Kitimtim Kipawa - JK azuiliwa kupita

Kitimtim Kipawa - JK azuiliwa kupita

Mkuu si unajua tena hii sirikali yetu ikiamua kitu imeamua?
Vijana wa hapa jirani na kipawa (FFU) ndio walikuwa na haka kajizoezi maana yamekaa muda mrefu kwenye ile stoo yao hayajatumika nao hawajafanya mazoezi ya kupiga na kukamata watu.

Ili muheshimiwa apite asibughuziwe.

Wameona hiyo ndio njia sahihi ya kuwatawanya wananchi but hali halisi walikuwa wafunge barabara wakatu mkuu anaporejea kutoka butihama ili wamweleze kilio chao kwanini serikali yake haiwatendei haki hao wakaazi wa huku Kipawa.

Kwasababu amechoka anahitaji kupunzika

Umuhimu wake ni kupita kwenda Ikulu .......

huyu mheshimiwa kwa nini nae asisime hata 1 min tu na kuchonga na raia wake?
 
This time hakuwa na "PIPI KIFUA" kwenye gari?
 
Great,

Kwanini rais asiwasikilize kabla ya kuendelea na safari yake? Kipi muhimu kwake?

Mdau yaani unauliza kwa nini Rais asiwasikilize, hivi unafikiri atawajibu nini la maana? Hana chochote cha kuwajibu, nchi hii imeishamshinda viongozi wanafanya wanavyotaka na yeye anawaangalia tu. Samahani Mhe Rais huu ndio mtazamo wangu. "YOU NEED TO BE TOUGH MR PRESIDENT"!
 
Congo,
eneo lile linarudi serikalini ili kuruhusu upanuzi wa uwanja wa ndege wa JKN. Nakuunga mkono, wangewalipa kama wale ndugu zetu wa Tabata. Wamesoteshwa sana pale.

Sawa.Lakini maelezo yaliyopo ni kuwa, baada ya wananchi kuondoka vile viwanja tayari vimekwishapimwa upya kwa akili ya kugawia wawekezaji amao watajenga vitu kama mahteli, migahawa na vitu ambavyo vinaendana na viwanja vya ndege na mambo ya utalii. Sasa argument yangu ni kuwa unamnyang'anya mwananchi ardhi yake na kumkodishia mwekezaji. Kwa nini mwekezaji asimnunue mwananchi na serikali iwe mwangalizi tu wa hiyo transaction kama ilivyofanyika kurasini?
 
Yeah,

Wananchi hawataki kulipwa fidia kwa sheria ya mwaka 1967. Wanataka sheria mpya ndo itumike. Leo ndio siku iliyokuwa imepangwa kuanza kulipwa kwa wananchi hawa lakini walitoa tamko kuwa hawakubaliani na serikali na hivyo leo wakaamua kutanda barabarani kumzuia JK kwenda Airport.

Ngongo,

Ndicho chanzo, kuna mtu yupo jirani na eneo hilo, nitakufahamisheni hatma ya wananchi hawa.

Mkuu USIYEONEKANA,
Mara nyingi huwa najiuliza uwezo wa network yako. Yaani INTELIGENSIA yako. Inaonekana ni kubwa sana. Vitu vingi huwa uko very sharp tena toka eneo la tukio.
Bravo sana mkuu.
 
Kusema ukweli hii nchi inamaudhi sana wakati mwingine unaweza kukasirishwa ukajiuliza hivi hii nchi yenye sifa kwa wenzetu wanayo yafanya hi ya haki. Mfano hawa jirani zangu hapa kipawa wanataka kuwalipa fidia ya mwaka 1967 !!!!! kweli hii hi haki maana wakati sheria ya mwaka 67 inatungwa laki moja ya pesa ilikuwa ni nyingi sana mtu waweza nunu hata na gari ukajenga nyumba yako na balance ikabaki kubwa tu ya kutunza heshima mtaani.

Karne hii ya sasa mfuko mmoja wa simenti unauzwa sh. 14500/ ukitaka kujenga nyumba ya vyumba viwili vya kulala na kajisebule potelea mbali kule posta tukakuweka nje na kuzungushia magunia n kikawa cha passport size.
uje upewe shilingi laki 5 utazifanya nini?

Mkuu usemayo ni kweli hawa jamaa huwa wanajifanya hawaelewi kuwa lazima ubadilishe hela ya mwaka 1967 kuileta mwaka 2009. Kwani hata thamani ya hela ya sasa iko chini sana hivyo lazima kuwepo convention. Vinginevyo huo ni wizi wa wazi ambao lazima ulaaniwe kwa njia zote.

Wamezidi kufanya uhuni walifanyia wazee wa africa mashariki tunayajua yaliyotokea na sasa wamehamia kwa hawa. Its not fair.
 
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote,nchi yangu Tanzania jina lako nitamu sana.............. Tuwaambie viongozi wetu waje wajifunze huku Kigali kwa Kagame.
Kagame ananunua makazi ya watu na anatoa stahiki ya thamani halisi ya makazi ya mtu. Watu wanahama na mipango ya serikali inatekelezwa na nchi inasonga mbele. Amini nawaambia baada ya miaka 5 Kigali itakuwa imetuacha mbali. Ni wakati muafaka wa viongozi wetu na watanzania mmoja mmoja kaja huku kujifunza.
 
Sawa.Lakini maelezo yaliyopo ni kuwa, baada ya wananchi kuondoka vile viwanja tayari vimekwishapimwa upya kwa akili ya kugawia wawekezaji amao watajenga vitu kama mahteli, migahawa na vitu ambavyo vinaendana na viwanja vya ndege na mambo ya utalii. Sasa argument yangu ni kuwa unamnyang'anya mwananchi ardhi yake na kumkodishia mwekezaji. Kwa nini mwekezaji asimnunue mwananchi na serikali iwe mwangalizi tu wa hiyo transaction kama ilivyofanyika kurasini?
Serikali yetu, nikimaanisha mawaziri, makatibu wao wakuu na watendaji wengine ni WADHAIFU sana kwa kiasi ambacho wao wanaamini kuwa maendeleo au kukua kwa uchumi wa nchi yetu kutawezekana tu pale ambapo wawekezaji watakuwepo na kufanya kazi au biashara zao hap kwetu. Ni watendaji ambao hawaamini uwezo wao kwahiyo wanataka waamini na uwezo wa Watanzania wenzao ni dhaifu kama wa kwao.
Kwahiyo mkuu hii tabia ya kunyang'anya wananchi ardhi yao na kupewa wawekezaji ipo sana tena sana kwenye maeneo mengi nchini, kwa mfano Kilombero, Kisarawe, Bagamoyo, Mbarali, Korogwe, Arumeru, Hanang' na kwingine kwingi.
 
Kama kuna mtu anayo compulsory acquisition act atuwekee hapa; nielewavyo mimi ni kwamba....compensation package ita-reflect ile market value ya wakati land ilipokuwa officially acquired....ofcourse it depends pia na location...i.e. commercial, residential or industrial plus na whatever mali iliyokuwepo kwenye ardhi hiyo i.e. nyumba, mimea ya thamani........n.k

kuchelewa kwa serikali kuwalipa.....in a sense serikali ilitakiwa iwafikirie wananchi hao kwa ku-add interest (compounded)....kwa kuwa si kosa la wananchi hao........

inawezekana kabisa kulikuwepo na makubaliano (MoU) baina ya serikali na wananchi husika..........nasema hivi kwa kuwa

1.kulikuwepo na dispute kutoka kwa wananchi kuhusu kiwango (value) cha compensation.......
2. Land ilipokuwa acquired for the first time......wengi wa wamiliki original wakaamua kuuzia watu wengine....(in this circumstances hawa watu hawastahili hata senti...in my opinion)

inawezekana wakti land inakuwa acquired most of it haikuwa na kitu i.e. pori and thus low compensation value (nadhani mnaelewa cost ya ardhi kwa bei ya serikali)

NOTE:
1. kwa jinsi sheria za umiliki wa ardhi zilivyo........ni ngumu sana kuishinda serikali..........but you can always defend your case.

2. Kudai fidia kwa kutumia kiwango cha sasa (i.e current market value)............its not fair for the rest of walipa kodi..........

Pendekezo
WATU WALIPWE FIDIA KWA MARKET VALUE YA ZAMANI PLUS INTEREST ofcourse notwithstanding makubaliano yaliyokuwepo.

kumzuia JK barabarani si tija (japokuwa message is sent)..........kwa kuwa serikali ina utaratibu wake............na huu utaratibu umewekwa makusudi ili ku-protect interests zetu sote.........

Mkuu Ogah,

Hapo nilipo highlight ''Mwaveja sana''!...watu wengine hawafikirii impliciation yakuwalipa zaidi kwa walipa kodi wengine, kama sheria inataka walipwe kwa sheria ya 67, kuwalipa kwa ile ya 2002 ni UFISADI mwingine huo!
 
Suala hili pia la kulipwa fidia isiyo stahiki linawatesa sana wakaazi wa Kwembe-Kibamba, Namwawala-Kilombero na maeneo mengi ambayo serikali inachukua maeneo lakini inatumia ubabe kuwahamisha wananchi kwenye maeneo yao.
 
Serikali yetu, nikimaanisha mawaziri, makatibu wao wakuu na watendaji wengine ni WADHAIFU sana kwa kiasi ambacho wao wanaamini kuwa maendeleo au kukua kwa uchumi wa nchi yetu kutawezekana tu pale ambapo wawekezaji watakuwepo na kufanya kazi au biashara zao hap kwetu. Ni watendaji ambao hawaamini uwezo wao kwahiyo wanataka waamini na uwezo wa Watanzania wenzao ni dhaifu kama wa kwao.
Kwahiyo mkuu hii tabia ya kunyang'anya wananchi ardhi yao na kupewa wawekezaji ipo sana tena sana kwenye maeneo mengi nchini, kwa mfano Kilombero, Kisarawe, Bagamoyo, Mbarali, Korogwe, Arumeru, Hanang' na kwingine kwingi.

Kuna siku itafika watu watadai ardhi yao. Kwani ya kenya mnadhani ni ukabila tu? Kuna mengi nyuma ya pazia. Ardhi hakuna watu wachache ndiyo wamehodhi kila kitu. Kuna wananchi wamewadai ardhi yao kwa mkapa na Sumaye (Jamaa walijigawia ekari kadhaa na hawazifanyii kitu). SIKU YAJA HATUTALALA....
 
Tanzania Tanzania nakupenda kwa moyo wote,nchi yangu Tanzania jina lako nitamu sana.............. Tuwaambie viongozi wetu waje wajifunze huku Kigali kwa Kagame.
Kagame ananunua makazi ya watu na anatoa stahiki ya thamani halisi ya makazi ya mtu. Watu wanahama na mipango ya serikali inatekelezwa na nchi inasonga mbele. Amini nawaambia baada ya miaka 5 Kigali itakuwa imetuacha mbali. Ni wakati muafaka wa viongozi wetu na watanzania mmoja mmoja kaja huku kujifunza.

Ha!ha!ha!ha!......hao walianza kwa kupigana mapanga ile miaka ya 1994.......then naona wakaona mapanga sio dili, wale walionusurika wamegeukia kuijenga nchi for real! Nasisi hapa TZ sijui itabidi wengine tuingie msituni kwanza..........?

BWT: Welcome JF, tiletea mambos ya kwa kagame!
 
Poleni wote mliopo huko,shikamaneni mpaka kieleweke,msikubali rudishwa nyuma While ukweli unajulikana!!
 
Imefika wakati ambao sasa serikali inabidi iliangalie hili suala la ARDHI kwa jicho la tofauti kabisa kwakuwa impact yake ni kubwa kuliko wanavyofikria wao. Kuna mifano hai ya hapo Zimbabwe, Kenya na kwingineko. Mimi niki-tathimini hali ya sasa nakumbuka yale mapendekezo ya Tume ya Rais ya Kushughulikia Masuala ya Ardhi iliyoundwa na Mzee Mwinyi mwaka 1991 na kuongozwa na Pro. Issa Shivji na kutoa mapendekezo ambayo baadhi ya yaliyopuuziwa kutekelezwa na serikali ndio leo yanaleta matatizo makubwa leo.

Lakini pia kurekebishwa kwa sheria za Ardhi mwaka 2004 kwa shinikizo la Mabenki kwenye eneo la mikopo na kuipa ardhi tupu thamani bado ni chanzo kikubwa kwenye migogoro ya Ardhi hasa na hawa wanaoitwa wawekezaji hasa kutoka nje ya nchi kwa mialiko ya viongozi wetu wa serikali.
 
NAAM; Bado USD 1 (I967) ilikuwa inaweza kununua Mafuta ya taa Lita 20 kwa hiyo hata wakiwalipa kwa USD kwa sheria ya 1967 bado sio haki kwani hata hiyo USD ime-devaluate.

Mwaka 1967
1USD =7Tsh; kwa hiyo ratio ni 1:7 ama 1/7
leo 2009
1USD=1200 TSH; kwa hiyo ili iwe sawa K*1/1200=1/7
K=1200/7.
Hivo K ni multiplying factor kwa pesa wanazotakiwa kwa kutumia sheria ya mwaka 1967.

yani mfano kwa kutumia sheria ya mwaka 1967 anapaswa kulipwa 1,000,000Tsh basi inatakiwa izidishwe na K-factor,yani
1,000,000*1200/7=171,428,571Tsh.

Nafikiri hapo watakuwa wametenda kitaalamu.
 
Kwenye makisio yako kumbuka pia Dolla Imeshuka thamani pia, fikiria kuweka K-factor nyingine kupata uhalali wake wa sasa!
 
Kwenye makisio yako kumbuka pia Dolla Imeshuka thamani pia, fikiria kuweka K-factor nyingine kupata uhalali wake wa sasa!

Delta K<<< K then weka delta K = negligible.Kwa hiyo una ignore hiyo small change ,nikiwa na maana ya kwamba pato la Taifa na utajiri unahesabiwa unamiliki USD ngapi unazo.
 
Balaa la kutokua na mipango miji, serikali itawalipa wangapi? maana upanuzi utaendelea tu si kiwanja cha ndege pekee, mabarabara na miundombinu mingine kazi ipo mpaka kufika tunapopataka.Tatizo kubwa ni kutokujifunza maana makazi holela yanaendelea kuchipua...!
 
Delta K<<< K then weka delta K = negligible.Kwa hiyo una ignore hiyo small change ,nikiwa na maana ya kwamba pato la Taifa na utajiri unahesabiwa unamiliki USD ngapi unazo.

Nimeishia kucheka tu, hayo Mahesabu Mimi hayapandi kihivyo.....nimeachana nayo almost 20 years ago...thanks kama hujafunga kamba!
 
Ai wewe kuna kitufe pale unabonyeza tu! Anyway usijali, nipo kwa Michuzi nasubiria picha za Kipawa hahahahahah ingawa najua hizi huwa haweki!

Masa, atawekaje wakati anasubiria ukuu wa Wilaya??? Ndiyo maana sitembelei sana kule maana kuko bias!!!!!??

Tunaomba member wetu aliyefanikiwa kupata picha adondoshe hapa tafadhali.

Ukweli ni kwamba mtanzania mzalendo hana nafasi tena katika nchi yake, anadharaulika katika nchi yake, sasa kwa nini na wageni wasitudharau ili hali uongozi unatudharau??? Eti hapao utategemea mhindi au wale wawekezaji uchwara waheshimu haki za mtanzania??? Ingekuwa hivyo yasingetokea ya Niorth Mara, Loliondo na kwingineko kwa aina hii.

Kama serikali inajali wananchi wake isingekubali kuwahadhaa wazalendo wa Mbagala waliopoteza maisha, mali na kila kitu kwa mabomu halafu wanapata fidia ambayo hata kujenga choo cha shimo haifai?? Ni mateso jamani. Tunahitaji mapinduzi.

Mungu nusuru utashi wa viongozi wetu ili wajali maslahi ya taifa na wazalendo wake ambao wanawaweka katika madaraka kwa ahadi hewa na za uongo!!!

Back
Top Bottom