Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
Baada ya uhuru mwaka wa 1961 palizuka hofu kubwa sana ya kuogopa Uislam na Waislam Tanganyika.
Mwaka wa 1963 ndani ya kikao cha Halmashauri Kuu ya TANU Ukumbi wa Karimjee palizuka ugomvi kati ya Bibi Titi Mohamed na Julius Nyerere kuhusu EAMWS.
Haukupita muda mrefu Baraza la Wazee wa TANU chini ya Mwenyekiti Iddi Tulio likavunjwa kwa shutuma za kuchanganya dini na siasa.
Mwaka huo huo wa 1963 pakaenea uvumi kuwa serikali inataka kuivunja EAMWS.
Uvumi huu ulimalizwa na mkutano wa pili wa Muslim Congress mwaka wa 1963 chini ya EAMWS uliofanyika Aga Khan Girls School pale Bilali Rehani Waikela alipotoa risala kali kwa Mwalimu Nyerere akionya kujitokeza kwa chokochoko za chinichini dhidi ya Waislam.
Juu ya haya yote serikali iliivunja EAMWS na kuunda BAKWATA mwaka wa 1968.
Soma hapo chini historia hii ya BAKWATA na Augustino Mrema:
"Baada ya miaka mingi ya Waislam kuisusia BAKWATA ikafika mahali ikawa inashindwa hata kufanya mikutano ya uchaguzi wa viongozi kwa mujibu wa katiba yake.
Kwa hali kama hiyo ilikuwa kwa Msajili wa Vyama kuivunja BAKWATA.
Serikali ilipoona imekabiliwa na hali hiyo ikachukua jukumu la kutayarisha mkutano ili kuihuisha BAKWATA.
Tarehe 28 Aprili 1993 Waziri wa Mambo ya Ndani na Makamo Waziri Mkuu Augustine Mrema aliitisha mkutano kati ya Waislam na Wakristo katika Ukumbi wa Diamond Jubilee Hall, Dar es Salaam.
Mkutano ulikuwa hauna agenda.
Kanisa lilipeleka ujumbe wa hali ya juu kabisa.
Waislam hawakutokea isipokuwa BAKWATA.
Katika mkutano ule Mrema alieleza kuwa uchaguzi katika BAKWATA umechelewa sana kwa kukosa fedha.
Kanisa paleplale lilijitolea fedha kuipa BAKWATA ili ifanye uchaguzi wake.
Halikadhalika Mrema alisaidia kukusanya fedha kutoka kwa wafanyabiashara kwa ajili ya uchaguzi wa BAKWATA.
Mkutano ulifanyika Dodoma tarehe 10th -12th Mei.
Badala ya kufanya uchaguzi BAKWATA ilirekebisha katiba yake ili iweze kumpa ruhusa Sheikh Mkuu wa BAKWATA haki ya kufukuza na kumweka katika uongozi au kumtoa mtu yeyote bila ya kipingamizi."
(Kutoka kitabu, "Maisha na Nyakati za Abdulwahid Sykes (1924 - 1968...").