Kitimtim Kipawa - JK azuiliwa kupita

swali!

Wananchi wamefahamuje kuwa mkulu angepita huo muda?
 
Mambo ya Mbeya, Mawe na Kuzomewa ....Leo tena kazuiwa

I am Smelling French Revolution very soon than later, wananchi tumechoka!
Wafaransa walichoshwa na mama antonnete sijui,sasa watanzania nao wanakaribia kuchoshwa na maisha bora kwa kila fisadi especially aliyeko kwenye mtandao wa JK.Pia na kasi mpya,ari mpya na nguvu mpya ya kuwanifaisha mafisadi na wanamtandao.
 
Kazi inaendelea na bado wananchi wamechoka na hii sirikali
 
Huu wizi wa mchana unaotaka kufanywa na JK na serikali yake wananchi wasikubali na ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa hawa mafisadi,hata mimi ningeingia barabarani hapo na bora wanifunge kuliko kukubali kudhulumiwa na hawa mafisadi..watu hawajakataa kuhama lakini hii biashara ya kulipana kwa bei za 1967 wakati tupo 2009 is a no no!
 

Naam hata mimi nawaunga mkono kwenye hili. Kwa nini walipwe fidia kwa kutumia sheria ya mwaka 67 ambayo itawafanya walipwe mafao madogo. Hii ndiyo mojawapo ya manyanyaso wanayofanyiwa Watanzania wanyonge nchi nzima.
 
,hata mimi ningeingia barabarani hapo na bora wanifunge kuliko kukubali kudhulumiwa na hawa mafisadi..watu hawajakataa kuhama lakini hii biashara ya kulipana kwa bei za 1967 wakati tupo 2009 is a no no!

Koba uko serious ama umeandika kwakuwa uko nyuma ya pazia la computer yako, mara nyingi nyie wasomi ndo mumeangusha taifa hili. Hodari kuongea na kuandika, ikija kwenye vitendo mnatafuta excuse...sina maana wewe nazungumzia kwa ujumla.
 
Mwaka 1967 USD 1 ilikuwa shilingi 7/=
 
Mambo ya Mbeya, Mawe na Kuzomewa ....Leo tena kazuiwa

I am Smelling French Revolution very soon than later, wananchi tumechoka!

Masa,
Huwezi amini kuwa wakati nasoma huu ujumbe wako, namsikia Peter Tosh akiimba "To fight the loosing battle, but to fight...."

French Revolution ilikuwa yenyewe. Hii imesaidia sana kuishape Europe the way ilivyo. Hakuna kitu kibaya kama watu wakikuambia " We have nothing to loose...." Ujuwe utawala wako uko hatarini. I hope viongozi wetu watapata Busara za kuhakikisha hatufiki huko......

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=3ccIcNTVVIM&feature=related[/ame]

The costs of basic items such as flour go far beyond the reach of the common family While the royals dined with the finest treats in the world most of France faced starvation. The fuse was finally lit and with a population that felt they had absolutely nothing to lose the French revolution was born.
 
Mwaka 1967 USD 1 ilikuwa shilingi 7/=
NAAM; Bado USD 1 (I967) ilikuwa inaweza kununua Mafuta ya taa Lita 20 kwa hiyo hata wakiwalipa kwa USD kwa sheria ya 1967 bado sio haki kwani hata hiyo USD ime-devaluate.
 
Kwani Rais alikuwa anakwenda kuongea nao au safari zake za nje ya nchi? Si angesimama na kuongea nao kama anavyofanya akizuiwa sehemu zingine?
 
hahaaaaa,JK utajuta kuwadanganya waTZ na ahadi zako hewa..watu wamechoka na utawala wako usio na muelekeo.
 
Koba uko serious ama umeandika kwakuwa uko nyuma ya pazia la computer yako, mara nyingi nyie wasomi ndo mumeangusha taifa hili. Hodari kuongea na kuandika, ikija kwenye vitendo mnatafuta excuse...sina maana wewe nazungumzia kwa ujumla.

....naweza kukubali kudhulumiwa mkopo wa shule wanaonipa wao lakini land yangu hapo niue tuu na ndio kitakachotokea sasa,JK na serikali yake watakuwa wanafanya kosa kubwa sana hapa na hakuna kitu kimeangusha serikali nyingi kama kuwahamisha watu kwa nguvu au bila compensation,JK anacheza tuu na hapa watapata revenge yao ambayo wataijutia!
 
Wengi niliowaona pale ni akina mama na watoto. Tayari wanasiasa wetu wameshafika pale na hotuba za kuwatuliza zimeanza! Tulipata malezi mabaya tangu zamani, hata kudai kilicho chetu hatujui.
 


Hivi hawa jamaa wa Intelligence – wako kweli kazini? Walipaswa kujua mapema kwamba pale Kipawa mambo yanasukwa ya kumfanyia rabsha JK wakati akipita.

Ni kama vile ilivyokuwa kwa wastaafu wa EAC ya zamani walipokusanyika na kulala Salender Bridge kwa mamia yao na kuzuia magari. Hebu fikiria -- vyombo vya usalama vilizidiwa kete na wazee wa miaka 70!.

Vile vile walishindwa kugundua na kuzui wizi mkubwa wa EPA uliokuwa unafanyika mwaka 2005. Idara hii ya Intelligence haina maana kabisa, ifutwe mara moja.

Kwa upande mwingine wakazi hao wa Kipawa wamwefanya jambo la nishai kabisa – hongera mara elfu.
 

Kwa kuongezea maelezo yako ni kuwa kwa sheria ya sasa ardhi inatathminiwa pia. Sasa wakitumia sheria ya sasa watalipa zaidi. Lakini cha ajabu, why double standards. Wakati jiji linabomoa pale Tabata wale wananchi walilipwa 20m/= harakaharaka. Na pia kule kurasini mwaka juzi wakati wananchi wanaondolewa walipewa 20m/= kama thamani ya ardhi kabla ya ya tathmini ya mali zao. Vipi kipawa. Kwa nini wasingeachiwa wenyewe wauze kwa hao wawekezaji watakaokuja kuhitaji hivyo viwanja?
 
lakini watalipwaje kwa sheria mpya wakati uamuzi umefanyika kwa sheria ya zamani? wenye kufahamu sheria nifafanulieni tafadhali...

Kama kuna mtu anayo compulsory acquisition act atuwekee hapa; nielewavyo mimi ni kwamba....compensation package ita-reflect ile market value ya wakati land ilipokuwa officially acquired....ofcourse it depends pia na location...i.e. commercial, residential or industrial plus na whatever mali iliyokuwepo kwenye ardhi hiyo i.e. nyumba, mimea ya thamani........n.k

kuchelewa kwa serikali kuwalipa.....in a sense serikali ilitakiwa iwafikirie wananchi hao kwa ku-add interest (compounded)....kwa kuwa si kosa la wananchi hao........



inawezekana kabisa kulikuwepo na makubaliano (MoU) baina ya serikali na wananchi husika..........nasema hivi kwa kuwa

1.kulikuwepo na dispute kutoka kwa wananchi kuhusu kiwango (value) cha compensation.......
2. Land ilipokuwa acquired for the first time......wengi wa wamiliki original wakaamua kuuzia watu wengine....(in this circumstances hawa watu hawastahili hata senti...in my opinion)

inawezekana wakti land inakuwa acquired most of it haikuwa na kitu i.e. pori and thus low compensation value (nadhani mnaelewa cost ya ardhi kwa bei ya serikali)

NOTE:
1. kwa jinsi sheria za umiliki wa ardhi zilivyo........ni ngumu sana kuishinda serikali..........but you can always defend your case.

2. Kudai fidia kwa kutumia kiwango cha sasa (i.e current market value)............its not fair for the rest of walipa kodi..........

Pendekezo
WATU WALIPWE FIDIA KWA MARKET VALUE YA ZAMANI PLUS INTEREST ofcourse notwithstanding makubaliano yaliyokuwepo.

kumzuia JK barabarani si tija (japokuwa message is sent)..........kwa kuwa serikali ina utaratibu wake............na huu utaratibu umewekwa makusudi ili ku-protect interests zetu sote.........
 
Fundisho kwa maamuzi yanayofanyika yasiyokuwa na tija wala mashiko. Na wananchi wa maeneo mengine kama Kigamboni na kwinginepo wanajifunza vilevile.
 
Point za kampeni hizi vyama vya upinzani. Hapa nyie ni kuja kumalizia kufunika tu! Point za ku-kampeni mnazo nyingi. Trick ni kujua wapi kuzitumia. Watu kama hawa mnahakikisha wanachagua mbunge mpinzani...hakuna discussion nyingine. Sio kila siku mnaimba wimbo wa mafisadi! Sasa hapa kwenye picha mtasema kweli huyu ni fisadi kama bado anakula meza moja na hawa 'wasafi'?
 
Congo,
eneo lile linarudi serikalini ili kuruhusu upanuzi wa uwanja wa ndege wa JKN. Nakuunga mkono, wangewalipa kama wale ndugu zetu wa Tabata. Wamesoteshwa sana pale.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…