Kitu gani cha thamani ambacho panya aliwahi kukuharibia mpaka sasa unawachukia hata kuwaona

The Watchman

JF-Expert Member
Joined
Nov 7, 2023
Posts
896
Reaction score
1,427
Hawa wanyama wa ajabu sana waharibifu mpaka wanakeraa, wanaweza wakaingia kwenye begi wakaacha vitu visivyo vya maana wakatafuna vyeti vya shule au hela. kwakweli mimi nikiwaona hawakai kwa amani kabisa nitafanya kila jambo kuwasambaratisha.

Your browser is not able to display this video.
 
Kuna siku nimepigika vibaya mno, ndani nna vidagaa mafuta na kaunga kama nusu hivi, nikasema acha hili buku jero nikachukue viungo nije nitoe kitu. Nikapika ugali na dagaa nikawaunga vizuri walikuwa watam sana, si mnajua dagaa ukitia ndimu hilo harufu lake na utam nazi ikasome.

Nilipomaliza kupika nikafunika fresh kabisa nikasema acha nifuate maji ya kurefill nikafanya hivyo, nimerudi na njaa yangu sikuamini macho yangu na ndani sikuwahi kuona panya, nikashinda njaa.
 
wadudu wanakeraaa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…