BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Mbunge wa Ubungo (CCM), Profesa Kitila Mkumbo ameitaka Serikali kutolea ufafanuzi kuhusu Tanzania iko katika daraja gani la uchumi duniani ili kuondoa sintofahamu iliyopo.
Akichangia jana kuhusu mapendekezo ya Mpango wa Taifa wa Maendeleo pamoja na Mapendekezo ya Mwongozo wa Maandalizi ya Mpango na Bajeti kwa Mwaka 2023/24, Mbunge wa Musumo Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo alisema Tanzania haiko tena katika uchumi waka kati.
Hata hivyo, akichangia leo Profesa Kitila amesema miongoni mwa mafanikio iliyoipata Tanzania ni kufikia uchumi wa kati mwaka 2021.
“Ni muhimu mheshimiwa waziri akalitolea ufafanuzi baadaye, tunasikia takwimu nyingine zinasema tumeshuka ni muhimu Serikali ikaliweka jambo hili vizuri. Si jambo la kupita hivi hivi leo,”amesema.
Amesema kwa mujibu wa taarifa za Benki ya Dunia (WB), za mwaka 2021 nchi yetu ilikadiriwa kuwa na pato Tanzania lilikuwa ni Dola za Marekani Bilioni 67.78 na sio Dola za Marekani Bilioni 62.
Amesema ukifanya hesabu kwa idadi ya watu wa sasa inawapa kuwa pato la Mtanzania ni ni Dola za Marekani 1133.5 kwa mwaka na hivyo kuonyesha kuwa imepanda kidogo ukilinganisha mwaka 2020.
“Hoja kwamba tumeshuka haiwezi kuwa ni kweli. Ni muhimu tukalinda mafanikio yetu kwa wivu mkubwa sana. Ningeomba mheshimiwa Waziri atakapohitimisha, atolee hoja nzinto ya kueleweka ili nchi isibabaike kama uchumi umeshuka ama uko pale,”amesema.
Aidha, amesema suala la kupambana na umasikini ni muhimu lakini kwenye mpango haionyeshi mikakati ya mahususi ya kupambana na umasikini.
“Ni muhimu mpango wa maendeleo uoneshe jitihada za kushughulikia umasikini bayana. Hata neno umasikini limetajwa mara moja (kwenye mpango) tena kwenye Tasaf (Mpango wa Kunusuru Kaya Masikini),”amesema.
Ameishauri wataalam wawapelekee mikakati ya kupunguza umasikini nchini katika mpango wa maendeleo. Profesa Kitila amesema kumekuwa na ongezeko kubwa la watu katika sensa ya mwaka 2022 kuliko sensa zilizopita ambazo ongezeko la watu lilikuwa ni chini ya asilimia 3.2.
Amesema mpango huo unatakiwa uwekeze katika kupunguza umasikin, chakula cha kutosha lakini bahati mbaya kila kitu hakitoshi.
“Maana yake turejee katika miaka ya 1970, 1980, tuanze kuzungumzia suala la uzazi wa mpango halikwepweki lazima lifanyike,”amesema.
Ameshauri Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS) kuongezewa kazi ya kusimamia uzazi wa mpango.
MWANANCHI