Uchaguzi 2020 Kitendo cha Tundu Lissu kukubalika Kanda ya Ziwa kwa kiwango hiki inaashiria nini?

Jiandaeni kuiba maana hakuna mbinu nyungine.
 

..hili ndilo kundi hatari sana kwa yeyote atakayeongoza Tz kuanzia mwaka huu.

..Robert Mugabe alipata upinzani mkubwa kutokana na kushindwa kutimiza ndoto za vijana waliosomeshwa baada ya uhuru.

..plan ya ccm imeishia kuandikisha wanafunzi mashuleni tu, haina majibu ya vijana hao watafanya nini watakapohitimu.
 
Kwa mujibu wa wataalam wa magonjwa ya akili , mtu yeyote anayedhani ana akili kuliko wote huyo ni kichaa , yaani wewe Maghembe wa milimani ndio unajua sana mambo kuliko kamati kuu ya chadema !

Mbona unaenda nisiko kutegemea, mimi najaribu kuonyesha ulazima wa kuhakikisha tunakata keki katika eneo ambalo kesho litatujazia sahani.

Kamati kuu ina watu, na hata siku moja sifikirii nitakuwa na ufahamu kuliko Kamati kuu kwa ujumla wao, lakini ninaweza kuwakumbusha kitu ambacho wanaweza wakapitiwa. Jee kuna ubaya kukumbushana ?. Kuna uzuri sana kusikiliza na ndio uongozi.
 
Hakika umewaambia ukweli wafuasi wake humu.

Nawachokoza kwa chambuzi za kufikirisha ili zisaidie kumrejesha mgombea wao kwenye reli, wao wanapumbazwa na nyomi. Nyomi hizo nk vijana wanaoshabikia udaku wa mgombea wao. Shangilia yao ni ya kejeli kuliko yeye anavyomkejeli Rais.
 
Watu wanakwenda kwenye mikutano ya TundA Lisu kupoteza muda na kutizama Futuhi!
TundA ana vichekesho sana... Eti anawahutubia wakulima kuhusu tozo za mazao na wakati Magufuli alishazifuta tangu zamani za kale!

Anawambia watu ati wajawazito wanalipa kodi kwa huduma inayowahusu, kumbe kalishwa matango pori na yule mdada mlowezi. Hao akina mama wanasikia na kushangaa.

Anadai wakulima wa korosho wanadhulumiwa, wakati walilipwa hadi wakanunua pombe ya kunywesha mifugo yao. Hawa wanasikia na kushangaa

Anadai vitambulisho vya machinga ni feki. Wahusika wanasikia na kumshangaa anaishi Tanzania ipi.

Yako mengi ya uzushi wake usiokuwa na chembe ya aibu, lakini udaku wa kufurahisha.
 
Hayo ni majigambo ya wizi wa kura kama kawaida yenu. Sasa, hata wale waliokuwa wanawabeba wameanza kunywea na kulegea. Ibeni kura muone mwaka huu.
 
Wewe utakuwa umepewa buku 7 yote,wenzio wanalipwagwa nusu kwanza kisha wanamaliziwa kesho yake
 
Ccm walichobakiza ni vurugu tu, Leo walijaribu kurusha mawe msafara wa lissu kule geita vijijini lakini walidhibitiwa na umma, mbaya zaidi baadhi ya wanaccm wanamtisha babaake upendo peneza eti ajitoe kugombea ubunge.ccm imechokwa.
 
Leo Askofu nimemuelewa sana. In short kumbe kuna viongozi wa dini wenye maono. Nilijua hatuna kabisa Kiongozi wa dini zaidi ya Baba Bagonza.
 
Ungetuambia ni nini kinakupa uhakika kwamba wale wote wanao hudhuria mikutano ya ccm hawatampa kura lisu na wale wote wanao hudhuria mikutano ya lissu watawapa kura çcm. Tatizo umetawaliwa na ubinafsi kuona kwamba unaijua yaliyopo miiyoni mwa wananchi.
 
Sera ya majimbo kama watu wamgejua wangeikubali. Nchi zote zenye maendeleo ya watu wana sera za majimbo. Huwezi kuendelea kwa kusubiri mawazo na maamuzi ya mtu moja katika nchi kubwa kama Tanzania.
Kutakuwa na sheria na miradi/huduma za pamoja kwa nchi nzima ila maamuzi yanayohusu mambo ya kila kijiji yatatokana na maamuzi ya watu wakifuata malengo ya taifa! Fedha zikikusanywa hakutakuwa na ucheleweshaji wa maamuzi!
Tukubali kujaribu tuone maajabu!
 
Tumeshawaambia hadi tumechoka picha zenu za kuchakachua za kitengo chenu cha uchakahuaji CHADEMA tumezichoka.Mwacheni Lowasa apumzike picha zake za mikutano yake mlizochakachua inatosha.
Unachoka mwenyewe acha kulazimisha wengine wachoke kitu ambacho hakipo, wee lazimisha ni za zamani lakini wenye Akili wanakuwepo kwenye mikutano wanajua CCM mnatengeneza propaganda za kijinga kulazimisha kuwa ni picha za zamani na ndipo CCM inazidi kudharaulika zaidi
 
28/10/2020 ndio kila kitu

Ila kujifariji pia muhimu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…