Kitendo cha jeshi la Polisi kukamata wapinzani kwa kuwadhalilisha na kuacha chama tawala na mawakala wao wakitamalaki ni cha kipuuzi!

Kitendo cha jeshi la Polisi kukamata wapinzani kwa kuwadhalilisha na kuacha chama tawala na mawakala wao wakitamalaki ni cha kipuuzi!

G Sam

JF-Expert Member
Joined
Apr 20, 2013
Posts
11,795
Reaction score
36,704
Jeshi la Polisi linafanya upuuzi kukamata viongozi na wafuasi wa vyama vya upinzani na kuacha wale wa chama tawala na mawakala wao.

Kitendo hiki kinadhihirisha jinsi vyombo vya dola vinavyotumika kwa maslahi ya kuhakikisha chama tawala kinapata kwa ukamilifu kile kinachokitaka kwa nguvu. Kwenye nchi inayojinasibu kuwa ya kidemokrasia na inayofuata mfumo wa uchaguzi huru na wa haki kuwapata viongozi wa wananchi, kufanya hivi ni upuuzi mtupu kwa vyombo vya dola. Aidha ni dalili ya ukomavu duni wa vyombo hivyo.

Huwezi kujitapa hadharani kuwa demokrasia itatamalaki kwenye uchaguzi mkuu huku mafichoni vyombo vinavyoshughulikia hayo vikionyesha udhaifu mkubwa kiutendaji na kwenye matokeo.

Tumuombe na tumpe rai Rais Magufuli kuwa haya yanayotokea yana dhamana juu ya mikono yake. Hii ni nchi yenye watu wa kada mbalimbali kisiasa. Nimkumbushe tu kuwa kilichoharibu ustawi wa nchi nyingi duniani ni mwenendo mbovu wa shughuli za kisiasa ndani ya mataifa hayo huku chama tawala kikijipa ufalme mbele ya kada nyingine za kisiasa.
 
Mwenye taarifa sahihi juu ya kukamatwa kwa akina Zitto please, maana nashindwa kutoa comment kwani sijui sababu hasa ya wao kukamatwa. Unaweza kutoa maoni kumbe wanamakosa.
 
Ndio lockdown wanayotaka wacha yawapate
 
Wakusanye ushahidi watume UN na nchi kubwa zote za magharibi
 
Back
Top Bottom