Kitendo cha Wanachama wa Yanga SC Kumzomea Katibu Mkuu wa TFF ni Kukosa Heshima

Kitendo cha Wanachama wa Yanga SC Kumzomea Katibu Mkuu wa TFF ni Kukosa Heshima

Ni Kitendo cha kusikitisha sana kimejiri leo kwenye Mkutano Mkuu wa Yanga ndani ya Ukumbi wa DYCCC Chang'ombe, kumzomea Katibu Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania TFF, Wilfred Kidao ambaye alikuwa Mwakilishi kutoka katika Shirikisho hilo.

Kwakweli hiki Kitendo si cha kistaarabu, ni Kitendo cha kihuni kwenye Mkutano wenye Heshima na Mustakabari wa Soka la Tanzania tena mbele ya viongozi wengine waalikwa ambao wanaheshimika sana nchini akiwemo mgeni rasmi Rais Mstaafu Jakaya Kikwete, na ni kukosa heshima kwa mamlaka yenye dhamana ya kuongoza mpira nchini Tanzania.

Viongozi wa Yanga acheni kupelekeshwa na mihemko ya mashabiki wasiojielewa. Kwani haya ndo matunda ya Makamu/Kiti kuita Press Conference na kuaminisha Mashabiki na Wanachama kwamba timu inaonewa madai ambayo hata Rais Mstaafu Kikwete alipinga kwenye Kubwa Kuliko (Yanga Day).

Mpira ni mchezo wa wazi Uwanjani, mnataka TFF wafanye nini? Wafunge mabao wao badala ya Sarpong ama mnataka TFF wasajili wachezaji wenye viwango wao badala ya Engineer? Au mnataka TFF waandae timu badala ya Viongozi?

Kwakweli Viongozi Jitafakarini, kisha mpige hatua mbele na muombe radhi kwa Katibu Mkuu Wilfred Kidao pamoja na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania.
Maneno mengi lakini pointi hakuna...Kama amezomewa anastahili kabisa...TFF ni wahuni na washenzi pamoja...hovyo kabisa
 
Maneno mengi lakini pointi hakuna...Kama amezomewa anastahili kabisa...TFF ni wahuni na washenzi pamoja...hovyo kabisa
Kuna neno hapo wasiojielewa linakuhusu vilivyo..!
 
Write your reply...MPAKA SASA SIMBA NDIO CLUB PEKEE AFRICA YENYE VIPORO.... APO NDIO UTAJUA KWA NINI WAMEZOMEWA
Sorry hivi wakati wa maombolozo ya mwezi mzima ligi ilikuwa inaendelea?,kipolounachopigia kelele kilisababishwa na Utopolo kutokucheza na Simba kwa kisingizio Cha kusimamia kanuni,wakati UkWeli mchungu mmepewa muda ili muiandae timu,mna kocha mgeni Kuna deby,mnafeli Sana Utopolo fc.
 
Na wewe pia
Paragraph ya kwanza nimelezea Kitendo, kisha kukosa nidhamu, kisha Viongozi wache kujazwa upepo na kuendelea.

Ukiona huelewi jua lipo nje ya uwezo wako.
 
Paragraph ya kwanza nimelezea Kitendo, kisha kukosa nidhamu, kisha Viongozi wache kujazwa upepo na kuendelea.

Ukiona huelewi jua lipo nje ya uwezo wako.
Sawa...hata wewe pia
 
Hivi TFF wanaihujumu vipi Yanga ?

Hebu Rudia kusoma vizuri nilichoandika

Feedback ni notification or alert or alarm

Inanotify kitu gani ndio nikasema TFF wajichunguze au warekebishe.

Hao wote sio vichaa
 
Tatizo ni viongozi wa utopolo waliowaaminisha wapenzi wa utopolo kuwa Sarpong hafungi kwa sababu wanaonewa na tff.
Kwa kuwa wanachama nao ni aina hiyo hiyo mwalimu wao hata alithubutu kuwaita nyani,tegemea hayo kutokea tu
 
Lete hiyo video tuone alipozomewa maana si wengine hatuamini vitu kirahisi.
 
Kwanini Tff wajichinguze,wakati ukweli unajulikana,misimu mitatu nyuma yanga wameshindwa kujenga kikosi imara,wanasajili mwanzo wa msimu na Kisha kikibomoa kikosi katikati msimu.Ukweli mchungu menejimenti ya Yanga na mashabiki wa Yanga mjitathimini,mnapenda UwOnGo MtAmU kuliko UkWeli mchungu.Yanga hawana kikosi Cha ushindani,Jambo ambalo wamefaulu viongozi wa Yanga ni kueneza Propaganda kwa mashabiki wao.
Wanataka TFF wawafungie mabao..!
 
Back
Top Bottom