Kitu gani huwa kinasababisha miguu kutoa harufu kali?

Kitu gani huwa kinasababisha miguu kutoa harufu kali?

King Jody

JF-Expert Member
Joined
Oct 8, 2022
Posts
1,834
Reaction score
3,456
Kuna rafiki yangu ana tatizo la miguu kutoa harufu kali, yani akivua viatu ni balaa, akinitembelea home huwa namwambia aingie na viatu, wapo waliomshauri aloweke miguu kwenye maji ya betri mwisho wa siku akaishia kuchubuka miguu lakini wapi, kwa kifupi amehangaika sana bila mafanikio.

Kwa yeyote ambaye amewahi kupitia changamoto kama hii na akafanikiwa kuitatua atujuze tafadhali.
 
Kwa yeyote ambaye amewahi kupitia changamoto kama hii na akafanikiwa kuitatua atujuze tafadhali.
Mafuta na sabuni anazotumia kujipaka na kuogea ndio Chanzo

Sabuni atumie za asili
Mafuta atumie ya asili mfano ya Nazi au mafuta yaliyotengeneza kwa matunda na asali
 
Mafuta na sabuni anazotumia kujipaka na kuogea ndio Chanzo

Sabuni atumie za asili
Mafuta atumie ya asili mfano ya Nazi au mafuta yaliyotengeneza kwa matunda na asali
Sawa
 
Osha miguu vizuri, sugua magaga, fua socks, safisha viatu.
Mbona harufu haitokuwepo. LOL
 
1. Kama una fungus miguuni, tibu fungus mpaka zipone kabisa. Na pendelea kuosha/kuloweka miguu yako kwa sabuni ya unga au dettol.

2. Epika kuvaa soksi miguu ikiwa na unyevunyevu, kausha miguu vizuri, especial katikati ya vidole hakikisha ni pakavu.

3. Usivae viatu kwa muda mrefu, pendelea kuvaa viatu vya wazi. Vaa viatu pale inapolazimu tu.

4. Kama miguu yako inatoa jasho, hakikisha unavaa soksi za cotton na ziwe nene kidogo, na badilisha soksi kila siku.
 
Ulikuwa unatumia mafuta gani mkuu, mimi nilikuwa nahisi labda ukipaka mafuta ndo tatizo linaondoka.
Mafuta ya asili ndio yameondoa hilo tatizo ndio maana nikamwambia atumie mafuta ya asili iwe ya Nazi au mafuta mengine yoyote ya asili tatizo linapotea lenyewe taratibu

Kuna mafuta nilikua napaka km lotion hivi yanaharufu nzuri sana Ila yakishakutana na Jasho la Mwili unaanza kunuka vibaya yaan sio Miguu tu Mwili wote unatoa harufu mbaya hadi unajiuliza umepakaa nini ndio nikagundua hilo nikaacha mara 1 kutumia hayo Mafuta/lotion nikaanza kutumia mafuta za asili yaan organic tatizo limepotea mpaka sasa

Kingine viatu asivae vinavyobana sana maana Miguu inakosa pumzi inapelekea kunuka Miguu au kupatwa na magonjwa ya Miguu km kupasuka Kucha nk
 
Chukua jiwe la kusugulia miguu lile la miatano au elfu moja, chukua beseni, maji ya vuguvugu, kias weka sabuni ya unga humo loweka kama dakika tatu miguu halafu sugua miguu na lile jiwe vizuri mguu wote hadi sehemu ya kukanyagia , katikati ya vidole, na kwenye ngozi ya juu ya mguu, halafu toa mguu ukauke paka maji ya limao, tulia kabisa,
 
Sawa mkuu
 
Hio inaondoa tatizo siku 1 baada ya hapo tatizo linaendelea vile vile
 
Unaeza pia baada ya hayo ujitahidi kua walau na sendoz hata pea moja ili muda mwingine kuacha mguu upate hewa, hasa jioni unapiga sendo yako safi na kuzingatia usafi
 
Fua soksi na zikauke vizuri, hakikisha kiatu kinakua safi, ukimaliza kuoga uwe na taulo ndogo maalumu ya kufutia miguu usivae kiatu kama miguu haijakauka vizuri, kausha miguu vizuri ndio uvae kiatu
Ongezea Kiatu kisiwe cha kubana sana Mguu maana kikibana sana Jasho likitoka mguuni kifuatacho balaa

Soksi pia avae za Cotton zinazoweza kufyonza Jasho mguuni, mguuni kuna vinyweleo Mguu ukipigwa Jua unatokwa na Jasho kwa hio ni vizuri akivaa soksi za cotton yaan Pamba
 
Unaeza pia baada ya hayo ujitahidi kua walau na sendoz hata pea moja ili muda mwingine kuacha mguu upate hewa, hasa jioni unapiga sendo yako safi na kuzingatia usafi
Ndio sendoz ni muhimu kwa mtu km huyo
 
Back
Top Bottom