Kitendo cha Zitto Kabwe kutumia " ubunge" wake kuikosesha serikali mkopo wa WB kimethibitisha kauli ya Prof Assad kwamba Bunge si Imara

Kitendo cha Zitto Kabwe kutumia " ubunge" wake kuikosesha serikali mkopo wa WB kimethibitisha kauli ya Prof Assad kwamba Bunge si Imara

johnthebaptist

JF-Expert Member
Joined
May 27, 2014
Posts
97,869
Reaction score
171,716
Bunge limemtaka AG ambaye pia ni mbunge kuchunguza kama kitendo cha mbunge wa Kigoma mjini mh Zitto kutumia nyaraka za bunge kuishtaki serikali huko benki ya dunia hakina chembe chembe za Jinai ndani yake.

Hapa nina maswali mawili:

Mosi, Jinai inachunguzwa na mwanasheria mkuu wa serikali?

Pili, kwanini Spika asiripoti tukio hilo polisi ili Zitto ashughulikiwe kwa mujibu wa sheria kama watuhumiwa wengine wa uhalifu?

Binafsi nimejikuta nikitafakari kwa mapana kwamba bunge letu linapungukiwa uimara katika maeneo fulani.
Najaribu tu kutafakari kama wabunge hawajui matumizi sahihi ya karatasi zenye nembo ya bunge kama alivyofanya Zitto basi silioni kabisa kosa la alhaj Assad.

Tafakuri yangu imetokana na taarifa ya habari ya ITV

Maendeleo hayana vyama!
 
Zitto anaweza fanyiwa kama Assad. Timbwili litaanzia Bungeni then Jiwe anamalizia nje. Hata ikibainika Zitto hana makosa Kikatiba, kwavyovyote CCM hawana aibu ya kukubambikia kesi yoyote ile kama wakiamua kukushughulikia kwa maslai yao.
 
Hili Bunge ambalo Mbunge wa upinzani akisimama akaanza kuongea mambo yenye maslahi kwa nchi anasimama mbunge wa CCM akidai kumpa TAARIFA na Spika anaruhusu mbunge wa Ccm anamsomea mistari 2 ya biblia kutoka kitabu cha Nabii Ezekiel? Na spika anamuuliza mbunge wa Upinzani umeipokea taarifa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nilimuangalia Zitto siku anahojiwa na Zuhura Yunus kuhusu hii issue, duh niliogopa. Nyie Zitto ana sura ya kutisha hasa camera ikimzoom kwa karibu yale macho. Hamna aisee huyu mwamba anapaa usiku. Na huenda ndio maana dola inamshindwa inapotokea stand off kama hizi
 
Kwani shida iko wapi? wamkalishe Zitto chini wamuombe ''chonde chonde'' akawaombee kwa Mabeberu, wasiwekewe vikwazo, si basi!

Zitto anasikilizwa nje! Bashite ana sikilizwa ndani! Si ngoma Drooo jamani! tunamaliza wini bila sababu!
 
Kwani shida iko wapi? wamkalishe Zitto chini wamuombe ''chonde chonde'' akawaombee kwa Mabeberu, wasiwekewe vikwazo, si basi!

Zitto anasikilizwa nje! Bashite ana sikilizwa ndani! Si ngoma Drooo jamani! tunamaliza wini bila sababu!
 
Back
Top Bottom