Kitovu kikubwa cha mtoto

Kitovu kikubwa cha mtoto

ntagunga

JF-Expert Member
Joined
Aug 13, 2011
Posts
704
Reaction score
285
Wadau wa afya salam.

Nini chanzo cha mtoto kuwa na kitovu kikubwa kama puto? Na je, mtu akisha kuwa na kitovu hicho, kuna dawa ya kukifanya kiwe kidogo?

Mtu anaweza fanyiwa upasuaji kukiondoa?

Natanguliza shukrani.

Siamini kama ni maumbile, naona kama kuna kitu kimekosewa. Ushauri wenu utasaidia
 
Walikosea kukifunga.. Au kilipata infection alipokuwa mdogo.. Yote yanaweza changia
 
Wadau wa afya salam.

Nini chanzo cha mtoto kuwa na kitovu kikubwa kama puto? Na je, mtu akisha kuwa na kitovu hicho, kuna dawa ya kukifanya kiwe kidogo?

Mtu anaweza fanyiwa upasuaji kukiondoa?

Natanguliza shukrani.

Siamini kama ni maumbile, naona kama kuna kitu kimekosewa. Ushauri wenu utasaidia
Nini chanzo, dawa kwa mtoto kuzaliwa na kitovu kikubwa

Mkuu, hizi mambo zilisha wahi kujadiliwa kwa kina sana humu ndani.
Nakushauri upitie hiyo link hapo juu, pengine utapata machache yatakayo kusaidia.
Asante.
 
Anafanyiwa oparesheni tu,nilishuhudia Bugando mtoto tena wakike ,kwa Sasa Ni mdada mkubwa ,
 
Modes kuna uzi kama huu wa siku nyingi, nadhani ingekuwa vema zikaunganishwa
 
Hiyo inaitwa Umbilical Hernia, kama umeishwahi sikia kitu kinachoitwa Hernia basi alichonacho huyo mtoto ni aina mojawapo kati ya aina nyingi tofauti tofauti za Hernia zikiwa na sababu nyingi tofauti tofauti pia.
Hilo la wewe kutokukubali kuwa inaweza kuwa ni maumbile sijaelewa unamaanisha nini ila kwa watoto sababu mojawapo ya Umbilical Hernia kwao ni kwamba wapo wanaozaliwa wakiwa na udhaifu wa misuli ya tumboni, ikimaanisha wapo hivyo genetically/kwa kurithi au misuli yao inachelewa kukaza kulingana na umri, hivyo basi mkandamizo(ie pressure) wowote ukiongezeka tumboni ni rahisi kwa utumbo kupenya kwenye misuli laini na kutokezea kitovuni ikajionyesha kwa kitovu kuwa kikubwa.
Wapo ambao huwa inapotea yenyewe na wale ambao haitopotea tiba iliyo ya uhakika ni Upasuaji na kurudisha utumbo ndani kisha kushona kuziba upenyo uliokuwepo kuzuia kutojirudia tena, ingawa haimaanishi haiwezi jirudia japo uwezekano huo ni asilimia ndogo.
 
Wadau wa afya salam.

Nini chanzo cha mtoto kuwa na kitovu kikubwa kama puto? Na je, mtu akisha kuwa na kitovu hicho, kuna dawa ya kukifanya kiwe kidogo?

Mtu anaweza fanyiwa upasuaji kukiondoa?

Natanguliza shukrani.

Siamini kama ni maumbile, naona kama kuna kitu kimekosewa. Ushauri wenu utasaidia
Hilo puto ukaliuze ila akikua kinapungua
 
Uzushi !! Mchane chali saba kwa kiwembe kisha mpanguse na tango pori na utupe hilo tango jalalani (maumivu yakizidi muone daktari)
 
Wadau wa afya salam.

Nini chanzo cha mtoto kuwa na kitovu kikubwa kama puto? Na je, mtu akisha kuwa na kitovu hicho, kuna dawa ya kukifanya kiwe kidogo?

Mtu anaweza fanyiwa upasuaji kukiondoa?

Natanguliza shukrani.

Siamini kama ni maumbile, naona kama kuna kitu kimekosewa. Ushauri wenu utasaidia
Anaweza leo hii mimi nilikuwa tmj, mwanangu alikuwa anafanyiwa suna, kuna mdada nae mwanae alikuwa anapunguzwa kitovu, inafanyika wala usiwe na shida
 
Anaweza leo hii mimi nilikuwa tmj, mwanangu alikuwa anafanyiwa suna, kuna mdada nae mwanae alikuwa anapunguzwa kitovu, inafanyika wala usiwe na shida
Gharama zake zinakuaj3 au bima inagharamia.?
 
Back
Top Bottom