Nga...
Kuandika na kuzungumza mambo yenye kuongeza elimu katika jamii na ulimwengu hakuui mtu.
Ingekuwa kunatoa uhai mimi ningeshakuwa marehemu miaka mingi iliyopita.
Zaidi kalamu yangu imenipa manufaa makubwa maishani.
Leo nikiweka video ya somo lolote lile ''viewers'' wanafika 80K.
Vyombo vya habari binafsi na umma vinapishana kizingitini kwangu kutaka mahojiano na mimi.
Vijana wadogo waandishi ambao ndiyo wanaanza kazi wamekuwa wapenzi wangu wakubwa na huchekeshana sana katika mahojiano.
Namuuliza ushasoma DOT Command.
Blank face.
Hajui nazungumza kitu gani.
Ananiuliza mchango wa Bibi Titi katika kupigania uhuru wa Tanganyika.
Jibu langu nampa swali.
''Umepata kumsoma Schneider Plantan katika historia ya uhuru?''
''Mjerumani huyu?''
Ananiuliza kwa mshangao.
''Hapana Mzulu huyu jina lake Schneider Abdillah Plantan.''
Tukimaliza ananiambia, ''Mzee Mohamed una madini sana.''
Tunacheka sote.
''Nikuoneshe picha zangu za ujana?''
Sasa vicheko vinaongozeka mpiga picha kesha maliza kazi yuko ''relaxed'' na yeye sasa anaingia katika mazungumzo anacheka.