Kitabu: Simba wa Tsavo

Kitabu: Simba wa Tsavo

SURA YA IX

KUMALIZIKA KWA DARAJA YA MTO WA TSAVO

WASIWASI WOTE ulipotuondokea pakawa hapana tena shaka juu ya simba, kazi iliendelea upesi mno, na daraja ya Tsavo ikawa karibu kumalizika. Katika kujenga misingi, na nguzo zilipozidi kwenda juu, tukawa twafikiri namna ya kunyanyua yale mawe mazito na kuyapandisha juu. Hatukuwa na winchi (mashine ya kuyainulia), na kwa sababu hiyo nikashughulika kutengeneza majukwaa ya mataruma mawili ya reli yenye kimo cha futi thelathini thelathini. Mataruma haya, kwa juu yakafungwa pamoja na kwa chini yakatanuliwa kwa nafasi ya futi kumi kumi, tukayakita katika magogo makubwa ya miti. Hekima hii ilitufaa, nasi tukawa twapandisha yale mawe kwa kuvuta kamba katika roda, baada ya kuyafunga huku chini; naam baada ya muda mfupi tu tukamaliza kazi yetu ya kujenga.

Kazi yetu ya pili ikawa ni kupima urefu ule tuutakao wa futi sitini kati ya nguzo kwa boriti za chuma. Kwa kuwa sikuwa na winchi wala magogo ya kutosha kuvutia boriti za chuma na kuzilaza sawasawa, nikapata fahamu za kutengeneza nguzo za kujishikiza kati ya kila tao, zilizojengwa kwa magogo ya miti namna ya kihero. Zikachukuliwa boriti kubwa za miti zikalazwa toka huku kwenye nguzo za mawe mpaka kwenye vile vihero, halafu zikapangiliwa reli; kisha zile boriti za chuma zikavutwa juu sawasawa hali ya kuwa zimo katika mabehewa yake zilimoletewa kutoka Mombasa.

Kisha zikanyanyuliwa katika yale mabehewa, tukatekua zile nguzo na ile boriti ikateremka sawasawa taratibu. Ile boriti ya pili ilipokwisha wekwa tayari, hatukusubiri mara tukaanza kuunga reli, hapo tena nikawa na hamu mno ya kuona gari la moshi la kwanza likijaribu kupita juu ya daraja ile.

Ajabu niliyoona ni kuwa baada ya siku au mbili hivi tangu kumalizika ile daraja na kuondolewa ile mihimili ya katikati, ilinyesha mvua kubwa ajabu. Mto ukaanza kujaa upesi upesi nao mara ukafurika, maji yakawa mfano wa gharika, ukang'oa miti mizima mizima na kuibingirisha kama vitakataka. Mto ukazidi kujaa nami nalisimama juu ya daraja yangu mpya nikitazama daraja mbili ndogo ndogo za troli tulizozijenga kwa sababu ya kutuletea mawe na mchanga kama zitasalimika au vipi. Kutahamaki nikaona zege la mataruma ya reli na ghasia nyingine ambazo nilijua ni troli vikipitishwa yosa yosa kwenye gurufa ya mto kwa mbali kidogo. Kuona hivyo nikadhani kuwa pengine ni troli inavuka kwa juu. Ilivyokuwa, nikaona inazidi kuja kule nilikokuwa nayo imejaa maji tele kabisa. Moyo wangu ulishtuka kidogo nilipoona daraja ya pili nayo ikikumbwa nalisikia mshindo mkubwa ajabu, kumbe ni mbao zikibabaduliwa na kuvunjwa, hizo zikaelemezwa upande wangu, kusiachwe hata alama ya daraja. Mkumbo huo hakika ulikuwa mkubwa kwani hata zile reli zilipondekapondeka kwa kunyongwa na mashina ya gogo ya miti kama kwamba ni nyuzi za simu.

Ghasia zote hizo za daraja hizo mbili zikawa zinachukuliwa na maji kwa kasi na kugongana na zile nguzo za daraja kubwa. Ama nalifadhaika sana bali kwa tumaini la moyoni juu ya kazi niliyofanya, hakika nikaona daraja yangu salama, na mara nikaona ghasia nyingine za zile daraja zilizokumbwa zikipitishwa kati ya matao ya nguzo na kwenda kwa kasi kabisa wa moja mpaka baharini.

Naam, naliyashuhudia hayo yakitendeka hali moyo umejaa furaha kabisa kwa kazi yangu njema niliyoifanya. Hatukukaa sana mara tukaingiliwa na vituko vingine Tsavo. Kwani ingawa tulisalimika na simba, sasa tunahangaishwa na chui, mafisi, mbwa wa mwitu, shume, na wanyama wengine wengi wa mwituni. Wanyama hawa walitutia hasara nyingi juu ya makundi ya kondoo na mbuzi waliokuwa wamefugwa kwa ajili ya maziwa na kitoweo. na watu walikuwa wakifurahi mno kama mmoja wao atanaswa mtegoni.

Katika wanyama wasumbufu, chui ametia shani kwani yeye haui kwa sababu ya kutaka kula bali kiasi cha mchezo tu: nami nalikuwa na chuki nao mno tangu siku ile yule mmoja alipokuja usiku akaua kundi zima. Wakati ule wanyama wangu walitimu kadiri ya thelathini wa kila aina ambao naliwafuga kwa ajili ya maziwa na kwa sababu ya kitoweo, wamefungiwa katika kibanda kimoja cha nyasi kando kidogo ya boma langu.

Usiku mmoja tulifadhaishwa mno kwa ghasia nyingi humo kibandani, bali kwa kuwa wakati ule ulikuwa kabla ya nyamaume hawajauawa, hakuna aliyethubutu kutoka kuangalia sababu ya udhia huo. Basi palipita muda mrefu kabla ya vituko vyote havijamalizika kabisa. Nilipotoka kwenda kule kibandani kutazama yaliyotokea, maskini, nikaona si mbuzi wala si kondoo, kila mmoja amenyooka twaa, mkavu wa juzi na kutazama tena nikaona hakuna aliyeliwa ila kukatwa kooni tu. Katika kuzidi kuangalia nikaona kuwa kile kibanda kilitobolewa tundu pana, na kwa ishara ya nyayo zilizoenea pale pote nikajua kuwa hakuna mnyama mwingine ila chui. Kwa jeuri yake hakuna hata mnyama mmoja aliyemla, ila wote aliwauma na kuwaua tu, kiasi cha kufurahisha moyo wake.

Nikatumai kuwa bila ya shaka, usiku atarudi kuja kula nyama zake. Kwa sababu ya dhana hiyo ile mizoga nikaiacha vile vile ilivyolala, nikatafuta mtego madhubuti wa chuma uwezao kumzuia chui hodari, nikautia mle kibandani nikaufunga kwa mnyororo mrefu wa kutosha kuburutika hata nje. Tukakaa kimya kabisa mle bomani mwangu, giza likaanza kufungamana, tukawa twasikiliza chui apige kelele atakapokuwa ameshikwa na mtego mle kibandani. Katikati ya usiku tukasikia mchupo wa nguvu na papo hapo tukasikia mlio wa hasira na kuchugachuga. Wakati wote huo nalikuwa nimekaa na bunduki yangu tayari pamoja na taa ikiwaka, nami kusikia hivyo nikatoka upesi huku nimeandamiwa na askari wangu mmoja amechukua ile taa.

Kiasi cha kukikabili kile kibanda, yule chui akaturukia kwa ghadhabu kiasi cha urefu wa ule mnyororo, hivi yule askari akaogopa mno akakimbia pamoja na ile taa akaniacha gizani kabisa. Giza la usiku huo lilikuwa zito mno kama la usiku wa jana nami sikuweza kuona chochote; walakini nalijua upande gani wa kupigia bunduki, nami kiasi cha kuielekeza ikanitoka risasi.

Kwa kiasi nilichoweza kuona, nalimwona akichugachuga nje na ndani mle bandani. Nikapiga kelele kuwaambia watu kuwa nimemwua, nao wote wakatoka nje pamoja na taa zote wakaja nazo. Akaja msimamizi wangu mmoja wa Kihindi, naye pia akasema kuwa atataka kujilipiza kisasi kwa kuwa baadhi ya mbuzi wengine walikuwa wake. Papo hapo akachomoa bastola yake akamwelekeza nayo yule chui hali amekwisha kufa, akafunga macho, akammiminia risasi nne mara moja. Hakuna hata moja iliyompiga mnyama yule bali aliwatisha wenzake waliokuwa wakitazama na mara hiyo wakatawanyika huko na huko. Asubuhi yake, kwa bahati pakapita kikosi cha Wakamba, ambao sina shaka walishikwa mno na njaa, wakanishauri niwape ruhusa ya kumchuna, wao wapate kuchukua ile nyama yake. Kwa kweli sikusita kuwapa ruhusa na kwa muda wa dakika chache ngozi ikawa imekwisha chunwa tena vizuri kabisa, kisha wao wenyewe wakaanza kunyang’anyana ile nyama.

1631202473376.png
 
SURA YA X

BAHATI YA KUGUNDUA MASKANI YA NYAMAUME

KUSINI-MAGHARIBI ya Tsavo kulikuwa na magenge ya miamba niliyokuwa na hamu sana kwenda kuyatembelea, ikatukia siku moja kazi iliposimama kwa sababu ya upungufu wa vifaa, tukatoka mimi na Mahina, pamoja na kuli mmoja wa Kipanjabi aliyejiita Moota(yaani, mnene). Kwanza katika kuzungukazunguka kwangu kando ya pale mjini nikaona kuwa naweza kufuata upande wowote kwa kupita katika chochoro za wanyama nilizokuwa nimezichungua vizuri wakati ule nilipokuwa nikienda. Kwa maarifa haya niliyoyatunga, tukapata bahati ya kuona njia ya kifaru inayokwenda upande ule ule tuuendao sisi na kwa hiyo ikaturahisishia safari yetu. Tulipozidi kuendelea na safari yetu katika changarawe za mchanga, nikaona ule mchanga kwa ndani, kila palioweza kufikiwa na mwanga wa jua, pameremeta. Bongo langu likanipiga kuwaza labda ni mchanga wa vito vya thamani, na kwa kuwa mahali penyewe palishabihi namna zote za vito vya thamani, nikachomoa shembea langu nikaanza kuchimba kwa tamaa. Baada ya kuchimba kidogo, nikatoa kitu kilichofanana kabisa na almasi kwa kumeremeta kwake: urefu wake ulipata nusu inchi, na pembe zake zilionyesha kama kwamba zilikatwa na fundi wa Amsterdam. Pia nisikubali, nikaichukua kujaribu kuandika juu ya kioo changu cha saa, nikaona yakata vizuri bila kukwaruza, na ingawa huenda zamaradi nayo ikaweza kukata kama vile bali umbo lake haikuonyesha mfano wa zamaradi yoyote niliyopata kuiona. Kwa kitambo cha dakika au mbili hivi nikawa katika matumaini makubwa ya kugundua mashimo ya almasi; ajabu, katika kuzidi kuitazamatazama mno na kuijaribu matumizi yake nikadhihirikiwa kuwa kiokosi changu si almasi kweli, ingawa haifanani na vito vingine nilivyopata kuviona.

Nilipoona kuwa tumaini langu la kuwa tajiri wa mara moja halikuwa, tukaendelea na safari yetu, tukazidi kuingia ndani msituni. Tulipoendelea mbele kidogo nikaona tawi lililovunjika na mbele yake amesimama mzee faru mahali peupe karibu na ukingo wa genge. Hatukuwa na bahati, yeye upesi akatuona, akavuta pua yake kwa nguvu na papo hapo akatumwagia vumbi akipenya katika vichochoro vyao. Nilipokuwa nikilifuata genge hili kushotoni kwangu nikagundua mchanga wa changarawe kidogo uliendelea kutokeza nje, kumbe ni mkondo wa handaki kubwa uliopita katikati ya msitu na mitambaazi. Nikaona upenyo mzuri, yumkini ni njia maalum ya faru na kiboko, nikaazimia kuuingia nikatazame yaliyo huko mbele. Kabla sijavuka hatua kubwa nikafika mahali penye hori kubwa iliyochimbwa na mafuriko ya mto, niliona nyayo za wanyama kadha wa kadha wa aina mbalimbali. Katika pembe moja karibu kwa chini ya jiti moja lenye matawi mengi, palikuwa na kichuguu cha mchanga, na nilipotazama mbele yake nikaona pango moja kubwa la kutisha lililokwenda ndani chini chini katika genge la mwamba. Pale langoni pa kuingilia na humo ndani ya pango lenyewe nalishtuka mno kuona mifupa ya wanadamu na mavazi yaliyovaliwa na wenyeji wa nchi vimetapakaa kila mahali. Nikashuku kuwa bila ya shaka ndilo pango la wale nyamaume! Yanipasa kusema kuwa ni bahati tu iliyonifanya kugundua maskani ya nduli hawa walionihangaisha siku kadha wa kadha nikiwasaka katika misitu na vichaka wakati walipokuwa wakitusumbua kule Tsavo. Kwa kweli sikuwa na moyo wa kuingia ndani zaidi, bali kwa shaka kuwa huenda mkawa na simba jike au mtoto aliyebaki, nikapiga bunduki mara mbili mle ndani katika tundu kwa huku na huku juu ya jabali. Zaidi ya popo, hakuna kitu kilichotoka; nami baada ya kupiga picha lile pango, nikashukuru kuondoka mahali pale pa hatari salama u salimini, kadhalika nikashukuru kuwa habithi wale waliokuwa wakikaa humu sasa hawako tena duniani.

MWISHO
 
Safi sana... Bonge la story...

Chapter Closed...
 
SURA YA IV

RABSHA NA WAFANYAJI KAZI

NI KWELI, kwamba kujengeka kwa Daraja ya Tsavo hakukuwa kwa raha. Nimekwisha eleza mashaka yetu yaliyokuwa yametupata juu ya simba; ilivyokuwa, hapakupita muda tangu tuondokewe na baa la simba, pakazuka baa jingine adhimu jipya la wafanyaji kazi.

Baada ya kwisha kulipata jiwe la kusimamishia daraja, nikaagiza mafundi waashi Mombasa kuja kulichonga na kufanya kazi ile. Watu nilioletewa kwa kazi hiyo baadhi yao wengi walikuwa Mapatani nao ndio waliodhaniwa kuwa mafundi stadi; katika kufanya kazi kwao nikagundua kuwa wengi wao hawakuwa wakijua namna ya kuchonga mawe, ila walikuwa vibarua tu waliojitia ufundi ili wapate mshahara wa ufundi badala ya ujira wa ukibarua. Kwa kuligundua jambo hili mara nikaanzisha mtindo mpya wa kufanya kila mtu peke yake, nikapanga taratibu za mishahara ili aliye fundi wa kweli apate haki yake pengine na zaidi kama akistahili na kukata mishahara ya wale waliojitia ufundi nao ni vibarua tu. Sasa basi, kama ilivyo katika ulimwengu wetu huu, wale vibarua wadanganyifu walikuwa wengi mno kupita mafundi wa kweli, na kwa wingi wao wakajaribu kuwatisha wenzao wajilegeze ili wawe nao katika hali moja ili nami nipate kuondoa mpango huu wa kazi ya kila mtu peke yake juu ya mishahara kwa hayo sikukubali kwani naliona mtindo huo ni wa haki juu ya kufanya kazi kwa kila mmoja.

Hata siku moja nilipofika kule maweni, niliona mambo yote yanakwenda barabara bila ya upungufu, wala hapakuonyesha ishara yoyote ya udhia. Watu wote, kila mmoja alikuwa akishughulika na kazi yake, bali punde kidogo, kwa kuona wakikonyezana, nikang'amua kuwa mambo hayajatulia asawa. Nilipokabili genge la kwanza la wafanyaji kazi, jemadari wao, mtu mmoja ayari hivi, akanishtakia kuwa watu wafanyao kazi juu gengeni wamekataa kusikiliza amri yake na kwa hiyo ananitaka niende nikaonane nao mwenyewe. Papo hapo nikafahamu kuwa ile ni hila ya kunitega mimi ili nikifika katikati ya lile genge wapate kunizingira mbele na nyuma nisipate pa kutokea. Lakini hata hivyo nikapiga moyo konde, na kwamba yote yatakayonizukia haidhuru bali mradi nitakwenda nikaone yatakayokuwa. Hivyo nikaandamana na yule jemadari katika lile genge. Tulipofika kwenye genge la pili la wafanyaji kazi, nikamwona anatangulia upesi mbele, ati kunionyesha wale watu aliosema wamekataa kutii amri yake-nikashuku kwamba moyoni mwake alidhani kuwa sitaondoka mahali pale salama. Nikaandika majina yao katika kitabu changu kidogo kisha nikageuka kurudi mahali pangu. Punde ukapigwa ukelele wa kupandisha watu umori, kiasi cha watu sitini hivi, ukajibiwa na wale wenzao wa kwanza niliowapita kadiri ya mia moja hivi. Kila mtu alishika mtaimbo au nyundo, kisha wakanisonga katikati. Mimi nikasimama kimya na papo hapo mmoja wao akanijia, akanishika mikono yangu yote miwili akiwapigia kelele wenziwe kuwa 'atanyongwa na kuuawa kwa bunduki kwa sababu yangu'. Nikamkutua kwa nguvu kutoa mikono yangu nikamsukumilia mbali; bali nilipotazama nikaona hakika nimezingirwa na watu ambao kila mmoja uso wake umembadilika kwa umori wa kutaka kuniua. Lilikuwapo jitu moja ambaye alimsukumiza mwenziwe aliyekuwa naye jirani, na kwa kweli angaliniangukia. Ilivyokuwa basi, naliwahi upesi kunyaguka kando, hivyo yule mtu aliyedhamiriwa kunikumba, alijipiga penye mwamba.

Jambo hili kidogo lilileta vurugu ambayo mimi nalipata nafasi kidogo. Upesi nalirukia juu ya jiwe, na kabla hawajajiweka tayari tena nikawahi kuwakemea kwa Kihindustani. Mara wakatulia kusikiliza niliyokuwa nikitaka kuwaambia, nikawahubiria kuwa nimefahamikiwa na njama yao waliyoiunga kutaka kuniua, na kwamba hakika wanaweza kufanya hivyo wakitaka; walakini, katika kuniua kwao wengi wao wangenyongwa, kwani Serikali upesi ingegundua kweli na hivyo uongo wao wa kusingizia kuliwa na simba ungejulikana. Nikazidi kuwaambia kuwa nafahamikiwa mno kwamba ni mtu mmoja au wawili hivi waliowatia nia ya kijinga kama hiyo nikawakanya kuwa wasikubali kutiwa ujinga wa namna hiyo. Nikaendelea kuwaambia kuwa hata kama watatimiza nia yao ya kuniua, lakini atakuja Bwana mwingine kuwasimamia na je, sivyo pengine atakuwa mkali zaidi kunipita? Hapo kila mmoja akakiri moyoni mwake kuwa hakika mimi sikuwa na nia mbaya nao ila haja yangu ni kutaka haki kwa kila mmoja. Kiasi cha kuwaona kuwa wamekubali kunisikiliza hapo kidogo nikajiona katika hali ya salama, nami kwa sababu hiyo nikaendelea kuwaambia kwamba wale wasiokubali kuendelea na kazi watapewa ruhusa ya kurudi Mombasa, na ya kuwa wale watakaobaki, wakihiari kuendelea na kazi yao bila ya manung'uniko yoyote, upuuzi wao waliokwisha fanya sitautia maanani tena. Mwishowe nikawaambia kuwa kila aliyekubali kuendelea na kazi anyoshe mkono wake juu, hapo karibu wote wakainyosha mikono. Kwa wakati huo nikaona kuwa nimefaulu kuwatiisha kidogo na baada ya kuwapa ruhusa, nikashuka pale juu ya jiwe nikaendelea kutazamatazama kazi kama kwamba hapakutukia lolote nikijitia kupima jiwe hili na hili na kujaribu kutoa makosa baadhi ya kazi zilizofanywa, na baada ya kitambo cha saa moja nikarudi zangu Tsavo, salama u salimini.

Lakini baadaye nikaarifiwa kuwa matata hayajakwisha kabisa, basi nikapiga simu kwa askari polisi ya reli. Baada ya muda muda wa siku mbili tatu, askari wakafika, wakawakamata ale waliokuwa viongozi wa uasi ule wakapelekwa Mombasa, na huko wakahukumiwa na Bwana Crawford, Balozi wa Kiingereza.
Huyu mwandishi anayefokea wafanyakazi kwa lugha ya ki Hindustan yeye ni mtu wa wapi?? Najua Kenya kwa kina MK254 ndugu yangu wa kihisia wao walikuwa ni koloni la Mwingereza ndio maana balozi wa Uingereza ndiye aliyewahukumu vibarua wahaini
 
Umenikumbusha utotoni kwa kweli. Asante sana.
 
Niliwahi kusoma kitabu hiki utotoni, woga ulionipata mpaka leo sipendi kukaa gizani
 
Nacho jiuliza hao Wahindu walishindwa kulala na majambia na mikuki ili Simba akiwa vamia wamshambulie?
 
Back
Top Bottom