Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Na Chato pia hawakwenda.Weka akiba ya maneno.Bado kuna kwenda Chato kwa maziko.Shida yako nini ? Kama wakiamua kwenda huko je?
Chato wzlienda kuaga..misaaidiewataenda CHATO hao
Ndani ya muungano wa EAC nchi ya Kenya imekuwa mstari wa mbele katika kuleta chokochoko za hapa na pale, hasa ikiichokonoa Tanzania mara kwa mara. Ingawa hivyo, Rais wa Kenya Hon Uhuru Kenyatta amefika yeye mwenyewe mubashara kuja kumuaga hayati Dr Magufuli.
Nchi za Uganda na Rwanda hazijawahi kujiingiza kwenye utata wowote ndani ya EAC mbali na lile tukio ambalo Kenya iliishawishi Uganda kusaini makubaliano ya ujenzi wa reli kutoka Mombasa hadi Kampala pasipo kuishirikisha Tanzania.
Utawala wa hayati Rais Magufuli ulikuwa unafanana sana na ule wa Kagame, hadi watu kufikia hatua ya kudhani kuwa huenda staili yake ya utawala alikuwa ameinakili kutoka kwa Kagame. Pia Museveni amekuwa mara kwa mara akiitembelea Tanzania na amesikika mara nyingi akiufagilia utawala wa hayati Magufuli.
Sasa swali ni ni: Je, kwanini Kagame na Museveni wametuma wawakilishi kuja kuomboleza kifo cha Magufuli lakini Kenyatta amekuja yeye mwenyewe mubashara? Hawa majirani wawili wanaogopa nini kuja Tanzania? Is there any hidden agenda behind their absecnce in this crucial occasion?
Marais wametoka all the way from Southern Africa up to Tanzania lakini hawa jamaa wapo hapa karibu wame-mute tu! Kama nauli ya ndege ni tatizo wangeweza kusafiri hata kwa basi na kufika Dodoma mapema kabisa kumuaga kiongozi mwenzao aliyelala mauti. Hata wangeweza kukodi basi moja wakasafiri wote kwa pamoja ili kuokoa gharama. Lakini wameamua, kwa makusudi kabisa, kutuma wawakilishi. Je, hii ni sawa?
Viongozi wote wa Afrika wamekuja Dodoma wao waende Chattle kusababisha usumbufu wa kiusalama kwani wao ni sehemu ya familia?
Sidhani kama hata huko Chattle wataenda ikiwa wameshindwa kuja Dodoma. Hawa jamaa ni wanafiki wakubwa, leo ndio nimewagundua.
Mungu hamfichi mnafiki. Wameumbuka mchana kweupe. Walikuwa wanasifia utawala wake kumbe walikuwa wanampaka mafuta kwa mgongo wa chupa? Wanafiq wakubwa!🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄🙄
MUOGA WA KIFO INGAWA HAVAI HELMET KICHWANI KUZUIA RISASIKagame bwana sijui anafikiriaje, kila kitu yeye ni opposite tu.
KAGAME NA M7 WOTE NI WAJINGA KATIKA ARDHI YA TANZANIA. MAGUFULI KUNA KITU ALIWAFUNDISHA NA WAMEJIFUNZA KUTOKA KWAKE KWA BAHATI MBAYA WAMECHELEWA MAANA WAMEMWAGA DAMU SANA ZISIZO NA HATIAJamaa walikuwa na 'urafiki' na mzee kwa interest zao tu.