RIGHT MARKER
Senior Member
- Apr 30, 2018
- 129
- 473
📖Mhadhara (72)✍️
Ni siku nyingi sana sikutembelea ofisi ya NHIF. Lakini jana nilikwenda kwenye ofisi ya NHIF kuchukua kadi ya Bima ya afya ya mtegemezi, nikaambiwa kuwa sasahivi mambo yamebadilika. Kwa sasa mtu mzima hapewi kadi ya Bima ya afya bali atatumia NIDA (NAMBA YA NIDA) kutibiwa hospitalini.
Kwa ufafanuzi zaidi ni kwamba ukiomba Bima ya afya na ikishahidhinishwa hupewi kadi, bali ukienda hospitalini utatumia NIDA (NAMBA YA NIDA). Kadi za Bima ya afya zinatolewa kwa watoto pekee.
Hongera sana kwa ofisi ya NHIF kwa hii hatua nzuri, na idara nyingine ambazo zinafanya kwa mtindo huo kwani inamsaidia mtu kutokutembea na mzigo mkubwa wa vitambulisho kwenye pochi yake.
Kupitia uzi huu napenda kuwashauri wananchi wenzangu waende kuchukua vitambulisho vyao vya NIDA kwenye ofisi walizojiandikisha kwasababu kitambulisho cha NIDA ni muhimu sana kwenye mambo mbalimbali.
Vitambulisho vya NIDA vya Wananchi wengi vimetoka na vimepelekwa maeneo husika lakini wananchi hawaendi kuchukua vitambulisho vyao. Ukienda kwenye ofisi za maafisa watendaji wa mtaa/kata utakuta vitambulisho ni vingi sana vimekaa muda mrefu mpaka vinachakaa, nendeni mkachukue vitambulisho vyenu vya NIDA.
RIGHT MARKER,
DAR ES SALAAM.