Kitendo cha CCM kumleta Wassira mzee wa miaka 80 inaonyesha upungufu wa human resource katika chama hicho

Kitendo cha CCM kumleta Wassira mzee wa miaka 80 inaonyesha upungufu wa human resource katika chama hicho

Wassira na Mbowe wamepishana miaka 14 tu

Wassira anafanya Mikutano 12 Kwa Siku 🐼
We Yohana, huo ulinganisho wa idadi ya mikutano si sawa. Mmoja hana haja ya kuomba kibali cha kufanya mikutano wakati yule wa pili anatakiwa afanye hivyo. Mara nyingi akiandaa tu mkutano tayari anapata zuio kwamba Mzee atatumia kiwanja hicho kwa wiki nzima hivyo hawawezi kufanya hapo.
 
Issue ni busara,experience na mtu ambaye hatamsumbua Mwenyekiti
Ukiweka vijana nao mara wanataka uenyekiti haipendezi
 
Sasa huko CCM vijana wenyewe ndio hawa akina Doto Magari, Joketi, Diamond Platinum, Ally kiba, Makonda, Nape, January Makamba nk.
 
Mtu asiyestahili akipewa fadhila ya nafasi kuongoza..maana yake waliompa hiyo fadhila ndio wanatumikia hiyo nafasi! Ccm iko chini ya tiss zitto alishasema jambo hili mara nyingi, wao ndio wanafadhili wanaowataka..chama kinaongozwa na mercenaries!
Ndio tatizo la nchi hii, kumpa mtu cheo sababu ya fadhila, si sababu ya efficiency au uwezo wa mtu
 
Issue ni busara,experience na mtu ambaye hatamsumbua Mwenyekiti
Ukiweka vijana nao mara wanataka uenyekiti haipendezi
Basi mwenyekiti anaogopa competitions, or ana fear ya kugeukwa na mtu akiwa kijana

Means nchi haimani vijana kwneye uongozi wa juu. Hili ni tatizo
 
Wameamua kuifanya CCM Mali ya celebrities, wasanii, madalali, watoto wa viongozi na watumishi wa Serikali, matokeo yake critical thinkers wameamua kufanya kazi zingine.

Wanasahau hawa wazee watakufa huku nyuma hakuna serious generation matokeo Tutsi, Asians, Arabs, Chinese, Kenyan nk wanapandikiza watu wao Taifa linatekwa huku tunachekacheka na akina Shilole, Jokate, Doto Magari, Ommy dimpoz, Juma lokole, Mwijaku, baba Revo nk.
 
Makamu Mwenyekit ana majukum gani yanayohitaj nguvu?

Makamu Mwenyekit anahitaj kukijua chama ikiwemo kanuni na taratibu zake.

Makamu Mwenyekit anahitaj kuwa na busara.
Makam Mwenyekit wa chama dola anahitaj uelewa kuhusu serikali na taasisi zake.

Lakin pia makamu Mwenyekit anahitaj kulijua bunge na taratibu zake.

Sifa ipi unadhani Mzee Wassira Hana?
Huyu aliyekuwa akisinzia bungeni muaka kumi iliyopita sababu ya uzee,Kwa nini watu wanastaafu ,umri ni factor kubwa
 
sijaelewa stress zote za nini? raisi samia anamaliza muda wake 2025/10 , na raisi ajaye atakuwa mkuu wa chama na atakuja na timu yake pia, hivyo wasira ni wa miezi michache tu, chini ya mwaka …
 
sijaelewa stress zote za nini? raisi samia anamaliza muda wake 2025/10 , na raisi ajaye atakuwa pia mkuu wa chama na atakuja na timu yake pia, hivyo wasira ni wa miezi michache tu, chini ya mwaka …
Wee kuna azimio huku naona TBC
Mama la Mamaa CCM wanaenda kuamua
 
'Warumi 2:2'
2 Wala msiifuatishe namna ya dunia hii; bali mgeuzwe kwa kufanywa upya nia zenu, mpate kujua hakika mapenzi ya Mungu yaliyo mema, ya kumpendeza, na ukamilifu.


Soma kwa Makini maelezo hapa chini
Ndugu zangu watanzania nawapa msaada wa bure. Taifa la Tanzania kwa sasa password za kuendesha zimebadilika huko rohoni na yeyote atakayetaka kupingana na ukweli huku mwilini atapoteza Uhai.
Mungu amefuta utawala wa siasa kwa sasa tupo kwenye utawala wa kifalme. Utawala wa Mungu sio wa democracy
Mkitaka maelezo/maelekezo zaidi nitafuteni niwasaidie bure
Taifa la Tanzania limekuwa Taifa la kwanza duniani kuingia kwenye wokovu kwa sasa ndio Taifa lenye nguvu duniani.
Rais Samia kwa sasa ndiye Rais mwenye nguvu zaidi ya maraisi wote duniani kote na hakuna taifa lolote linaweza vamia au shambulia ndani ya Tanzania.
Tunaelekea kuipata Tanzania aliyoikusudia Mungu tangu kuumbwa kwake.
Huu sio unabii ni ukweli and I can proof whatever I m saying.
Kwa sasa kinachoendelea kwenye Taifa ni kwasababu ya haya mabadiriko aliyoyafanya Mungu.
Taifa lipo kwenye utawala wa haki kila kinachofanyika Mungu anaweka wazi hata ukifanya kwa siri kinafunuliwa.
 
Of all the people ndani ya chama cha mapinduzi eti CCM wanamleta Stephen Wassira. Mzee wa miaka 80 eti awe ndiyo makamu mwenyekiti wa chama hicho. Hili ni jambo la kustaajabisha sana kwa viwango vyovyote vile. Na hii ni kwa sababu zifuatazo.

1. Tulitegemea CCM ijifunze kwa Kujiuzulu Kinana.

Kinana aliyekuwa ni makamu mwenyekiti wa CCM mara kibao alisikika akisema kuwa amechoka anaomba apumzike. Kinana yeye ana miaka 74, Huku Stephen Wassira ana miaka 80. Katika hali ya kawaida tulitegemea CCM ijiulize mara mbilimbili kuwa kama huyu mwenye 74 anaona kazi inamuelemea (kwa changamoto za mambo mengi zikiwemo za uzee), Je huyu wa miaka 80 ana nafuu gani kumshinda mdogo wake wa miaka 74?.

2. Mzee siyo kweli kuwa yuko fit kiafya

Mzee Wassira anaishi Mbweni, watu wanazijua changamoto zake za kiumri, ikiwemo hata kufanya mazoezi kwa kusaidiwa. Kwa nini CCM isilione hili?. Huyu mzee anayehitaji utulivu ili angalau aweze kutumia nguvu zake ndogo uzeeni, kwa nini CCM inakuwa na ubinafsi kiasi hiki, haionei huruma wazee, kwa nini isimuache mzee wa watu kupumzika?

3. Yumkini CCM imepungukiwa na pool ya watu wenye uwezo.

Mzee Wassira ni mtu aliyehudumu katika chama na serikali tangu miaka ya 1970's wakati huo Rais ni Nyerere, na wakati huo Makongoro Nyerere akiwa shule ya Sekondari. Mtu kama huyu ana kipya gani kwa CCM ya sasa na ana mawazo gani ya kuendana na nyakati za sasa. Hili jambo linatupa ishara moja, kuwa CCM ya sasa haina watu wenye gravita kubwa ya kisiasa, wenye uwezo na kwa hiyo inaenda kukopa kwa watu wa zamani wa enzi za Nyerere. Hii ni aibu na fedheha kwa CCM ya hivi karibuni kushindwa kutengeneza viongozi. Ukianhalia safu za makada wa CCM walio wengi ni wepesiii hakuna manguli wa kisiasa.

4. Huenda Samia anataka aendelee na mazungumzo na Upinzani anadhani Wassira atamsaidia.

Ni kweli, katika watu ndani ya CCM waliokuwa na Intellectual prowess (uwezo mkubwa wa kiakili) wa kudeal na Wapinzani na kwenda nao hoja kwa hoja ni Wassira. Kwa hiyo kama mazungumzo ya maridhiano yatahuishwa, Wassira ndo atachukua nafasi ya Kinana ktk mazungumzo hayo. Nadhani ni matumaini ya Samia kufikiri kuwa Wassira ataweza. Hata hivyo Samia amesahau kuwa Wassira wa sasa, siyo Wassira wa enzi za Jakaya miaka 10 iliyopita. Huyu wa sasa ni mzee sana. Na ukizeeka sana hata akili inaslow.

5. Ni kudhihaki waasisi wa CCM waliohudumu na kuamua kung'atuka uongozi wa chama ili chama kipate uelekeo mpya.

Kawawa alistaafu siasa za CCM akiwa na umri mdogo tu kulinganisha na Wassira, akiwa chini ya miaka 70. Nyerere akaacha siasa za uongozi wa CCM mwaka 1990 akiwa na miaka 68 (Wakati huo kofia za mwenyekiti na rais zilikuwa tofauti). Sasa huyu mzee wa miaka 80 wa nini, alete nini?

6. Mwenyekiti wa CCM haonyeshi umakini kwenye kuunda timu za kumsaidia kazi.

Hili limedhihirika katika teuzi anazozifanya kama rais, teua tengua zisizoisha, recycling isiyoisha, na sasa amefanya kituko cha karne kwa kumleta mtu wa mwaka 45 ili eti awe makamo wake. Inashangaza sana!
Huwezi elewa
 
Hicho cheo hakiwafai vijana wa sasa hivi wa hovyo...

Ni cheo kikubwa sana ndani ya chama na nchi...


Cc: Mahondaw
 
Makamu Mwenyekit ana majukum gani yanayohitaj nguvu?

Makamu Mwenyekit anahitaj kukijua chama ikiwemo kanuni na taratibu zake.

Makamu Mwenyekit anahitaj kuwa na busara.
Makam Mwenyekit wa chama dola anahitaj uelewa kuhusu serikali na taasisi zake.

Lakin pia makamu Mwenyekit anahitaj kulijua bunge na taratibu zake.

Sifa ipi unadhani Mzee Wassira Hana?
Hivi Busara ndo ujinga gani? Maana kila mda mnasemaga busara,Hivi hizi busara zilishatufanyia nini mpaka muone ni kitu cha muhimu sana!
Viongozi wa kitanzania wanapenda sana kuongelea busara sijui busara gani hiyo inayowafanya wengi wao kuwa wezi,wasiowajibika na wanafiki!
Tunahitaji kiongozi wa kufanya mambo kwenda busara haileti chakula mezani ni unafiki tu wa kuwafunika watu mabaya yao!
 
Au Mama hataki mtu wa kumchallenge??...maana ni kama Mzee wetu ZALI LA MENTAL limemuangukia
 
Back
Top Bottom