- Thread starter
-
- #21
Kwenye upishi shida yetu wengi ni muda. Tunadhani hatuwezi kupika kwa sababu tuko busy etc. Ili kuweza kupika vizuri na haraka unahitaji haya:
1 wekeza kwenye gadgets. Jiko zuri, kisu kikali (hii ni must kwangu), sijui peeler, veggie chopper, dough maker, pressure cooker etc.
2 vitunguu swaumu nunua vingi, menya na kutwanga na chumvi kisha weka kwenye chupa ya kioo ambayo inafunga tightly. Chupa iliyokuwa na mayonnaise inafaa zaidi
3nunua green groceries kwa wingi na osha zote na kukausha maji (unaweza kuzilaza kwenye strainer hadi asubuhi) kisha panga kwenye friji. Wakati wa kupika ukishaosha mikono yako huhitaji kuosha kila kitu upya. You chop and throw into the steaming pot
4mi napenda nazi ya kiswahili. Nunua nazi nyingi kama zinapatikana ulipo. Kuna zote zikiwa fresh na weka kwenye freezer kwa kugawa portions ndogo. Unaweza kutumia film ya kufunikia chakula ama mifuko laini
Hapo no 2....waweza saga vitunguu pamoja na giligilini (coriander) then ukahifadhi ndani ya friji....
Kwa vile giligilani zinaharibika mapema so hapo utakua umeshaihifadhi vizuri ili kuepuka kutupa na kununua nyengine...