POTOSHI Kitima amshukia vikali Nchimbi, anaigiza na kutudanganya. Je, kuna ukweli hapa?

POTOSHI Kitima amshukia vikali Nchimbi, anaigiza na kutudanganya. Je, kuna ukweli hapa?

Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Kitima huwa hapindishi kanyooka kama rula. Kumbe Nchimbi anaigiza! Anatudanganya.

Roma Locuta; Causa Finita est.!


1785153676408.png
 
Tunachokijua
Julai 24, 2026 makamu wa Rais, Dkt. Emmanuel Nchimbi, akizungumza katika Mkutano wa Wanachama wa Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) uliofanyika Jijini Dar es Salaam, alisisitiza Watanzania kupambana kupata Katiba Mpya na kwamba taifa linahitaji Katiba yenye mwafaka na makubaliano ya wadau wote itakayolinda haki za raia na kulipeleka taifa mbele kwa miaka ijayo.

"Kama nina kitu cha kuwaambia watanzania ningeambiwa hebu makamu wa Rais waambie watanzania jambo moja tu, wakisema una jambo la kuwaambia watanzania moja tu, unapewa nafasi ya mwisho, nitasema pambaneni mpate katiba mpya"

Madai

Ipo video inayodai Padre Charles Kitima amejibu hoja ya Makamu wa Rais na kwamba anatudanganya.

Dkt. Charles Kitima ni padre ambaye ni Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC). Kumekuwapo na video inayosambazwa mtandaoni ikimuonesha Padre Kitima akisisitiza umuhimu wa viongozi kuendesha masuala ya nchi kwa kutumia matendo badala ya maneno pekee huku ikiwekewa kichwa cha habari kinachosema "Kitima amshukia vikali Nchimbi" huku nyingine ikisema "Nchimbi anacheza na watanzania kuna kitu anakitafuta"

Je, ni upi uhalisia wa video hiyo?


Video inapotosha uhalisia kwani imetumiwa katika muktadha tofauti na uhalisia wake.

Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kupitia utafutaji wa maneno muhimu (Key Words Search) na Google Reverse Image Search imebaini video hiyo ilikuwa ni mahojiano ya Mwezi Disemba 01, 2025 aliyofanya Padre Kitima na Jambo TV ambayo pia yalichapishwa katika chaneli ya TEC YouTube.

Katika sehemu ya kipande hicho cha video Padre Kitima aliulizwa kuhusu matukio ya Oktoba 29, 2025, ambapo hatua ambazo serikali nzima kuanzia kwa Rais ilikuwa inazichukua, kama zitasaidia kuepuka kutokea tena kwa yaliyotendeka?

Padre Kitima alijibu kwa kusema ingawa kuna jitihada zinazoonekana kuzuia kujirudia kwa matukio mabaya ya nyuma, jitihada hizo hazina maana bila kukiri ukweli na kuchukua hatua za dhati za kimatendo, kwani wananchi wameshachoshwa na ahadi za uongo kuhusu haki na usalama na wanahitaji viongozi wanaotenda badala ya "wasanii" wanaotenda maigizo.​

Kwa nyakati za hivi karibuni, Padri Charles Kitima hajafanya mahojiano na chombo chochote cha habari. Kutokana na ufuatiliaji uliofanyika, video inayosambazwa kwa sasa si ya hivi karibuni, bali ni video ya zamani ambayo imetumika nje ya muktadha wake ili kuhusishwa na matukio ya sasa.
 
Back
Top Bottom