Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,478
- 3,659
Wakuu za Jumapili
Imenitokea mara tatu. Nimetokea kuwasahau watu hawa kabisa. Mmoja nikawa najaribu kuvuta kumbukumbu nimemwona wapi. Mwisho wa siku hawa watu hudhani ni makusudi kumbe sio.
Wa kwanza ni dada mmoja hivi aliyekuwa kama na down syndrome. Miaka ya 2000 hivi. Tuliishi nyumba moja na kila leo tunaonana na stori za hapa na pale. Ikatokea nimeenda boarding. Yani miaka miwili tu namaliza form six niko na bi mkubwa tunaelekea church tukakutana nae njiani. Akawa ananichangamkia nami sikujivunga ila sikuwa namkumbuka KABISA. Nikamuuliza bi mkubwa ni nani huyo, akaniambia si fulani, tumekaa nae nyumba fulani? Nilistaajabu sana. Hadi leo hilo halijanitoka
Mwingine mpangaji mwenzangu miaka ya 2018. Tumekaa nyumba moja mwaka.hivi akaja kuhama. Siku moja tuko mitaa ya mcity na wife, kituoni pale. Ndani ya daladala mitq kama tatu mwanamke mmoja akawa anatupungia na wife. Nilimwona awali nikamwambia unasalimiwa. Alipogeuka wakapungiana kwa uchangamfu. Nikamuuliza muda huohuo ni nani huyo akajibu si mama nanii? Nikamkumbuka nami nikapunga ila daladala ikawa inaondoka. Hadi leo nakumbuka
Wa tatu ni dada mmoja tulikutana Kanisani Segerea mwaka 2021. Wakati tunatoka ibadani dada mmoja ana mtoto akawa ananiangalia kwa kunichangamkia. Nikawa mashangaa tu ila nikawa nahisi nimemwona sehemu ila sijui wapi, na simkumbuki. Wakati tunaendelea kusalimiana nje huku nikipambana kumkumbuka nikashindwa. Baadae nikammwambie anikumbushe ni nani. Loh! Nilim disappoint sana. Hadi leo haijanitoka.
Ni dada mmoja ambaye tulipanga fremu zilizopakana maeneo ya mabibo hostel. Ye saluni mi steshenari na studio. Muda mwingi tulikutana na kupiga stori. Hata nilipotoka hapo tuliendelea kuwasiliana na tulishaonana njiani. Ni mwaka 2016 hivi wakati huo. Baada ya kunikumbusha ni nani, na jina nikawa nimemsahau pia. Alijisikia vibaya. Tatizo alibadilika kidogo. Alinenepa na kuwa mfupi. Hadi leo nakumbuka.
Hii si kwa upande wangu tu, bali nami nimewahi kusahauliwa na jamaa mmoja ambaye kwa kweli hakunikumbuka kabisa hata baada ya kujieleza. Hapo mi nina nafuu sana.
Huyu jamaa alinitangulia A level mkoani miaka hiyo ya 2000 mwanzoni. Tukaja kukutana udsm tukakumbukana na mawasiliano yakaendelea. Hadi anamaliza chuo nae akaondoka tukaja kukutana Makumbusho nikielekea TSJ, sasa IJM, naeakiwa mwalimu shule jirani hapo. Tukapiga stori sana, na tukawa tunakutana nikielekea DSJ.
Sasa nikiwa Kkoo miaka ya 2015 akaja shop kwangu kufanya mahitaji akiwa na rafiki yake. Hakuonyesha kunijua kabisa. Nikawa namchangamkia tu ila sioni response. Nikamwambia, fulani umenisahau? Wewe si fulani? Tumesoma shule fulani, tumekutana udsm, tumekutana Makumbusho, umenisahau? Jamaa kavuta memori wapi. Ikagoma kabisa. Basi tukapiga stori za kawaida tu akafanya yake akaondoka. Nikabaki nastaajabu sana.
Hii hali bila shaka huwakuta wengi. Mimi nakumbuka mambo mengi sana hadi mengine nikiwa na miaka minne bila shaka. Nakutana na mtu na memori inasachi na na taarifa inakuja instantly. Sijajua ni kwa nini hao watatu taarifa zao zilifutika kichwani mwangu