Ni siku ya kumi sasa tangu vodacom wapandishe bei za vifurushi vya matumizi ya simu. Baada ya malalamiko ya wateja, serikali kupitia TCRA walitoa tamko la kutaka makampuni yote yarudishe bei za zamani wakati suala hilo likishughulikiwa. Pia na rais Samia S Hassan naye akakazia kwa kutaka suala hilo la upandishaji holela wa vifurushi lisijirudie tena. Baadhi ya makampuni ya simu ikiwemo Hallotel walitii agizo hilo na kurudisha bei za mwanzo. Lakini sijui ni kwa kiburi au dharau, vodacom mpaka leo wamekaidi agizo hilo na kuendelea na bei zao mpya ambazo kwa hakika ziko juu mno.
Hivi hawa jamaa nani anawalinda kiasi cha kukaidi hata agizo la rais? Je TCRA au waziri husika mbona nanyi mko kimya?
Hivi hawa jamaa nani anawalinda kiasi cha kukaidi hata agizo la rais? Je TCRA au waziri husika mbona nanyi mko kimya?