SoC01 Kitendawili cha Katiba ya Wananchi - Tanzania

Stories of Change - 2021 Competition

Emekha Ikhe

Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
43
Reaction score
62
MALENGO YA ANDIKO-KITENDAWILI CHA KATIBA YA WANANCHI

Andiko hili la kitafiti na linganishi kwa nchi ya Afrika Kusini limelenga kutoa uelewa mpana juu ya Safari ya Mchakato wa Upatiakanaji wa Katiba ya Wananchi Tanzania, Changamoto zake na namna ya kutegua kitendawili cha Upatikanaji wa Katiba ya Wananchi. Kwa Ujumla, andiko hili limelenga kutoa maoni ya kutatua baadhi ya vitendawili dhidi ya Kujikwamua na Mkwamo wa Kupata katiba ya Wananchi.​

UTANGULIZI-UELEWA

Wananchi wanapaswa kuelewa na Kuelimishwa juu ya nani anamamlaka na nini haswa katika masuala ya kuamua juu ya Sheria zinazopaswa kuongoza Taifa. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,1977 imeweka msingi mama kwamba; wananchi ndio msingi wa Mamlaka yote, na Serikali itapata Madaraka na Mamlaka yake yote kutoka kwa wananchi kwa mujibu wa Katiba hii .

Tafsiri ya Ibara hii kwa lugha nyepesi ni kwamba, Katiba imeweka Msingi mama kuwa Wananchi ndio Watuma/Mabosi/Waajiri wa Viongozi wa Nchi hii Kuanzia nafasi ya Urais, Uwaziri, Ubunge, Udiwani, Serikali za Mitaa nk.., inatafsiri kwamba kiongozi bila kujali cheo chake ni Mtumwa wa Wananchi hivyo anapaswa kutekeleza matakwa ya Wananchi na Si Vinginevyo.

Katiba sio takwa la Watawala/Viongozi ni takwa la Wananchi, kwa Msingi huo, tuendeleze mapambano ya Kuelimisha Wananchi kuchukua hatua na kuwashawishi walio madarakani kuhusu Umuhimu wa Kupata Katiba ya Wananchi.​

HISTORIA FUPI YA MCHAKATO WA KATIBA MPYA 2010-2021

Historia ya Kupigania Katiba ya Wananchi na Tume Huru ya Uchaguzi nchini ilianza hata kabla ya Mfumo wa Vyama Vingi Vya Siasa(1990’s), Rasmi, Tar,31.12.2010 kwa mara ya kwanza katika historia ya kupigania Katiba ya Wananchi, aliyekuwa Rais wa awamu ya nne wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk.Jakaya Mrisho Kikwete baada ya joto kubwa Kutoka kwa Wananchi na Wadau wa Katiba alitangaza nia ya Serikali kuanzisha Mchakato wa Katiba Mpya. Mwaka 2011, Mchakato wa kutungwa kwa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba Na. 83/2011 uliratibiwa na baadaye kufuatiwa na Sheria ya Kura ya Maoni Na. 11/2013.

Kwa Mujibu wa Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, ilianzisha Vyombo vikuu Vitatu, Mosi, Tume ya Mabadiliko ya Katiba kama chombo cha uratibu wa mchakato wa kukusanya maoni ya wananchi na kuandaa rasimu ya kwanza ya katiba, Rasimu ya Kwanza ya Katiba ilihaririwa na Mabaraza ya Katiba na hatimaye kupatikana kwa Rasimu ya Pili ya Katiba. Pili, Bunge Maalumu la Katiba ili kuboresha maoni ya Wananchi katika Rasimu ya Pili ya Katiba, Tatu, Tume ya Uchaguzi (NEC) kama Chombo cha Kusimamia Kura ya Maoni dhidi ya Katiba Pendekezwa baada ya Bunge Maalumu la Katiba.

MCHAKATO WA KATIBA YA WANANCHI ULIPOINGIZWA GIZANI

(A) Bunge Maalumu la Katiba na Mapinduzi ya Maoni ya Wananchi

Dhambi ya Kuua ndoto ya Taifa kupitia Mchakato huu wa Katiba ya Wananchi ilianza baada ya Rasimu ya pili ya Katiba maarufu kama Katiba ya Warioba) ilipofikishwa katika Bunge Maalumu La Katiba. Rasimu ya Pili ya Katiba ya Wananchi ilipoka madaraka makubwa ya Watawala na kurejeshwa kwa Wananchi wenyewe na ilisheheni Mapendekezo ya Wananchi yaliyoakisi kiu ya wananchi juu ya namna ambavyo wanataka kuongozwa.

Baada ya Rasimu ya Pili kuwasilishwa kwenye Bunge Maalum la Katiba ambalo kwa kiasi kikubwa lilitawaliwa na Mvutano wa kisiasa, Mipasho na Vijembe baina ya wanasiasa waliotokana na Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi-Zanzibar. Wanasiasa Waliowengi Walibeba ajenda zenye Maslahi binafsi na ya Vyama Vyao na kusaliti maslahi mapana ya Taifa.

Kwa Mujibu wa Ripoti maalumu iliyotolewa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), 2018. Bunge Maalumu la Katiba Liliondoa Mapendekezo takribani 50 katika Vifungu Mbalimbali Vya Rasimu ya pili ya Katiba yaliyopendekezwa na Wananchi. kitu ambacho kilisababisha Mpasuko wa Wadau wa katiba ambapo Watetezi wa Maoni ya WananchI Wakajitoa kwenye Bunge Maalumu la Katiba na kuunda Umoja wa kutetea Katiba ya Wananchi (UKAWA ). Wajumbe waliobaki katika walipuuza madai ya UKAWA na hatimaye Mwezi Oktoba 2014 kuja na tokeo la Katiba Inayopendekezwa ambayo sio zao la muafaka wa wadau wa Katiba.

FUNZO NA NINI KIFANYIKE:

Bunge Maalumu la Katiba Halikuwa na Usawa wa Uwakilishi wa Wadau wa Katiba na Wanasiasa wa Vyama Vya Siasa hivyo kufanya wanasiasa wa chama tawala kwa uwingi wao kumeza vyama Vingine.

Bunge Maalumu la Katiba lifutwe na kuundwe Kamati Maalumu ya Kitaalam ambayo itawakilisha Makundi yote nchini kwa uwiano sawa na kwa kuzingatia jinsia na Kamati husika iongezwe Wataalam wa Masuala ya Sheria na Katiba.

(B) TUME YA UCHAGUZI (NEC) UFUTWE NA TUME HURU YA UCHAGUZI IUNDWE.

Sheria ya Kura ya Maoni (Referendum Act No. 11/2013) iliipa Mamlaka Tume ya Uchaguzi kuanzia tarehe 30 Aprili 2015 kuratibu kura ya maoni dhidi ya Katiba pendekezwa. Zoezi hili lilikwama kufanyika mpaka sasa. Swali kuu hapa ni kipi kianze kati ya kupigania Tume Huru Ya Uchaguzi au Katiba ya Wananchi?

Kufanikisha upatikanaji wa Tume Huru ya Uchaguzi ni kama kuandaa daraja imara la kupita kwa Katiba ya Wananchi, Kwa Kuwa Tume ya Uchaguzi ndio chombo chenye mamlaka ya kusimamia kura ya Maoni dhidi ya Katiba ya Wananchi, ni Muhimu Kutegua kitendawili hiki cha Upatikanaji wa Tume Huru ya Uchaguzi kama ilivyo Tume ya Uchaguzi nchini Afrika Kusini au Kuboresha Zaidi (Rejea hapo chini funzo Kutoka Afrika Kusini).​

FUNZO NA NINI KIFANYIKE;

Tume ya Uchaguzi ifutwe kwa Kuwa Muundo na Upatikanaji wa Watendaji wa Tume haupo huru na sio zao la muafaka wa wadau wa Uchaguzi.

Tuunde Tume Huru ya Uchaguzi itakayokuwa ni zao la Muafaka wa Wadau Mbali Mbali wa Uchaguzi ili isimamie Mchakato wa Upatikanaji wa Katiba (Rejea hapo chini juu ya Muundo wa Tume Huru ya Uchaguzi nchini Afrika Kusini).

NJIA PENDEKEZWA KUPATA KATIBA YA WANANCHI

1. Utoaji wa Elimu kwa Umma Juu ya Historia ya Mkwamo wa Mchakato wa Kupata katiba ya Wananchi, Changamoto zilizojitokeza na namna ya kujikwamua ili Kupata Katiba.

2. Maboresho ya Sheria zinazoongoza Mchakato wa Katiba i.e. Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na Sheria ya Kura ya Maoni ili kukidhi matakwa ya Uhitaji wa sasa

3. Kuanza na Rasimu ya Pili ya Katiba maarufu kama Katiba ya Warioba kwani ndio Msingi wa Maoni ya Wananchi.

4. Bunge Maalumu la Katiba lifutwe na Kuunda Kamati maalumu ya Kitaalamu ambayo itakuwa na Uwakilishi wa Makundi yote kwa uwiano sawa na kwa Kuzingatia Jinsia pamoja na wataalamu wa Katiba na Sheria.

5. Tume Ya Uchaguzi ifutwe na Kuundwa Kwa Tume Huru ya Uchaguzi ambayo itaratibu zoezi la kura ya maoni dhidi ya Katiba Pendekezwa baada ya Kamati maalumu ya Katiba kuboresha.

6. Kupigwa kura ya Maoni dhidi ya Katiba pendekezwa na Kupata Katiba ya Wananchi.

TUME YA UCHAGUZI NCHINI AFRIKA KUSINI

Tume ya Uchaguzi imeundwa chini ya Sura ya Tisa ya Katiba ya Afrika Kusini kama moja ya taasisi inayounga mkono demokrasia ya kikatiba. Sheria ya Tume ya Uchaguzi Na.51 ya 1996) . iliundwa kwa mujibu wa Katiba yao ili kuenzi demokrasia ya Uchaguzi. Jopo la Tume lina jumla ya wajumbe 5 (mmoja wao anasifa ya kuwa jaji) na Jopo hili la wataalamu lina Rais wa Mahakama ya Katiba na wawakilishi kutoka kwa taasisi zifuatazo; Tume ya Haki za Binadamu; Tume inayojishughulisha na Ulinzi wa Umma na na Usawa wa Kijinsia .

(A) UIDHINISHWAJI WA WAJUMBE WA TUME WALIOTEULIWA

Wajumbe wa Tume ya Uchaguzi Walioteuliwa na jopo hili la Wataalam (Panel of expertes) lazima waidhinishwe na kamati ya Bunge, iliyo na idadi sawa ya Vyama vyote vya siasa vinavyowakilishwa katika Bunge na pili, lazima waidhinishwe na azimio la wabunge wengi wa Bunge la Afrika Kusini.

(B) UWAJIBISHWAJI WA MAKAMISHNA WA TUME YA UCHAGUZI

Huondolewa na Rais kwa sababu ya utovu wa nidhamu endapo ikigunduliwa na kamati ya Bunge ambayo inauwakilishi sawa wa Vyama Vya siasa vilivyopo Bungeni au pendekezo la Mahakama ya Uchaguzi. Uondoaji lazima uidhinishwe na wajumbe wengi wa Bunge la Afrika kusini.

(C) UWAJIBIKAJI WA TUME YA UCHAGUZI-AFRIKA KUSINI

Tume ya Uchaguzi haiwajibiki kwa Rais au Kamati ya Wataalamu, bali inawajibika moja kwa moja kwa Bunge la Afrika Kusini.

FUNZO NA HITIMISHO LA NINI KIFANYIKE-TANZANIA

Ukilinganisha Muundo wa Tume Huru ya Uchaguzi baina ya Afrika Kusini na Tanzania kwa Utafiti huu umedhihirisha kwamba Tanzania bado ipo gizani katika Michakato ya kuenzi kanuni za Kidemokrasia na bado tupo katika Utawala wa Kifalme. Mamlaka yote ya Uteuzi na Uwajibikaji kwa Upande wa Tanzania yapo kwa Rais wa Nchi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama tawala.

Tanzania inapaswa kuiga au kuboresha zaidi mfumo wa hatua za kuwapata Wajumbe na Makamishina wa Tume Huru ya Uchaguzi, namna ya Uwajibikaji na Uwajibishwaji wa Wajumbe na Makamishna wa Tume ya Uchaguzi kama ilivyo Afrika Kusini, Rais hana mamlaka ya moja kwa moja ya Kuwawajibisha Makamishna na Makamishna hawawajibiki kwa Rais ila Kwa Kamati ya Bunge iliyo na Uwakilishi sawa wa Vyama vya siasa na Kwa Bunge zima.​
 
Upvote 104
Hakuna lisilowezekana chini ya jua kama wanasiasa wangeacha ubinafsi pembeni na kutanguliza maslahi mapana ya nchi mbele. Ifahamike kwamba watawala watakuja na kupita ila taifa litabaki! Katiba mama wa sheria zote duniani na mlezi mzuri ni lazima awe na familia bora!
 
well said Comrade
 
Duh! Natamani andiko hili lisambazwe kwenye ma group mengi ili ijulikane tulipokwama isijirudie tena.
 
Naam comrade. Naomba kura yako tafadhari. Mwisho wa andiko kuna kitufe cha VOTE please click hapo kunipigia kura

Andiko zuri nimepata kitu 🙏
 
Back
Top Bottom