Yaani wakulima wa Tanzania katika kilimo ni sawa tunacheza,Kwakweli kuandika mpango kazi ni 1 na utekelezaji ni 2, hapo ukiziangalia hizo namba zina muundo miwili tofauti sasa ni tuna malengo ya kweli hizo namba tuzielewe na kuzifwata? Ni mtihani mkubwa sana ktk utekelezaji wa mambo mengi tunayoyaandikia taarifa nzuri kama hizo.
Hebu tuangalie kilimo cha Pamba na Korosho peke yake kungewekezwa nguvu nzuri na ma bwana shamba kushinda humo mashambani kutueliemisha na pembejeo upatikanaji wake basi na upande wa masoko ungalikuwa vyema sana tukaweza kupata faida kwa wakulima na Taifa kwa ujumla.
Hebu tuangalie zao la Kahawa hali kadhalika kila kitu kimebakia kwenye makalabrasha na wakulima kuvunjika moyo uzalishaji umeshuka sana.
Hebu tuangalie uchimbwaji wa malambo kwaajili ya kilimo cha umwagiliaji, kuna kipindi kuliletwa taarifa ya mpango kazi kuchimbwa malambo ya maji kwaajili ya umwagiliziaji na kunwesha Mifugo lakini vyote vimebakia kwenye makalabrasha. Tujifunze kujikosoa na tukubali kukoselewa tutafika mahala kila mmoja wetu akifurahie kilimo.
Umeongea pointi na ushauri mzuri sana1). Utafiti wa kilimo(TARI)
2).Uthibitishaji wa mbegu(TOSCI)
3).Kudhibiti wa pembejeo(TPHPA & TFRA)
4).Uzalishaji na Usambazaji mbegu(ASA)
5). FIELD(condition) CROP PRODUCTION (FCP).
Mashamba darasa yawe darasa kweli kweli sio kuzugazuga... Kama tunaingia gharama kubwa ku-fund utafiti na Uzalishaji mbegu kwa lengo la kuleta tija(mapato), sasa kwanini dhumuni lenyewe tusilifanye kwa ukubwa wake (seriousness).
Kupitia Maafisa Kilimo kwa kila kanda wanakua na vituo, vilivyowezeshwa kitaalamu, kufanya Uzalishaji bingwa wa mazao... Kwa (tija)faida na elimu ya vitendo yenye hamasa kubwa kwa wakulima.
Huku wakishirikiana na extension officers kwa issues za ku-coordinates na local government.