Kitendo cha Mashabiki wa Yanga kuonyesha picha ya Mwenyekiti wa CCM kwenye tamasha lao kilaaniwe na wapenda soka dunia nzima

Erythrocyte

JF-Expert Member
Joined
Nov 6, 2012
Posts
128,308
Reaction score
245,426

Hili jambo halikubaliki na likemewe kwa nguvu zote na TFF na mamlaka zingine , michezo ndio eneo pekee linalokutanisha wananchi wote na wenye itikadi tofauti , kuingiza siasa za ccm ni kuleta mkanganyiko wa kijinga sana .

Wako wana Yanga kibao ambao si wanaccm , siku wakiamua kupeperusha hewani picha za Wenyeviti wa vyama vyao itakuwaje ?

Jifunzeni kutoingiza siasa kwenye michezo , vinginevyo na sisi tukileta picha za viongozi wetu ambazo zinapendeza kuliko hiyo yenu , msije kuturushia mabomu , kwanza ni ushamba wa kiwango cha kutisha sana !

Naomba kuwasilisha .
 
Mbona unaweweseka na vitu vidogo sana mkuu !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…