Kiongozi wa CHADEMA Freeman Mbowe ameonekana kwenye video akikamatwa wakati anaongea na waandishi wa habari. Hapo ni kabla ya kufanya maandamano ambayo hata kama angeyafanya katiba ya Jamhuri ya Muungano haimkatazi. Mheshimiwa Mbowe amekamatwa pamoja na viongozi wengine wa CHADEMA akiwepo mkamu mwenyekiti Tundu Lissu na mwenyekitii wa CHADEMA kanda ya kaskazini Godbless Lema.
Jambo hili limezidi kuichafua serikali ya Tanzania mbele ya macho ya wananchi na jumuiya ya kimataifa. Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaruhusu maandamano lakini cha kushangaza Jeshi la Polisi mwishoni mwa wiki iliyopita lilitoa amri ya kukataza maandamano ya CHADEMA. Hii sio mara ya kwanza kwa serikali ya awamu ya 6 chini ya uongozi wa Samia Suluhu Hassani kuzuia maandamano ya vyama vya upinzani hususan CHADEMA.
Ni vyema serikali ikaheshimu katiba na uhuru wa kujieleza kama inavyoelezwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Soma Pia: Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe ajitokeza Magomeni, akamatwa na Polisi