Kitendawili cha picha ya waasisi wa TANU 1954

Kitendawili cha picha ya waasisi wa TANU 1954

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KITENDAWILI CHA PICHA YA WAASISI WA TANU 7 JULAI, 1954: "NOW YOU SEE HIM NOW YOU DONT"

Nimepokea ujumbe huo hapo chini:

Asalam Aleikum Warahmatullah Wabarkatuh,

Poleni kwa msiba, wanasema hiyo picha ya waanzilishi wa TANU imewekwa CCM kama ulivyoshauri, ni kweli, imewekwa wapi, Chamwino au Lumumba?

***

Waleikum Salaam Warahmatullah Wabarakatuh.

Tushapoa ndugu yangu.

Mwaka 1987 nilikwenda Maktaba ya CCM Dodoma wakati huo nafanya utafiti wa kitabu cha Abdul Sykes.

Nilikuta picha ya Waasisi wa TANU imetundikwa.

Sina taarifa ni hii picha uliyoniletea.
Nakushukuru sana.

Lakini ningependa kukufahamisha kuwa picha hii uliyoniletea si ile picha halisi yenyewe.

Picha hii ina kasoro kubwa ya kutiwa mkono na kubandikwa ndani picha ya Kasella Bantu ambae hayumo kwenye picha iliyopigwa pale ofisi ya TAA New Street tarehe 7 Julai 1954.

Wengine ambao hawamo katika picha ya Waasisi wa TANU ni Tewa Said Tewa na Ally Sykes.

Hawa watatu walikaa pembeni kwa kuwa walikuwa watumishi wa serikali na sheria ilikuwa inawakataza kujihusisha na siasa.
1616584553747.png
 
Nashindwa kuona kitendawili kinachozungumziwa. Kwani picha ilisema wanaoonyeshwa peke yao ndiyo waanzilishi wa TANU? Kama picha ingemwonyesha Mwalimu na Kambona na maandishi yakasema hapo juu ni waanzilishi wa TANU, siwezi kuwa na ugomvi na hiyo picha maadam tu haisemi hao peke yao ndiyo walianziasha TANU. Ni tofauti na kuweka picha ya Mwinyi na kusema huyo ndiye Rais wa kwanza wa Tanzania kwa kuwa Rais ni mmoja tu ambapo waanzishi wa TANU ni wengi kuzidi hata hao watu 10 au 20 unaowataja. Kuna wengi tu waliotoa mchango katika kuanzisha TANU na wengine walikuwa 'behind the scenes' hawaonekani hata kwenye picha ya watu 50.
 
Back
Top Bottom