Kitendawili cha wasiojulikana hatimaye kimeteguliwa na Spika Tulia?

Kitendawili cha wasiojulikana hatimaye kimeteguliwa na Spika Tulia?

Mag3

Platinum Member
Joined
May 31, 2008
Posts
13,413
Reaction score
23,592
Nimetulia namsikiliza kwa makini Spika Tulia akiwataka vijana wanaosadikiwa ni wa CCM kuwashughulikia wanaowakosoa viongozi wa chama na serikali. Moja kwa moja nikamkumbuka kijana machachari Ben Saanane kwa jinsi alivyokuwa anahoji sifa za Rais na Mwenyekiti wa CCM, John Pombe Magufuli (RIP).

Sina hakika na kilichompata kijana huyo lakini hadi leo hajulikani yuko wapi na kama yuko hai au la. Hivyo hivyo hali kama hiyo ikawatokea wengi hadi maiti zikaanza kuokotwa kwenye viroba. Kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili, kumkosoa kiongozi wa chama na serikali kukawa ni kujitafutia makuu.

Pamoja na kuwa na vyombo vya ulinzi na usalama, wananchi waliendelea kuishi kwa hofu bila maelezo ya kutosheleza. Waliopotelewa na ndugu zao walipewa majibu ya mkato kwamba wahusika hawajulikani. Basi neno wasiojulikana likawa wimbo kila akipotezwa mtu huku raia wakizidi kutekwa na kupotezwa.

Kuna wakati utaupenda ukweli na kuna wakati utauchukia ukweli. Kama ni mtenda maovu lazima utauchukia ukweli kwani kila utakapotaka kuuzikao hautakubli. Lakini kama ni mtenda wema utaupenda na kuulinda wabaya wasije wakapata nafasi ya kuuzika hata kama ni kwa muda mfupi tu kabla ya kujitokeza tena.

Nimemsikia Spika Tulia...je alichoagiza kinatoa kamwanga kadogo kwa kitendawili cha wasiojulikana? Nikitazama sura za wale vijana wanaoamrishwa kuwashughulikia wakosoaji wa viongozi wa chama na serikali napata woga. Fikiria hawa wanikute nikimkosoa Spika Tulia, je nitapona? Je ndugu zangu wataniona tena?
 
Mimi binafsi nina wasi wasi hivyo napenda kumuuliza Spika Tulia, ungependa hao vijana wanishughulikie vipi wakinikuta nakosoa utendaji wako kama Spika wa Bunge?

Je Bunge kweli litaendelea kulinda uhuru wangu wa maoni kama ilivyoainishwa kwenye Katiba kama wewe Spika ndiye unatoa kauli kama hiyo kwa vijana wa CCM?
 
Matamshi ya viongozi wetu saa nyingine yanaleta utata Sana
Utata uko wapi ndugu yangu, Spika Tulia kawaagiza hao vijana yeyote yule atakayekutwa anamsema vibaya kiongozi yeyote wa chama na serikali ashughulikiwe.

Akikazia amewataka wamshughulikie yeyote atakayekutwa akihoji utendaji wake yeye binafsi! Kwa kweli naogopa.
 
Nimetulia namsikiliza kwa makini Spika Tulia akiwataka vijana wanaosadikiwa ni wa CCM kuwashughulikia wanaowakosoa viongozi wa chama na serikali. Moja kwa moja nikamkumbuka kijana machachari Ben Saanane kwa jinsi alivyokuwa anahoji sifa za Rais na Mwenyekiti wa CCM, John Pombe Magufuli (RIP).

Sina hakika na kilichompata kijana huyo lakini hadi leo hajulikani yuko wapi na kama yuko hai au la. Hivyo hivyo hali kama hiyo ikawatokea wengi hadi maiti zikaanza kuokotwa kwenye viroba. Kwa mara ya kwanza katika historia ya taifa hili, kumkosoa kiongozi wa chama na serikali kukawa ni kujitafutia makuu.

Pamoja na kuwa na vyombo vya ulinzi na usalama, wananchi waliendelea kuishi kwa hofu bila maelezo ya kutosheleza. Waliopotelewa na ndugu zao walipewa majibu ya mkato kwamba wahusika hawajulikani. Basi neno wasiojulikana likawa wimbo kila akipotezwa mtu huku raia wakizidi kutekwa na kupotezwa.

Kuna wakati utaupenda ukweli na kuna wakati utauchukia ukweli. Kama ni mtenda maovu lazima utauchukia ukweli kwani kila utakapotaka kuuzikao hautakubli. Lakini kama ni mtenda wema utaupenda na kuulinda wabaya wasije wakapata nafasi ya kuuzika hata kama ni kwa muda mfupi tu kabla ya kujitokeza tena.

Nimemsikia Spika Tulia...je alichoagiza kinatoa kamwanga kadogo kwa kitendawili cha wasiojulikana? Nikitazama sura za wale vijana wanaoamrishwa kuwashughulikia wakosoaji wa viongozi wa chama na serikali napata woga. Fikiria hawa wanikute nikimkosoa Spika Tulia, je nitapona? Je ndugu zangu wataniona tena?
Huyo asiyetulia ambaye wazazi wake katika kusisitiza, baada ya kuona tatizo lake tangu utoto, wakamwambia 'tulia', ni miongoni mwa wasiojulikana. Alipewa hiyo nafasi na marehemu katika ule utaratibu wake wa kuwapachika wasiojulikana kwenye nafasi nyingi za uongozi na utendaji ili kuwa na watu wasiohoji chochote.

Wengi wao uwezo wao na maadili yao ni zero. Hawa, tukibahatika kuwa na mfumo mzuri wa utawala (katiba nzuri mpya), ni wa kuwasafisha kabisa, kwa sababu ni uchafu katika nyumba.
 
Nimemsikia Spika Tulia...je alichoagiza kinatoa kamwanga kadogo kwa kitendawili cha wasiojulikana? Nikitazama sura za wale vijana wanaoamrishwa kuwashughulikia wakosoaji wa viongozi wa chama na serikali napata woga. Fikiria hawa wanikute nikimkosoa Spika Tulia, je nitapona? Je ndugu zangu wataniona tena?
Licha ya yote, kinachosikitisha zaidi ni kuona mtu anayehimiza uvunjifu huo wa sheria.

Huyu ni kiongozi, tena Spika kabisa wa Bunge..., na kama hiyo haitoshi, huyu ni msomi wa kiwango cha juu kabisa, tena katika maswala ya sheria.

Sasa kama mtu kama huyu ndiye anakuwa mstari wa mbele kuhimiza sheria na haki zivunjwe, nchi yetu hii itakuwa na matumaini na nani?

Kuna mawili wanayoweza kuchagua waTanzania kati yake yawe kawaida ya maisha yao.

Moja ni kwamba watii bila ya shurti vitisho hivi vinavyotolewa na hawa watu, na wakubali kwamba hawana lolote wanaloweza kufanya kuondokana na hali hiyo ya kunyanyaswa.

Lakini pia, kauli kama hii inaweza kuwa mwanzo wa kuchochea watu kukataa kunyanyaswa na kutafuta kila njia kuwawajibisha viongozi wa aina hii kwa njia yoyote, ikiwa ni pamoja na njia hizo anazohimiza zitumike kwa raia wanaowashutumu hawa miungu watu.

Nadhani wakati umefika sasa kuwatia adabu hawa watu waliolewa madaraka.
 
Watawala wa Sheria kwenda kwa watawaliwa wa sheria.
 
Dah, kumetokea nini mkuu Mag3 hadi uandike haya hapa!
Tayari shatishiwa na hao "wasiojulikana"?
Ah hapana, nimeona nyuzi nyingi tu kuhusu hili, sikucheki mapema. Watu wa kutishwa wapo na mimi siko katika hiyo list ndugu yangu. Kilichonisukuma ni wale vijana wa UVCCM walivyokuwa wanamshangilia huyo SPIKA TULIA!

Ni kama vile wana kiu ya damu ya mtu! Hapo hapo nikawakumbuka wale WASIOJULIKANA, nikajisemea ebo kumbe ndio maana vyombo vyetu vya usalama vilipatwa na kigugumizi kushughulikia utekaji, utesaji na upotezwaji!

Labda zilikuwa ni maagizo kutoka juu.
 
"Nyooka nae"

Lakini hiyo tungo ni tata, hata akipelekwa mahakamani sidhani kama atafungwa, na inawezekana alijua ndio maana akaitumia.

Inaonekana wengi wanaitafsiri kwa namna wanavyoona/taka wao, hasa kutokana na mazingira ya kisiasa yaliyopo kati ya CCM na wapinzani.

Lakini hiyo pekee kwangu naona haitoshi kumtia hatiani Tulia pale atakapotakiwa kujitetea.

Anaweza kusema "nyooka nae" alimaanisha kuwaambia vijana wa CCM wajibu hoja kwa hoja, sasa nani ataweza ku prove vinginevyo?
 
K
Utata uko wapi ndugu yangu, Spika Tulia kawaagiza hao vijana yeyote yule atakayekutwa anamsema vibaya kiongozi yeyote wa chama na serikali ashughulikiwe.

Akikazia amewataka wamshughulikie yeyote atakayekutwa akihoji utendaji wake yeye binafsi! Kwa kweli naogopa.
Ukweli ni kwamba viatu havimtoshi. Watateteana lakini wote viatu haviwatoshi. Hata nyani akitaka kudondoka hushikilia matawi ya pembeni, sasa nyani huyu ndio kaona tawi hili linamfaa.
 
Tulia ni mkuu wa mhimili unaotunga sheria. Akiwa Spika anafahamu nchi inaendeshwa kwa sheria
Kitendo cha kutoka na kumasisha vurugu katika jamii ni cha kulaani na kulaaniwa na yoyote

Leo hatujui vijana aliowaelekeza 'wanyooke' na wenzao watachukua hatua gani.

Tunakumbu kumbu ya UVCCM wakisema wanaopinga JPM wauawe.
Spika ni mjumbe wa kamati kuu ya CCM katoa maagizo wasiokubaliana na wenzao wa CCM '' Nyooka naye'.

Hatujui kunyooka ni kwa namna gani, iwe kwa risasi kama Tundu Lissu au kwa mapanga kama Alphonce Mawazo au kupopotezwa kama Kanguye na Ben Saanane

Hatujui vijana wasio wa CCM wata react vipi pindi watakapokabiliwa na wenzao wa CCM wakati wa 'kunyooshwa'

Kwa kiongozi wa Bunge (Spika), Mbunge na Mjumbe wa kamati kuu ya CCM kuhamasisha vijana ' wanyooshane' ni kulitakia mabaya Taifa hili. Mauaji ya kimbari huanza na hamasa kama hizi zikiwahusisha vijana

Tulia Ackson amepoteza sifa ya kuwa kiongozi kwa kuhamasisha vurugu zinazoweza kupekelea mauaji na uvunjifu wa amani nchini.

Vurugu zozote zitakazotokea nchini kati ya vijana wa CCM na wasio , Spika Tulia atakuwa ima 'mtuhumiwa au Shahidi' hili hatalikwepa

CCM watoke watueleze ikiwa Tulia alikuwa anatumia ILANI ya chama chao ili kumsafisha
Ikiwa CCM watakaa kimya basi hili nalo ni lao

Katika mazingira ya kawaida, Tulia alitakiwa ajiuzulu Uspika au alazimishwe kujiuzulu kutokana na kauli inayohatarisha amani na usalama wa Taifa.

Mag3 Pascal Mayalla JokaKuu Kalamu Tindo
 
Back
Top Bottom