Kitanda cha Semadari

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KITANDA CHA SEMADARI
Picha hiyo hapo chini ni picha ya kitanda ambacho nimeamka leo asubuhi.
Jana usiku nilipopanda kulala sikukiangalia vizuri kwa mchoko wa safari.

Kitanda cha semadari nimekilalia miaka 70 iliyopita Mtaa wa Kipata katika nyumba ya makuti juu na chini hakuna sakafu ila ni ardhi yenyewe.

Sihitaji kukueleza zaidi kwani naamini umenielewa.
Kitanda cha semadari kikapotea kwa miaka mingi.

Hakuna mtu anaelalia kitanda hiki siku hizi.

Naambiwa hivi sasa kitanda hiki Semadari kimekuwa kitanda cha thamani kubwa kinachowekwa katika mahoteli makubwa kuvutia wateja.

Samadari siyo 'Semadari' bhana!
 
We mzeee hichoo kitandaaa umesahau kusema kiligunduliwa na waislam...... hata hata selemara ni muislamu..... pia sema kitanda hii akilala mtu sio muislam kina mtupa chini....... maaana ww mzee tushakuzoea kila kitu waislam
 
Hiki nacho pia ni mfano wake tu.Kimechongwa na miti ya karibuni.
Semadari nilichokiona kwa bibi yangu kinakuwa na picha za tausi au mauwa kwenye kioo
 
Ashampoo...
Hakika Waislam wana historia ya pekee kuanzia enzi za Germany Ostafrika hadi kufika Tanganyika na leo Tanzania.

Angalia video hiyo hapo chini:

View: https://youtu.be/93_HwHT0HMU?si=oge2VbjqSyAaicEb
 
Hiki nacho pia ni mfano wake tu.Kimechongwa na miti ya karibuni.
Semadari nilichokiona kwa bibi yangu kinakuwa na picha za tausi au mauwa kwenye kioo
Uko sahihi kabisa vile halisi kabisa vina picha ya tausi ndege kule Tanga kwenye jamii za wadigo wale wa ndani ndani bado wanavyo vile
 
Mzee Mohamed Said, nimevutiwa sana na kitanda hiki. Natamani kusikia mnakiuza, my bid is 5m. Nakuja inbox.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…