Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,681
- 8,887
Wakati akiongelea hali ya uchumi na mpango wa maendeleo bungeni leo Juni 13, waziri Kitila Mkumbo amesema wataendelea kuzingatia nafasi ya madini kukuza ujazo wa mauzo nje ya nchi na kuzingatia umuhimu wa madini ya kimkakati kutimiza azma ya dunia kuzalisha nishati safi na salama kwa mazingira.
Serikali imesema itaweka mazingira mahsusi kuvutia wawekezaji watakaokuwa tayari kujenga viwanda vitakavyoongeza thamani ya madini hayo nchini.
'Tunataka kuona tunasafirisha nje ya nchi betri za magari na sio madini yetu ya kimkakati. Tumesema wazi, wakati dunia inaelekea mwaka 2050 ikizungumzia kwa na 0 emission, tunataka kuona rasimali hizi zinatusaidia na sisi ifikapo mwaka 2050 tunakuwa 0 poverty' Alisema Kitila.