Mkutano ufuatao ulifunguliwa na Mwl.Nyerere: Utamaduni wa siasa na hatima ya demokrasia Tanzania
Vitabu vifuatavyo vinaelezea hayo:
Utamaduni wa siasa na hatima ya demokrasia Tanzania. By: Rwekaza S Mukandala Samuel S. Mushi and Saida Yahya-Othman (Editors). 2000.
Kitabu hiki na mkusanyiko wa mada zilizotolewa katika mkutano wa sita wa hali ya siasa Tanzania uliofanyika katika chuo kikuu cha Dar esSalaam Julai 1998. Mkutano huo ambao ulifunguliwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, ulijadili na kuchambua utamaduni wa siasa na hatima ya demokrasia Tanzania. Kitabu hiki chenye kurasa 185, ni mchango muhimu ambao utawasaidia wanasiasa, watafiti, wasomi, wanafunzi na watu wa kawaida kuelewa mwelekeo wa siasa ya Tanzania.
Pia kipo kitabu cha: Ujenzi wa Uwezo wa Tanzania by: Rwekaza S Mukandala na Joshua S. Madumulla. (Editors). 2000.