Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Watu wa Mapokezi ya Wagonjwa katika Hospitali ya Rufaa Mbeya hawana huduma nzuri kabisa kwa Wananchi wanaofika kituoni hapo.
Mfano kuna mtumishi mmoja anaongea na simu muda mwingi bila kujali wagonjwa walio mbele yake, amekuwa na kawaida ya kufanya hivyo na hajali wanaohitaji kuhudumiwa.
Mbali na hapo hata miundombinu pia si salama sehemu hiyo, inasababisha Mgonjwa anaanza kuzungushwa muda mwingi mpaka inakatisha tamaa kuhudumiwa.