Kitendo cha Simba kutaka kumpima akili Mkude ni udhalilishaji

Kitendo cha Simba kutaka kumpima akili Mkude ni udhalilishaji

Wakiona afya ya akili haiko njema sijui watatutangazia! Huu utakuwa uzalilishaji sana.

Kama walikuwa na lengo hilo wangefanya kimya kimya tu.
Ila wakuu mkude kiboko bana dah!!..
Hizo story zake ukiziskia utashka kiuno.
Kwanza fkiria t mchezaji ambae makocha zaid ya wanne wote wanamsmamisha we unam define
Vp uyo.
 
Ni kweli Mkude anayo Makosa ya utovu wa nidhamu, lakini kitendo cha kumpeleka Muhimbili kumpima akili ni kumdhalilisha sana.

Kwanini wasimuondoe tu ikiwa wanadhani haendi sawa na utaratibu wa Simba?
Wamuondoe bila kumpiga vidole? Yule hafai kuwa Simba kwanza kipaji cha kimataifa hana, ni zezeta tu la kombe la mbuzi ama Kinesi wachezalo Yanga.
 
Huyo wanamtafutia "timing" tu wamle kichwa hiyo ya kupimwa afya Muhimbili watoto wa mjini wanaita "bosheni". Wakimla kichwa bila kumtafutia sababu itakuwa shida kwani kuna baadhi ya mashabiki wanamkubali vibaya mno na huwaambii chochote japo uwezo wake umeshuka kidogo kwa siku za karibuni. Inavyoonekana sasa hivi viongozi wengi wameshamchoka japokuwa Mkude ni mmojawapo wa wa wachezaji waandaamizi na "icon"ya timu. Na mbaya zaidi nafasi yake ipo majaribuni kutokana na ujio wa Lwanga. Kwa hiyo viongozi sasa hivi hawana wasiwasi tena hata akiamua kwenda Yanga tofauti na zamani ndio maana walikuwa wanambembeleza. Ila Mkude na yeye kazidi anashindwaje kusoma alama za nyakati na kuona hatari iliyo mbele yake au labda sisi wengine hatujui huenda yale maneno kuwa tayari ameshasaini klabu nyingine wakati ule alipokuwa amefungiwa huenda yana ukweli. Muda ndio msemakweli ngoja tusubiri tuone mwisho wa hii filamu.
 
Ni kweli Mkude anayo Makosa ya utovu wa nidhamu, lakini kitendo cha kumpeleka Muhimbili kumpima akili ni kumdhalilisha sana.

Kwanini wasimuondoe tu ikiwa wanadhani haendi sawa na utaratibu wa Simba?
Hivi kupima akili nalo ni udhalilishaji? Ko ulitaka waendelee kumhukumu kumbe kuna vitu vimemuathiri kiakili. Mi nafikiri mkunde asisikie ushauri wa wajinga kua ni kumdhalilisha zaidi aone faida za kujua afya yake. Itamsaidia katika maisha yake ya mpira
 
Ukute mtu anadai malimbikizo yake hawampi chake,wanakimbilia homa,mkimpa pesa zake anapona huyo.
 
Wapi Kamati wamesema akapimwe akili..Yaani kupima afya ndo kupimwa akili..?

Kama kwenye utetezi wake ripoti inasema alikuwa anaumwa au mpaka sasa ana matatizo ya kiafya sasa huoni kuwa Kamati lazima ijiridhishe kwa taarifa yake ili kufanya maamuzi sahihi..!

Peleka mbele chuki zako zisizokuwa na mantiki huko.

Yaani huyo ana mindset ya ajabu sana! Anajifanya mashabiki wa Simba lakini siku zote kazi yake ni kuponda Maamuzi ya Timu tu. Sijui kama sio Maulid Kitenge huyu.
 
wakampime tu, akili, mkojo everything, kama kuna sababu ya msingi.
 
Back
Top Bottom