kITOVU CHA HIP HOP TANZANIA JIJI LA MWANZA

Joined
Nov 8, 2018
Posts
38
Reaction score
43
KITOVU CHA HIP HOP TANZANIA JIJI LA MWANZA.

Katika miaka ya 1990, Mwanza ilikuwa bado inajulikana rasmi kama Manispaa ya Mwanza, lakini ulikuwa ni mwongo wa dhahabu ulioweka msingi mkubwa wa mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yaliyofanya mji huo kupandishwa hadhi na kuwa Jiji la pili nchini Tanzania ifikapo miaka ya mapema ya 2000.

Mara nyingi tunapozungumzia chimbuko na ukuaji wa muziki wa Hip-Hop hapa nchini Tanzania, fikra za wengi hukimbilia haraka katika majiji ya Dar es Salaam na Arusha. Miji hii miwili imejipatia umaarufu na sifa kubwa kama vitovu vikuu vya harakati hizo za Muziki wa Hip Hop.

Hata hivyo, historia ya Historia ya Hip hop Tanzania haiwezi kukamilika kabisa bila kulitaja Jiji la Mwanza. Ukiondoa Dar es Salaam na Arusha, Mwanza kilikuwa kitovu kikubwa cha utamaduni huo wa Hip hop Tangu miaka ya 1990s.

Tangu katikati ya miaka ya 1990, mitaa mbalimbali ya Mwanza kama vile Kirumba, Capri Point, Igogo na Nyamanoro haikuwa tu maeneo ya makazi ya kuishi watu, bali ilikuwa ni Mitaa ambayo ilisifika kwa kuzalisha ma-Emcee wenye vipaji vya hali ya juu, waliobeba maono, kupitia uwezo mkubwa wa kuandika .

Katika chapter hii, tunamulika mizizi ya mwanzo kabisa na kuangazia jinsi muziki huu ulivyoanza kushika kasi jijini humo kupitia makundi na wasanii binafsi walioanzisha harakati hizi za msingi.

Mwanzo wa Harakati Rasmi (1992)

Harakati rasmi za Hip-Hop jijini Mwanza zilianza kushika kasi mnamo mwaka 1992. historia ilifunguliwa na kuanzishwa kwa kundi la kwanza kabisa la Hip-Hop jijini humo lililofahamika kwa jina la 2 TWO MEN. Kundi hili lilikuwa na safu thabiti ya wasanii watatu:

Mbega (Marehemu) aliyetambulika kama M-Bang, Gerald aliyejulikana kama Gerry-G, na Yusuf aliyejulikana kama Tod1.

Harakati ziliendelea Ndani ya mwaka huo huo wa 1992, vuguvugu lilizidi kukua na kupelekea kuzaliwa kwa kundi la pili maarufu jijini Mwanza, lililojulikana kama N.W.P (Niger With Power).

Safu ya N.W.P ilipambwa na vichwa kama Ahmad (Marehemu) A.K.A Teminter X, Jontua Jokery, Benard Masanga A.K.A Icet, Venture, pamoja na Moluta.

Wakati makundi haya yakiongoza jahazi, pia kulitokea Solo MC aliyefahamika kama King Kiff Nigger, aliyekuwa akifanya harakati zake binafsi na kuongeza hamasa kwenye muziki huo wa Hip hop.

Kuibuka kwa Kundi la Wep'waa Harakati zilipoingia hatua nyingine, kundi la tatu kuingia kwenye historia ya Mwanza lilikuwa ni WEP'WAA A.K.A QMB. Kundi hili lilijipatia heshima kubwa na kuwa mabingwa wa Rap jijini humo kuanzia mwaka 1993 hadi 1997.

Katika kipindi chake cha dhahabu, WEP'WAA iliundwa na Paul James A.K.A Stone Ice, Yusuf A.K.A Snipy Pupy, Kassim A.K.A K-phunk, Salum A.K.A K-Solo, Hafidh A.K.A Fizz Dogg, na Ahmad (Marehemu) A.K.A Teminator X.

Kama ilivyo katika safari nyingi za makundi ya muziki, ulitokea mvutano wa ndani uliowasilisha upepo wa mabadiliko na hatimaye kupelekea kuvunjika kwa WEP'WAA. Kuvunjika huko kulizaa makundi mawili mapya na kuendeleza Harakati:

WEP'WAA MPYA:

Kundi hili liliendelea kutumia jina hilo likiwa na wajumbe wapya na wa zamani kama Yusuf A.K.A Snip Puppy, Kassim A.K.A K-phunk, Salum A.K.A K-Soloh, Ameen A.K.A Q-Tip, na Sada A.K.A G-rataataatat.

GGV (Gankstas With Great Voice):

Likiwa kundi la nne kuanzishwa jijini Mwanza, GGV liliundwa na waliokuwa member wa WEP'WAA ambao ni Fizz Dogg, Ahmad (Teminator X), na Paul James (Stone Ice). Pia lilipata ushirikiano wa karibu kutoka kwa washikaji waliokuwa wakiwaunga mkono harakati zao kama George, Y-Cube, na Hamidu.

Ilipofika mwaka 1998, kundi la WEP'WAA lilipitia mabadiliko mengine ambapo lilibaki na member mmoja wa asili, Yusuf A.K.A Snip Puppy PE1, aliyeungana na mjumbe mpya aliyefahamika kwa jina la Dust D. ili kuendeleza gurudumu hilo.

Kuibuka kwa Nature Boys (1995)

Katikati ya miaka ya 90, mnamo mwaka 1995, kundi la tano la Hip-Hop lilizaliwa jijini Mwanza likijulikana kama " NATURE BOYS" . Kundi hili lilikuwa na uzito wa kipekee kwani lilileta vipaji vilivyokuja kuacha alama kubwa sana kwenye kiwanda cha Muziki na Vyenye viwango vya kitaifa.

Kabla ya kujulikana kama msanii Fid Q alianza safari yake ya muziki jijini Mwanza miaka ya 1990, akiwa sehemu ya kundi la Nature Boys. Baadaye ndipo akaanza kujijenga kama msanii binafsi na mwaka 2000 akatoa “Huyu na Yule” akiwa na Mr Paul.

Nature Boys liliundwa na Fareed Kubanda A.K.A Fid Q, Ashraf Kichwabuta A.K.A Hardone, Hussein Cheppe A.K.A Chussa, pamoja na producer Rajab Marijani Jr.

Kundi hili lilikuwa sehemu muhimu ya mwendelezo wa mabadiliko ya kiharakati kwenye muziki wa Hip hop uliotokea Mwanza na baadaye kusikika nchi nzima.

Uk
1791098085703.jpg
waju wa kitambo
0767 542 202
 
UkView attachment 3683440waju wa kitambo
0767 542 202
Dar inaanza wengine ndo wanafuata RIP Nigga One, the Legend.
 
Samahani ninaomba unitajie rapper mmoja tu undisputed kutoka Chuga mmoja tu kama moyo
Chugga wana aina yao ya michano ambapo ni sawa na wanakubalika sana kwenye uwanja wa nyumbani ambacho ni kitu kizuri,kwa watu tuliopita hisabati na ithibati ya hip hop ili iliyo deep tunapata ukakasi kidogo kuwaelewa ninachoweza sema Arusha wanaishi culture ya hip hop ila sad to say hawana spear mceez, kuanzia mathematics I mean flows, content na utulivu wa kuapproach beat tofauti tofauti kutokana na hisia yake ya asili 😃
 
CHAPTER 2: HISTORIA YA HIP HOP MWANZA — 1995–1998

Katika Chapter 1, tulizungumzia kuhusu jiji la Mwanza kama moja ya vitovu muhimu vya Hip Hop nchini Tanzania, tukifuatilia mizizi ya muziki huu na namna ulivyoanza kujijenga katika jiji hilo.

Sasa tunaingia kwenye Chapter 2

Katika sehemu hii, tunaanzia kwenye Kundi la sita la Hip Hop Mwanza lililoanzishwa mwaka 1995, hadi kufikia Kundi la " Jita Dunia" mwaka 1998.

Haya ni majina na kumbukumbu zinazosaidia kuonesha namna ambavyo Hip Hop Mwanza ilikuwa ikikua kwa kasi, huku makundi mapya, wasanii wa solo na mitindo mingine kama Dancehall ikiendelea kujitokeza.

DA FAD

Kundi hili lilishika nafasi ya pili katika mashindano ya mwaka 1995.

Liliundwa na:

1. Fide
2. Alio
3. Dady D

---

WASANII WA DANCEHALL

JOUNTWA JOHN AKA JOUNTWA JOKERY

Msanii solo wa Ragga/Dancehall, Jountwa John aka Jountwa Jokery, alikuwa Bingwa wa Mkoa wa Mwanza katika Dancehall kwa miaka:

1992, 1993, 1994, 1995, 1996 na 1997.

JOHN MAKOKO AKA COCO SLYDER

Msanii wa Dancehall aliyeshika nafasi ya pili Tanzania nzima mwaka 1993.

---

KUNDI LA DANCEHALL — THE RAGGA NATION, 1994

Liliundwa na:

1. Rweyman aka Dady Mamu
2. Shija Kimenyi aka Frog Shapper

---

KUNDI LA SABA LA HIP HOP — BH MOBB, 1994

Liliundwa na:

1. Ndida Brown
2. Seif Bitebo aka Mr Ice

---

KUNDI LA NANE LA HIP HOP — WAGUMU WA AKILI WAGWA, 1997

Kundi hili lilikuwa na:

  • Neymia aka Primitive Soja
  • Taqwa Boys

---

DA HOOD — 1997

Kundi hili liliundwa na:

1. Amour Mohamed aka Kaz A
2. Dicson Nyema aka Dic B
3. Shaban Mahita aka Kay Supp

---

WASANII WA SOLO — 1997

  • Edward Tibasima aka City Geez — Hip Hop
  • Jet Man aka Sam — Ragga
  • Amosy Kamanzi aka Phantom Ranks — Dancehall
  • Jaffe aka Jafe Banton — Dancehall

---

WHITE SOX — 1997

Kundi la Hip Hop lililoundwa na:

1. Yusuf Hamza aka Bab Shido
2. Rashid Hussein aka Rato B
3. Ally aka Twist
4. Salum aka Salum Mkali
5. Ally Tyti
6. Sele Bansele

---

KUNDI LA HIP HOP — KINA, 1997

Liliundwa na:

1. Yusuf Kiyobwa aka Cops
2. Denis Mfutuki
3. Gamali

---

LA FACE — 1997

Kundi la Hip Hop lililoundwa na:

1. David Majukano aka Dau Mashikolo Mageni
2. Ally Masanga aka Ally Mashoto

---

KWR — 1997

Kundi hili liliundwa na:

1. Joseph Kashushula aka Joe
2. Kiyaruzi Kashushula aka KIA Boy
3. Edson Lutaraka aka Dogo Eddy

---

ROTEN BROTHERS — 1997

Kundi la Hip Hop lililoundwa na:

1. Seif Bitebo aka Mr Seif aka Ice B
2. Fareed Kubanda aka Little Cub

---

JR PABLIC — DANCEHALL, 1995

Kundi la Dancehall lililoundwa na:

1. Jemsy aka Jay
2. Radi

---

WASANII WA SOLO

1996

  • Jackson Mwakatobe aka Mad Monkey — Dancehall
  • Sami Msindae aka 2Pac aka Sumy Boy — Hip Hop
  • Lukas aka Nigga Luka — Hip Hop
  • John aka John MC — Hip Hop

---

MAKUNDI MENGINE — 1996–1997

BWAY BWAY FAMILY — 1996

Founder: Rweyman

THE DOLPHIN POSSE — 1996

Founder: Jountwa John

---

KUNDI LA HIP HOP — OTO, DAVI MTETEMELA & MZEE KILELE AKA TEGZ — 1997

Kundi hili lilihusisha:

  • Oto
  • Davi Mtetemela
  • Mzee Kilele aka Tegz

---

KUNDI LA R&B LA KWANZA — 1998

Kundi hili liliundwa na:

1. Francis Lymo
2. Batuly
3. Stellah Gora

STELLAH KISSINGA AKA RED CHATA

Msanii wa kike wa Dancehall, aliyetajwa kama msanii wa tatu wa kike Tanzania nzima katika Dancehall, mwaka 1998.

---

KIZAZI YA SWAHILI AKA KYS — 1998

Kundi la Hip Hop lililoundwa na:

1. Abdallah Ngaupila aka Mwambungu
2. Hamza Yusuf aka Bob Shido

---

SWAHILI BY NATURE — 1998

Kundi hili la Hip Hop liliundwa na:

1. Ngulyat Mohamed aka Chief Nguli
2. Jafar Mzonge aka Jeff Jery
3. Juma Mrisho Zangalo aka Jay Zaga
4. Ahmad Mshamu

---

THE BLACK FAMILY — 1998

Kundi la Hip Hop lililoundwa na:

1. Shaban Masnga aka Mzee Black
2. Shaban Black aka Sheby Rastar

---

THE MECCA FRASH — 1998

Kundi hili la Hip Hop liliundwa na:

1. Bwire aka Yego B
2. Bukoli aka Ice B
3. Mathwe Mzee aka Messo Rasta
4. Haruna Kregina aka Buster
5. Nuhu Banda aka Nuhu Buster
6. Fulo aka Swiqilo
7. Lup9ndije aka Diwani
8. Kurwa aka Kay Prince
9. Shaban aka Sheby
10. Choma aka Mzawa
11. Mzee aka DJ Pelish Smith
12. Fareed Kubanda aka Fid Q
13. Ahmad aka Hard Mad
14. Khalid

---

MAKUNDI NA WASANII WENGINE WA KIPINDI HIKI

WADE WADE — DANCEHALL

Kundi lililoundwa na:

1. Hippopotamus
2. Chesco

SOLO ARTIST — 1998

  • Yusuf Mkodanda aka Jungle Man — Dancehall
  • Ahmad aka Mad Ice — Dancehall

---

JITA DUNIA — 1998

Na katika safari hii ya historia tunafikia Kundi la Hip Hop la Jita Dunia, lililoanzishwa mwaka 1998.

Jita Dunia ni miongoni mwa majina yanayoongeza picha ya namna ambavyo scene ya Hip Hop Mwanza ilikuwa ikiendelea kupanuka na kuibua makundi mbalimbali katika miaka ya mwisho ya 1990.

Hapa ndipo tunafunga sehemu hii ya Chapter 2.

Katika sehemu inayofuata, tutaendelea na majina mengine, wasanii wa solo, makundi, DJs, MCs pamoja na waandaaji wa matukio waliokuwa sehemu ya historia hii.

UKWAJU WA KITAMBO
0767 542 202
 
Chugga wana aina yao ya michano ambapo ni sawa na wanakubalika sana kwenye uwanja wa nyumbani ambacho ni kitu kizuri,kwa watu tuliopita hisabati na ithibati ya hip hop ili iliyo deep tunapata ukakasi kidogo kuwaelewa ninachoweza sema Arusha wanaishi culture ya hip hop ila sad to say hawana spear mceez, kuanzia mathematics I mean flows, content na utulivu wa kuapproach beat tofauti tofauti kutokana na hisia yake ya asili 😃
Upo sahihi bro
 
KITOVU CHA HIP HOP TANZANIA JIJI LA MWANZA.

Katika miaka ya 1990, Mwanza ilikuwa bado inajulikana rasmi kama Manispaa ya Mwanza, lakini ulikuwa ni mwongo wa dhahabu ulioweka msingi mkubwa wa mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yaliyofanya mji huo kupandishwa hadhi na kuwa Jiji la pili nchini Tanzania ifikapo miaka ya mapema ya 2000.

Mara nyingi tunapozungumzia chimbuko na ukuaji wa muziki wa Hip-Hop hapa nchini Tanzania, fikra za wengi hukimbilia haraka katika majiji ya Dar es Salaam na Arusha. Miji hii miwili imejipatia umaarufu na sifa kubwa kama vitovu vikuu vya harakati hizo za Muziki wa Hip Hop.

Hata hivyo, historia ya Historia ya Hip hop Tanzania haiwezi kukamilika kabisa bila kulitaja Jiji la Mwanza. Ukiondoa Dar es Salaam na Arusha, Mwanza kilikuwa kitovu kikubwa cha utamaduni huo wa Hip hop Tangu miaka ya 1990s.

Tangu katikati ya miaka ya 1990, mitaa mbalimbali ya Mwanza kama vile Kirumba, Capri Point, Igogo na Nyamanoro haikuwa tu maeneo ya makazi ya kuishi watu, bali ilikuwa ni Mitaa ambayo ilisifika kwa kuzalisha ma-Emcee wenye vipaji vya hali ya juu, waliobeba maono, kupitia uwezo mkubwa wa kuandika .

Katika chapter hii, tunamulika mizizi ya mwanzo kabisa na kuangazia jinsi muziki huu ulivyoanza kushika kasi jijini humo kupitia makundi na wasanii binafsi walioanzisha harakati hizi za msingi.

Mwanzo wa Harakati Rasmi (1992)

Harakati rasmi za Hip-Hop jijini Mwanza zilianza kushika kasi mnamo mwaka 1992. historia ilifunguliwa na kuanzishwa kwa kundi la kwanza kabisa la Hip-Hop jijini humo lililofahamika kwa jina la 2 TWO MEN. Kundi hili lilikuwa na safu thabiti ya wasanii watatu:

Mbega (Marehemu) aliyetambulika kama M-Bang, Gerald aliyejulikana kama Gerry-G, na Yusuf aliyejulikana kama Tod1.

Harakati ziliendelea Ndani ya mwaka huo huo wa 1992, vuguvugu lilizidi kukua na kupelekea kuzaliwa kwa kundi la pili maarufu jijini Mwanza, lililojulikana kama N.W.P (Niger With Power).

Safu ya N.W.P ilipambwa na vichwa kama Ahmad (Marehemu) A.K.A Teminter X, Jontua Jokery, Benard Masanga A.K.A Icet, Venture, pamoja na Moluta.

Wakati makundi haya yakiongoza jahazi, pia kulitokea Solo MC aliyefahamika kama King Kiff Nigger, aliyekuwa akifanya harakati zake binafsi na kuongeza hamasa kwenye muziki huo wa Hip hop.

Kuibuka kwa Kundi la Wep'waa Harakati zilipoingia hatua nyingine, kundi la tatu kuingia kwenye historia ya Mwanza lilikuwa ni WEP'WAA A.K.A QMB. Kundi hili lilijipatia heshima kubwa na kuwa mabingwa wa Rap jijini humo kuanzia mwaka 1993 hadi 1997.

Katika kipindi chake cha dhahabu, WEP'WAA iliundwa na Paul James A.K.A Stone Ice, Yusuf A.K.A Snipy Pupy, Kassim A.K.A K-phunk, Salum A.K.A K-Solo, Hafidh A.K.A Fizz Dogg, na Ahmad (Marehemu) A.K.A Teminator X.

Kama ilivyo katika safari nyingi za makundi ya muziki, ulitokea mvutano wa ndani uliowasilisha upepo wa mabadiliko na hatimaye kupelekea kuvunjika kwa WEP'WAA. Kuvunjika huko kulizaa makundi mawili mapya na kuendeleza Harakati:

WEP'WAA MPYA:

Kundi hili liliendelea kutumia jina hilo likiwa na wajumbe wapya na wa zamani kama Yusuf A.K.A Snip Puppy, Kassim A.K.A K-phunk, Salum A.K.A K-Soloh, Ameen A.K.A Q-Tip, na Sada A.K.A G-rataataatat.

GGV (Gankstas With Great Voice):

Likiwa kundi la nne kuanzishwa jijini Mwanza, GGV liliundwa na waliokuwa member wa WEP'WAA ambao ni Fizz Dogg, Ahmad (Teminator X), na Paul James (Stone Ice). Pia lilipata ushirikiano wa karibu kutoka kwa washikaji waliokuwa wakiwaunga mkono harakati zao kama George, Y-Cube, na Hamidu.

Ilipofika mwaka 1998, kundi la WEP'WAA lilipitia mabadiliko mengine ambapo lilibaki na member mmoja wa asili, Yusuf A.K.A Snip Puppy PE1, aliyeungana na mjumbe mpya aliyefahamika kwa jina la Dust D. ili kuendeleza gurudumu hilo.

Kuibuka kwa Nature Boys (1995)

Katikati ya miaka ya 90, mnamo mwaka 1995, kundi la tano la Hip-Hop lilizaliwa jijini Mwanza likijulikana kama " NATURE BOYS" . Kundi hili lilikuwa na uzito wa kipekee kwani lilileta vipaji vilivyokuja kuacha alama kubwa sana kwenye kiwanda cha Muziki na Vyenye viwango vya kitaifa.

Kabla ya kujulikana kama msanii Fid Q alianza safari yake ya muziki jijini Mwanza miaka ya 1990, akiwa sehemu ya kundi la Nature Boys. Baadaye ndipo akaanza kujijenga kama msanii binafsi na mwaka 2000 akatoa “Huyu na Yule” akiwa na Mr Paul.

Nature Boys liliundwa na Fareed Kubanda A.K.A Fid Q, Ashraf Kichwabuta A.K.A Hardone, Hussein Cheppe A.K.A Chussa, pamoja na producer Rajab Marijani Jr.

Kundi hili lilikuwa sehemu muhimu ya mwendelezo wa mabadiliko ya kiharakati kwenye muziki wa Hip hop uliotokea Mwanza na baadaye kusikika nchi nzima.

UkView attachment 3683440waju wa kitambo
0767 542 202
Mbeya na Arusha kings of hiphop
 
Katika sura hii tunaendelea kufuatilia safari ya Hip-Hop jijini Mwanza, tukianzia kwenye makundi, wasanii binafsi, Dancehall, DJs, MCs, waandaaji wa matukio pamoja na mazingira yaliyosaidia kukuza utamaduni wa Hip-Hop katika jiji la Mwanza kuanzia miaka ya 1990.

Lengo ni kuonyesha kwamba Mwanza ilikuwa na mchango mkubwa katika harakati za awali za Hip-Hop, Rap na Dancehall nchini

KUNDI LA HIP-HOP LA JITA DUNIA — 1998

Kundi la Hip-Hop la Jita Dunia 1998

WASANII SOLO ARTS WA DANCEHALL

Jaffe aka Jafe Banton — 1997

Jita Man — 1998

Kid Bway — 1997

KUNDI LA HIP-HOP GSM — 1998

Likiundwa na:

1. Emma aka Big MO
2. Amarido Charles aka Mkristo
3. Othuman aka Rayotti
4. Omary aka OGC

WASANII SOLO ARTS WA HIP-HOP

Radof Ramju aka Rado Uso wa Mbuzi — 1999

Chamba Boy — 1998

Slay G — 1998

Mohamed aka East T

WASANII SOLO ARTS WA DANCEHALL

All Beka — 1998

KUNDI LA HIP-HOP IGOGO ARMY — 1998

MA-DJ

1. Rich Dillon
2. DJ Summer Dancer
3. DJ Hamad
4. DJ Yusuf aka Yudolife
5. DJ Young Milioner
6. DJ SureBoy
7. DJ Fred Mpemba
8. DJ Eddy Glant
9. DJ Young Pasadena
10. DJ Muhina
11. DJ Paul Ilonga
12. DJ Maliz
13. Paul James
14. DJ Yusuf
15. DJ Young Sedo
16. DJ Ommy Kula Moto
17. DJ Cutter
18. DJ Mwangi
19. DJ Jeff Jerry
20. DJ Aleco

MA-MC

1. Adam aka Super Engineer — East Africa Number 1
2. Mukhusin Mambo Stopper
3. Godwin Gondwe aka Double G

WAANDAJI WA SHUGHULI

1. Najib — Deluxe Hotel Disco, likiitwa Up Town Disco Tech, 1993–94.

Akiwaleta wasanii kutoka Dar es Salaam kwa mara ya kwanza.

Wasanii walioletwa ni:

1. Rankim Ramadhani
2. Cuty Ranks
3. Young Millionaire
4. Deo Mtui aka Flesh XE
5. Coni Way

Sababu ya kuleta MC kutoka Dar es Salaam kina Rankim ni kwa sababu Felician Muta wa FM Studio alikuwa mmiliki wa Disco la Natta Hotel. Aliandaa mashindano ya kudance, ndipo Najib wa Up Town Disco Tech akaamua kuwa tofauti kwa kuleta wasanii wa Hip-Hop, jambo lililosaidia kukuza Hip-Hop Mwanza.

MC Stopper alikuja akiletwa na Mzee TK, akirap kwa Kiingereza kutoka Uganda na kuchana juu ya beat za Funk.

Kisha akaanzisha mashindano ya kwanza ya Rap mwaka 1993–94 kwa wasanii wa Mwanza.

2. DJ Young Millioner & DJ Eddy Glant — 1995

Ghand Hall na Ilemela Beach, 1995.

3. Jountwa — Tennis Court, 1996

4. Yusuf Qasim aka Bob Suyo — Tivol 2Pac Day, 1996

5. Bway Bway Entertainment — Jeans Party, Tivol, 1997

6. David Ratta — Summer Jam Party, Saa Nane Island, 1996

Pamoja na Concert Liberty Cinema, 1996.

7. Emma GMB — Who's Da Man, 1997

New Mwanza Hotel.

8. Bway Bway Entertainment — Lake Zone Who Da Man, 1998

New Mwanza Hotel.

MATUKIO NA SHOW MBALIMBALI

  • Beach Party — Yarch Club Mwanza, 1997
  • Pool Side Party — Mwanza Club, 1998
  • Beach Party — Macoco Beach, Musoma Town, 1996
  • House Party — Magereza Hall, Musoma Town, 1996
  • Concert Show — Mamndali Hall, Bukoba Town, 1997
  • Concert Show — Butiama Hotel, Shinyanga Town, 1996
  • Beach Party — Tembo Beach, Musoma Town, 1998
  • Beach Party — Palm Beach, Musoma Town, 1998
  • Lake Zone Who Da Man — New Mwanza Hotel, 1998
  • Lake Zone Who Da Man — Vijana Hall, Kirumba Mwanza, 1999
  • Beach Party — Peninsula Beach, Musoma Town, 1999
  • Style and Fashion — Capri Cabanna Mwanza, 1999
  • Music Concert Show — Capri Cabana, 1999
  • Pure Talent Show — Capri Cabanna, 1999
  • My Love Is Your Love Valentines Day — Capri Cabanna, 2000Hii nimeanzia Jita Dunia 1998
 
KITOVU CHA HIP HOP TANZANIA JIJI LA MWANZA.

Katika miaka ya 1990, Mwanza ilikuwa bado inajulikana rasmi kama Manispaa ya Mwanza, lakini ulikuwa ni mwongo wa dhahabu ulioweka msingi mkubwa wa mabadiliko ya kiuchumi na kijamii yaliyofanya mji huo kupandishwa hadhi na kuwa Jiji la pili nchini Tanzania ifikapo miaka ya mapema ya 2000.

Mara nyingi tunapozungumzia chimbuko na ukuaji wa muziki wa Hip-Hop hapa nchini Tanzania, fikra za wengi hukimbilia haraka katika majiji ya Dar es Salaam na Arusha. Miji hii miwili imejipatia umaarufu na sifa kubwa kama vitovu vikuu vya harakati hizo za Muziki wa Hip Hop.

Hata hivyo, historia ya Historia ya Hip hop Tanzania haiwezi kukamilika kabisa bila kulitaja Jiji la Mwanza. Ukiondoa Dar es Salaam na Arusha, Mwanza kilikuwa kitovu kikubwa cha utamaduni huo wa Hip hop Tangu miaka ya 1990s.

Tangu katikati ya miaka ya 1990, mitaa mbalimbali ya Mwanza kama vile Kirumba, Capri Point, Igogo na Nyamanoro haikuwa tu maeneo ya makazi ya kuishi watu, bali ilikuwa ni Mitaa ambayo ilisifika kwa kuzalisha ma-Emcee wenye vipaji vya hali ya juu, waliobeba maono, kupitia uwezo mkubwa wa kuandika .

Katika chapter hii, tunamulika mizizi ya mwanzo kabisa na kuangazia jinsi muziki huu ulivyoanza kushika kasi jijini humo kupitia makundi na wasanii binafsi walioanzisha harakati hizi za msingi.

Mwanzo wa Harakati Rasmi (1992)

Harakati rasmi za Hip-Hop jijini Mwanza zilianza kushika kasi mnamo mwaka 1992. historia ilifunguliwa na kuanzishwa kwa kundi la kwanza kabisa la Hip-Hop jijini humo lililofahamika kwa jina la 2 TWO MEN. Kundi hili lilikuwa na safu thabiti ya wasanii watatu:

Mbega (Marehemu) aliyetambulika kama M-Bang, Gerald aliyejulikana kama Gerry-G, na Yusuf aliyejulikana kama Tod1.

Harakati ziliendelea Ndani ya mwaka huo huo wa 1992, vuguvugu lilizidi kukua na kupelekea kuzaliwa kwa kundi la pili maarufu jijini Mwanza, lililojulikana kama N.W.P (Niger With Power).

Safu ya N.W.P ilipambwa na vichwa kama Ahmad (Marehemu) A.K.A Teminter X, Jontua Jokery, Benard Masanga A.K.A Icet, Venture, pamoja na Moluta.

Wakati makundi haya yakiongoza jahazi, pia kulitokea Solo MC aliyefahamika kama King Kiff Nigger, aliyekuwa akifanya harakati zake binafsi na kuongeza hamasa kwenye muziki huo wa Hip hop.

Kuibuka kwa Kundi la Wep'waa Harakati zilipoingia hatua nyingine, kundi la tatu kuingia kwenye historia ya Mwanza lilikuwa ni WEP'WAA A.K.A QMB. Kundi hili lilijipatia heshima kubwa na kuwa mabingwa wa Rap jijini humo kuanzia mwaka 1993 hadi 1997.

Katika kipindi chake cha dhahabu, WEP'WAA iliundwa na Paul James A.K.A Stone Ice, Yusuf A.K.A Snipy Pupy, Kassim A.K.A K-phunk, Salum A.K.A K-Solo, Hafidh A.K.A Fizz Dogg, na Ahmad (Marehemu) A.K.A Teminator X.

Kama ilivyo katika safari nyingi za makundi ya muziki, ulitokea mvutano wa ndani uliowasilisha upepo wa mabadiliko na hatimaye kupelekea kuvunjika kwa WEP'WAA. Kuvunjika huko kulizaa makundi mawili mapya na kuendeleza Harakati:

WEP'WAA MPYA:

Kundi hili liliendelea kutumia jina hilo likiwa na wajumbe wapya na wa zamani kama Yusuf A.K.A Snip Puppy, Kassim A.K.A K-phunk, Salum A.K.A K-Soloh, Ameen A.K.A Q-Tip, na Sada A.K.A G-rataataatat.

GGV (Gankstas With Great Voice):

Likiwa kundi la nne kuanzishwa jijini Mwanza, GGV liliundwa na waliokuwa member wa WEP'WAA ambao ni Fizz Dogg, Ahmad (Teminator X), na Paul James (Stone Ice). Pia lilipata ushirikiano wa karibu kutoka kwa washikaji waliokuwa wakiwaunga mkono harakati zao kama George, Y-Cube, na Hamidu.

Ilipofika mwaka 1998, kundi la WEP'WAA lilipitia mabadiliko mengine ambapo lilibaki na member mmoja wa asili, Yusuf A.K.A Snip Puppy PE1, aliyeungana na mjumbe mpya aliyefahamika kwa jina la Dust D. ili kuendeleza gurudumu hilo.

Kuibuka kwa Nature Boys (1995)

Katikati ya miaka ya 90, mnamo mwaka 1995, kundi la tano la Hip-Hop lilizaliwa jijini Mwanza likijulikana kama " NATURE BOYS" . Kundi hili lilikuwa na uzito wa kipekee kwani lilileta vipaji vilivyokuja kuacha alama kubwa sana kwenye kiwanda cha Muziki na Vyenye viwango vya kitaifa.

Kabla ya kujulikana kama msanii Fid Q alianza safari yake ya muziki jijini Mwanza miaka ya 1990, akiwa sehemu ya kundi la Nature Boys. Baadaye ndipo akaanza kujijenga kama msanii binafsi na mwaka 2000 akatoa “Huyu na Yule” akiwa na Mr Paul.

Nature Boys liliundwa na Fareed Kubanda A.K.A Fid Q, Ashraf Kichwabuta A.K.A Hardone, Hussein Cheppe A.K.A Chussa, pamoja na producer Rajab Marijani Jr.

Kundi hili lilikuwa sehemu muhimu ya mwendelezo wa mabadiliko ya kiharakati kwenye muziki wa Hip hop uliotokea Mwanza na baadaye kusikika nchi nzima.

UkView attachment 3683440waju wa kitambo
0767 542 202
DR KB YUKO WAPI HALAFU NGOMA ZAO HUJATAJA,
 
Back
Top Bottom