Ileje
JF-Expert Member
- Dec 20, 2011
- 13,667
- 21,296
Kitengo cha maafa tangu kuanzishwa kwake chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu hakujawahi kusaidia waathirika wo wote na badala yake kimekuwa ni kitega uchumi na chanzo cha mapato cha serikali.
Tulishuhudia wakati wananchi wenzetu wa mkoa wa Kagera walipopatwa na mkasa wa tetemeko la ardhi michango ya wananchi na mashirika mbalimbali ya ndani na nje ya nchi iliyolenga kuwasaidia waathirika ilivyokwapuliwa na serikali na kuitumia kwa shughuli zingine.
Aidha tumekuwa tukishuhudia wananchi wanaoathirika na majanga yakiwemo ya mafuriko na moto sehemu mbalimbali nchini wakikosa misaada kutoka kitengo hiki. Kitengo hiki kimekuwa hodari kuhamasisha na kukusanya michango halafu kinaishia kusikojulikana bila kugawa michango.
Hata kule Arusha baada ya wanafunzi kupata ajali na baadhi yao kufariki na kupata vilema vya kudumu kitengo hiki kwa kushirikiana na aliyekuwa Mkuu wa mkoa kilikula rambirambi.
Hivi sasa baada ya wafanyabiashara wa Kariakoo kupata janga la moto kitengo hiki kimekaa kimya kama hakijaona janga hilo. Inawezekana kabisa kuwapa waathirika wa moto huu kifuta machozi kwa kutumia viwango vyao vya kodi ambazo serikali imekuwa ikikusanya kutoka kwao. Kwamba kiwango cha kifuta machozi kinawiana na kodi muathirika amekuwa akilipa.
Hivyo ili kuepuka wizi na kujinufaisha kwa wachache kupitia mgongo wa maafa kitengo hiki kivunjwe mara moja.