Kitendo cha Manara kumpiga madongo ya wazi Barbara ni ukatili, binti wa watu almanusura azimie

Kitendo cha Manara kumpiga madongo ya wazi Barbara ni ukatili, binti wa watu almanusura azimie

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Huu ni udhalilishaji

Kwa kweli kitendo cha Manara kumtupia madongo huyu binti ilikuwa ni ukatili, yani Barbara alikuwa anaombea tu muda uende haraka Manara amalize maana si kwa makombora ya madongo haya Manara aliyokuwa akimfyatulia binti, Manara ana mdomo mchafu aiee.

Ilibidi binti wa watu aangalie pembeni na aikaze sana mikono na meno ili kujizuia asitetemeke na kuzuia machozi

1654193481298.png


Manara kaona haitoshi bado anapasha kiporo kaweka hii video insta, huu sio ukatili kweli?

 
ha ha ha! kipato huleta majivuno! huu msemo anaupenda sana Msemaji wa Makolo FC!

Feisaaaaaaaaalll!! anachanja mbuga ndugu msikilizaji , anaachia kombora kali, la la la la, Goooooooooooal!
Mnyama anachinjwa na kisu kikali ndugu msikilizaji!! CCM Kirumba kumekucha!! Yanga moja Simba sifuri na sidhani kama watarudisha bao hili la karne, bao la kideoni!! Ama kwa hakika timu ya Mikia ni mbovu kabisa!!Onyango wa Makolo FC anaanguka ovyo!!

Goli moja la Fei Toto aka "Zanzibar finest" limeipasua Makolo FC vipande vipande na kuisambaratisha kabisa na kuleta utani unaokera sana na kuumiza sana mioyo ya wanasimba!

Yanga ni BRAND KUBWA Ili kuacha kutembeza bakuli forever, Yanga, kupitia GSM au mkopo wa benki ijenge Petrol stations nchi nzima zenye nembo ya Yanga , inunue mabasi ya kwenda mikoani yenye rangi na nembo ya Yanga au itengeneze vinywaji baridi kama juice na maji na labda pia viwanda vya unga wa ngano na sembe na vyote viwe na Lebo ya Yanga na picha za Mayele , Manara na Feisal , mashabiki wa Yanga ni mamilioni dunia nzima watakunywa , watanunua , watalipia na kula bidhaa zenye brand ya Yanga tu hasa siku tunazoifunga Simba na hivyo kujaza pesa mfuko wa Yanga , "mwananchi" gani hatapenda kupiga picha au selfie akiwa amekamata "juice" yenye picha ya Feisaaaaaaaaalll!!

sisi wabongo ni wagumu sana kuchangia timu bila return yaani kulipia kitu bila kupata kitu . Yanga wasinisahau kwa wazo hili just 1% share of profit please !
 
Manara bado anaipenda simba na hata yanga kule nafsi yake haijaridhika ila ukiona kwenye social network yuko happy ila inside bado haja move on.
Manara ni Yanga damu from home Baba yake Sunday Manara alikuwa mchezaji wa kutegemewa Yanga akiwafunga Simba alivyotaka, Manara amekua home akiona Yellow and Green tu Simba alikuja kusalimia na kupiga hela na kuchota siri zenu tu na sasa unaona matunda yake pale Yanga! Mganga gani wa Simba asiemjua? Njia gani ya kupita kuipasua Simba asiyoijua?

Msijidanganye Manara ni Yanga toka utotoni angalia uwanja wa Taifa wazazi huja na watoto wao wakiwafundisha kushangilia timu zao na kuwavalisha jezi za timu zao!!
 
Mtu mmoja hawezi kushindana na taasisi iwe Yanga ama Simba,Manara kaondoka lakini SImba itakuwepo na hata hapo Yanga kwenyewe Manara atakuwepo na ataondoka ila taasisi itaendelea kuwepo
Ninazungumzia sasa,akiondoka tutazungumza mengine
 
Back
Top Bottom