Kitu gani cha ajabu ulichokifanya utotoni?

Niliwasha moto nyuma ya nyumba ya jirani nilipojaribu kuuzima ukanishinda,nikaamua kutoka nduki mpaka home na kujificha kwenye uvungu wa kitanda.Kuuzima moto ule ilibidi mtaa mzima ukusanyike.Baadae nikadakwa raia wakanisamehe kwa kua nilikua mdogo sana.
 
Mimi na crew yangu tulikua tumetoka shule primary bas tumepita karib na nyumba moja hiv tukaona kuna kifurush kiko nje ni aina ya vifurush flan kama paper bags ilikua imewekwa kwenye mlango kutokana na utundu wetu tulikichukua kufungua ndan tukakuta bagia..tulizifakamia zote ...had leo nakumbuka na kuishia kucheka tu japo sijui kwanini zilikua pale.nje
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Pia nakumbuka kua nikiingia bafun kuoga naingia ndan ya karai lemye maji.ya moto.ambayo yshapoozwa kwaio.naingia ndan ya karai nauchapa usingiz tena saio.na kile kibarid cha.asubuh na yale maji ya moto aise acha tu ..bada ya muda nashtuka.nimeanza kugongew mlango wa bafuni hahahhh
 
Ulikuwa kichaaaaa[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
ha ha ha ha ha

wangeku-scorpion pambaffu.

[emoji23] [emoji23]
 
mimi ndio nilikuwa refa wa ngumi,yaani muda wa kutoka shule wanafunzi wenzangu walikuwa wanakuja kuniuliza kama kuna pambano.Yaani walikuwa wakitibuana tu,wanakuja kwangu kutoa taarifa nami nawaingiza kwenye ratiba.Wakati mwingine nilikuwa naratibu mapambano mpaka matatu kwa siku.Sheria ilikuwa ukitoka damu basi pambano limeisha na wewe uliyetoka damu ndio umeshapigwa.Kimbembe ni siku siri ilipovuja kwa walimu baada ya mtoto mmoja kula kichapo mpaka jino likatoka na mzazi akaja kesho yake shule.Yaani nilipomuona tu kijana yuko na mzazi wake wanaenda ofisi ya mwalimu mkuu,nilikula kona na sikutokea shule wiki nzima.Nilikua nikitoka nyumbani naaga naenda shule kumbe naishi porini.Bahati mbaya kuna siku dogo mmoja aliniona nimebana miembeni,daaah akaenda kumtonya ticha.Asikuambie mtu,darasa zima lilitumwa kunikamata,kuna watu wana mbio sio mchezo.Nilichezea fimbo sana siku hiyo na ndio nikastaafu rasmi urefa na kuratibu ndondi.
 
Kwenye ule mchezo wa kibabababa,Mama mkwe kanifumania namvua mtoto wake chupi!
 
Hahahaaa kama sio Ustadhi Yasin Abdallah basi wewe utakuwa J Msangi
 
Hahahaaa kama sio Ustadhi Yasin Abdallah basi wewe utakuwa J Msangi
hahaaaaaaaa,walitakiwa walimu wavumbue kipaji na sio kunilamba fimbo na kusitisha ndoto zangu za kuwa refa wa ndondi bora duniani
 
Nilikuwa na kamchezo ka kuiba togwa nakunywa nikiulizwa namsingizia mtoto kainywa kuna siku nilisingizia mtoto kanywa togwa ilikuwa kwenye chupa ya bia mother ku prove ikajazwa tena mtoto akapewa anywe akashindwa kuinyanyua chupa kibano kikanigeukia
 
kipindi nikiwa miaka 7,8 hv kuna mbaba mmoja aliwafunga ng'ombe wake kwenye jiwe ili wapate malisho..sasa mm nikaenda na kuanza kuwapaka maji kwenye manyonyo kisha mafuta halafu nikaanza kuwakamua maziwa ,.nikaenda mbali nikawafungua wakawa wanazagaa sasa kuwarudisha ikawa mtiti

Yule mbaba kumbe aliniona ile anakuja nikatoka nduki mpk nyumbani yule mzee kwa hasira akaja na bunduki nyumbani nilivyoona vile nikaruka ukuta nikasepa mpk saa nne usiku nilirudi,home walinitafuta sana ile siku

Yule mzee mikwara tu alikuwa ananitishia ili nisiwasogelee tena ng'ombe wake ila kwa akili ya utoto nilidhan alikuja kuniua
 
Mbona humu sijaona mtu anaandika kwamba alikuwa kikojozi wa kuozesha magodoro ya pamba kila kukicha? Wengine humu mlikuwa mnajisaidia haja kubwa kitandani usiku wa manane mkiwa mnaota ndoto, kwamba mpo msalani. Mbona hayo yote hamsemi? Au mmeyasahau? Kama mmeamua kusema mambo yenu ya utotoni hadharani basi semeni yote tuujue ukweli. Msitubabaishe hapa.
 
kwa saikolojia ya haraka haraka ni kwamba umetoa ya moyoni kwa namna nyingine,kwamba wewe ulikuwa ukitenda hayo.Very brave of u
 
Nakumbuka kulikuwa na misumari fulani nilipenda kuichezea,sasa siku hiyo usiku mida ya saa mbili nimeshika zangu misumari yangu natembea mara msumari mmoja ukanidondoka. Nikautafuta wee sikuuona nikaupotezea,kumbe bana ule msumari ulidondokea kwenye sufuria ya mboga tena ilikuwa mchuzi wa maini.

Katika kupakua pakua ule msumari ukawa katika bakuli la mdingi,alipoona msala ukamwaangukia bi mkubwa. Mi nikanyamaza kimya kama sijui,ikabidi mdingi aniagize chips maana hakutaka tena kula kile chakula. Mi nikaenda kununua chips kuja nazo zikawa za baridi akasusa akaamua kulala na njaa,mi nikazipiga chips zote.
 
Mie nilimcharanga shoka kuku aliekua anaataga na kupasua mayai yake yote baada ya kuanza kunipigia kelele nikiwa natengeneza gari languu la mbaoo.... Nilikua sipendagi ujinga mimi nikiwa kwenye kazi zangu
[emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
OK tuanze na wewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…