Kitanda cha Semadari

Mzee wangu nakiomba bure usafiri nitagharamika
 
Hongera Mzee Leo umeandika bila kuweka udini
Uzalendo...
Udini uko wapi?

Kuandika historia ya kweli na kueleza mchango wa Waislam katika kupigania uhuru wa Tanganyika ndiyo udini?

Je, kule kufuta historia ya Abdul Sykes na baba yake, Sheikh Hassan bin Ameir, Sheikh Suleiman Takadir na wengine wengi mfano wa hao katika historia ya Tanganyika ndiyo si udini?

Ingekuwa naandika udini kitabu cha Abdul Sykes kingekuwa katika Cambridge Journal of African History?
 
We mzeee hichoo kitandaaa umesahau kusema kiligunduliwa na waislam...... hata hata selemara ni muislamu..... pia sema kitanda hii akilala mtu sio muislam kina mtupa chini....... maaana ww mzee tushakuzoea kila kitu waislam
Mdini sana huyu
 
Mdini sana huyu
Otoro...
Sijasahau nilikuwa nina hakika hili halihitaji kuelezwa kwa kuwa liko bayana sana.

Hiyo ndiyo sababu sikusema kuwa waliokuwa wakichonga vitanda hivyo ni Waislam na waliokuwa wakivilalia ni Waislam.

Kwani leo nikikutajia majina ya walioasisi African Association 1929 na Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika 1933 majina yao yatakushangaza?
 
Mohamed Said asante sana nimekuona kwenye Interview yako ya "Uncensored"

Ukiongelea Mapinduzi ya Zanzibar nimefurahi sana.
 
Basi nilipokuona kwenye ile video sikuamini kama ndio wewe naye kusoma hapa JFs.

Hakika wewe mzee ni hazina.
Bush...
Naweka link ya hiyo video wengine hapa na wao waione.

Hadi hivi tunapozungumza imetizamwa na watu 69,000 (69K).
 
Uzuri wako unaandika historia ya kweli iliyofichwa kwa makusudi. Vijana wanaosema wewe mdini wanahitaji kujitafakari zaidi. Huwezi kuutenganisha uislamu na historia ya kupigania uhuru wa Tanganyika.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…