Tanzania ni moja ya nchi chache barani Afrika ambazo zimebarikiwa kuwa na rasilimali nyingi sana ikiwemo madini, lakini isivyo bahati pia ni miongoni mwa nchi ambazo hazinufaiki na madini hayo hii ni kutokana na technolojia duni ikiwepo ni ukosefu wa nishati ya umeme ya uhakika ya kuendeshea mitambo ya kisasa.
Serikali hii ya awamu ya sita chini ya kiongozi mahiri Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan imeliona hilo na kulifanyia kazi na sasa kuja na majawabu chanya juu ya kizungumkuti hicho,
Akiwa ziarani mkoani Geita waziri wa Nishati, January Makamba ameahidi kupeleka umeme kwenye migodi ya wachimbaji wadogo katika Kijiji cha Wisolele ifikapo mwezi Oktoba 2022 ikiwa ni utekelezaji wa moja ya vipaumbele vya Wizara ya Nishati katika kupeleka umeme kwenye maeneo ya uzalishaji ikiwemo migodi.
Serikali imepanga kupeleka umeme katika migodi 336 nchini kupitia Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa gharama ya takriban shilingi Bilioni Sita ili kazi za uchimbaji wa madini nchini zifanyike kwa tija na hivyo kukuza uchumi wa nchi.
Endepo mradi huu ukifanikiwa hakika Mhe Rais Mama Samia Suluhu Hassan atakuwa amejiwekea historia ya kipekee kwa wachimbaji wadogo wadogo waliopo nchini.