Kitendo cha Simba kutaka kumpima akili Mkude ni udhalilishaji

Kitendo cha Simba kutaka kumpima akili Mkude ni udhalilishaji

Wakiona afya ya akili haiko njema sijui watatutangazia! Huu utakuwa uzalilishaji sana.

Kama walikuwa na lengo hilo wangefanya kimya kimya tu.
 
Udhalilishaji kivipi wakati Simba wanataka kujiridhisha kabla hawajamuadhibu, wanataka kujua kama hilo kosa la kujirudia (utovu wa nidhamu) hulifanya makusudi au kwasababu ni mgonjwa wa akili.

Kama ni mgonjwa Simba watampeleka hospitali akatibiwe, unachotaka kusema wewe Simba wamuadhibu bila kujua chanzo cha tatizo lake ndio unakosea.
 
Wapi Kamati wamesema akapimwe akili..Yaani kupima afya ndo kupimwa akili..?

Kama kwenye utetezi wake ripoti inasema alikuwa anaumwa au mpaka sasa ana matatizo ya kiafya sasa huoni kuwa Kamati lazima ijiridhishe kwa taarifa yake ili kufanya maamuzi sahihi..!

Peleka mbele chuki zako zisizokuwa na mantiki huko.
 
Kwani utovu wake wa nidham ..alifanya nini?
 
Watu wa karibu wa huyu kijana wamshauri abadilike.Afanye juhudi za kucheza mpira,ajenge maisha yake vyema. La sivyo ataishia kubaki kama wakina Boban
 
Ni kweli Mkude anayo Makosa ya utovu wa nidhamu , lakini kitendo cha kumpeleka Muhimbili kumpima akili ni kumdhalilisha sana .

Kwanini wasimuondoe tu ikiwa wanadhani haendi sawa na utaratibu wa Simba ?
Mkuu nimesoma ile taarifa mara kumi kumi ila sijaona sehemu wamesema Mkude aende Muhimbili Kwa ajili ya kupima Akili....!

Inawezekana kwenye utetezi wake amesema alikuwa anaumwa na kapeleka vyeti za hospital za vichochoroni, kama umesoma utajua mambo kama haya wanafunzi wamefanya Sana kama visingizio vya kukwepa adhabu Kwa kupeleka vyeti vya matibabu feki

sasa ili kujiridhisha inachaguliwa hospital moja ambayo ndio inapaswa kutoa vyeti vya matibabu, ndo walichofanya Simba ni kumtaka Mkude akapime Muhimbili Kwa sababu ni hospital ya uhakika ili kujiridhisha kama ni kweli alikuwa anaumwa na kupelekea yeye kufanya makosa ambayo anahukumiwa

Tuwe makini Sana kwenye kuandika haya mambo mengine, wewe unachokifanya ndio udharirishaji wenyewe

Sent from my M2004J19C using JamiiForums mobile app
 
Tuendelee kusubiri
 
Back
Top Bottom