Kitendo cha Mwigulu kumtaja Rais kuhusika na ufisadi Ripoti ya CAG ni sahihi?

Kitendo cha Mwigulu kumtaja Rais kuhusika na ufisadi Ripoti ya CAG ni sahihi?

Huyo ameamua kumtaja kwasababu anamdharau na amemuona kitonga. Hivi kweli enzi za giza angethubutu kumhusisha bwana yule na wizi wao?

Yaani mpaka hapo lingekua lishamkuta jambo
Lazima wamdharau tu; haiwezekani watu wanapiga pesa mtu amekaa kimya. Ni kweli mama anahusika
 
Na mimi naamini kuwa hili deal lilifanywa na mwendazake akiwa na watu wake kule BOT na Hazina tayari palikuwa na MTU wake SASA mama kaingia akafanya mabadiliko ya ghafla hapo ndipo lilipobumbuluka na vocha ilipokuja ikabidi wafanye nao "Betting" wapime kina cha maji wakakuta mzanzibari kiberiti kimejaa sio Tena kama vile viberiti vya zamani vya Kibo match box toka Moshi.,MKEKA UMECHANIKA
Akili huna. JPM aliacha invoice ya 37M bwana zako waneongeza Uko hapa unaandika upumbavu
 
Mwinguru hapo amesema toka awamu ya nne imekuwa ikifanyika hivyo... Mm kama mwananchi wa kawaida nimepata majibu... ndio maana hakuna wa kukamatwa hata kama wageiba fedha zote za bajeti ya mwaka fedha... so far rais hashitakiwi... Asanteni Sana.
Atupishe si kahusika
 
Mwigulu Nchemba kwenye utetezi wake bungeni amemtaja Rais kuwa ndiye anayeidhinisha fedha zote za Serikali jambo ambalo limezua utata na hisia kubwa kwa wananchi kuhusiana na ufisadi mkubwa uliotajwa na CAG kwenye maeneo mbalimbali .

Ufisadi mkubwa umetajwa kwenye Wizara ya Fedha, Wizara ya Nishati, Wizara ya Afya, Wizara ya Ujenzi, Wizara ya Habari na Wizara ya Maji, TAMISEMI na maendeleo mbalimbali.


Nyie ndio mnaopenda kusema mama ametoa pesa kwahiyo zikiibwa lazima atakuwa anaujua wizi huo kwani hizo pesa huwa hazitelekezi barabarani.
 
BAADA YA WAZIRI HUSIKA MWENYE UTAALAMU WA MAMBO YA KIFEDHA THIBITISHA UHALALI WA MALIPO NA KUUPELEKA WARAKA KWA RAIS, RAIS HUWA HANA LINGINE TENA KWA ALIYEMTEUA KUMSAIDIA, RAIS HUTIA SAHIHI, RAIS HUWA AMEMWAMINI MTEULE WAKE KWA KAZI HIYO, MAMBO YA TATHMINI YA GHARAMA SIO RAHISI KWA RAIS WETU KUYATAMBUA HIVYO HAYO HUFANYWA NA TAASISI NYINGINE ZA UMMA.
 
Pesa zikiibwa hahusiki zikijenga vyoo anahusika.

Waafrika sisi ni wanafiki sana na tutachelewa kwenye mambo mengi
 
Pumbavu zako mjadili mama yenu aliyeshindwa kuendesha nchi achana na JPM! Mnapenda sana kujificha kwa Magufuli! Wajinga sana mkosoe Mama yenu!

Punguza hasira, sifa za kijinga zilianza kipindi Cha jiwe kwani uongo?. Mama naye akabeba juujuu sifa za kijinga na kuruhusu chawa wa mama na mabango katengeneza kujisifu.

Leo yanamtokea puani. Unaposema fulani katoa pesa pia usiogope kusema fulani kaiba pesa.
 
Wala hakuna utata au chochote cha ajabu, Waziri yuko sahihi, hajakosea chochote, sijaona kosa lolote, Waziri hajamtaja Rais kuhusika na ufisadi..

Kamtaja indirectly, kwamba linapotokea sintofahamu ya pesa, Rais ndio aulizwe maana yet ndio muidhinishaji mkuu.
 
Wametulia bilioni 85 kuandaa mabango ya kumpongeza, hii nchi Ina wezi hatari wasio na huruma.
 
Lazima wa, usharau tu; haiwezekani watu wanapiga pesa mtu amekaa kimya. Ni kweli mama anahusika

Mimi siku ile anajisemesha stupid niliona Ni Kama anaigiza, hakuwa anamaanisha hata kidogo.
 
Mama ametoa hela ndio ulikuwa wimbo wa kila mahali

USSR
Huu utaratibu wa fedha za nchi kuitwa za MTU FULANI tulisema ipo siku itawatokea puani. Kama wanawaaminisha Wananchi zahanati imejengwa na Samia, Kwa nini wanakataa zinapoliwa hazijaliwa na Samia?? Ukitaka Sana sifa jua na dhihaka inakunyemelea.
 
Back
Top Bottom