelea maeneo mbalimbali huku nikiwaza kuwa baadhi ndugu zangu wa zamani walikuwa na mawazo kuwa wataonekana mashujaa ndani ya Taifa la Kiislamu iwapo wataniua. Nilifahamu fikra za wafuasi wa Elijah Muhammad; niliwafundisha wengi jinsi ya kufikiri. Nilifahamu vyema kuwa hakuna mtu anayeweza kukuua haraka kuliko Muislamu iwapo atahisi kuwa hilo ndilo Allah anamtaka afanye.

Kulikuwa na jambo lingine kubwa nililotakiwa kufanya. Nilikuwa nalo kichwani kwa muda mrefu sana nikiwa kama mtumishi wa Allah. Lakini lilihitaji pesa ambazo sikuwa nazo. Nilipanda ndege hadi Boston. Kwa mara nyingine nilimgeukia dada yangu Ella. Japo kuna nyakati nilimkasirisha Ella toka nitoke Michigan nikiwa kijana mshamba, lakini Ella hajawahi kutoka karibu yangu.

“Ella,” nilisema, “Ninataka kwenda Mecca kuhiji.” Ella alisema, “Unahitaji kiasi gani?”

Mwisho wa sura ya 16​
 
Back
Top Bottom